Nehemia Kilave
JF-Expert Member
- Jan 9, 2022
- 449
- 1,009
Nchi wamejaa wanachi na viongozi lia lia wanasahau hakuna Maendeleo yanayo weza kuja Jasho , ukiwabana kidogo ili mapato mengi yaingie serikalini huwezi kueleweka , Hayati Benjamin mkapa aliwahi kusema..
"Napenda kuwakumbusha kuwa njia ya maendeleo imejaa jasho na vumbi. Tuzingatie utamaduni wa kupenda kufanya kazi kwa bidii, maarifa, ubunifu na kujituma. Lawama ni tamu ikitoka mdomoni, lakini peke yake haitapeleka mkono kinywani. Na katika kila mfanyakazi akumbuke kuwa la muhimu si muda anaotumia kufanya kazi, bali kiasi cha kazi anayoweza kufanya katika muda aliopewa."
Nchi kutawala ni rahisi sana pia , yaani wanachi wanathamini mambo mengi ya kijinga na yasiyo ya muhimu , mfano unaweza zuia au toa huduma duni kwenye Maji na Umeme wakatulia tu ila ukapandisha Bando la internet au vifurushi vya sms hapo kila mtu atafumbua mdomo .
Hayati Mwalimu Nyerere aliachia madaraka ili watu na viongozi lia lia wafanye wanayotaka kufanya kufanya
Hayati Magufuli alipata ugumu na bado haeleweki mpaka sasa hivi sababu alitaka watu wapitie njia Ngumu wapate maendeleo .
Kwa Hali ilivyo hata wakiingia CHADEMA madarakani watu hawatoacha kulia
Watu tubadilike fikra , Kiuhalisia hata uende Nchi yoyote huwezi kutana na Tajiri mvivu .