Maelezo muhimu kuhusu majini!

2. Aina ya pili ni majini yanayonuizwa kupitia vinasaba vya mwanadamu, yaani inachukuliwa mimba ya miezi minane tumboni kwa mamamjamzito (Hapa pia kuna siri nzito ya mimba zinazotoka
Mfano wa aina hii ni Hittler,Iddi Amin,Bokasa,Mao hawa ni majini wa kibinadamu
Mi nilikuwa naona una upeo kiasi kumbe waquote pumba mpo wengi siku hadi siku
 
Hacha mafundisho potovu ,majini hayajaumbwa na Mungu kwa lengo la kumuabudu Mungu Bali Mungu aliumba malaika na wanadamu wamuabudu na si majini.

Majini ni malaika waliomuasi Mungu wao pamoja na Shetani.Wale malaika wote waliokubali kumuasi Mungu ndio wanaitwa majini na wao wanamuabudu Shetani.

Mafundisho hayo Ni batili.

Namna ya kuyashinda majini na Shetani Ni kuwa na mahusiano na Mungu kwa kumuamini Yesu kuwa Bwana na Mokozi wa maisha yako.Ukimpokea Yesu unakuwa na mamlaka ya kumshinda Shetani na majini zake.
Ndio akili yako imekutuma hivyo na upeo wako umeishia hapo sasa wewe amini unga wa sembe na mwingine akiamini unga wa ngano kila mtu na maisha yake acha kupotosha watu kwa kuamini unavyoamini wewe unavyomuona mwenzio kapotoka ndio na yeye anavyokuona wewe umepotoka kiasi gani.
Si ajabu kwa kichaa kumuona mwenye akili ni kichaa na yeye ni mzima
 
Mi nilikuwa naona una upeo kiasi kumbe waquote pumba mpo wengi siku hadi siku
We ndo mweupe ungekuwa unayo elimu kuhusu ulimwengu usioonekana,ungejua nani yupo nyuma ya hitter, Iddi Amin, Bokasa
 
Hii ndio elimu niliyonayo kuhusu hawa viumbe:

Kwanza ijulikane kuwa majini ni malaika walioasi wakatupwa duniani kwa hiyo ni kweli waliumbwa na Mungu kwa lengo la kumwabudu lakini walimwasi na kutupwa duniani na hivyo kuwa kinyume chake na serikali yake ndio wakawa majini, hivyo basi Mungu hakuumba majini bali aliumba malaika watakatifu ambao baadae waliasi na kuwa majini.

Na kwa aina zipo aina kuu tatu za hawa malaika walioanguka (fallen angels) au Majini, ambazo ni kama ifuatavyo.

1. Malaika wale waliotupwa kutoka Mbinguni.
Hii ni aina ya majini ambayo walishiriki ile vita ya Mbinguni na kushindwa na hivyo kutupwa pande za mwisho za shimo (sheol) katika ulimwengu wa roho lakini in physical world ni hapa duniani na hapa kuna milango au gates zinazokuwezesha kuelekea huko kwenye makao yao ingawa mara nyingi huzunguka humu duniani kwa ajili ya kutesa watu kusababisha magonjwa,ajali na vitu mbali mbali kwa ruhusa za wanadamu wenzetu wanaowafuga, maana hakuna jini linatoka kuzimu kumwingia mtu isipokuwa limetumwa na mtu kama yeye au lina mkataba na huyo mtu yaani amelikaribisha kwa kujua au kutokujua .

2. Aina ya pili ni majini yanayonuizwa kupitia vinasaba vya mwanadamu, yaani inachukuliwa mimba ya miezi minane tumboni kwa mamamjamzito (Hapa pia kuna siri nzito ya mimba zinazotoka zikiwa na miezi nane )then inasomwa dua maalum ambayo siwezi kuitaja hapa halafu linanuizwa jina la jini anayetaka kutengenezwa kwa kinasaba cha binadamu, mfano maimuna hii ni kabila yenye mamilioni ya majini kwa hiyo ile mimba ikinuiziwa hili jina kwa dua maalum, (ingawa vingine vinavyofanyika sitavisema) jini mmoja kutoka kabila husika iliyotajwa huja na kuvaa kinasaba cha binadamu kwa hiyo mimba ya miezi minane na hawa ndio unasikia wanaitwa jini mtu na huyu anaweza kuishi kama binadamu akachumbia akaoa ,akazaa na kuwa na watoto kwa sababu ya kile kinasaba cha ubinadamu lakini jini yule malaika aliyetupwa kutoka Mbinguni yeye haoi wala hazai maana yeye ni roho tu isiyo na mwili, na mwisho wake aina hii ya majini hupotea tu duniani huwa hawafi na anakuwa tofauti na binadamu wa kawaida kwa uwezo wa kufanya vitu vya ajabu au kimiujiza

3. Lakini aina ya mwisho hii huitwa Tego hii ni aina ya majini ambayo hutengenezwa kwa kutumia viungo vya mwili wa binadamu mfano ubongo maini ,damu iliyo ganda nk vitu hivi huchanganywa kitaalamu na kunuizwa kwa dua maalum akatokea jini aina ya Tego ndio hizi tunaita roho zinazofatilia hatima ya maisha ya binadamu baada ya tendo la kishirikina kufanyika, hawa ndio huusika na vifo vya design au aina moja kwa ukoo au familia umasikini wa kurithi ,magonjwa ya kurithi laana za ukoo hawa ndio hufuatilia utimizwaji wa vitu hivyo na wao hutumwa na kutengenezwa na kufugwa na watu kama wewe na ni wanadamu wenzetu ila wana elimu ya falaki na hutumia maarifa hayo kuharibu maisha ya watu.

