Madiwani wa CHADEMA Arusha wagawanyika

Unakubaliana na mimi hakuwa na sababu za kujiuzulu wadhifa wowote ?.

Amepewa barua yenye sababu za yeye kujiuzuru. Ana haki yakutokujiuzuru kwa sababu zake; lakini hatua za kichama zitafuata. WEWE SI RAHISI KUKUBALIANA NA WEWE KWA LO LOTE KWA SABABU WEWE HUKUBALIANI NA WENZIO HASA PALE MNAPOTOFAUTIANA KIMTAZAMO
 
Heshima kwako Ngonini.

Mkuu wangu JF imewahi kulaumiwa na CCM kwamba ni mtandao wa CHADEMA.Ukiwalaumu sana waliofikia uamuzi wa kuinasibisha JF na CHADEMA unaweza kujikuta unakosea sana.Najua ninachokiandika si popular hapa JF na pengine waliohitimisha upacha wa JF na CHADEMA wanakuwa sahihi ingawa kuna hoja kibao hawataki kuzijibu.

Napenda kukuhakikishia simwakilishi Mallah hapa JF pia sijali watu wangapi wananiunga mkono au wangapi hawapendi kuona au kusoma mabandiko yangu.JF ni jukwaa huru natumia uhuru wangu kutoa mawazo yangu kama wewe ulivyo huru kutoa mawazo yako.

Mengine nimeshajibu ebu jaribu kupitia majibu ya baadhi ya wanajamvi labda utafunguka na kuelewa ninachokizungumzia.

Mkuu mbona ni wewe tu peke yako ndo uke kinyume na waliowengi. Wewe ni mchawi?Kama unadhani wewe ni watofauti kuliko wengine basi si kwenye haya mambo ya siasa labda ungeenda kwenye physical science kule hakuna cha kubisha kwa hoja, bali ni facts zako.Kwenye siasa mkuu wengi wape huwezi kupingana na wengi hutapata kitu!Inavyoonekana na wewe ni swahiba mzuri wa Mallah ndo maana unapambana kwa ajili yake humu jamvinini. Kwa bahati mbaya sana chadema ni chama chenye watu makini na wanaheshimu haki zaidi kuliko chochote. Hawatakuwa tayari kuharibu sifa hii hata kama Mallah ni Mungu pale kimandoro. Chadema wanamuuliza Mallah je kwanini aliandamana Jan. 5? Kama anajua aliandamana kwa nini basi ajibu swali la pili je yale aliyokuwa anayadai yametekelezwa? Lakini juu ya hayo je madhara yaliyotokana na maandamano yale nani anayalipia? Je Mallah sasa anawasaliti wana Arusha walioshiriki maandamano kwa ushawishi wake na wengine wakafa na kuapata majeraha?Je ni kweli mtu kama mke wa Dr. Slaa ambaye damu ilibubujika anaweza kukubaliana na Mallah kwamba basi yameisha?Kama maswali haya na mengine mengi ambayo sikuyauliza yanaweza kujibiwa na Mallah basi anayo haki ya kuwa na kiburi anachokionyesha.Kwa kifupi watu wengi watafurahia kufukuzwa kwa huyu anayetaka kufaidika kwa mngongo wa wengi walioumia kwa ajili ya mgogoro huo!Mimi binafisi naona chadema wako very reasonable na huyu jamaa na kweli wanampenda sana la sivyo angekuwa ameshalimwa barua ya kufukuzwa zamani tu.
 
wanasema watu wapwani wanapenda mipisho,na kuna mwanajamii mwenzetu hua anapenda sana kuleta michango kwa kupasha flani,na amewai toa wazo kuwe na jukwaa la majungu.sasa sijui anafikiria kwa kutumia tumbo au makalio.

Hanaga jipya zaidi ya kuchangia kwa unafiki na kujikombakomba kwa watu wenye madaraka na nchi hii.

Kweli mbwa hachagui chakula hata Makombo kwake sawa.ila kama ni mtu safi hawezi fanya kama MbWA MTU HUYU.
 
Mimibaba.

