Maendeleo Makubwa ya CHATO na tafsiri ya Makongoro Nyerere na Madaraka Nyerere kupata kura 5 na 2 respectively za maoni CCM 2020!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,651
5,126
Watanzania wenzangu heri ya Mwaka Mpya 2021.

Nimewiwa kutoa mawazo yangu kufuatia kelele nyingi za " kijinga" zinazopigwa kuhusu maendeleo makubwa na ya haraka zinazopigwa Wilayani CHATO katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano.

Fact kubwa ambayo hatuwezi kuipinga ni kuwa Wilaya hiyo kwa sasa imetoa kiongozi mkubwa wa Taifa letu.

Fact nyingine ni kuwa kwa sasa na baadaye CHATO iko kwenye "spot light" na hivyo kwa vyovyote vile lazima ipewe na itapewa "attention" iwe " positive" or " negative".

Suala la maendeleo hayo kupigwa kwa msukumo gani au budget zipi si msingi wa mjadala wangu!

Anayetaka kujua msukumo na budgets za maendeleo ya CHATO anaweza kuanzisha mjadala wake na siyo kuchanganya kwenye mjadala wangu.

Mimi mtazamo wangu ni kuwa ni uoni hafifu kuwa anakotokea Kiongozi Mkubwa wa Nchi basi pawe sehemu duni kimaendeleo.

Tutambue kuwa Kiongozi mkubwa wa Nchi tayari anakuwa " icon" na anatakiwa ku- interact na watu mbalimbali kitaifa na kimataifa!

Hivyobasi sehemu hiyo kama inawezekana iwe inafikika, inakalika na iko friendly.Hapo nazungumzia miundombinu ya aina zote!

Wapiga kelele kama kina Tundu Lissu wanatumia Butiama ya Mwl.Julius Nyerere kama "benchmark" wanapojadili suala maendeleo ya CHATO na vitu vingine vya " kijinga" kama historia ya Mobutu Sese Seko Kuku wa Zabanga !

Kwa hadhi na IQ aliyokuwa nayo Mwl.Julius Kambarage Nyerere mimi binafsi nampongeza kwa mengi ila siwezi kumpongeza kwa vitu viwili ,mosi, jinsi alivyowa " groom" watoto wake na pili maendeleo ya Butiama!

Kuhusu watoto wa Mwalimu, ukiwaangalia vizuri Makongoro na Madaraka na wengine unaona kabisa hawakuandaliwa kwa " kazi kubwa" au tuseme " very challenging jobs"!

Pia kuhusu Butiama, hii ni sehemu masikini ya kutupwa! Kwa muda mrefu imekuwa haina hudumu za msingi na zenye hadhi kama za afya,elimu,mawasiliano, miundombinu n.k!

Leo tunapopiga kelele ndo Barabara ya lami tena ya kiwango duni ndo inajengwa kupitia Butiama kwa Mwl.Julius Kambarage Nyerere na Nyamuswa kwa Joseph Sinde Waryoba!

Leo tunapopiga kelele za CHATO ndo hapa juzi kati Serikali imesaini mradi wa maji wa Bilioni 70 kutoka Mugango, Kiabakari kwenda Butiama kwa Mwl. Nyerere na labda baadaye unaweza kufika Nyamuswa kwa Jaji Joseph Sinde Waryoba!

Huwa ninaposikia mtu " Mkubwa" au " Maarufu" katika Nchi yetu akifa anakuwa ameacha wosia kuwa akifa azikwe Kinondoni Makaburini basi najua huko alikotoka basi hakujipanga au hakuwa na mahusiano mazuri na wenzake huko nyumbani.

Kwa mila na tamaduni za makabila mengi kuzikwa nyumbani au shambani kwako ni heshima kubwa!

Babu yangu mimi aliwahi kuniambia kwa utamaduni na mila za kabila langu nikifa na nikazikwa makaburini ( makaburi ya wengi ) basi sina tofauti na mtu aliyekufa na akaliwa tu na fisi!