Ingawa kuna imani moja ya dini inahusishwa sana na hawa viumbe siitaji mnaijua, ukweli ni kwamba wao wameingia agano nao kwa kukubali wapo kuwa wapo wema ambao bado hawajaasi na hao ndio hushirikiana nao, lakini kama yupo mmoja humu anijibu wanashirikiana nayo kufanya nini na kwanini huwafuga kwa matumizi gani hasa?

Ndio utakuja kushangaa kwanini wakristo wengi ndio hupagawa sana na hivi viumbe kuliko wanaokaa nayo,wanaoishi nayo na kuyafuga, uzuri nimesoma shule za imani hiyo na katikati ya shule ilikuwepo nyumba yao ya ibada na madarasa ndio yamezunguka, mabinti wengi wa imani tofauti ndio walikuwa wakianguka kila kukicha hata dada yangu ilimpata hadi kuhamishwa kabisa maana tulikuwa tunasoma wote, mpaka nilivyokuja kujua kuwa imani hii ya Kikristo (Kafiruna) ni kinyume cha imani hiyo na wao huwa wahanga zaidi wa mashambulizi ya adui zao sio kwa kuwa ni wanyonge la bali hawana maarifa ya kutosha ya walichokibeba katika ulimwengu wa roho, laiti wangepata hata robo ya nilichonacho, wangeipindua duniani kufumba na kufumbua.

Na kwa mujibu wa elimu ya falaki chuo cha maarifa, pepo hatoi pepo ndio maana nawasikitikia wanaoenda kwa waganga wa kienyeji au watu wanaofuga majini kutafuta msaada, maana msaada wanaoweza kukupa ni kukuwekea jini mwingine mwenye uwezo kuliko kuliko yule uliye naye ili amtoe akae yeye kwa hiyo unajikuta unasolve tatizo moja unaamsha lingine, au kukupa masharti magumu ya kumtimizia huyo jini ili asisumbue lakini ukweli ni kwamba hawana nguvu za kumwamuru kwa lazima atoke badala yake hufanya kitu kinaitwa makubaliano au maridhiano ili likae kwa kutulia na hivyo hakuna msaada utapata kwao zaidi ya kumaliza pesa zako

Na kuhusu jina la Yesu kama yupo mchawi humu au mtu mwenye elimu kubwa ya falaki anaelewa au mfuga majini yoyote ki ukweli hakuna watu wenye uelewe mzuri kuhusu uwezo na nguvu ya jina hili kama hao, hata wakristo wengi kama sio wote hawajui mamlaka halisi ya jina hili maana wao huishia kutamka tu na hawaelewi nini kinaendelea katika spiritual realm, lakini ndugu siegemei upande wowote ila najaribu kueleza kile nilichokipata kupitia elimu hii, ki ufupi ni hatari kubwa sana ambayo siwezi kueleza hapa ila hao wahusika niliowataja hapo wanaelewa vizuri sana hata wakikataa ila mi najua wanaelewa maana ni kitu ninachokifahamu sio kwa kubahatisha. Na ndio maana utashangaa kwanini jina Yesu huitwa issa katika Quran tukufu badala ya Yeshua maana hii ndio tafsiri ya kiarabu ya jina Yesu(hapa pia kuna siri yake) kuna Siri kubwa sana ya jina hili ingawa wenye nalo hawazifahamu, wanaozijua ni watu wa elimu ya giza na wao hutumia nafasi hii ku crash kila jambo kuhusu jina hili ,mpaka wanao litumia sio kwa nia mbaya au chuki ila ni kujilinda na hatari iliyomo maana nashindwa kueleza ni hatari namna gani lakini najua wazee wa shughuli wananielewa vizuri ila kwa hawa wanaolitumia nikutie moyo "Umeshika chenye nguvu ila bila maarifa na imani sawasawa ya ulicho nacho".

Any question please?.

Source: Elimu yangu.
Noma sana!
 
Nyuma ya KILA dikteta ipo nguvu ya shetani nyuma yake, kwa makubaliano ya damu na madaraka.
 
Ukitaka kuyaona majini, mapepo mengi yanaonyeshwa kwenye katuni za watoto, katuni nyingi za watoto ni picha halisi za majini yanayooneka katika ulimwengu usioonekana. Mfano katuni ya Monster University. Watengenezaji wa katuni wanajua wanachokipandikiza kwa watoto, maana watoto ndio walengwa wakuu kama Jamii ijayo. Hivyo ni lazima wapande wa watakacho.