Ebu soma habari kwa kufuata mtiririko utaelewa nilikuwa namzungumzia nani ?.

Amepewa barua yenye sababu za yeye kujiuzuru. Ana haki yakutokujiuzuru kwa sababu zake; lakini hatua za kichama zitafuata. WEWE SI RAHISI KUKUBALIANA NA WEWE KWA LO LOTE KWA SABABU WEWE HUKUBALIANI NA WENZIO HASA PALE MNAPOTOFAUTIANA KIMTAZAMO
 
Wakuu,

Kwa kuwa JF ni jukwaa huru....ningeshauri tuwe na subira tu hadi maamuzi yatakayotolewa.Kwa wafuasi wa CCM na wale ambao hawaitakii CHADEMA mema msisubiri kuona mgogoro mkubwa kutokana na hili suala la Arusha.Chadema imeshapita katika political turmoil kali kuliko hizi.Nawapa pole

Na kwa wafuasi wa CHADEMA mlioko huku,ningewashauri kabisa mjenge hoja against anayoandika NGONGO.Hebu tuonyeshe tofauti na CCM kama inatulazimu kujibu mapigo kwa ngongo kwa kuonyesha umahiri wa kujenga hoja.tuache matusi,hayo tuwaachie CCM kwa sababu hiyo ndiyo silaha,mtaji na hazina pekee waliyobaki nayo.chadema tuna hoja.Si kila anayekukosoa ni adui yako bali kuna wenye mapenzi.tujenge tabia ya kutafakari,kutathmini na kupata sababu za kukataa ushauri,maoni au hoja otherwise tuvute subira

Mojawapo wa faida za JF ni kupata mawazo huru.CCM imefika huku kwa sababu ya kuendeleza fikra za kulindana,kuogopana matumizi mabaya ya vyeo na nafasi za uongozi.Ni lazima tujiandae kujenga taifa lenye nidhamu na uwajibikaji uliotukuka kwa kusimamia misingi ya haki,demokrasia na utashi wa nguzo tatu za kiuchumi,kijamii na kisiasa katika maamuzi ya jambo lolote linalohusu watu,viongozi wao nk.
 
1) Tulisikia kuna muafaka kati ya Mbowe na Pinda kuhusu Arusha. Si Mbowe wala Pinda waliokanusha mpaka sasa.

Siyo suala la Mbowe au Pinda kukanusha kwa sababu hakuna muafaka wewe unasema mlisikia sisi wengine hatujasikia

2) Mara tukamsikia Slaa anasema madiwani wamekula rushwa (kutokana na usemi wa Mala kupitia TV.)

Umekuwa mkweli hapa kuwa madiwani wamekula rushwa "kutokana na usemi wa Mala kupitia TV"

3) Tukasikia Marando kapelekwa kuchunguza. Matokeo ya uchunguzi wake ni siri mpaka leo.

Matokeo ya uchunguzi yako Lumumba na amekabidhiwa Mallah ili aendelee kukaidi chama.

4) Slaa akawapa siku tatu wajiuzulu vyeo vyao lakini si udiwani. Inashangaza, mla rushwa umwache nawe ndi u mstari wa mbele kufichua mafisadi?

Slaa alitaja list of shame akiwemo JK hata gamba hajivui. Sasa subiri wafukuzwe warudi CCM waliko na thamani.

5) Malla akataa kujiuzulu live na ansema uchunguzi wa Marando umebaini ukweli (TV) kwa hiyo hajiuzulu mpaka uongozi umsafishe, umsafishe vipi? Kagoma kujiuzulu,

Asafishwe kwa kujinyea mwenyewe halafu source yako ni TV na siajabu TBC. Ni CCM pekee yenye uwezo wa kusafisha wanachama wake.

6) Siku ya pili Slaa akasema watafata katiba.

Katiba itafuatwa na ilifuatwa hadi hapa, sasa washauri kina Mallah kuwa katiba itafuatwa.

7) Mara Slaa akaacha na hoja ya kujiuzulu akawataka waombe radhi. Akasema saa 7:20 ikifika katiba itaamua. Saa hiyo haijafika bado!

