Chonde chonde Chadema mnaona wenzenu CUF wanavyozimika kama moto wa mshumaa, licha ya hii taarifa ya gazetini tayari kuna taarifa za ndani ya chama kutaka kupewa msaada na mafisadi ili kujiimaarisha tunaonya tena.
TUNAONYA Chadema kutochukua senti moja ya hawa mafisadi maana mtafikiri ni siri lakini itagundulika tu, na hiyo ya mafisadi kutaka kujipendekeza chadema ni baada ya kuona uwezekano mkubwa wa Chadema kuchukua dola kipindi kijacho na wao hawatakuwa na pa kukimbilia maana lazima wajibu tuhuma zote sasa ili kuwa on safe side na tusiweze kuwahoji watakuja na hizo senti zao kutoa support ili chadema ichukue nchi.
Nasema tena narudia Chadema ni mali ya Wanachama wa Chadema tumeifikisha hapo ilipofika kimasikini na hata kama hatutakuwa na senti ni bora twende kigumu hivyo hivyo lakini si kuchukua senti moja ya mafisadi maana hao hao watatoa siri na watakimaliza chama kabisa.