Screenshot_20220521_111613.jpg
 
2. Aina ya pili ni majini yanayonuizwa kupitia vinasaba vya mwanadamu, yaani inachukuliwa mimba ya miezi minane tumboni kwa mamamjamzito (Hapa pia kuna siri nzito ya mimba zinazotoka
Mfano wa aina hii ni Hittler,Iddi Amin,Bokasa,Mao hawa ni majini wa kibinadamu
Hahaha mi sijui
 
Hahaha mi sijui
Ukiingia kwenye ulimwengu wa giza utaona nani waliokuwa nyuma yao, Hittler alikuwa anabadilika sura hata zumarid anabadilika sura pindi yule aliye nyuma yake akimvaa na kutamka maneno ya kufuru.
Hittler akisisitiza jambo baada ya ile roho au yule mtu wa nyuma yake kumvaa mwilini na kutamka ule ujasiri.
 
Elimu ya falaki inabeba nini na nini
Duu , ni elimu pana sana na inavitu vingi lakini kwa uchache ni elimu ya giza kuhusu majini na utendaji wao katika ulimwengu wa roho, lakini pia ndani yake kuna elimu ya nyota, ila sio hizo za angani, maana kuna aina 12 tu za binadamu duniani na hii ni kwa sababu ya nyota zao, lakini pia elimu ya maumbo na mambo mengine kama haya, kugeuka roho nk, inshort ni elimu pana sana na ni wachache walio hata na masters yake mfano mzuri ni huyo sheikh uliyenitajia inbox maana yeye ndio alikuwa mkufunzi mkuu kwenye hio idara, na yeyote aliyepita pale chuoni lazima atakuwa anamjua hata kwa kusikia tu, nashangaa hata na wewe umemjuaje au umepita pale nini , wengi wao ni beginners au wanayo ya kawaida sana wamejifunza ila sio darasani labda kwa kusikia kama humu jf, au kwa watu wao wa karibu.
 
Huyu siku hizi ni mtumishi wa Mungu alitaka kuuliwa na majini salama yake akakimbilia kanisani akaacha uislamu na kuokoka.Amejaa youtube anafundisha kuhusu Yesu Kristo na sio shetani,ameeleza historia yake episode kuanzia alipozaliwa pangani Tanga, kuwa mchawi , mganga hadi alivyomuua Mwalimu wake kwa uchawi shehe Mwaimu na hadi alivyotekwa na alshababu na akatoroka somalia, alipata bilioni moja kwenye Kazi ya uganga akaenda zitumbua dubai na Miami beach USA aliporudi akataka kuacha uganga majini yakapanga kumuua akaamua kukoka. Pia ndie aliyeshiriki tambiko la mwaka 1990 mkoani lindi anazijua siri zote za nchi kuhusu ulimwengu wa giza, yakiwemo mambo ya Mwenge nk. Mtafute YouTube jina Shehe Omari Mnyeshani utapata episode zake mamia kwa mamia akizungumza kuhusu mambo mbalimbali kuhusu dini.
Unamjua Katekela chief wa wageregere Huyu nae alifundishwa falaki na huyu, sasa hivi wote wamemgeuka shetani wanamuhibiri Kristo.
 
Nimeacha kuendelea kusoma maelezo yako nilipofika tu hapo nilipo highlight na wino mwekundu kwa maana mwanzo wa maelezo ya mtu unatosha kabisa kujibu hoja yake hilo ni kosa na kama unaamini hivyo elimu yako ni changa sana na unachokisema.
Ndio maana pia umeitoa katika source nyingine ambayo pia huna uhakika nayo vile vile nikushauri urudi darasana kusoma unachokiandika ili ukijakuleta hoja basi iwe umejitosheleza mkuu sio utumbo uliojitosheleza.

Huyu Mungu unaemuamini kwa maelezo yako ni dhaifu kiasi gani ambaye anaweza kuumba viumbe ambao anawasifu kuwa ni watiifu na wanachoambiwa hawamuasi leo wewe unazua kusema kuna malaika walimuasi mbunguni? kabla ya kuzungumzia ya mbinguni wewe unaweza kujizungumzia mwenyewe kweli? au ndio bendera fuata upepo?

Rejea kwa jina la yesu...... Yesu mwenyewe humjui na Yesu sio jina lake jina lake ni Masiah mwana wa Maryam.
Hii Yesu mnamuita nyie na Lugha yenu mliyoona bora kuliona ni lenye nguvu. Hilo ni jina tungo tu la kiswahili pia Yesu ni jina limetokana na Jesus kwa wazungu mnaowafuata na asili yake sio mzungu na wala hakuwa mzungu nae kabila lake halijulikani achilia mbali anajulikana kuzaliwa na Maryam mwanamke anaesifika kwa imani nyingi tu za dini sasa kabla hujalopoka kitu unatakiwa ukifahamu kwanza yesu hata wewe leo unaweza kuzaa mtoto ukaita yesu na watu wasikushangae lakini tafuta mtu anaeitwa Masiah Bin Maryam (masihi son of marry) sasa usije ukawa unatukuza jina la kutunga na bila kujua jina husika.
Hapo kwanza nakutoa tongo tongo.