Saa imefika lakini sikio la kufa halisikii dawa, yaani ni lazima life.

8) Mala bado uzi uleule,anasema hajiuzulu wala haombi radhi na tunasikia anaongoza vikao vya manispaa huko.

Mallah ni sawa sawa na wewe FF; INZI KUFIKIA KWENYE KIDONDA SI HASARA

9) Slaa hasikiki, mfupa mgumu!

Wewe si ndiye bosi wa Slaa mfukuze kazi. Aliyeutoa huu mfupa ndiye anajua ugumu wake si Dr. Slaa.

10) Mala nampa heko.

Anastahili kupewa Heko na wapuuzi wenziwe, ILA MAJUTO NI MJUKUU

11) Tutasikia Sloaa anajiuzulu kwa kushindwa kuongoza.

Anza kujiuzuru wewe najua ungependa Dr. Slaa siyo ajiuzuru bali asiwepo kwenye uso wa dunia. LAKINI KUMBUKA MNALO MPAKA KIELEWEKE
 
Wakuu,

Na kwa wafuasi wa CHADEMA mlioko huku,ningewashauri kabisa mjenge hoja kutetea anayoandika NGONGO. Hebu tuonyeshe tofauti na CCM kama inatulazimu kujibu mapigo kwa ngongo kwa kuonyesha umahiri wa kujenga hoja.tuache matusi,hayo tuwaachie CCM kwa sababu hiyo ndiyo silaha,mtaji na hazina pekee waliyobaki nayo.chadema tuna hoja.Si kila anayekukosoa ni adui yako bali kuna wenye mapenzi.tujenge tabia ya kutafakari,kutathmini na kupata sababu za kukataa ushauri,maoni au hoja otherwise tuvute subira

Huu ushauri mpe NGONGO.

Kwa sisi wengine tunaoamini CDM kuwa ni chama ni taasisi yenye viongozi na uongozi makini HATUTETELEKI BALI TUNAONA FURSA KWENYE HILI YA KUTUPELEKA MBELE kwa sababu tunajua tunachokiamini na tunaowaamini.

NGONGO IS GUIDED BY INDIVIDUAL HATE; HE CAN NEVER BE ABLE TO EVALUATE A SITUATION OBJECTIVELY RATHER CHARACTERISE IT.

MUNGU AMEWEZA KUTUUMBA KWA JINSI TULIVYO LAKINI MAISHA YANAENDELEA
 
Wakuu,

Kwa kuwa JF ni jukwaa huru....ningeshauri tuwe na subira tu hadi maamuzi yatakayotolewa.Kwa wafuasi wa CCM na wale ambao hawaitakii CHADEMA mema msisubiri kuona mgogoro mkubwa kutokana na hili suala la Arusha.Chadema imeshapita katika political turmoil kali kuliko hizi.Nawapa pole

Na kwa wafuasi wa CHADEMA mlioko huku,ningewashauri kabisa mjenge hoja kutetea anayoandika NGONGO.Hebu tuonyeshe tofauti na CCM kama inatulazimu kujibu mapigo kwa ngongo kwa kuonyesha umahiri wa kujenga hoja.tuache matusi,hayo tuwaachie CCM kwa sababu hiyo ndiyo silaha,mtaji na hazina pekee waliyobaki nayo.chadema tuna hoja.Si kila anayekukosoa ni adui yako bali kuna wenye mapenzi.tujenge tabia ya kutafakari,kutathmini na kupata sababu za kukataa ushauri,maoni au hoja otherwise tuvute subira

Mojawapo wa faida za JF ni kupata mawazo huru.CCM imefika huku kwa sababu ya kuendeleza fikra za kulindana,kuogopana matumizi mabaya ya vyeo na nafasi za uongozi.Ni lazima tujiandae kujenga taifa lenye nidhamu na uwajibikaji uliotukuka kwa kusimamia misingi ya haki,demokrasia na utashi wa nguzo tatu za kiuchumi,kijamii na kisiasa katika maamuzi ya jambo lolote linalohusu watu,viongozi wao nk.
Huwa namsoma Ngongo kwa makini,he is one of the great thinkers in here.Wewe unadhani Ngongo ni CDM?
 
