SoC01 Madhara ya P2 (njia 15 bora za kuzuia mimba/uzazi wa mpango)

Stories of Change - 2021 Competition
Sep 9, 2021
17
38
Hello ,Mimi ni daktari mafunzoni ,karibu katika uzi wangu.

Punde tu baada ya wapenzi wawili kukutana kimwili wengi wazo la kwanza kuja kichwani ikiwa hawajapanga kuwa na mtoto huwa ni P2(morning after pill),haijalishi wanakutana mara ngapi,kila wakutanapo ni P2 tu.
Hivi hizi ni kanakwamba hazina madhara?
Au Pipi kifua?
Sasa ni zipi njia bora zaidi za kuzuia mimba zisiyotarajiwa pamoja na njia ya kalenda au P2 ambazo ni maarufu zaidi miongoni mwa watu?

Ninakuletea njia 15 za kisayansi zinazoweza kutumika kuzuia mimba(uzazi wa mpango) pamoja na faida na hasara kwa kila njia pendekezwa,pamoja na mapendekezo yangu binafsi kama mdau wa afya.

Uzazi wa mpango ni nini?
Wapenzi wawili wanapokaa kujadili na kuamua idadi ya watoto ambao wangependa kuwa nao na kwa wakati gani,ili wapewe mapenzi ya kutosha,matunzo na elimu bora kwa kila mtoto
• Kupanga idadi na wakati wa kuwa na watoto ni jukumu la wote wawili ,sio tu mwanaume au mwanamke tu.
Ni njia zipi za kuzuia mimba (Contraception)?

Zipo njia mbali mbali kulingana na malengo ya wapenzi, malengo yanaweza kuwa;
• Kuchelewesha mimba ya kwanza
• Kuacha muda kati ya mimba na mimba nyingine
• Kupunguza ukubwa wa familia

CATEGORIA ZA NJIA ZA KUZUIA MIMBA
1.Pharmacological and Non pharmacological
2.Short acting and Long acting contraceptives
3.Reversible and Non reversible techniques

SIFA ZA NJIA NZURI ZA KUZUIA MIMBA
1.Ni salama
2.Ifanye kazi kwa 100%
3.Free/ minimum side effects
4.Affordable
5.Acceptable to the user
6.Free of effects on future pregnancies

NJIA ZA UZAZI WA MPANGO ZINAZOTUMIA HOMONI
01.KIPANDIKIZI(IMPLANT)

Kipandikizi ni kibomba kidogo (chenye urefu wa milimita nne) ambacho huingizwa chini ya ngozi ya mkono wa mwanamke. Hutua homoni ambazo hulizuia yai la mwanamke kupevuka na kukuepusha kupata mimba.
Kipandikizi hiki kinauwezo wa kukaa kwa miaka minne lakini hakitakuzuia kupata/kuambukizwa magonjwa ya ngono.
Typical use failure rate: 0.1%
Picha:Google
20210915_120257.jpg

02.VIDONGE
Vidonge vya uzazi wa mpango ambavyo hutumiwa na mwanamke huwa na homoni ambazo hukuepusha kupata mimba kwa kuzuia yai la mwanamke kutokupevuka na hivi hutumiwa kila siku muda ule ule.Hivi sio sawa na P2.
Vidonge vya uzazi wa mpango havizuii maambukizi ya magonjwa ya ngono.
Typical use failure rate: 7%
Picha:Google
20210915_120441.jpg

03.SINDANO
Sindano nikama vidonge na kipandikizi – Huzuia yai la mwanamke kupevuka kwa kutumia homoni,hukuzuia kupata mimba na hii huchomwa matakoni au mkononi kila baada ya miezi mitatu. Njia hizi hazitakuzuia kupata/kuambukizwa magonjwa ya ngono.
Typical use failure rate: 4%.
Picha: Google
Screenshot_20210915-120621_Chrome.jpg

FAIDA
• Hufanya kazi kwa muda mrefu.
• Hazina athari katika uzalishaji wa maziwa kwa mama
• Uwezekano mdogo sana kupata upungufu wa madini chuma
HASARA
• Hedhi huvurugika
• Kushindwa kuzalisha mayai kwa muda fulani hata baada ya kuacha kutumia sindano.
• Kwa watumiaji wa muda mrefu wa medroxyprogesterone,mifupa kungua uzito ni tatizo.