Rakims
Hakuna haja ya makasiriko ndugu yangu, tunachofanya hapa ni kutoa katika elimu zetu tulizonazo kuwapa wale wasiojua mambo haya, sasa shida inakuja pale wenye elimu moja kupingana kwenye maeneo fulani huku mmoja akinadi elimu ya mwenzake ni changa tena sana kuhusu hayo maswala, anyway wanasema za kuambiwa changanya na zako , nafikiri mahakimu wazuri ni wasomaji na wauliza maswali ili kupima ufahamu wa kila mmoja.

Labda nikuambie kitu usichojua Messiah, Masiha, masihi ni neno lenye asili ya kiebrania maana yake ni mpakwa mafuta au unaweza kusema (anointed one) tafsiri yake ya kigiriki ndio Kristo au Old Latin Kristus na wapakwa mafuta katika maandiko (maana tunamzungumzia Yesu) walikuwa ni wafalme, Manabii na Makuhani kwa hiyo unaposema Kristo unakuwa too general ni yupi unamaanisha na ndio maana ili ku specify, mfano lazima useme Yesu Kristo, Kwa hiyo Yesu ndio jina lake specific na Masihi au Kristo au Kristu ni Sifa yake maana Kristo waliku wengi na ni wengi hata sasa maana wote waliopakwa mafuta ya Roho wake wanaitwa masihi Wake.
Na kuhusu kwanini iwe jesus wengine waite Yesu wengine Yeshua hayo ni matamshi tu kulingana na lugha lakini kinachomaanishwa ni kitu kile kileo. Mfano kwani Tanzania hakuna watu wanaitwa Omar, haya niambie katika kiarabu kuna irabu "O" au neno Sheikh katika kiarabu kuna "e" Kwanini watamke kitu ambacho hakipo ni kwa sababu ya lugha tuanayoitumia na nature ya matamshi yake lakini kinachomaanishwa ni kilekile kama jina la asili la kiarabu.

Lakini kuhusu malaika, haimanishi malaika kumuasi Mungu ni kwa sababu ni mdhaifu, kwani wanadamu wanapoasi kwa kufanya dhambi inamaasha aliyewaumba ni mdhaifu?. Iko hivyo kwa sababu Mungu aliwaumba wakiwa na free will of choice kama ulivyo wewe na mimi na ndio wakaweza kuchagua njia yao ya giza, lakini haimanishi hakuweza kuwaumba kama Robots wafuate tu maelekezo yake, Maana asili ya Mungu ni mwenye upendo hufurahia zaidi na huridhika na huduma au ibada ya hiari kuliko ya lazima, na hata kama angetaka iwe hivyo ingewezekana bado,kama mwanadamu tu anaweza kumtengeneza mwanadamu mwenzie(msukule au limbwata) na kumtumikisha anavyotaka unafikiri kwa Mungu aliyeumba vyote hilo ni swala dogo kiasi gani lakini ni kinyume cha asili yake.

Source: Elimu changa.

#Zakuambiwachanganyanazako.
 
Huyu siku hizi ni mtumishi wa Mungu alitaka kuuliwa na majini salama yake akakimbilia kanisani akaacha uislamu na kuokoka.Amejaa youtube anafundisha kuhusu Yesu Kristo na sio shetani,ameeleza historia yake episode kuanzia alipozaliwa pangani Tanga, kuwa mchawi , mganga hadi alivyomuua Mwalimu wake kwa uchawi shehe Mwaimu na hadi alivyotekwa na alshababu na akatoroka somalia, alipata bilioni moja kwenye Kazi ya uganga akaenda zitumbua dubai na Miami beach USA aliporudi akataka kuacha uganga majini yakapanga kumuua akaamua kukoka. Pia ndie aliyeshiriki tambiko la mwaka 1990 mkoani lindi anazijua siri zote za nchi kuhusu ulimwengu wa giza, yakiwemo mambo ya Mwenge nk. Mtafute YouTube jina Shehe Omari Mnyeshani utapata episode zake mamia kwa mamia akizungumza kuhusu mambo mbalimbali kuhusu dini.
Unamjua Katekela chief wa wageregere Huyu nae alifundishwa falaki na huyu, sasa hivi wote wamemgeuka shetani wanamuhibiri Kristo.
Duu basi Mwisho umekaribia sana hadi Magwiji wa falaki wanakimbilia chenye nguvu, sisi wanafunzi ni kina nani sasa hata tuache . Kama ni kweli nimefurahi sana, maana jamaa kwa elimu ya dini aliyokuwa nayo sikutegemea kama angekuja kuacha Imani yake.
 
Zaidi ya miaka 25 alishatoka huko.Walishafika level ya chief satanism wakaamua kutoka lakini sio rahisi still wanawindwa.
Wao waliamini shetani ana nguvu kuliko Mungu. Katika harakati zao za giza shetani alishindw waokoa dhidi ya Mapigo ya Mungu wakamua kumuacha shetani na kumgeukia Mungu. Leo wanatoa siri za giza.
 