Mmh! Chadema ianze kuandaa makada wake mapema, hawa wa kuazima wanawasumbua/watawasumbua sana!
 
Heshima kwako Ben.

Mkuu kwanza nakupongeza kwa ustaharabu.

Pili wengi hapa JF wanadhani ukikosoa madhaifu ya CHADEMA wewe ni CCM kitu ambacho si kweli nina hakika wengi hapa wameujua upinzani juzi baada ya Dr Slaa kumpeleka puta JK.Ukichimbua sababu za Dr Slaa kupendwa na kuaminiwa na waTanzania wengi wenye akili nzuri ni uwezo wake wa kujenga hoja na kuzisimamia bila kutetereka.Leo CCM inajivua gamba ni kwakuwa CHADEMA imewalazimisha kufanya hivyo laiti CHADEMA kisingekuwa na nguvu hakika CCM ingelala.Natamani CHADEMA isonge mbele lakini kamwe kama chama lazima na chenyewe kichukue hatua za kuachana na wanachama na viongozi wabovu.

Tanzania baada ya kusambaratika kwa NCCR Mageuzi CCM ililala rushwa ikatamalaki,mikataba mibovu na uwizi wa mali za umma ukashika kasi bila kikomo.Wangapi leo wamewahi kujiuliza NCCR ingekuwa na nguvu Mkapa angejiuzia Kiwira,EPA ingekuwepo ?.kusambaratika kwa NCCR kumeichukua CHADEMA miaka kumi kuziba nafasi ya upinzani Tanzania.Jiulize leo hii CHADEMA ikisambaratika itachukua miaka mingapi kurejesha upinzani mwingine wa maana?.Ninapokosoa CHADEMA na viongozi wake sina maana mbaya bali kukitaka chama kijitazame na kukubaliku kosolewa.Natamani sana CHADEMA ijenge system nzuri ya kuzuia na kutatua migogoro yake bila kuathiri nafasi yake ya kukua na kukamata dola.

Wanazi wa CHADEMA JF hakika Dr Slaa anagekuwa mvivu wa kujibu hoja na kufanya utafiti chama kisingefikia hapa leo.Natambua wapo baadhi ya wabunge na madiwani wengi wamefikia kuitwa waheshimiwa kwasababu ya Dr Slaa na ukienda mbele zaidi hawana mchango wa maana.Mwaka 2015 wengi wa waheshimiwa wa CHADEMA hawatavuka kwa mgongo wa Dr Slaa tena wataulizwa na wananchi wamefanya nini ?.Sijui watasema tulisusa ?,tulikuwa tunafanya vikao vya muafaka miaka mitano ?,tuliambiwa tujiuzulu ? na nk.

Kwa kuwa JF ni jukwaa huru....ningeshauri tuwe na subira tu hadi maamuzi yatakayotolewa.Kwa wafuasi wa CCM na wale ambao hawaitakii CHADEMA mema msisubiri kuona mgogoro mkubwa kutokana na hili suala la Arusha.Chadema imeshapita katika political turmoil kali kuliko kama hizi

Na kwa wafuasi wa CHADEMA mlioko huku,ningewashauri kabisa mjenge hoja kutetea anayoandika NGONGO.Hebu tuonyeshe tofauti na CCM kama inatulazimu kujibu mapigo kwa ngongo kwa kuonyesha umahiri wa kujenga hoja.tuache matusi,hayo tuwaachie CCM kwa sababu hiyo ndiyo silaha,mtaji na hazina pekee waliyobaki nayo.chadema tuna hoja.Si kila anayekukosoa ni adui yako bali kuna wenye mapenzi.tujenge tabia ya kutafakari,kutathmini na kupata sababu za kukataa ushauri,maoni au hoja otherwise tuvute subira

Mojawapo wa faida za JF ni kupata mawazo huru.CCM imefika huku kwa sababu ya kuendeleza fikra za kulindana,kuogopana matumizi mabaya ya vyeo na nafasi za uongozi.ni lazima tujiandae kujenga taifa lenye nidhamu na uwajibikaji uliotukuka kwa kusimamia misingi ya haki,demokrasia na utashi wa nguzo tatu za kiuchumi,kijamii na kisiasa katikamaamuzi ya jambo lolote linalohusu watu,viongozi wao nk.
 
