Ngongo,
Mkuu wangu labda kwa sababu watu wengine kama sisi hatuchangii sakata lenu ndio maana unafikiri unachokiandika kina maana. Madiwani ni wawakilishi na watekelezaji wa sera na ilani za chama kama chama kilivyowaahidi wananchi, na hawawezi kuchukua jukumu la kuingia Mufaka na CCM pasipo kuwasiliana na makao makuu ya chama ktk kupanga jinsi ya kutumia fursa walizopata...
Unachoshindwa kufahamu ni kwamba hata kabla ya muafaka wananchi walipinga hatua zozote za chama tawala kujipa vyeo vya juu ktk uongozi wa Halamashauri ya mji huo na ilifikia hadi wananchi kupoteza roho zao kupinga kile ambacho leo hawa madiwani wamekikubali.
Kwa hiyo hawa madiwani kwanza hawana ridhaa ya wananchi wala makao makuu hawana taarifa yeyote kuhusiana na makubaliano baina yao na madiwani waCCM..kisha wewe unataka kusema hili sio swala kubwa bali ni matatizo binafsi kati ya Lema na Mallah na ukaacha nje sababu hizi.. Na zaidi ya hapo unashindwa kabisa kuelewa kwamba diwani yeyote anaifanya kazi ya chama na sii yake binafsi au iliyopangwa na CCM. Na kikubwa zaidi pengine unashindwa kuelewa madaraka na mamlaka alokuwa nayo Meya ktk utendaji kazi kiasi kwamba wewe unaona hakuna tatizo kwa CDM kukubali nafasi walizopewa na CCM..
Hawa Madiwani walichokifanya hakina tofauti na Muafaka wa Zanzibar ambao Seif Hamad alikubali kuchukua rushwa la vyeo na Nnauye majuzi tu kasema tamaa yake ndio ilimponza. Tofauti iliyopo ni kwamba Seif alipata ridhaa ya Wazanzibar lakini sio ridhaa ya wanaCUF hasa wa bara. Na kwa mtaji huo Seif alikiuka sheria na taratibu za chama kwa kuunda Uzanzibar dhidi ya Ubara ndani ya chama. Bara hawakuridhia muafaka ule na matokeo yake CUF wamekosa viti bara na pengine chama ndio kinakufa bara kwa faida ndogo ya kupewa vyeo ktk wizara na taasisi ambazo hazina mamlaka ya kuleta mageuzi ambayo wananchi wa Zanzibar waliyategemea...
Hawa madiwani kwa jeuri wametoa majibu ambayo wao hawakutakiwa kabisa kuyasema tena wakiita waandishi wa magazeti kujibu maamuzi ya makao makuu. Huu ni utovu wa adabu, kukosa hekima na shukran kwa chama na wananchi waliowapa nafasi hizo..Ni jeuri ambayo tumeizoea kuiona toka CCM ambapo viongozi wabunge, madiwani na hata makatibu kata wanapopewa dhamana hizi hugeuka na kuwa wajeuri wakapenda kuheshimiwa kama Waheshimiwa na hubadilika toka mwendo, mavazi na makazi yao..
Hatutaki viongozi kama hawa! kama wanafikiria mila na desturi ya jeuri wanazowaona viongozi wa CCM wakizifanya kwa wananchi basi wakumbuke kwamba CDM ni chama cha wananchi na nguvu imepelwa wananchi ambao waliingia barabarani kwa maandamano kupinga hicho hicho walichokubali wao pasipo ridhaa ya wananchi, kisha wanatafuta wachawi toka makao makuu hali wachawi ni wao wenyewe..