Ndio akili yako imekutuma hivyo na upeo wako umeishia hapo sasa wewe amini unga wa sembe na mwingine akiamini unga wa ngano kila mtu na maisha yake acha kupotosha watu kwa kuamini unavyoamini wewe unavyomuona mwenzio kapotoka ndio na yeye anavyokuona wewe umepotoka kiasi gani.
Si ajabu kwa kichaa kumuona mwenye akili ni kichaa na yeye ni mzima
Huwaga tunayakemea tu. Kwa jina la Yesu, toka na yana tii. Tunayaambia, kaa chini, simama na ondoka kwa Jina la Yesu na yanatii.
 
Hakuna haja ya makasiriko ndugu yangu, tunachofanya hapa ni kutoa katika elimu zetu tulizonazo kuwapa wale wasiojua mambo haya, sasa shida inakuja pale wenye elimu moja kupingana kwenye maeneo fulani huku mmoja akinadi elimu ya mwenzake ni changa tena sana kuhusu hayo maswala, anyway wanasema za kuambiwa changanya na zako , nafikiri mahakimu wazuri ni wasomaji na wauliza maswali ili kupima ufahamu wa kila mmoja.

Labda nikuambie kitu usichojua Messiah, Masiha, masihi ni neno lenye asili ya kiebrania maana yake ni mpakwa mafuta au unaweza kusema (anointed one) tafsiri yake ya kigiriki ndio Kristo au Old Latin Kristus na wapakwa mafuta katika maandiko (maana tunamzungumzia Yesu) walikuwa ni wafalme, Manabii na Makuhani kwa hiyo unaposema Kristo unakuwa too general ni yupi unamaanisha na ndio maana ili ku specify, mfano lazima useme Yesu Kristo, Kwa hiyo Yesu ndio jina lake specific na Masihi au Kristo au Kristu ni Sifa yake maana Kristo waliku wengi na ni wengi hata sasa maana wote waliopakwa mafuta ya Roho wake wanaitwa masihi Wake.
Na kuhusu kwanini iwe jesus wengine waite Yesu wengine Yeshua hayo ni matamshi tu kulingana na lugha lakini kinachomaanishwa ni kitu kile kileo. Mfano kwani Tanzania hakuna watu wanaitwa Omar, haya niambie katika kiarabu kuna irabu "O" au neno Sheikh katika kiarabu kuna "e" Kwanini watamke kitu ambacho hakipo ni kwa sababu ya lugha tuanayoitumia na nature ya matamshi yake lakini kinachomaanishwa ni kilekile kama jina la asili la kiarabu.

Lakini kuhusu malaika, haimanishi malaika kumuasi Mungu ni kwa sababu ni mdhaifu, kwani wanadamu wanapoasi kwa kufanya dhambi inamaasha aliyewaumba ni mdhaifu?. Iko hivyo kwa sababu Mungu aliwaumba wakiwa na free will of choice kama ulivyo wewe na mimi na ndio wakaweza kuchagua njia yao ya giza, lakini haimanishi hakuweza kuwaumba kama Robots wafuate tu maelekezo yake, Maana asili ya Mungu ni mwenye upendo hufurahia zaidi na huridhika na huduma au ibada ya hiari kuliko ya lazima, na hata kama angetaka iwe hivyo ingewezekana bado,kama mwanadamu tu anaweza kumtengeneza mwanadamu mwenzie(msukule au limbwata) na kumtumikisha anavyotaka unafikiri kwa Mungu aliyeumba vyote hilo ni swala dogo kiasi gani lakini ni kinyume cha asili yake.

Source: Elimu changa.

#Zakuambiwachanganyanazako.
Umetoa Elimu mujarabu kabisa. Hongera mtumishi. Mbona ipo wazi. "Yaheshua" kwa kiebrania ikimaanisha "Yehova is my salvation" ndio Yesu kwa kiswahili. Yeye ndiye mwana wa mmiliki na ndiye mtu mkubwa na mwenye nguvu kuliko watu wote waliowahi kuishi duniani.

Huyo mganga anawatisha vijana tu humu kwa kueleza hao viumbe dhaifu na vinavyosubiri kuhukumiwa tu.
 
Mzee naona unaingia na kutoka tu. Kuna sehemu unaenda vizuri lakini sehemu nyingine unachanganya haki na batili yaani unakataza dhambi kwa mgongo wa dhambi nyingine.

Umeongelea mambo ya midoli hapa; haya makitu kwenye uislamu ni haramu lakini naona wewe unashauri tu watu wasichome pini badala ya kuwaambia kabisa wasiwe na midoli kwenye nyumba zao maana ni haramu. Maana yake unashauri watu waweke midoli/vinyago ndani ila wasivichome pini tu! Sub-hanallah!

