Kila kitabu ambacho kimewazungumzia vya dini na visivyo vya dini na kwa kuishi nao wenyewe? wewe umeipata wapi?
Hii ndio elimu niliyonayo kuhusu hawa viumbe:
Kwanza ijulikane kuwa majini ni malaika walioasi wakatupwa duniani kwa hiyo ni kweli waliumbwa na Mungu kwa lengo la kumwabudu lakini walimwasi na kutupwa duniani na hivyo kuwa kinyume chake na serikali yake ndio wakawa majini, hivyo basi Mungu hakuumba majini bali aliumba malaika watakatifu ambao baadae waliasi na kuwa majini.
Na kwa aina zipo aina kuu tatu za hawa malaika walioanguka (fallen angels) au Majini, ambazo ni kama ifuatavyo.
1. Malaika wale waliotupwa kutoka Mbinguni.
Hii ni aina ya majini ambayo walishiriki ile vita ya Mbinguni na kushindwa na hivyo kutupwa pande za mwisho za shimo (sheol) katika ulimwengu wa roho lakini in physical world ni hapa duniani na hapa kuna milango au gates zinazokuwezesha kuelekea huko kwenye makao yao ingawa mara nyingi huzunguka humu duniani kwa ajili ya kutesa watu kusababisha magonjwa,ajali na vitu mbali mbali kwa ruhusa za wanadamu wenzetu wanaowafuga, maana hakuna jini linatoka kuzimu kumwingia mtu isipokuwa limetumwa na mtu kama yeye au lina mkataba na huyo mtu yaani amelikaribisha kwa kujua au kutokujua .
2. Aina ya pili ni majini yanayonuizwa kupitia vinasaba vya mwanadamu, yaani inachukuliwa mimba ya miezi minane tumboni kwa mamamjamzito (Hapa pia kuna siri nzito ya mimba zinazotoka zikiwa na miezi nane )then inasomwa dua maalum ambayo siwezi kuitaja hapa halafu linanuizwa jina la jini anayetaka kutengenezwa kwa kinasaba cha binadamu, mfano maimuna hii ni kabila yenye mamilioni ya majini kwa hiyo ile mimba ikinuiziwa hili jina kwa dua maalum, (ingawa vingine vinavyofanyika sitavisema) jini mmoja kutoka kabila husika iliyotajwa huja na kuvaa kinasaba cha binadamu kwa hiyo mimba ya miezi minane na hawa ndio unasikia wanaitwa jini mtu na huyu anaweza kuishi kama binadamu akachumbia akaoa ,akazaa na kuwa na watoto kwa sababu ya kile kinasaba cha ubinadamu lakini jini yule malaika aliyetupwa kutoka Mbinguni yeye haoi wala hazai maana yeye ni roho tu isiyo na mwili, na mwisho wake aina hii ya majini hupotea tu duniani huwa hawafi na anakuwa tofauti na binadamu wa kawaida kwa uwezo wa kufanya vitu vya ajabu au kimiujiza
3. Lakini aina ya mwisho hii huitwa Tego hii ni aina ya majini ambayo hutengenezwa kwa kutumia viungo vya mwili wa binadamu mfano ubongo maini ,damu iliyo ganda nk vitu hivi huchanganywa kitaalamu na kunuizwa kwa dua maalum akatokea jini aina ya Tego ndio hizi tunaita roho zinazofatilia hatima ya maisha ya binadamu baada ya tendo la kishirikina kufanyika, hawa ndio huusika na vifo vya design au aina moja kwa ukoo au familia umasikini wa kurithi ,magonjwa ya kurithi laana za ukoo hawa ndio hufuatilia utimizwaji wa vitu hivyo na wao hutumwa na kutengenezwa na kufugwa na watu kama wewe na ni wanadamu wenzetu ila wana elimu ya falaki na hutumia maarifa hayo kuharibu maisha ya watu.
