Madiwani wa CHADEMA Arusha wagawanyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani wa CHADEMA Arusha wagawanyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Jul 23, 2011.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  MADIWANI saba kati ya 11 wa Chadema jijini hapa wamegoma kujiuzulu nyadhifa zao au kuomba msamaha kama walivyotakiwa kufanya na uongozi wa juu wa chama hicho.

  Miongoni mwa waliogoma ni pamoja na Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Estomih Mallah ambaye jana aliongoza vikao vya Halmashauri ya Jiji.

  Hata hivyo, madiwani wanne waliomba msamaha kutokana na kukubali mwafaka na madiwani wa CCM wiki tatu zilizopita.

  Madiwani waliogoma walisisitiza, kwamba hawatatetereka hadi uongozi wa juu wa chama hicho utakapowasafisha kutokana na kuwatuhumu kuhongwa na CCM ili waridhie mwafaka wa CCM kuishika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

  Madiwani walioomba msamaha ni Ephata Nanyaro wa Kata ya Levolosi, Isaya Doita, wa Ngarenaro na wawili wa viti maalumu, Viola Lazaro na Sabina Francis.

  Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Mallah alisema hakulazimishwa wala kushurutishwa na mtu au kiongozi yeyote kufikia mwafaka na CCM, bali ni utashi na mawazo yake ni namna gani anaweza kuwatumikia wananchi wa Kata yake ya Kimandolu.

  Alisema kila diwani alikuwa na kila sababu ya kutaka mwafaka kwa maslahi ya wakazi wa kata waliyochaguliwa juu ya maendeleo, lakini kwa sababu watu wanataka migogoro ya mara kwa mara ili waweze kufaidika, hilo kwao kama madiwani halina sababu ya msingi.

  ‘’Mimi niko tayari sasa kwa lolote, kwani sioni sababu ya kuomba msamaha kwa kitu ambacho naona natenda haki kwa maslahi ya wakazi wa Kata yangu,’’ alisema Mallah.

  Akizungumzia kushiriki kikao cha Baraza la Madiwani jana, Mallah alisema yeye kama Naibu Meya ameshiriki kikamilifu na madiwani wengine `wasio na woga’ katika kikao hicho.

  Mallah alisema katika kikao chao cha jana, mambo mengi ya msingi yamezungumzwa katika kuleta maendeleo katika Jiji la Arusha, hiyo ndio kazi ya diwani na si kuzusha mgogoro.

  Wakati hayo yakiendelea Arusha, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa alisema amepokea barua kuhusu sakata la madiwani wa Arusha.

  Akizungumza kwa njia ya simu jana, Dk. Slaa alisema alipokea barua (hakutaja idadi) saa tatu asubuhi na kuahidi kutoa taarifa baada ya kuzifanyia kazi.

  Alisema kwa kuwa suala hilo linahitaji umakini wa hali ya juu, anahitaji muda wa kutosha bila kuingilia ratiba yake ya mikutano ya hadhara ambayo anatarajiwa kuifanya leo na kesho.

  “Tafadhali naomba mnipe muda, kwani suala lenyewe ni zito na linahitaji muda wa kutosha kulijadili na kutoa uamuzi … nitatoa taarifa kamili baada ya kuifanyia kazi barua niliyopokea,” alisema Dk. Slaa ambaye chama chake awali kilipinga kumtambua Meya wa Jiji la Arusha kutoka CCM, Gaudence Lyimo.

  Chadema ilimkataa kwa madai kuwa uchaguzi wake haukufuata utaratibu na misingi ya haki.

  Pamoja na madai ya Lema ya usaliti kutokana na mwafaka kutokuwa na baraka za viongozi wa juu wa chama, madiwani hao waliendelea kudai kuwa uamuzi wa kumkubali Lyimo ulizingatia maslahi ya wananchi wa kata zao na Jiji la Arusha na si vyama.
   
 2. M

  Mzee Wa Maono Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbe ni viti maalum na wahengeze wa lema tu ndio walioomba radhi kwa kuogopa kutimuliwa hahaaa yaani wewe nanyaro pamoja na kuchaguliwa na watu wa kata yako, bado ni kitumwa cha lema? pole sana na upembele wako na kumbe ulikubali muafaka kwa rushwa basi jiuzulu haraka pa...ka wewe!! na hao vitu maalum wenzako.
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  yaani jina lako na ulichoandika mkuu mbona vina pishana...
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  No one is perfect and no politica party is perfect. Kwenye saga ya Arusha nadhani msingi wa mtafaruku wote ni poor communications between HQ na Arusha. Binafsi sikubaliani na muafaka kwa wa 'VYEO' kwa sababu Africa nzima (sio Tanzania peke yake) kumekuwa na kasumba mbaya sana ya kugawana vyeo na hivyo kuondoa dhana nzima ya utawala wa demokrasia na uchaguzi. Na hii kasumba inachangia kwa kiasi kikubwa uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi na hasa wapiga kura maana wanajua hata wakishindwa watafanya 'makubaliano' ya amani!

