Mbunge Dkt. Paulina Nahato Awafunda Wasomi wa Vyuo na Vyuo Vikuu, Dar es Salaam

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

Mbunge Dkt. Paulina Nahato Awafunda Wasomi wa Vyuo na Vyuo Vikuu, Dar es Salaam

Mbunge wa Viti Maalum aalum Anayewakilisha Makundi ya Wasomi nchini wa Vyuo na Vyuo Vikuu, Mhe. Dkt. Paulina Nahato ametoa wito kwa vijana kujiepusha na matumizi ya mitandao ya kijamii isiyofaa ikiwemo mitandao inayomchafua Rais, Bunge na viongozi wengine wa Serikali

Mhe. Paulina Nahato amesema
badala yake vijana wasomi wanapaswa kutumia mitandao ya kijamii kufuatilia masuala yatakayowasaidia kwenye maisha ikiwemo kuwajengea uwezo wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi

"Vijana wa Seneti Mkoa wa Dar es Salaam ndiyo vijana wa Tanzania nzima. Tumeongea Mipango mikakati yetu mikubwa sana namna ya kukiendeleza Chama Cha Mapinduzi katika Vyuo Vikuu na namna ya kutatua changamoto zetu wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wana CCM" - Mhe. Paulina Nahato, Mbunge wa Viti Maalum Vyuo na Vyuo Vikuu

Mhe. Paulina Nahato Ametoa rai hiyo akiwa kwenye mkutano Mkuu wa Seneti ya UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam mnamo Machi 10, 2024
 
Back
Top Bottom