Napenda kuwapa salamu wana jamii wenzangu,
na pia nimefurahishwa na hili jambo jinsi linavyojadiliwa.
Kwa maoni yangu Wana JFs, nadhani jambo muhimu hapa ni kuwaachia uongozi wa CHADEMA kuifuta KATIBA YA CHAMA inasema nini katika hili suala ya madiwani wa CHADEMA Arusha.
Itakuwa ni kipimo kizuri cha utawala bora katika yale yanayohubiriwa ktk majukwaa,
Jan 5, watu walikufa na wengine wengi waliumia....., je yale yaliyokuwa yanahubiriwa yametekelezeka? binafsi jibu NO!
Uongozi wa CDM umepata changamoto za utendaji katika mawasiliano kati hili sakata na utashi wa madiwani husika.
Katika ujenzi wa utawala bora katika demokrasia ya kweli kuna changamoto nyingi tuu...,
CCM chama kikongwe..., kimeshindwa ktk hilo, CDM wanajitahidi ktk hilo.
Ni imani yangu Uongozi wa CDM ukifuata katiba yao, yataisha tu. ni heri kuwa na madiwani bora wachache kuliko kuwa na bora madiwani!
 
Ngongo, tatizo lako wewe humpendi Lema na hujawahi kumsema kwa jema hata siku moja. Sasa unaweza kuwa unayosema mengine ni kweli ila watu huwa tunakutilia mashaka maana msimamo wako unajulikana.

Huyu Mallah sijui, kama alitukanwa na Lema kuwa kahongwa, huu ndiyo ulikuwa muda mzuri wa kumburuza Lema mahakamani na huko wakayamalize. Kama sivyo basi walau kwenye vikao vya Chama na huko adai waziwazi kuwa "alitukanwa wakati hakuhongwa." Kama Lema akishindwa kuthibisha kuwa Mallah alihongwa basi aitishe waandishi wa habari na KUMUOMBA MSAMAHA. Jacob Zuma alishitakiwa makosa kibao na Mbeki na mwisho akamuondoa hata kwenye Urais na yeye kashinda, itakuwa Mallah?

Ila kuna kesi nyingine ambayo ni wao kufanya muafaka. Uongozi wa Chadema uliwaambia wajiuzulu nyadhifa zao. Uongozi wa Chadema hawakusema kuwa wao wamehongwa. Sasa Mallah anatumia maneno ya Lema kupata kisingizio cha kukataa kujiondoa kwenye unaibu-meya. Kitakachotokea hapa ni Chadema kufanya maamuzi magumu. Watafukuzwa wote na wakagombee kwa kutumia ticket ya CCM. Wakishinda basi uchaguzi halali ufanyike na CCM washinde kihalali sasa na Arusha iendelee kama kawaida chini ya utawala wa CCM.

Kama kweli wao lengo lao ni kurudi CCM basi watarudi na huko tutawatakia maisha mema ingawa nako kuna moto unawaka kati ya Lowassa na Chatanda. Sisi yetu macho.

Chadema ni heri wakose viti vyote vya Udiwani uchaguzi ukirudiwa kuliko kuwa na madiwani hawa ambao kweli ukiwachunguza, unaona kuna kila dalili mkono wa Lowassa unafanya kazi. Anyway, uchaguzi wa mwaka 2015 ndiyo unanukia. Patachimbika Arusha.
 
kumbe ni viti maalum na wahengeze wa lema tu ndio walioomba radhi kwa kuogopa kutimuliwa hahaaa yaani wewe nanyaro pamoja na kuchaguliwa na watu wa kata yako, bado ni kitumwa cha lema? pole sana na upembele wako na kumbe ulikubali muafaka kwa rushwa basi jiuzulu haraka pa...ka wewe!! na hao vitu maalum wenzako.

