Mafanikio ya Rais Samia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na utoaji wa huduma za kijamii, na katika Sekta mbalimbali

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,323
8,236
Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imeshuhudia mafanikio makubwa katika kuimarisha miundombinu hususan barabara, reli, viwanja vya ndege, bandari, huduma za kiuchumi na kijamii, ujenzi wa madarasa, hospitali, zahanati na vituo vya afya, huduma za maji, utawala bora, mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, pamoja na kuhamasisha uwekezaji na utalii.

Serikali ya Dk. Samia imehakikisha sera za mapato na matumizi zinajikita katika kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa. Msukumo mkubwa umejikita katika kuhakikisha usimamizi madhubuti wa fedha za umma na kuzielekeza kwenye maeneo yatakayoongeza tija, ajira na kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.

Aidha, Serikali imehakikisha miradi ya kipaumbele na kimkakati inayoendelea kutekelezwa inakamilika kwa wakati ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi mipya.

Serikali ya Awamu ya sita imetuhakikishia kwamba miradi ya kipaumbele na kimkakati inayoendelea kutekelezwa inakamilika kwa wakati ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi mipya.

Miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali katika sekta ya Rais Dk. Samia ni pamoja na:
  • Ujenzi wa Reli ya Kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway- SGR) kipande cha Dar es Salaam - Morogoro (Km 300), kipande cha Morogoro - Makutupora (Km 422), na Mwanza - Isaka (Km 341).
  • Miradi mingine ni pamoja na utekelezaji wa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (Megawati 2,115).
  • Kukamilika kwa ulipaji wa fidia katika maeneo ya kipaumbele ya Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleani - Tanga (Tanzania) pamoja na kusaini Mkataba kati ya Nchi Hodhi na Wawekezaji (Host Government Agreement - HGA) na Mkataba wa Ubia (Shareholding Agreement - SHA).
Miradi mingine ni:
  • Ujenzi wa Barabara na Madaraja Makubwa ambapo ujenzi wa barabara ya mzunguko katika Jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3.
  • Kuboresha Usafiri wa Abiria na Mizigo katika Maziwa Makuu.
  • Ujenzi wa viwanja vya ndege pamoja na uendelezaji wa ujenzi wa mji wa Serikali.
  • Kujenga miundombinu ya elimu kwa lengo la kuhakikisha watoto wanapata elimu katika mazingira bora na yenye staha.
  • Kupitia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19, serikali ya Rais Dk. Samia imefanikiwa kupunguza msongamano wa wanafunzi kwa kuongeza madarasa 12,000 katika shule za sekondari, madarasa 3,000 katika vituo shikizi na mabweni 50 kwa wanafunzi wenye ulemavu. Ujenzi huo wa vyumba vya madarasa umewezesha wanafunzi wote waliochaguliwa katika mwaka 2022 kujiunga na kidato cha kwanza kwa mkupuo mmoja.
  • Lakini pia serikali ya Rais Dk. Samia, imeendelea kuimarisha upatikanaji wa elimu ya juu kwa kuongeza fedha za mikopo kwa ajili ya wanafunzi ambapo katika mwaka 2021/2022, jumla ya shilingi bilioni 570 zilitumika ikilinganishwa na shilingi bilioni 464 zilizotumika mwaka 2020/2021. Vilevile, idadi ya wanufaika iliongezeka kutoka 149,398 mwaka 2020/2021 hadi wanafunzi 177,605 mwaka 2021/2022.
  • Katika sekta ya Afya serikali imeendelea na ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma za afya nchini, Miundombinu hiyo, inahusisha hospitali za rufaa za kanda, hospitali za rufaa za mikoa, hospitali za halmashauri, vituo vya afya na zahanati.

Kuhusu ukuaji wa uchumi katika kipindi cha Januari hadi Septemba, 2021, uchumi wa Taifa ulikua kwa asilimia 4.9 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 4.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2020.

Mwaka 2022 Benki ya Dunia iliisifu serikali ya Dk. Samia kwa usimamizi mzuri wa uchumi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayopata fedha kutoka kwenye taasisi hiyo ikilinganishwa na nchi nyingine nyingi za Afrika.

Benki ya Dunia ilisema kuwa Tanzania ni nchi ya mfano katika usimamizi wa uchumi ambapo licha ya majanga ikiwemo changamoto za UVIKO 19 na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine, tathimini inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania uko imara na nchi inakopesheka.

Katika robo ya kwanza ya mwaka 2022/2023 uchumi ulikua kwa asilimia 5.4 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 5.0 katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha uliotangulia 2021/2022 na kwamba kutokana na mipango kabambe iliyowekwa na Serikali uchumi utakua zaidi hadi kufikia wastani wa asiliia 6.3. Kuongezeka kwa kasi ya ukuaji kumetokana na jitihada mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ikiwemo utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO - 19 na miradi mbalimbali ya maendeleo.

Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kufanya maboresho makubwa katika Sekta ya Kilimo ambapo pia. Serikali ya Awamu ya Sita iliipatia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania mtaji wa shilingi bilioni 208 ikiwa ni nyongeza kwenye mtaji wa awali wa shilingi bilioni 60 uliowekwa na Serikali wakati wa uanzishwaji wa benki mwaka 2012.

Serikali imeendelea kusimamia kikamilifu sekta ya madini na kuhakikisha inakuwa na mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa ambapo Mchango wa sekta ya madini katika kipindi cha Januari hadi Septemba umeongezeka kutoka asilimia 6.5 mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 7.3 mwaka 2021.

Na kuiwezesha Serikali kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 406.6 za maduhuli sawa na asilimia 62.6 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 650 kwa mwaka. Mafanikio hayo ni kielelezo tosha cha kuendelea kuimarika kwa sekta hii kufuatia usimamizi thabiti unaowekwa na Serikali.

Kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji Serikali ya DK. Samia ina dhamira ya dhati kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji mijini na vijijini unafika zaidi ya wastani wa asilimia 95 na 85 mtawalia ifikapo mwaka 2025.
 
Back
Top Bottom