Ingawa kuna imani moja ya dini inahusishwa sana na hawa viumbe siitaji mnaijua, ukweli ni kwamba wao wameingia agano nao kwa kukubali wapo kuwa wapo wema ambao bado hawajaasi na hao ndio hushirikiana nao, lakini kama yupo mmoja humu anijibu wanashirikiana nayo kufanya nini na kwanini huwafuga kwa matumizi gani hasa?
Ndio utakuja kushangaa kwanini wakristo wengi ndio hupagawa sana na hivi viumbe kuliko wanaokaa nayo,wanaoishi nayo na kuyafuga, uzuri nimesoma shule za imani hiyo na katikati ya shule ilikuwepo nyumba yao ya ibada na madarasa ndio yamezunguka, mabinti wengi wa imani tofauti ndio walikuwa wakianguka kila kukicha hata dada yangu ilimpata hadi kuhamishwa kabisa maana tulikuwa tunasoma wote, mpaka nilivyokuja kujua kuwa imani hii ya Kikristo (Kafiruna) ni kinyume cha imani hiyo na wao huwa wahanga zaidi wa mashambulizi ya adui zao sio kwa kuwa ni wanyonge la bali hawana maarifa ya kutosha ya walichokibeba katika ulimwengu wa roho, laiti wangepata hata robo ya nilichonacho, wangeipindua duniani kufumba na kufumbua.
Na kwa mujibu wa elimu ya falaki chuo cha maarifa, pepo hatoi pepo ndio maana nawasikitikia wanaoenda kwa waganga wa kienyeji au watu wanaofuga majini kutafuta msaada, maana msaada wanaoweza kukupa ni kukuwekea jini mwingine mwenye uwezo kuliko kuliko yule uliye naye ili amtoe akae yeye kwa hiyo unajikuta unasolve tatizo moja unaamsha lingine, au kukupa masharti magumu ya kumtimizia huyo jini ili asisumbue lakini ukweli ni kwamba hawana nguvu za kumwamuru kwa lazima atoke badala yake hufanya kitu kinaitwa makubaliano au maridhiano ili likae kwa kutulia na hivyo hakuna msaada utapata kwao zaidi ya kumaliza pesa zako
Na kuhusu jina la Yesu kama yupo mchawi humu au mtu mwenye elimu kubwa ya falaki anaelewa au mfuga majini yoyote ki ukweli hakuna watu wenye uelewe mzuri kuhusu uwezo na nguvu ya jina hili kama hao, hata wakristo wengi kama sio wote hawajui mamlaka halisi ya jina hili maana wao huishia kutamka tu na hawaelewi nini kinaendelea katika spiritual realm, lakini ndugu siegemei upande wowote ila najaribu kueleza kile nilichokipata kupitia elimu hii, ki ufupi ni hatari kubwa sana ambayo siwezi kueleza hapa ila hao wahusika niliowataja hapo wanaelewa vizuri sana hata wakikataa ila mi najua wanaelewa maana ni kitu ninachokifahamu sio kwa kubahatisha. Na ndio maana utashangaa kwanini jina Yesu huitwa issa katika Quran tukufu badala ya Yeshua maana hii ndio tafsiri ya kiarabu ya jina Yesu(hapa pia kuna siri yake) kuna Siri kubwa sana ya jina hili ingawa wenye nalo hawazifahamu, wanaozijua ni watu wa elimu ya giza na wao hutumia nafasi hii ku crash kila jambo kuhusu jina hili ,mpaka wanao litumia sio kwa nia mbaya au chuki ila ni kujilinda na hatari iliyomo maana nashindwa kueleza ni hatari namna gani lakini najua wazee wa shughuli wananielewa vizuri ila kwa hawa wanaolitumia nikutie moyo "Umeshika chenye nguvu ila bila maarifa na imani sawasawa ya ulicho nacho".
Any question please?.
Source: Elimu yangu.