Kwanini mijadala huru imetoweka vyuo vikuu vyetu?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,315
12,614
Zamani mwanafunzi wa chuo kikuu alikuwa ni tanuru la fikra kwa jamii. Ilikuwa hakuna linalopita bila kuhojiwa na kudadavuliwa hadi mwisho ili kupata kiini na undani wa jambo husika kabla halijatekelezwa. Jumuiya ya Chuo Kikuu ilikuwa inaweza kuutafuta ukweli kutoka kwa yeyote bila hofu wala woga hata ikibidi kwenda Ikulu kuutafuta ukweli huo. Kabla wanasiasa hawajapanga na kutekeleza jambo lolote walikuwa wakihofia jumuiya ya vyuo vikuu kwanza kuliko wananchi wengine. Vyuo vikuu vilikuwa chemchem ya fikra huru inayozalisha makada wa vyama vya siasa, viongozi wa serikali na wanaharakati mbalimbali.

Leo hii vyuo vikuu ni sehemu shwari yenye watu waliogandishwa kwenye mabarafu wanalalamikia na kunung'unikia matumboni mwao wakisubiri graduations kwa udi na uvumba. Wanafunzi wa vyuo vikuu wa sasa ni pungufu ya wanafunzi wa high schools wa enzi zile za miaka ya 70's. 80's na 90's kifikra. Wasomi wa vyuo vikuu walimu na wanafunzi wa siku hizi ni waoga na wasioelewa mambo ya nchi wasiweza kujitetea wala kudai haki zao na zile za wengine. Wasomi wa sasa wanawaza kumaliza chuo tu kwa wakati kwa kusoma maswali ya mitihani iliyopita na kunakili kazi za watu wengine.

Nimefanya utafiti kidogo usio rasmi sana na kugundua chanzo cha kukosekana kwa mijadala vyuo vikuu ni pamoja na yafuatayo:

1. Hali ngumu vyuoni: Zamani elimu ilikuwa bure; chakula kizuri bure, sehemu ya kulala bure, vitabu bure, stationeries bure, usafiri wa kwenda na kurudi shuleni bure, na kila kitu bureee. Wanafunzi walikuwa na muda mwingi wa kufikiria mambo makubwa badala ya zile basic needs (Maslow's theory). Wanafunzi wa sasa wamegawanywa na ada za chuo, mahali pa kulala, chakula, usafiri, nk. Mwanafunzi asiyekuwa na ada, chakula au mahali pa kulala hawezi kuwazia kufanya mijadala. Muda mwingi anawaza nitaishije, nitamalizaje mapema niondoke.

2. Walimu hafifu: Wanafunzi wetu vyuo vikuu wanafundishwa na walimu hafifu sana, mwalimu mwenye GPA kubwa kwa kunakiri kazi za wengine na kusoma maswali kuanzia shule ya msingi, sekondari, A level na chuoni. Walimu hawa wanatengeneza vitini na kuwauzia wanafunzi wao (vicious cycle).

3. Smart phones: wanafunzi wetu sasa hivi hawana muda wa kufikiria mambo ya nchi kwakuwa muda wote wako Facebook, You tube, Instagram, google, WhatsApp (internet) kulambaza na kuchati.

4. Wanasiasa: Wanasiasa wanatumia nguvu kubwa kuzuia fikra huru vyuoni,
5. Umri mdogo wa wanavyuo, wanafunzi wengi bado wana utoto na wanaishi kitoto kumudu kujadili maswala mazito ya nchi.

View: https://www.youtube.com/watch?v=4G5FdvZpKGY
 
Back
Top Bottom