Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 397
- 993
Mwanaharakati Fatma Karume, amekosoa mfumo anaotumia Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Paul Makonda katika kukusanya malalamiko ya watu na kueleza kuwa ni udhalilishaji.
"Sipendi kuona wananchi wanarundikana wako kwenye mistari wanamsubiri Makonda kulalamika, ni udhalilishaji. Lakini tujiulize kwa nini kuna udhalilishaji wa wananchi kiasi hiki, kwa sababu kuna kufeli kwa mfumo,"alieleza Fatma Karume.
"Wananchi wanajua kuna mahakama, kuna ofisi za mkuu wa mkoa, ofisi za wilaya, tatizo lao ni kwamba wakienda hawashughulikiwi, kuna kuanguka kwa mfumo. Tuache kufanya hii michezo, wapeni Watanzania mfumo wa haki unaofanya kazi, wanastahili hilo," alisisitiza zaidi.
Fatma aliongea haya katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo Februari 03,2024, kuzungumzia mifumo ya haki,akiangazia suala la usalama wa mawakili.
The Chanzo