Nilibishana naye sana lakini sasa nafanyia kazi changamoto hiyo ( planning my life after death).

Tukirudi katika hoja ya msingi ni kuwa Butiama kilikuwa ni kijiji duni wakati wa Mwl.Nyerere na bado ni sehemu duni sana kulinganisha na hadhi ya Mwl.Nyerere.

Mtu mwenye "negative mind" atajaribu kuni - challenge kuwa hakuna umuhimu wa kwao Kiongozi mkubwa wa Nchi kuwa na maendeleo wakati sehemu zingine ni duni au ni dalili ya kujipendelea na ubinafsi!

Inaweza kuwa kweli lakini binadamu wote ni wabinafsi!
Jaribu kujiuliza kama atajitokeza mtu akupe machaguo mawili kwamba ufe wewe au mwenzako, utajibu nini!?

Nenda harusini halafu muda wa kula MC anaamusha waalikwa kila mtu anawahi kupakuwa " best food for himself or herself" ! Huo wote ni UBINAFSI.

Cha msingi hapa ni sisi kuona kitu ninachoweza kukiita " constructive selfishness " . Namaanisha SGR, Nyerere Power,Hospitali kila Wilaya, Barabara zinajengwa na CHATO ikijengwa kuna ubaya gani?! After all CHATO ni Tanzania pia.

Inawezekana kura 5 na kura 2 za maoni CCM walizopata Makongoro Nyerere na Madaraka Nyerere respectively ni hasira za Wana Butiama kuona hawana impact na ni irrelevants kwa maendeleo yao pamoja na majina yao mkubwa na backgrounds zao!

Mimi siwasikilizi Tundu Lissu na wapiga kelele ( mediocres) wengine wenye chuki na maendeleo ya CHATO.

Nakwenda CHATO soon kuangalia na kuchukua fursa.
Fursa za haraka nazoziona pale ni hizi!
Wakati nyie mnachukia CRDB kuweka tawi kubwa pale CHATO ambako hakuna wateja wengi, mimi naona benki kubwa iliyoko pale CHATO yenye wakopaji wachache!

Wakati nyie mnachukia uwanja wa Ndege wa kimataifa CHATO alikotuwa Waziri wa Nje wa China direct from Beijing na kukagua samaki Mwaloni mimi naona fursa ya kuanzisha kiwanda cha Samaki pale CHATO na zitabebwa na ndege za mizigo direct from CHATO to the markets! na fursa nyingine KIBAO!
 
Narudia tena wewe ni msukuma, mbona lupaso hakuna mataa ya kuongozea magari,hapa kongowe kuna pori kubwa la hifadhi mbona hajaongeza hao tausi, tunataka vipaumbele vya msingi kuna maana gani kujenga uwanja wa utalii wakati hapa Mwanza uwanja wa kirumba wanacheza fisi!
Acha ukabila, mimi wala siyo musukuma! Jina langu lisikuchanganye! Kwa upeo wako duni nadhani ningeitwa Zeng Ti ungesema mimi ni Mchina!
Jikite kwenye Hoja!
 
Hata Mobutu alipojenga uwanja wa ndege huko kijijini kwake alikuwa na watetezi kama ww, leo hii watetezi wote wa uhuni ule kama wako hai wanaona aibu ya dhahiri. Hebu tupe mrejesho wa ule uwanja wa ndege wa katavi Pinda akiwa PM kuwa utainua utalii wa kule?
 
Dunia enzi za Nyerere na sasa na aina ya fikra na maendeleo ni tofauti sana. Leo Kutoendeleza maeneo yakiwemo ya chimbuko lako ni ujinga na utumwa. No way!
 
Bado mmeshindwa kujibu hoja za msingi!Hizi ni porojo tu na hakuna majibu!
Kwamba leo imekuwa ni sifa kuoendelea maeneo unakotoka kisa wewe ni Rais?Kweli dunia inakwenda kasi sana!
Je,ni wilaya gani ina miradi mingi kwa pamoja kama Chato?Taja miradi ya wilaya moja tu uipendayo!
 
Back
Top Bottom