Mafisadi kuhamia CHADEMA?

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,728
2,259
Lisemwalo lipo, kama halipo laja.

Kuna tetesi kuwa baadhi ya mafisadi wana uhusiano wa karibu na uongozi wa juu wa CHADEMA.

Nukuu ya gazeti la Raia Mwema la leo linaeleza kwa undani jinsi vikao vya mafisadi vitakavyofanyika huko Arusha Pasaka hii.
Arusha ndiko wanatoka Dr Slaa na E Lowassa, sijui kama kuna uhusiano hapo!

Nape Nnauye alitonesha suala hili la uhusiano kwa mbali kati ya genge la mafisadi na CHADEMA, wakati akituhumu kuwa kuna magezeti, chama fulani na viongozi fulani wa dini wameanza kutumiwa(taarifa za kiintelijesia?).

Jamani pesa hiyo inatembea.

Ikija thibitika CHADEMA will have lost all credibility.

============
Mafisadi wadandia CHADEMA kujiokoa


  • Wajipendekeza upinzani kupenyeza ajenda
  • Benno Malisa ajiunga rasmi kuwatetea
  • Watukana viongozi wa juu wa CCM
BAADA ya mambo kuzidi kuwaelemea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), watuhumiwa wa ufisadi sasa wameanza kwa nguvu kubwa kutaka ‘kudandia mgongo' wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kujinusuru na kutafuta kuungwa mkono na umma, KuliKoni limefahamishwa.

Habari kutoka kwa baadhi ya watu walio karibu na watuhumiwa hao na matukio ya hivi karibuni yanadhihirisha pasi shaka kwamba, watuhumiwa hao sasa wameanza kutumia umaarufu wa CHADEMA kutaka kupata kuungwa mkono na umma na pia kuitisha CCM iogope kuendelea kuchukua hatua dhidi yao.

Kwa mujibu wa habari hizo, mkakati wa mwanzo ulikuwa ni kuhakikisha kwamba CCM inapoteza kiti cha Ubunge jimbo la Igunga kilichoachwa wazi na Rostam Aziz, aliyelazimika kujivua gamba ili ionekane ni hasara kuwalazimisha wengine kujiondoa katika nafasi zao.

Baada ya kukwama Igunga imeelezwa kwamba hatua inayofuata sasa ni kuwashambulia na kuwahujumu viongozi wa juu wa CCM na watu walio karibu nao huku wakizidi kujisogeza karibu na Chadema kwa kuwasifia, lakini wakipenyeza ajenda zao za kutetea mafisadi na miradi yao.

"Baada ya kushindwa kuzuia ushindi wa CCM Igunga ili kuonesha kwamba dhana ya kujivua gamba ina madhara kwa chama, sasa wameanza kujionesha wazi wazi kuwa wanaunga mkono Chadema ili wananchi wawaunge mkono pia na kuwatisha CCM waone kwamba watatoka CCM wakifuatwa na wafuasi wengi.

"Walifanya hujuma kubwa sana Igunga. Mchana walionekana wenzetu lakini usiku wanatuhujumu lakini hawakufanikiwa. Kuna wengine walidiriki hata kusaidia wapinzani kwa njia tofauti na wengine kuwaambia watu wao kutoichagua CCM na sasa wanaeneza propaganda kwamba CCM imechakachua kuhalalisha uovu wao," anasema mtoa habari wetu aliye karibu sana na mafisadi.

Imeelezwa kwamba watuhumiwa hao wamekuwa na mkakati wa muda mrefu wa kujiunga na vyama vya upinzani vyenye nguvu lakini baada ya Chadema kuzidi kupata wafuasi wengi, ndicho chama pekee wanachokiangalia kwa sasa japo hakuna dalili za kupokelewa huko kwa wakati huu.

KuliKoni limefahamishwa na mmoja wa viongozi wa Chadema kwamba, hoja ya kuwapokea baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi iliwahi kujitokeza lakini ilipata upinzani mkubwa kutoka kwa viongozi wa juu wa chama hicho, pamoja na kuwapo mawasiliano yasiyo rasmi ya baadhi ya wafuasi wa watuhumiwa hao na viongozi hao.

