Yaliyomkuta Ngasa, Ajibu, Domayo na sasa Fei na Mayele na uwepo wa Majini Yanga

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,222
103,827
Tuhuma za Yanga kutupia majini wachezaji wake imenikumbusha nyuma kidogo. Imenikumbusha nyakati kina Ngasa, Ajibu, Domayo, Niyonzima (orodha ni ndefu) wakati wanaondoka Yanga.

Wakiwa kwenye piki wakataka kwenda kwingine kutafuta maisha mazuri zaidi ya waliyopata Yanga. Wote hawa walitamani kuondoka kwa amani kwani waliisaidia Yanga kufikia mafanikio na walitamani kuondoka kwa heshima. Ajabu hali ilikiwa tofauti kwani uongozi haukuwa tayari kuwaacha kwa wema. Hata pale walipolazimisha hatimaye waliondoka kwa chuki na kisununu, wakilaaniwa na kauli za "tutaona kama utatoboa"

Haya yalifanyika nyakati za Ajib kuja Simba, kina Ngasa na Domayo kwenda Azam. Hali hiyo imejirudia kwa Feitoto na Mayele. Uondokaji wa watu hawa ulifichwa sana kwa sababu za husda tu huku viongozi wakiamini vitisho vitasaidia.

Kipindi Niyonzima anakuja Simba, wana Yanga mpaka wakachoma jezi kumlaani. Hiyo ni roho ya kawaida kweli. Si ujini huo. Kumbuka kina Bangala na Djuma walivyoondoka Yanga.

Kwa hali hii hata kama ni kweli hawafugi majini, lakini kumbania mtu maisha ni zaidi ya kumtupia majini. Tazama suala ya Fei mpaka Rais wa nchi anaingilia kati, Hiyo roho ni zaidi ya jini. Nafikiri hata jini lenyewe lilishangaa. Fei sio kichaa mpaka aseme ili abaki Yanga basi Hersi aondoke.

Hizi tabia za kishwahili zinatakiwa kukemewa sio tu na wanasoka bali kina mpenda maendeleo.
 
Mkoba wa majini kwa sasa amekabidhiwa Ally Kamwe, ndio maana hanenepi, yanahitaji makafara sana, ndio maana wameanza utaratibu wa kuchinja ng'ombe kwa visingizio mbalimbali, mara birthday ya yanga, mara hiki na kile
 
We unadhani ashura cheupe anafanya kazi gani pale majini fc zaidi ya kufuga majini na kuwatupia watu
Majini FC wameumbuka. Ushirikina umetawala katika maisha yao. Si unakumbuka hata mechi yao na Dodoma Jiji walivyopata goli baada ya kufanya vitendo vya kishirikina kwenye goli la wapinzani wao?
 
Hii ishu nayo ukiiangalia kwa namna nyingine unaweza kupata maswali mengi.

Binafsi siamini kuwa Mayele ametupiwa majini, siamini kama mashabiki wa Yanga wanamuombea mabaya.

Kwasababu hata kwenye tuzo za mchezaji bora ambaoo Mayele alikuwa kwenye nominee, tuliona Yanga wakisimama naye bega kwa bega kujivunia pride yao.

Mashabiki wa Yanga wamekuwa wakifurahi kuona Mayele anaitwa kwenye timu yake ya Taifa, wanajivunia kuwa ni matunda ya Yanga na pale inapotokea anafunga basi wanakuwa very proud.

Hata wakati wa kupanga plot za makundi Mayele alipenda Pyramids ipangwe group moja na Simba, jambo ambalo watu wa Yanga walifurahia kuona bado Mayele anaipenda Yanga kwasababu ameonesha matamanio ya kutaka kuendelea kuifunga Simba.

Kile kipindi ambacho Mayele hakuruhusiwa kwenda Afrika Kusini kwasababu ya vibali, Mayele alikuja Tanzania na alipokelewa na viongozi wa Yanga tena peacefully.

Why leo hii aje na tuhuma mbaya kama zile kwa viongozi na mashabiki wa Yanga???