  Kwa maana hiyo nampongeza Nanyaro kwa kuwa na upeo juu ya utawala wa demokrasia. Arusha watu wamekufa na wengine wamepata vilema vya maisha wakitetea misingi ya utawala bora, then leo mtu asema wamefikia muafaka? In the name of those who died madiwani wa CHADEMA Arusha wanatikwa wajue huu muafaka wanaoupiginia umejaa damu - bloody muafaka!

  Na nilisema huko nyuma ili madiwani wa CHADEMA wawe na uhalali wa kupokea vyeo na kusema muafaka umepatikana basi ni sharti ndugu wa marehemu wa Jan 5, pamoja na majeruhi washirikishwe. Wamekufa watu hapa wakipigania haki, kwa nini madiwani wanaona ugumu ku-demand ccm na serikali yake wakomeshe tabia ya kukiuka sheria na taratibu za uchaguzi? Kwa vipi madiwani hawa wanaweza kusema wanaamini demokrasia na utawala bora ili hali wanaishi ukiukwaji huo? Hii tabia ya 'bwana yaishe' bila ku-address chimbuko la matatizo ndiyo imetufikisha hapa.

  Leo hii Mary Chitanda anatamba bungeni! utajengaje taifa kama viongozi wanakuwa na 'conscious' ya Mary Chitanda? Watoto wa Taifa hili wanakuzwa kuwa watu gani kama viongozi tulio nao ni Mary Chitanda na madiwani wasio simamia yale wanohubiri?. Huyu Mallah anaweza kusimama mbele ya umma akasema kwa nini aliandamana January 5? Kile kilichomfanya akawa barabarani kimefanyika? Kama hakusimamia alichokuwa anahubiri January 5 sisi wananchi tumwamini kwa lipi? Ni maendeleo gani hayo anatamba kuwatufutia wana-Arusha kama hakuna haki?

  Mtu kama Mary Chatanda hawezi leo hii akasimama bungeni kutetea wananchi kama anachokisema 'kitawaudhi' waliomuweka hapo? Kwa maana nyingine wananchi wanakuwa wamewekwa pembeni kama karai baada ya zege kuisha! Hatuwezi kuendelea kama msingi wenyewe ndio huo. Madiwani wa Arusha inabidi mtambue hilo.
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kwa hili Mallah ameingia choo cha kike ni muda tu atajikuta yuko nje ya ulingo na hatakuwa na jukwaa la kusemea.
   
 6. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu FJM, umesema yote.Nadhani chadema kuna kitu cha msingi sana hawajakifanya ambacho ni kuwaelezea wananchi haki yao ya kuiwajibisha serikali pamoja na kazi za diwani na mbunge.Watu bado wanaamini diwani na mbunge ndo wanaleta maendeleo. Wabunge wa cdm wanajua kabikuwa kazi ya kuleta maendeleo ni ya serikali na wao wabunge na madiwani ni kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi ili ifanye yale wanayotaka wao.Kitendo cha madiwani wa Arusha kujifanya kuwa bila kuingia kwenye mwafaka wa kugawana vyeo basi maendeleo hayatapatikana kwenye ward zao huu ni uongo na umbumbumbu wa madiwani hawa.Nadhani chadema haijafanya semina kwa madiwani wake ili wajuwe kazi zao ni nini na kazi za serikali ni zipi.Kwa mtu anayeelewa kazi ya kuleta mendeleo ni wajibu wa serikali bila kjali itikadi ya chama kwa kuwa wana nchi wote wanalipa kodi.Kzi ya diwani ni kuisimamia,kuishauri na kuiwajibisha serikali pale inapotaka kwenda kinyume na malengo ya wananchi. Siyo kazi ya diwani kwenda kuipigia magoti serikali ili ipeleke maji,barabara,au kitu chochote kwenye eneo lake.Vitu vyote hupangwa na kukubaliana na kwenye bajeti na madiwani hubaki kuhakikisha yaliyokubaliwa kwenye bajeti yao ndiyo yaliyotekelezwa.Hili la diwani kusema asipoingia mwafaka na ccm hakutakuwa na maendeleo, analitoa wapi kama si umbumbumbu wa kutaka kuendelea na fikira za kitumwa ambazo ndo zimetufikisha hapa tulipo.Badala ya kuwasidia wananchi waelewe kuwa maendeleo ni haki yao na ni wajibu wa serikali kuleta maendeleo na si kazi ya diwani au mbunge kuwapigia magoti serikali. Natamani ningekuwa na muda wa kuliingiza hili kwenye akili ya kila mtanzania. Na hiki kitu ndo kimetufanya tubaki hapa tulipo maana watu wengi hawajui hili wanadhani kuletewa maendeleo ni favour hivyo hukaa kimya wakisubiria.Watu wakielewa hili wataandamana kila mahali na watakuwa wananafatilia mipango ya serikali ya kila mwaka na kuhakikisha wanawabana pale wanaposhindwa kutimiza .Mungu tusaidie kuondoa huu umbumbumbu kwenye akili za watanzania.
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Naibu Meya Estonih Mallah, mpenda amani!
  Bora kufa umesima kuliko kuhishi umepiga magoti, ata ukipoteza kila kitu kwenye CDM hiyo ndio sifa ya mpambanaji
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Estomih Mallah, haitaji jukwaa la kusemea, sisi Wananchi wapenda Amani ndio tunaomkubali, kama wewe ni mateka wa Mbowe na Slaa usimuambukize Naibu Meya udhaifu wako wa fikra
   
