Hakuna haja ya makasiriko ndugu yangu, tunachofanya hapa ni kutoa katika elimu zetu tulizonazo kuwapa wale wasiojua mambo haya, sasa shida inakuja pale wenye elimu moja kupingana kwenye maeneo fulani huku mmoja akinadi elimu ya mwenzake ni changa tena sana

kuhusu hayo maswala, anyway wanasema za kuambiwa changanya na zako

, nafikiri mahakimu wazuri ni wasomaji na wauliza maswali ili kupima ufahamu wa kila mmoja.
Labda nikuambie kitu usichojua Messiah, Masiha, masihi ni neno lenye asili ya kiebrania maana yake ni mpakwa mafuta au unaweza kusema (anointed one) tafsiri yake ya kigiriki ndio Kristo au Old Latin Kristus na wapakwa mafuta katika maandiko (maana tunamzungumzia Yesu) walikuwa ni wafalme, Manabii na Makuhani kwa hiyo unaposema Kristo unakuwa too general ni yupi unamaanisha na ndio maana ili ku specify, mfano lazima useme Yesu Kristo, Kwa hiyo Yesu ndio jina lake specific na Masihi au Kristo au Kristu ni Sifa yake maana Kristo waliku wengi na ni wengi hata sasa maana wote waliopakwa mafuta ya Roho wake wanaitwa masihi Wake.
Na kuhusu kwanini iwe jesus wengine waite Yesu wengine Yeshua hayo ni matamshi tu kulingana na lugha lakini kinachomaanishwa ni kitu kile kileo. Mfano kwani Tanzania hakuna watu wanaitwa Omar, haya niambie katika kiarabu kuna irabu "O" au neno Sheikh katika kiarabu kuna "e" Kwanini watamke kitu ambacho hakipo ni kwa sababu ya lugha tuanayoitumia na nature ya matamshi yake lakini kinachomaanishwa ni kilekile kama jina la asili la kiarabu.
Lakini kuhusu malaika, haimanishi malaika kumuasi Mungu ni kwa sababu ni mdhaifu, kwani wanadamu wanapoasi kwa kufanya dhambi inamaasha aliyewaumba ni mdhaifu?. Iko hivyo kwa sababu Mungu aliwaumba wakiwa na free will of choice kama ulivyo wewe na mimi na ndio wakaweza kuchagua njia yao ya giza, lakini haimanishi hakuweza kuwaumba kama Robots wafuate tu maelekezo yake, Maana asili ya Mungu ni mwenye upendo hufurahia zaidi na huridhika na huduma au ibada ya hiari kuliko ya lazima, na hata kama angetaka iwe hivyo ingewezekana bado,kama mwanadamu tu anaweza kumtengeneza mwanadamu mwenzie(msukule au limbwata) na kumtumikisha anavyotaka unafikiri kwa Mungu aliyeumba vyote hilo ni swala dogo kiasi gani lakini ni kinyume cha asili yake.
Source: Elimu changa.
#Zakuambiwachanganyanazako.