Mafisadi kuhamia CHADEMA?

Mafisadi kuhamia CHADEMA?

CHADEMA hawezi kwenda fisadi bana.

Fisadi akitoka CCM anahamia CUF NCCR, TLP au UDP bana kwani umeambiwa CHADEMA ni chama cha mikataba feki.

(CCM) wacha hizo bana fikiri hata kidogo ukipata information bana au unasemaje mkuu.
 
EL NA AC WAMECHUKUA KADI ZA NCCR BADO PACHA MMOJA RA ANAONEKANA KAMA ATAENDA CUF aka CCM WIFE
 
Waanzishe Chama chao Cha Mafisadi, kama wakitoka Chama cha Magamba!
 
sijui kitawaleta nn ?watakuja na dhamira gan ?nadhani ni fikra fupi zisizonamashiko hasa ukiangalia ktk uhalisia wake,

Mkuu mbona waruka kimanga?
Watu wanaliona dili hilo waulizia tena mshiko? hapo(kwa mafisadi) uko nje nje!
 
CDM hamna siasa za undugu (Lowassa asingetajwa na Dr Slaa katika list of shame)
Pesa inaweza nunua kila mtu CCM ila sio CDM
vikao ARUSHA????vya EPA,RICHMOND,DOWANS,MERIMETA vilifanyika magogoni viwanja vya tausi kwa hiyo usishangae hili (eboo DAR jirani yake msoga BGMY)

Amka wewe, kungekuwa hakuna siasa za undugu mbona viti maalum mmechaguana ndugu tupu? mtoto, mkwe, mjukuu nk
 
siyo kuhamia huku tayari wapo.ila mwanachama ambaye ni minor hawezi kuliona hilo.
 
Hao MAFISADI watapitia "mlango"gani kuingia Chadema!!!?
 
Umechanganya kiswahili na kingereza.Kingereza ulichotumia hakifai kutumiwa kwenye mtandao ambao unaaminika ya kuwa unatumiwa na watu makini.

Sio Kingereza tu bali hata habari yenyewe, kwani mafisadi wangefanyia Mbeya inamaana Mwakyembe au Mwandyosa wanahusika???
 
Wajiunge wapi mkuu!! Nape keshaanza kazi huyo au huijui nafasi yake kwenye Chama?
Chadema sio kichaka cha kupokea vilaza wakujivua GAMBA...huku wanakaa wazalendo walio tayari kwa lolote ilimradi waitetee Inji yao hayo ma GAMBA hayana nafasi huku.
 
...Mada yako haina tija,mpangilio,wala muelekeo wenye maana,haina mvuto wa kusababisha watu wachangie kwa umakini.

Jaribu kufikiria kwanza kwa umakini kabla ya kupost hapa JF..........
 
only83

Huna haja ya kufikiri sana mkuu , kama unajua kusoma na kuandika soma Raia Mwema la leo 20/4/2011.

Na ukisha soma leave the rest to your best imagination,better and analytical minds, of which you are probably not, can read between the lines.
 
Last edited by a moderator:
Kama wewe unadhani kuna tofauti kati ya CCM na CHADEMA pole sana.

They have the same father, the Freemasons. Wanachofanya to me ni kama mchezo wa kuigiza.
 
Kama wewe unadhani kuna tofauti kati ya CCM na CDM pole sana.They have the same father,the Freemasons.Wanachofanya to me ni kama mchezo wa kuigiza.

sasa unafanya nini ndani ya jukwaa la siasa,.huamini CDM,huamini ccm,.sasa unaamini nini tz,maana kati ya CDM na ccm ni sawa na mwanga na giza au wema na uovu sasa wewe huamini kwenye hivyo viwili basi wewe hujui chochote kuhusu siasa za tz nenda jukwaa la bongo fleva kama lipo
 
  • Wajipendekeza upinzani kupenyeza ajenda
  • Benno Malisa ajiunga rasmi kuwatetea
  • Watukana viongozi wa juu wa CCM
BAADA ya mambo kuzidi kuwaelemea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), watuhumiwa wa ufisadi sasa wameanza kwa nguvu kubwa kutaka ‘kudandia mgongo' wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ili kujinusuru na kutafuta kuungwa mkono na umma, KuliKoni limefahamishwa.

Habari kutoka kwa baadhi ya watu walio karibu na watuhumiwa hao na matukio ya hivi karibuni yanadhihirisha pasi shaka kwamba, watuhumiwa hao sasa wameanza kutumia umaarufu wa Chadema kutaka kupata kuungwa mkono na umma na pia kuitisha CCM iogope kuendelea kuchukua hatua dhidi yao.

Kwa mujibu wa habari hizo, mkakati wa mwanzo ulikuwa ni kuhakikisha kwamba CCM inapoteza kiti cha Ubunge jimbo la Igunga kilichoachwa wazi na Rostam Aziz, aliyelazimika kujivua gamba ili ionekane ni hasara kuwalazimisha wengine kujiondoa katika nafasi zao.