 9. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ubora wa chadema hautokani na wingi wa madiwani wala wabunge bali ubora wa madiwani na wabunge wachache walio ndani ya chama.Chadema haihitaji kuwa na kundi la madiwani wenye fikra za ccm. Inahitaji madiwani na wabunge wenye fikra za chadema. Kama diwani au mbuge anafikra za ccm hafai na hahitajiki katika safari ya kutafuta haki na mabadiliko ya kweli.Chadema inahitaji wapiganaji kwa sasa siyo watu wa kuja kula starehe kama Mallah ambaye anang'ang'ania unaibu meya kwa maslahi yake binafsi. Awaambie wananchi wake, wanafaidika nini ikiwa yeye atakuwa naibu meya wa Arusha? Ukweli ni wazi kuwa unaibu meya ni kwa faida ya tumbo lake tu.Chadema kama Mallah na madiwani wengine wataendelea kung'ang'ania hayo madaraka basi hawatufai maana hawtaweza kufika tunakotaka kwenda watawaambukiza na wengine. Safari tuliyonayo ni ngumu inahitaji wapiganaji hasa waliojikana wenyewe kwa ajili ya wananchi. Matunda ya maisha mazuri ambayo chadema inayatafuta kwa ajili ya wanatzania bado hayajapatikana, hivyo kitendo cha Mallah kutaka kuanza kufaidika na matunda haya hata kabla ya muda wake si jambo linaloweza kuvumilika kwa urahisi tu.Madiwani hawa lazima wajuwe kuwa kazi yao si rahisi kama ya madiwani wa ccm. Kama wenzao wanawaona wana vitambi na maisha mzuri ni kwa ajili ya ufisadi wao. Kama Mallah anataka kufanana nao kwa haraka hivyo basi hatufai maana hatutaweza kupambanua cdm na ccm.Mungu ibariki Arusha!
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Vipi pesa za kuwalipa waandishi wa habari, zilitoka kwenye fungu gani?
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Naona ameamua kuyamaliza kinyumbani na Lyimo, mwambie awagawie vijisenti wapiga kura wake...
   
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Pesa za kumlipa Sarawatti wa Raia mwema Lema kazitoa wapi ?.
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Huyu hayuko kwenye hili sakata na wala hakupewa barua yoyote kati ya zile mbili walizopewa baadhi ya madiwani...
   
 14. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Ripoti ya Marando imewasafisha madiwani hawakupokea wala hawakutoa rushwa.
   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  amemlipa ili iweje...
   
 16. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Hivi Nanyaro alikuwa na wadhifa gani ukiondoa udiwani ?.
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Si zungumzii ripoti ya Marando na zungumzia kuwa lipa waandishi wa habari juzi na kuwa patia chakula na usafiri....
   
 18. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Una hakika?
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ni mwenyekiti Bavicha Mkoa..
   
 20. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Utakuwa uanishi ughaibuni Sarawatti wa Raia Mwema alikuwa akivuta vijisenti vya Lema tangu mwaka jana ukitaka fuatilia makala za Sarawatti kuanzia mwaka jana kipindi cha uchaguzi.Binafsi niliwahi kumuuliza Sarawatti ni kwanini makala zinazomhusu Lema suala la elimu hajawahi kulizungumzia akabaki anacheka !.Raia Mwema ni gazeti langu kabla Rai haijavamiwa na mafisadi nilijaribu mara kadhaa kuwasiliana na mhariri azifuatilie habari za Arusha kwa umakini sana kwakuwa hazikuwa balanced kabisa.Nafurahi toleo jipya Sarawatti kaanza kuandika habari balanced pengine wakuu wake waligundua mauza uza ya mwandishi.
   
Loading...