Ukaongelea swala la mbwa na paka; mbwa ni miongoni mwa zile najisi kubwa mbili (yaani mbwa na nguruwe ni levo moja ya najisi) lakini hapa naona unashauri watu wakijiwa na mbwa wasijali wala nini watulie tena wasome na Quran kabisa (halafu na neno ulilotumia sio zuri kwasababu mamlaka ya ulinzi kwa viumbe ni ya Allah peke yake )

Kuna mengi tu humo nimeona unakwenda tofauti (mfano dua ya wakati wa kujitazama kwa kioo hiyo uliyoweka hapo siyo yenyewe) ila kwa leo ngoja niishie hapo kwanza
 
Lakini pia niwaombe ndugu zangu tumtafute Mungu wa kweli maana yupo na anapatikana, lengo langu si kuwafundisha watu falakhi kama wanavyofanya wengine ila ni kuonesha ubaya wa haya mambo na udhaifu wake na ni kipi kilicho bora cha kushikamana nacho maana pande zote nazijua, najua udhaifu wa upande fulani na nguvu ya upande fulani. Ingawa najua masikio ya wengi hupenda zaidi kusikila mambo ya gizani kuliko ya nuru yenyikujenga na ndio maana kuna baadhi ya vitu nilikuwa sivisemi makusudi hasa baadhi ya dua maana wapo wakujaribu, wakajaribu yakawakuta ya kuwakuta na lengo sio yakukute ila lengo ni upate hamasa ya kuujua ukweli uondokane na elimu za giza zinazopofusha fahamu ambao wenye ujuzi nazo huzitumia ki maslahi zaidi na sio kwa sababu wanakupenda au kukuhurumia sana nasema hivi kwa sababu najua katika ulimwengu wa kiroho wa giza hakuna kitu kinaitwa upendo au huruma huwa kuna amri kali sana zaidi hata ya jeshini na wafuasi wake ni watii sana kwa uoga na wako makini ili kulinda maisha yao. Upendo huu tunaouona duniani ni sehemu tu ndogo ya upendo wa Mungu aliyekuumba yeye ndio anakuhurumia maana ndiye aliyekuumba na anajua thamani yako, maana uchungu wa mwana aujuaye mzazi, na ndio maana ana rehema ya kusamehe, lakini ule upande mwingine hakuna kitu kinaitwa msamaha au rehema, ila kuna adhabu za kuogofya ambazo hazijali ubinadamu wala hazipo kwa lengo la kukufunza bali kukuumiza au kukuua kabisa.

Mungu anawapenda ndio maana nimepewa nafasi hii ili kuwaeleza habari za upendo wake, kupitia maarifa niliyonayo, maana hakuna mfuga majini atakaye kusaidia sababu anakupenda maana najua kule gizani neno "upendo"huu msamiati hautumiki, Zaidi sana kuna ulaghai uongo na kujificha mazingira ombwe na wengi wanaingia bila ufahamu hata wakija kufahamu tayari wameshanaswa na kwa tahadhari tu ukinaswa kule kutoka ni neema usione naficha baadhi ya vitu maana najua ninaweza kukufundisha ukafanya kama kimzaha ukashikwa na hizo roho, kwa hiyo nakuwa nimekuangamiza baada ya kukusaidia ambalo ndio lengo langu kuu.
Nina mengi ya kusema lakini muda hautoshi, ila Itafute kweli itakuweka huru maana wengi hawasemi mambo kama yalivyo sasa sijui ni kwa maslahi au hawana shule yake. Mwisho kabisa Mungu anakupenda sana na anatamani umfahamu yeye na nguvu zake kuliko unavyotamani kujua mambo ya giza, maana haya yapo kama ushuhuda tu ila lengo ni kumjua yeye sana kuliko chochote maana kwake ndio kuna siri zote za maarifa yaliyodhahiri na yalifichika kwa wenye mwili .

Falaki, elimu ya nyota, elimu ya maumbo, kugeuka roho kutembea bila kuonekana ni vitu vidogo sana katika mamlaka za nuruni kwenye ulimwengu wa roho ndio maana usishangae kwa nini mchawi mpaka awange, atumie dawa hirizi, viungo vya mwili wa binadamu,atoe kafara wengine wanaenda mpaka kuzimu ili wapate nguvu za kufanya mambo yao lakini wanaomjua Mungu wa kweli nguvu zao ni katika vinywa vyao, hakuna tunguli hakuna hirizi hakuna mafuta, sijui maji ya upako,kutuma sijui jini nani wao wanatuma neno la kinywa lilitamkwa kwa imani thabiti na matokeo yake ni dhahiri katika spiritual realm.

Siku nikipata muda nafikiri nitaandaa uzi maalum kuhusu nguvu ya kinywa katika mamlaka za rohoni.
Asanteni

Source: Elimu changa

#Zakuambiwachanganyanazako.
 
Majini na jinsi ya kuwakwepa:
Jinn.jpg

Allah/Mwenyezi Mungu
Alisema katika kitabu chake kitukufu:

Chapter (51) sūrat l-dhāriyāt (The Wind that Scatter)

Sahih International: And I did not create the jinn and mankind except to worship Me.

Pickthall: I created the jinn and humankind only that they might worship Me.

Yusuf Ali: I have only created Jinns and men, that they may serve Me.

Shakir: And I have not created the jinn and the men except that they should serve Me.

Muhammad Sarwar: We have created jinn and human beings only that they might worship Me.

Mohsin Khan: And I (Allah) created not the jinns and humans except they should worship Me (Alone).
Arberry: I have not created jinn and mankind except to serve Me.