Baada ya kukwama Igunga imeelezwa kwamba hatua inayofuata sasa ni kuwashambulia na kuwahujumu viongozi wa juu wa CCM na watu walio karibu nao huku wakizidi kujisogeza karibu na Chadema kwa kuwasifia, lakini wakipenyeza ajenda zao za kutetea mafisadi na miradi yao.

"Baada ya kushindwa kuzuia ushindi wa CCM Igunga ili kuonesha kwamba dhana ya kujivua gamba ina madhara kwa chama, sasa wameanza kujionesha wazi wazi kuwa wanaunga mkono Chadema ili wananchi wawaunge mkono pia na kuwatisha CCM waone kwamba watatoka CCM wakifuatwa na wafuasi wengi.

"Walifanya hujuma kubwa sana Igunga. Mchana walionekana wenzetu lakini usiku wanatuhujumu lakini hawakufanikiwa. Kuna wengine walidiriki hata kusaidia wapinzani kwa njia tofauti na wengine kuwaambia watu wao kutoichagua CCM na sasa wanaeneza propaganda kwamba CCM imechakachua kuhalalisha uovu wao," anasema mtoa habari wetu aliye karibu sana na mafisadi.

Imeelezwa kwamba watuhumiwa hao wamekuwa na mkakati wa muda mrefu wa kujiunga na vyama vya upinzani vyenye nguvu lakini baada ya Chadema kuzidi kupata wafuasi wengi, ndicho chama pekee wanachokiangalia kwa sasa japo hakuna dalili za kupokelewa huko kwa wakati huu.

KuliKoni limefahamishwa na mmoja wa viongozi wa Chadema kwamba, hoja ya kuwapokea baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi iliwahi kujitokeza lakini ilipata upinzani mkubwa kutoka kwa viongozi wa juu wa chama hicho, pamoja na kuwapo mawasiliano yasiyo rasmi ya baadhi ya wafuasi wa watuhumiwa hao na viongozi hao.

Tayari kuna taarifa kwamba viongozi wawili wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wamekuwa na mazungumzo yasiyo rasmi na viongozi wa Chadema, lakini hakuna dalili zozote za kupokelewa huko hasa baada ya kubainika wazi kwamba wameanza kujiunga rasmi na kundi la watuhumiwa wa ufisadi bila kificho.

CHANZO: Gazeti la Kulikoni
 
Unajua Chadema sehemu kubwa ya umaarufu wake inatokana na kuonekana waziwazi kinawatetea wanyonge na kupambana na mafisadi, na hata CCM ilipata wafuasi kwa kupambana na mafisadi, na hata Igunga CCM ilishinda kwa kuwa imemuondoa fisadi na hiyo ndiyo hoja kuu kwa wananchi sasa bila kujali vyama vyao, kwa hiyo Chadema haiwezi kujiua kisiasa kubeba mafisadi," anasema kiongozi mmoja wa Chadema mkoani Arusha.

Tayari Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amekanusha waziwazi kutobeba watuhumiwa wa ufisadi na kwamba chama chake kimekuwa makini kisiasa wakati wote wa harakati zake nchi nzima.

Miezi michache iliyopita Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC ya chama hicho, Nape Nnauye, akiwa Zanzibar, alibainisha kwamba mafisadi wana mikakati ya kuhusisha baadhi ya vyama vya siasa, magazeti na asasi za dini kujibu mapigo dhidi ya CCM, mambo ambayo yameshaanza kutokea ikiwamo kutukwana kwa viongozi wa CCM akiwamo Nape mwenyewe.

Huo ni umbea wenye lengo na dhamira chafu ya kuvuruga Chadema. Ni wajibu wetu kuibua mafisadi kwa kadiri tunavyopata ushahidi. Tulianza 2007 na tutaendelea kwa awamu," alisema na kuendelea:

Tuhuma dhidi ya Chadema kutumika ziliibuka siku chache baada ya maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kutangaza kuwa imewataka wanachama wake watatu kujiondoa katika nyadhifa zao, ambako chama hicho kikuu cha upinzani kilifanya mkutano wake mkoani Tabora na kuonekana wazi kubadili mwelekeo.

Katika mkutano huo Chadema ilitoa orodha mpya ya mafisadi ikiwa na majina mapya.

Ilielezwa kwamba mkakati huo mpya ulilenga kuingiza majina mengi zaidi katika orodha ya mafisadi ili CCM ione uzito katika kutekeleza dhana ya kujivua gamba.

Akiongea na KuliKoni kwa njia ya simu, kiongozi mwingine wa Chadema alisema kwamba kinachoendelea CCM ni matatizo yao wenyewe na kwamba kwa vile chama hicho kililea ufisadi kwa muda mrefu makundi kilichoyazalisha yataendelea kutafunana kila kukicha.