Kumbuka Nanyaro hakuchaguliwa kwa sera zake alichaguliwa kwa sera ya chama kilichompa nafasi ya ugombea, hakusimama yeye kama yeye na kusema yeye anaweza kufanya sera zake mwenyewe. pia kumbuka hii ilikuwa pia ni kuwasaliti wananchi waliomchagua pia. kama wananchi walihitaji mabadiliko na udiwani ukapitishwa kinamna, hakuna maana ya kumpinga Mwizi na kumkubali si mwizi, kuna namna hapo.
 
Heshima kwako Sikonge.

Mkuu aliposhinda nilimpongeza lakini nikampatia ushauri wa bure akue aache mambo ya uchaliii.Mwaka mmoja umeshamalizika umejionea mwenyewe kama kunajmbo zuri Lema kalifanya eg tufunge milango tuchapane makonde ruksa kuandika.Mengine nimeshajibu kwa ufasaha.

Ngongo, tatizo lako wewe humpendi Lema na hujawahi kumsema kwa jema hata siku moja. Sasa unaweza kuwa unayosema mengine ni kweli ila watu huwa tunakutilia mashaka maana msimamo wako unajulikana.

Huyu Mallah sijui, kama alitukanwa na Lema kuwa kahongwa, huu ndiyo ulikuwa muda mzuri wa kumburuza Lema mahakamani na huko wakayamalize. Kama sivyo basi walau kwenye vikao vya Chama na huko adai waziwazi kuwa "alitukanwa wakati hakuhongwa." Kama Lema akishindwa kuthibisha kuwa Mallah alihongwa basi aitishe waandishi wa habari na KUMUOMBA MSAMAHA. Jacob Zuma alishitakiwa makosa kibao na Mbeki na mwisho akamuondoa hata kwenye Urais na yeye kashinda, itakuwa Mallah?

Ila kuna kesi nyingine ambayo ni wao kufanya muafaka. Uongozi wa Chadema uliwaambia wajiuzulu nyadhifa zao. Uongozi wa Chadema hawakusema kuwa wao wamehongwa. Sasa Mallah anatumia maneno ya Lema kupata kisingizio cha kukataa kujiondoa kwenye unaibu-meya. Kitakachotokea hapa ni Chadema kufanya maamuzi magumu. Watafukuzwa wote na wakagombee kwa kutumia ticket ya CCM. Wakishinda basi uchaguzi halali ufanyike na CCM washinde kihalali sasa na Arusha iendelee kama kawaida chini ya utawala wa CCM.

Kama kweli wao lengo lao ni kurudi CCM basi watarudi na huko tutawatakia maisha mema ingawa nako kuna moto unawaka kati ya Lowassa na Chatanda. Sisi yetu macho.

Chadema ni heri wakose viti vyote vya Udiwani uchaguzi ukirudiwa kuliko kuwa na madiwani hawa ambao kweli ukiwachunguza, unaona kuna kila dalili mkono wa Lowassa unafanya kazi. Anyway, uchaguzi wa mwaka 2015 ndiyo unanukia. Patachimbika Arusha.
 
Huwa namsoma Ngongo kwa makini,he is one of the great thinkers in here.Wewe unadhani Ngongo ni CDM?

Comrade Jmush1,

Asante,ila kwa bahati Mbaya huwa siangalii ni nani kaleta hoja kwa sababu nitakuwa biased nitakapojibu na sitamtendea haki ninayemjibu na hata wanajamvi kwa ujumla.huwa ninaangalia hoja inayoletwa mkuu,na hii ni changamoto kwa wengi

Mkuu umekuwa hapa JF siku nyingi kuna kipindi hoja nzito nzito zilikuwa zinashuka hapa enzi zile tukiwa na akina mtanzania(Geoorge Mwakalinga),Mugongomugongo,Fikira duni,Game theory,Waberoya,Mwafrika wa Kike, Dua,mama,Kichuguu,FMES nk....ukiangalia trend ya hii thread you'll just come into terms with a tragic reality,ni matusi matupu unnecessarily
.
 