"Hawakuumbwa wanadamu na majini ila wamuabudu"

Na wanadamu hawawezi kuwaona majini kwa sababu kawawekea membrane(uzio ambao utawafaya wasiweze kuwaona majini kwa macho ya dhahiri, hii ni kutokana na mwenyezi mungu kuwakinga wana wa adam kwa hofu ambayo ingewapelekea kuzimia au kupoteza maisha kwa kutokana na kuwaona so he will not see them, so that he will not be blinded or die for fear because their sight is shaken.

Persistent_Pupillary_Membrane_-_Fireinthexdisco.jpg

.

Nao wanaishi katika dunia hii hii bila kuonekana na hufanya maisha yao bila kuonekana:

kwa walivyoelezewa ni kwamba wapo katika aina tatu lakini wachunguzi wanaopenda kuwajua zaidi wawafuate huko walipo,

1: (Ifrit/Afreet)
aina ya kwanza ni Ifrit

Huyu huwa na uwezo wa kuhamisha kitu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine duniani umbali wowote na huwa na spidi zaidi ya mwanga wa taa ukifumba na kufumbua au kukapua tu macho basi yeye anakuwa kashafikisha kitu hata kama kipo magharibi na kinakwenda mashariki ya dunia na anaweza kumfurahisha master wake kwa kila anachokitaka na kumburudisha vyovyote na kumfanyia yote anayoyataka na ndiye huyu aliwahi kuiba ufalme wa Suleiman kwa kujifanya Suleiman kwa muda nisioufahamu na aliweza kufanya hivyo kwa kubabe pete ya King Solomon na kujibadilisha kuwa kama Suleiman Son Of Daud/David. hadi pale pete ya Suleiman ilipoletwa na samaki kule alipokuwa akisafisha samaki, wengi kati yenu mnaijua hii hadithi.

Aina ya pili ni (Ding/Ghoul)
348478565_o.jpg

Hawa ni majini wabaya kabisa wenye sura mbovu ambao wao huhakikisha wanaharibu maisha ya mwana wa adamu kwa sababu tu yeye alipewa ukhalifa au uongozi wa kumiliki dunia hii, hivyo wao hujihisi kudhulumiwa kwa maana mwanzo mamlaka hayo walipewa wao wakaishia kumwaga damu na kufanya uchafu ambayo ndio wanayofanya mwanadamu wa leo ayafanye ili waweze kuwa sawa na kulaumu hukumu ya mwenyezi mungu nao husumbua watu wanapokuwa wakifanya maisha yao kama kula,kuvaa,kuoga,kukaa,kuelewana n.k

Aina ya tatu hawa ni (Ghilan/Sila)

jinn116.jpg

Hawa hujitokeza katika maumbo ya watu,wanyama,vitu na kadhalika nao ni wengi zaidi walio karibu na watu kiasi kwamba huwaiga hadi sauti sura mavazi na hata ufanyaji mambo yote na hufanya kila anachofanya mwanadamu.

Yote kwa yote mwenyezi mungu Alishasema ya kuwa hivi ni viumbe dhaifu sana kwetu pamoja na nguvu zote vilivyopewa hakuna cha kumfanya mwanadamu vikamshindwa nguvu unless hajijui ananguvu kiasi gani juu yao.
wale waliojitambua uwezo wao basi utakuta anakituma kama kijakazi au kukifukuza na kukiulia mbali lakini ninaposema hivyo kwa kuwaonyesha kama wadudu haimaanishi kwamba ni wadogo maumbo yao akiingia ndani kwako chukua sitting room nzima ndio mfano wa nyoka aliyekunjwa akakaa, ili uweze kuwaona wadogo na wakuheshimu lazima uwe na imani thabiti kwa muumba wako lakini mwehu mwehu mzinzi mzinzi na mjinga mjinga, usithubutu kusema wala kuhisi hawa viumbe ni wadogo maana wana tabia ya kupima Imani,

Hivyo basi hawa hukimbia na kuumia sana pale mwana adamu anaposoma sifa za mwenyezi mungu katika aya za taji Quran (Ayatul Qursy)
na kutokumsogelewa kwa muda wa siku nzima

LAKINI YAFUATAYO YAKUPASA UWE NAYO MAKINI ILI UWEZE KUKWEPA VIUMBE HAWA:

1: Pale unapobadili nguo litaje jina la mola wako mlezi ili viumbe hivi visiweze kukuona ukiwa uchi,

2: unapolala lala kwa ubavu wako wa kulia na usome Al-Muadhatein(Surat Falaq and Naas) Kwa sababu ikiwa hautosoma basi majini kawaida yao humfata mtu aliyelala na kumkalia juu na kuanza kumkaba na kumsumbua na kumgeuzia ndoto zake na kuwa ndoto za kutisha sana