Katika kudhihirisha mkakati huo mpya, kundi linaloaminika kumuunga mkono Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, lilionesha wazi wazi kuasi na kushambulia viongozi wenzao wa CCM na kusifia Chadema huku wakionesha kutetea watuhumiwa wa sakata la Richmond.

Aliyewashangaza wengi alikuwa Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM kutamka hadharani kwamba serikali isiingilie vyama vya upinzani ikiwamo Chadema na kwamba wananchi waungane kutaka wanasiasa waliopinga Dowans wachukuliwe hatua kwa kupotosha umma.

Bila kujua hoja ya Chadema ni kutaka watuhumiwa waliohusika na mkataba wa Richmond akiwamo Lowassa wafilisiwe ili kulipa deni la Dowans, Malisa alitaka wapinzani kuungana na CCM kutaka walioipinga Dowans kuchukuliwa hatua.

Walioshiriki katika mkutano wa Malisa, ulioambatana na ufunguaji wa matawi bila kushirikisha uongozi wa CCM mkoa na wilaya ya Arusha, ni pamoja na Mbunge Catherine Magige, ambaye alielezwa kutamba kuwa haogopi polisi ambao walikataa kutoa kibali cha maandamano kwa maelezo kwamba ‘anawamudu.'

Wengine walioshiriki ni pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha, James Millya, ambaye alimtukana waziwazi Nape kwa kumuita kichaa na kumshauri mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, aangalie upya uteuzi wake.

"Haya ni matusi kwa Rais Kikwete, haiwezekani kwa kiongozi wa nchi kuteua kichaa na inaweza kutafsirika kuwa Millya ana mashaka na uwezo wa Mwenyekiti wake wa chama. Na hii ni hatari sana kwa uhai wa chama chenyewe. Anadiriki hata kukashifu familia ya Rais! Huyu anastahili kufukuzwa uanachama, sijui anapata wapi hii jeuri," anasema kiongozi mmoja wa UVCCM.

Katika hotuba yake iliyowashangaza wengi Malisa aliitaka serikali na CCM kutoingilia mambo ya Chadema na kuwaacha wawafukuze madiwani wao walioonekana kushirikiana na CCM.

"Nimesikia kuna madiwani wamefukuzwa Chadema na kuna viongozi ambao si wana Chadema wanawakingia vifua, niwaombe tusiingilie mambo ya vyama vyao na tusitumie nafasi tulizopewa na dhamana hizi kuingilia yasiyotuhusu niwatake vijana wa CCM kisheria kata hizo zitaenda katika uchaguzi jiandaeni kugombea," alisema Malisa na kuongeza;

"Sisi kama Chama kinachoongoza, tujitahidi kuheshimu demokrasia na maamuzi ya vyama vingine, tusipende kutumia vyombo vya serikali kuwakomoa kwani siku ya mwisho wanaoumia ni wananchi na si vyama vya siasa.

"Nitumie nafasi hii kumuomba Mbunge wa Arusha Mjini kaka yangu Lema (Godbless) kuwa mstari wa mbele katika kuleta umoja na mshikamano hapa mjini (Arusha) na kumaliza tofauti za u-CCM na u-Chadema ili wakazi wa Arusha wapate maendeleo."

Kuhusu Dowans, Malisa alisema; "CCM tunalalamika wakati sisi wenyewe tunaibomoa nchi na chama chetu. Tazama sakata la Dowans, waliosema wao watatusaidia kupinga kulipa Dowans na ambao walitushauri na kutumia nafasi zao tusinunue mitambo ya Dowans nao sasa wanalalamika na kuanza kutafuta wachawi, wawajibike walitudanganya kama taifa leo tumeshindwa kesi mitambo ileile waliyosema haifai leo inatumika na kampuni ya Symbion, wanatufanya Watanzania mazuzu."

Malisa alitaka vijana wa CCM kuungana na wa vyama vya upinzani kuwawajibisha waliopinga Dowans kununuliwa.

Hotuba ya Malisa ambaye sasa anaonekana wazi kuwa upande wa mafisadi, ilijaa kejeli na dharau kwa serikali na uongozi wa CCM Taifa, hali iliyotafsiriwa kuwa ni uasi wa waziwazi.

Dhana ya uvuaji gamba iliwagusa Lowassa ambaye anahusishwa na mradi wa Richmond, Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge, na Rostam ambaye tayari amekwishajivua gamba kwa kuachia nafasi zake za CCM. Chenge amekuwa akihusishwa na sakata la ununuzi wa rada kwa bei isiyo halali na kwamba wakati akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali nchi hii iliingia mikataba mingi mibovu inayolitafuna taifa hivi sasa.
 
Back
Top Bottom