Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 397
- 993
Balozi Said Shaibu Mussa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akijibu swali kuhusu sintofahamu ya sanamu la Mwl. Nyerere amesema;
Kwenye sintofahamu hiyo kuna waokubali kuwa sanamu lile linafafa na Nyeyrere na wengine wanaokataa.
Akisema kuwa Serikali imefuata maelezo ya kitaalamu yaliyotolewa na kamati maalum ya wataalamu ambayo ilishirikia kuanzia kwenye mjadala mpaka kupatikana kwa sanamu hiyo na, sanamu hiyo imefadhiliwa na SADC, lengo likiwa kutambua mchango wa Nyerere katika Ukombozi wa Bara la Afrika hususan Kusini mwa Afrika.
Kamati hiyo ilihusisha watu mbalimbali ikiwemo; familia ya Nyerere akiwemo Madaraka Nyerere, wizara ya mambo ya nje, wizara ya utamaduni sanaa na michezo, Wataalamu kutoka UDSM, pamoja na watu wengine.
Kuanzia hatua ya awali mpaka sananu linakamilika Kamati ililidhika.
Vigezo vilivyotumika kupatikana sanamu ile ni:
1. Kumlenga Nyerere wa miaka 60 na miaka 80, wakati Nyerere akiwa 'active' katika mapambano ya kusaidia kupatikana kwa uhuru na maendeleo katika nchi za Kusini mwa Afrika.
2. Kaiuli ya mtoto wa Nyerere, Madaraka Nyerere mara kadhaa na siku ya uzinduzi ameongea kwa kusisitiza kwamba yule ni baba yake, kama kuna mtu anabisha amuulize yeye.
3. Taratibu za kitaalamu zinasema unapotengeneza sanamu unatakiwa uipatie angalau kufikia 75%, lakini sanamu la Nyerere Addis Ababa kwa matokeo yake ni 92%, na Waziri wa Utamaduni na Michezo alitoa ufafanuzi wa kina juu ya hili.
Hivyo mapokeo ya wizara ya Utamaduni ndio mapokeo ya Serikali, ile ni sanamu ya Nyerere