3: Usichome pini kwenye midoli ya nyumbani kwako au kumruhusu mwanao kuchomeka, kwenye midoli ya nymbani kwako kwa maana majini wengine huishi kwenye mamidoli hivyo unapochoma unawaumiza baadae watakuja ukiwa haupo vizuri watakutandika na kukuumiza pia au kumuuguza mwanao mapele ya ajabu ajabu au wewe mwenyewe, kuchomeka pini ni ishara ya kichawi kwa kufunga muhusika ndani na kuanza kumtesa hivyo mwanao akikuweka kwenye meditation state wewe au yoyote akachoma pini utaona cha mtema kuni,

4: Usizungumze kwa sauti ya juu nyakati za usiku kwa sababu huwa kuna majini wanaozunguka nyakati hizo kelele huwaumiza nao hushindwa kujizuia kukunyamazisha kwa kukuumiza kichwa au kukufanyia chochote ili mradi ukae kimya,

5: Usilie ukiwa peke yako kwa sababu hapo majini hukusogelea na kuanza kukunong'oneza mambo mabaya na kukwambia hakuna wa kukusaidia wewe hufai n.k hivyo hupelekea wewe kufanya maamuzi mabaya,

6: Kumbuka kutaja jina la mola wako kila unapotupa au kurusha kitu au kuruka sehemu kwa sababu kuna asilimia nyingi za uwepo wa jini pale utakapotua ambae eidha kalala au kakaa, hivyo kama katumwa au kwa mapenzi yake anaweza kukuzulu na kukuumiza au hata kukumaliza.

7: Usimwage au kukoga maji ya moto bafuni bila kusema najikinga kwa ewe Allah kutokana na mashetani wa kike na kiume ambaye ni Kubuth na Khabaith na vitendo vyao na machafu yao.

8:Na kama utahisi maskio yako yanapiga kelele au yanalia mdudu na ukahisi joto mapuani na unaskia harufu ya kuungua na huoni kinachoungua basi fahamu kuwa mbele yako kuna jini mbele ya macho yako hivyo sema najikinga kwako mwenyezi mungu kutokana na mashetani wa kijini,au "audhu billah minal shaytwan rajiim" Na kama bado yupo toa Azaan (akiondoka utahisi kibaridi au upepo umekupuliza, Hivyo hivyo ukihisi baridi la ghafla

9:Kama unafuga paka au mbwa nyumbani na ukamuona analia kwa hofu au kukujia karibu yako kwa kuogopa na kuanza kuzunguka miguuni kwako basi msaidie kwa kusoma Muadhatein kwa sababu kuna jini mbaya anaetisha anamsogelea na kutaka kumzuru yeye au watu waliopo kwenye nyumba hiyo au eneo hilo, na akianza kucheza au kuondoka basi teyari upo salama, na akikaa hadi usingizi ukampitia basi wewe utakuwa teyari umekubwa na jini,

10: Usijiangalie kwenye kioo ukiwa uchi au nusu uchi au kujiangalia karibu na kioo kwa sababu majini huchukua sura yako na kuanza kuwafuata ndugu jamaa na marafiki zako na kuanza kuwapa ndoto mbaya za picha yako basi baada ya muda utaanza kuhisiwa mchawi. na ukiwa ni mpenzi wa kujiangalia angalia basi unatakiwa kusema "kwa jina la mwenyezi mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu" Bismillah rahman rahiim" Hakuna kitakachokuika sura wala mwili na kama usiku unalala na kioo ndani ya chumba kwa kulalia basi kifunike maana hicho ni msaada au geti la majini katika kukudhuru kizazi.

Usiogope na Mwenyezi mungu atakusaidia kuwafukuza na kujikinga nao na kila mtu kufanya maisha yake kwa uhuru,

Kwa haya na mengineyo:
Tembelea:

Rakims
Unayafuga????😂😂😂😂😂
 
Zaidi ya miaka 25 alishatoka huko.Walishafika level ya chief satanism wakaamua kutoka lakini sio rahisi still wanawindwa.
Wao waliamini shetani ana nguvu kuliko Mungu. Katika harakati zao za giza shetani alishindw waokoa dhidi ya Mapigo ya Mungu wakamua kumuacha shetani na kumgeukia Mungu. Leo wanatoa siri za giza.
Kweli Mungu ni mwema, na atamlinda sana maana amebeba siri nzito sana, na maarifa yao ya gizani, ndio maana wanamuwinda hata mimi ningekuwa ndio shetani lazima ningemuwinda mtu potential kama huyu asije akaniharibia kazi, maana mbinu zote anazijua,huenda hata wanasoma Elimu ya falaki chuo cha maarifa kwa sasa watakuwa na habari zake maana kwa Tanzania sijui kama kuna mtu anaweza kulingana nae kwenye falaki, we jiulize kama wanafunzi aliofundisha ni Magwiji je mwalimu atakuwaje? , Nimeona YouTube kumbe hata huyo sijui pastor nani uliemtaja anasema na yeye alikuwa student wake na jamaa anasema yeye alikuwa gwiji east and central Africa .Lakini utashangaa kuna watu humu watakuambia wanajua falaki, muulize kajifunzia wapi au ndio ile ya kurithi au falaki ya JF ya nyuzi za kina fulani .

No makasiriko ni maoni yangu tu

Source: Elimu changa

#Zakuambiwachanganyanazako.
 
Back
Top Bottom