Na sehemu inayoniacha na bumbuazi ni pale aliposema viongozi wa Yanga wanamtumia meseji ambazo yeye hazijamfurahisha.

Ukija kusikiliza na ile kauli ya Afisa Habari wa Yanga kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa Mayele inaweza kuongeza utata kabisa.

Afisa Habari wa Yanga alinukuliwa akisema "wazee wamekuja kwa ajili ya birthday yako, hawajawahi kusherehekea hata birthday zao lakini wamekuja leo hapa kwasababu wanakupenda"

"Sasa siku inatokea unaondoka Yanga hawa wazee watakupa laana"

Japo Afisa Habari aliongea katika tone ya utani lakini katika hili sakata lilipofikia kila neno lililowahi kutamkwa huko nyuma lenye elements zinazofanana na shutuma hii lazima lifikiriwe kama ndio sababu.
 
Sasa mchezaji kahama timu unayoshabakia kaenda kwa wapinzani unabaki na jezi yake ya nini ikiwa ulinunua kwa hela yako, cha msingi ni kuichoma tu hakuna namna.

Au mhasibu wa mchongo unasemaje hapo.
 
Tuhuma za Yanga kutupia majini wachezaji wake imenikumbusha nyuma kidogo. Imenikumbusha nyakati kina Ngasa, Ajibu, Domayo, Niyonzima (orodha ni ndefu) wakati wanaondoka Yanga.

Wakiwa kwenye piki wakataka kwenda kwingine kutafuta maisha mazuri zaidi ya waliyopata Yanga. Wote hawa walitamani kuondoka kwa amani kwani waliisaidia Yanga kufikia mafanikio na walitamani kuondoka kwa heshima. Ajabu hali ilikiwa tofauti kwani uongozi haukuwa tayari kuwaacha kwa wema. Hata pale walipolazimisha hatimaye waliondoka kwa chuki na kisununu, wakilaaniwa na kauli za "tutaona kama utatoboa"

Haya yalifanyika nyakati za Ajib kuja Simba, kina Ngasa na Domayo kwenda Azam. Hali hiyo imejirudia kwa Feitoto na Mayele. Uondokaji wa watu hawa ulifichwa sana kwa sababu za husda tu huku viongozi wakiamini vitisho vitasaidia.

Kipindi Niyonzima anakuja Simba, wana Yanga mpaka wakachoma jezi kumlaani. Hiyo ni roho ya kawaida kweli. Si ujini huo. Kumbuka kina Bangala na Djuma walivyoondoka Yanga.

Kwa hali hii hata kama ni kweli hawafugi majini, lakini kumbania mtu maisha ni zaidi ya kumtupia majini. Tazama suala ya Fei mpaka Rais wa nchi anaingilia kati, Hiyo roho ni zaidi ya jini. Nafikiri hata jini lenyewe lilishangaa. Fei sio kichaa mpaka aseme ili abaki Yanga basi Hersi aondoke.

Hizi tabia za kishwahili zinatakiwa kukemewa sio tu na wanasoka bali kina mpenda maendeleo.
Mtu anashindwa kuwika huko aliko anadai YANGA wamemloga!akili za waafrica aisee
 
Dunia ina mambo watu wanaojisifu kuwa wameelimika wanaamini mambo ya kufikirika, mfano mtoa mada, hivi mtoa mada unaamini mambo ambayo huwezi kuthibitisha.
Mimi sio shabiki wa mpira ila natoa pole kwa wanaoamini hizi habari kama mtoa mada.
 
Ni mambo ya kawaida kwa mashabiki na wapenzi wa timu kuwa na hicho umeita kisununu...

Nitakupa mifano ya huko duniani ambapo wachezaji waliocheza kwa mafanikio katika klabu moja, walipotangaza kuondoka walikutana na wakati mgumu...

1. Giuseppe Meazza, Inter to AC Milan

2. Carlos Tevez, Man U to Man City

3. Luis Figo kutoka Barca kwenda Real Madrid

4. Cristiano Ronaldo kutoka Man U kwenda Real Madrid

5. Neymar kutoka Barca kwenda PSG
.

Back
Top Bottom