1) Tulisikia kuna muafaka kati ya Mbowe na Pinda kuhusu Arusha. Si Mbowe wala Pinda waliokanusha mpaka sasa.
.

@FaizaFoxy, majadiliano kati ya CHADEMA na CCM yalikuwa yanaendelea hilo halina ubishi. Wether CCM ilikuwa na dhamira ya kweli au ilitaka kuhadaa watu that is something else, lakini historia ya ccm inanishawishi niseme wanahusika na kuhadaa watu Arusha kuwa muafaka umefikiwa kitu ambacho si kweli. Kwenye meza ya mazungumzo kati ya pande mbili hizi (CHADEMA & CCM) kulikuwa na vitu vya msingi vya kurekebisha moja ikiwa Mary Chatanda wa Tanga aondoke kwenye maamuzi ya ki-uongozi Arusha. Hakuna hata moja ambalo lilisababisha machafuko na hata mauaji ya January 5 limefanyika. Sasa huu muafaka unakuwa wa nani kama si wa CCM na wapambe 'wadanganywa'. As a a nation when will we stand on principles. Nelson Mandela alikaa jela miaka 27 na watoto wake wamekuwa bila malezi ya mzazi mmoja yaani baba kwa sababu alisimamia kile alichoamini. Kama Mandela angekubali 'yaishe' nani kati yetu leo hii anaweza kusema kuwa South Afrika ingepata Rais mweusi au M-south Africa mweusi angeruhusiwa kupiga kura (narudia kupiga kura)?

Whichever way we want to look at this Arusha saga, one thing is very clear -wananchi wa Arusha wamesahaulika. Kwa katiba yetu, pamoja na mapungufu yake inatamka waziwazi kuwa wananchi ndio wenye mamlaka ya mwisho. Tarehe 5 January wananchi wa Arusha waliandama kuwaambia viongozi wamekosea (mambo ya msingi) na hivyo wajirudi, sasa, anyone anayejidai 'yaishe' bila kurekebisha kile wananchi wanachodai, na wengine kupoteza maisha ni usaliti wa hali ya juu. Enough is enough. Tunakata viongozi watii katiba na watambue sisi wananchi ndio tuna mamlaka ya mwisho.
 
daktari slaa tumia busara za kufundishwa kwenye ukatoliki. ukimsikiliza lema utaua chama chako. lema angetaka ziwe zinapigwa kila siku ili apate kisingizio. diwani anayepokea amri toka makao makuu ni kibaraka sisi wananchi hatumtaki.
 
Mkuu Ngongo, mimi nakumbuka tu kampeni zako dhidi ya Lema tangu kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa mwaka jana, loo ulikuwa unatisha ! Kwa Lema umekuwa mlalamishi, mshitaki, mwendesha mashtaka na mtoa hukumu vyooote kwa pamoja na nabaki nikijiuliza ni chuki gani binadamu anaweza kuwa nazo dhidi ya binadamu mwenziye kiasi hiki. Nini hasa kilicho nyuma ya hizi chuki hadi ukilala unamwota Lema na ukiamka unamwaza Lema - hii obsession yako kwa Lema inasababishwa na nini maanake sasa imevuka mpaka. Sikutaka kabisa kuchangia thread hii lakini duh, imefikia hadi unaanza kutukera sisi wengine, the absurdity of it all !

Sasa tukirudi kwenye mada ya mwafaka huko Arusha kwa mbali namwona Nape akiingia kwenye anga za Arusha na kuanza kumsifia Mallah anavyoanza kung'ara baada ya kuukwaa Unaibu Meya, yale yale ya Seif Hamad wa CUF kugonga whisky Ikulu baada ya kuukwaa Umakamu Uraisi Zanzibar. Kumbe maandamano, vifo na kelele za Chadema mapema mwaka huu ni kulilia mwafaka na vyeo katika halmashauri ya Arusha ! Sitaki na nasema sitaki miafaka ya aina hii maanake inasababishwa na tamaa, ulafi na unafiki - fikiria kama kesho na kesho kutwaa Chadema wanaingia kwenye mwafaka na CCM na Dr. Slaa anaukwaa unaibu Waziri Mkuu, ya Rabi tupishie mbali !
 