Tayari kuna taarifa kwamba viongozi wawili wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wamekuwa na mazungumzo yasiyo rasmi na viongozi wa CHADEMA, lakini hakuna dalili zozote za kupokelewa huko hasa baada ya kubainika wazi kwamba wameanza kujiunga rasmi na kundi la watuhumiwa wa ufisadi bila kificho.

CHANZO: Gazeti la Kulikoni

 
Umechanganya kiswahili na kingereza.Kingereza ulichotumia hakifai kutumiwa kwenye mtandao ambao unaaminika ya kuwa unatumiwa na watu makini.
 
Arusha ndiko wanatoka Dr Slaa na E Lowassa, sijui kama kuna uhusiano hapo!

Nape Nnauye alitonesha suala hili la uhusiano kwa mbali kati ya genge la mafisadi na CDM.

Jamani pesa hiyo inatembea.
CDM hamna siasa za undugu (Lowassa asingetajwa na Dr Slaa katika list of shame)

Pesa inaweza nunua kila mtu CCM ila sio CHADEMA.

vikao ARUSHA???? vya EPA, RICHMOND, DOWANS, MERIMETA vilifanyika magogoni viwanja vya tausi kwa hiyo usishangae hili (eboo DAR jirani yake msoga BGMY)
 
umekalia upupu muwasho tu unakusumbua. Unaona Silaa(Dkt wa Ukweli) ni wa kukaa na fisadi meza Moja?
 
umekalia upupu muwasho tu unakusumbua. Unaona Silaa(Dkt wa Ukweli) ni wa kukaa na fisadi meza Moja?
na ikiwa wakipigiana simu itakuwa Dr SLAA anampa EL,RA,AC mbinu ya kulizamisha lichama la magamba ile design ya tukose wote kwani haiwezekani watatu tu waondolewe halafu ccm ijidai ni chama safi.
 
na ikiwa wakipigiana simu itakuwa Dr SLAA anampa EL,RA,AC mbinu ya kulizamisha lichama la magamba ile design ya tukose wote kwani haiwezekani watatu tu waondolewe halafu ccm ijidai ni chama safi.

Ndio maana orodha ya mafisadi imeongezeka!
 
Umechanganya kiswahili na kingereza.Kingereza ulichotumia hakifai kutumiwa kwenye mtandao ambao unaaminika ya kuwa unatumiwa na watu makini.

Jaribu kuchangia hoja na c kujifanya mwl wa kiingereza..ok!
 
wewe uliyeanzisha hii mada inaonekana jinsi gani hauna umakini,fanya utafiti kabla ya kuongea au uvccm?
 
wewe uliyeanzisha hii mada inaonekana jinsi gani hauna umakini,fanya utafiti kabla ya kuongea au uvccm?
Mkuu umakini gani zaidi ya kusoma?
Tena gazeti linaloheshimika la Raia Mwema, lisome and also read between the lines, kama una upeo wa kuelewa utaelewa tu.
 
Mkuu umakini gani zaidi ya kusoma?
Tena gazeti linaloheshimika la Raia Mwema, lisome and also read between the lines, kama una upeo wa kuelewa utaelewa tu.
wewe huoni ccm walitaka kutuchezea mchezo wa maigizo kwa kuwaondoa mapacha huku wengine wengi wakisalia?ufisadi serikalini mbona JK asiwaondoe wahusika???
ccm wangetembea kifua mbele kwa kuwaondoa mapacha na wangewadanganya watu kwamba na wao ni safi kama cdm
Alichofanya slaa ni kuzidisha ugumu wa mambo ndani ya ccm
Ili cdm izidi kukua lazima mafisadi wabakie ndani ya ccm
Dont u appreciate mchango wa MAKAMBA baba kwa kuikuza CDM kwa pumba zake??? MAFISADI SHOULD RETAIN THEIR SEATS NDANI YA CCM
 
sijui kitawaleta nn ?watakuja na dhamira gan ?nadhani ni fikra fupi zisizonamashiko hasa ukiangalia ktk uhalisia wake,
 
Back
Top Bottom