Comrade Jmush1,

Asante,ila kwa bahati Mbaya huwa siangalii ni nani kaleta hoja kwa sababu nitakuwa biased nitakapojibu na sitamtendea haki ninayemjibu na hata wanajamvi kwa ujumla.huwa ninaangalia hoja inayoletwa mkuu,na hii ni changamoto kwa wengi

Mkuu umekuwa hapa JF siku nyingi kuna kipindi hoja nzito nzito zilikuwa zinashuka hapa enzi zile tukiwa na akina mtanzania(Geoorge Mwakalinga),Mugongomugongo,Fikira duni,Game theory,Waberoya,Mwafrika wa Kike, Dua,mama,Kichuguu,FMES nk....ukiangalia trend ya hii thread you'll just come into terms with a tragic reality,ni matusi matupu unnecessarily
.
Brah Ben,fisrt of respect!

Since umeweka wazi kuwa wewe ni CDM,I respected you for that.Nilkuuliza kwasababu pia ulidai kuwa wenye chuki na CDM ama wenye kudhani kutatokea mgogoro basi they are wrong.

Ndiyo maana nikakuuliza lile swali hapo awali kuhusu Ngongo kwani nilisoma kama vile unataka wana CDM wauchukuwe ushauri wake.yeye anakuja very defensivelly na kusema ooh JF inahusishwa na CDM,eti sijui ukiwapinga CDM unaambiwa wewe ni CCM.

Everybody knows that this has been gping on for smtimes,sababu keshakiri kuwa JF si CDM,sasa why bringing it up kama si sababu ya kujikinga tu ili umwage unayoyataka?

kuwa na mawazo tofauti hakutusababishi wenye kukuheshimu kuiondoa hshma hiyo.Unless kuna maslahi ynahusika basi hapo utakuta watu wana paruzana humu.

Kwasababu huwa namsoma Ngongo na ni mmojawapo wa wana JF ninao admire mchango wao.Naamini kabisa kuwa yeye si CCM.However ninaamini pia kuwa yeye si CDM.

Kwamba mawazo yake ni mema kwa chama chenu,that i leave it with you CDM members.Nachoelewa ni kwamba he is a CDM critc,sina haja ya kujuwa lengo lake.However huwa naheshimu mawazo yake,japokuwa huwa sikubaliana na mawazo yake yote.
Shukran kamanda,tuendelee na mjadala.
 
ben
Kwanza nikupongeze kwa uwazi lakini nitofautiane na wewe kujaribu kuonyesha kuunga mkono utovu wa kimaadili unaofanywa na madiwani .
Hata kama wanahoja ya kupinga hawakupaswa kupinga hadharani maamuzi ya kamati kuu ya chama huku wakitishia kumshtaki katibu mkuu tena walimpa muda kabla ya jana awe ameitisha mkutano na kuwaomba radhi mbele ya wananchi lasivyo wanamuongezea kesi kwani kwa sasa anayo ya kuandamana jan .

Huu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu nakushangaa ww mwanacdm ambaye unajua maamuzi yale hayakuwa ya mtu mmoja kufurahia taasisi yenu kupuuzwa na kudhalilishwa ili mradi kundi lenu la zitto lipate kunyooshea kidole la mbowe its crazy
Mala sasa anajaribu kujificha nyuma ya bifu lao na lema kutaka kuhalalisha utovu wake wa nidhamu haiwezekani agome kwenda kujieleza kamati kuu halafu arudi kuhoji kwa nini kamati kuu iwahukumu na si wilaya huyu ameshaharibiwa akili kama si pombe basi fedha
Mala amelipa waandishi fedha nyingi kutoa tamko na wameandika wakati tamko linatolewa nje alikuwepo kada wa ccm gambo akiwasubiri madiwani wa cdm swala la kujiuliza gambo lini kawa swahiba wao wkt ni kijana na chatanda ukiunganisha dots u'l get something
Nina mengi ila kwa sasa naachia hapa
 
Back
Top Bottom