04.Patch
Patch hubandikwa sehemu za chini ya tumbo,matakoni na sehemu za juu za mwili pia(lakini sio kwenye matiti).Hii ni mpaka ipendekezwe na daktari.
Hufanya kazi kwa kutoa homoni kwenda kwenye damu kama njia ya vidonge na sindano.Unabandika Patch mpya mara moja kwa wiki ndani ya wiki tatu na wiki ya nne haubandiki patch ili upate siku zako.
Typical use failure rate: 7%.
Picha:Google
20210915_120811.jpg

05.Hormonal vaginal contraceptive ring.
Hii ringi hutoa homoni kama njia nyingine,huwekwa ndani ya uke na huvaliwa kwa wiki tatu na wiki ya nne hutolewa ili kuruhusu hedhi kisha unavaa ringi mpya.
Typical use failure rate: 7%
Picha.Google
Screenshot_20210915-120958_Chrome.jpg

INTRAUTERINE DEVICES ( Vifaa vinavyopachikwa kwenye kuta za kizazi)
06.LEVONOGESTREL DEVICE (MIRENA)
Hiki kifaa huachia Levonogestrel kwenye kizazi(uterus).
Picha.Google
Screenshot_20210915-121158_Chrome.jpg

07.Copper T intrauterine device
Ni kifaa kidogo ambacho hufanana na umbile la herufi T huwekwa katika kuta za kizazi(uterus) na kinaweza kukaa mpaka miaka 10.
Typical use failure rate:0.8%
Picha.Google
Screenshot_20210915-121320_Chrome.jpg

KAMA UNA HALI ZIFUATAZO HUTOPASWA KUTUMIA HIVI VIFAA IUD
• Mimba au kuhisi una mimba
• PID pelvic inflammatory disease
• Uvimbe katika kuta za kizazi
• Kuvuja damu sehemu za siri bila kujua sababu.
• Suspected Cancer.

NJIA ZINAZOWEKA KIZUIZI(BARRIER METHODS)
08.DIAPHRAGM

Hivi huwekwa ndani ya uke kufunika shingo ya mlango wa kizazi(cervix) ili kuzuia mbegu za kiume kuingia.
Ina umbile la kikombe kidogo na huwekwa na chemikali zinazoweza kuua mbegu za kiume(spermicide)
Typical use failure rate: 17%
Picha.Google
20210915_120342.jpg

09.KONDOMU
Kondomu ni njia pekee ya uzazi wa mpango ambayo
inazuia vyote, mimba, magonjwa ya ngono ukiwemo
virusi vya ukimwi. Zinazuia shahawa za mwanaume
kuingia kwenye uke wa mwanamke.
Typical use failure rate: 13%
Usitumie kondomu na mafuta ya kulainisha au chochote ,husababisha Kondomu kuchanika kirahisi.
Picha:Google
20210915_120311.jpg

NJIA ZA ASILI ZA UZAZI WA MPANGO
Hizi huusisha kujua siku ambazo mwanamke anaweza pata mimba ili aongeze umakini au kuepuka ngono katika siku hizo.
Ubaya wake: Mabadiliko ya siku za hedhi hufanya njia hii kuwa hatari.
Na hizi ni pamoja na;

• CALENDAR METHOD
Njia hii ni nzuri na ni njia pendwa zaidi miongoni mwa watu kwasababu haihusishi maumivu ya aina yoyote wala chemikali ila inapaswa kutumika kwa tahadhari.
Itumike ikiwa tu mzunguko wa mwanamke unaenda vizuri(regular) na sio usioeleweka,Tofauti na hapo unaweza pelekea ujauzito na tumeona wengi waliotumia njia hii wakapata mimba.

KUMWAGA NJE(WITHDRAWING)
Njia hii ina ufanisi mdogo kufananisha na njia nyingine kwasababu ni kweli unaweza ukafanikiwa vizuri kabisa kumwagia nje lakini kuna mbegu zinaweza kubaki katika kichwa cha uume na kwa asilimia fulani zikawa sababu ya mimba.
Wakati gani?. Pale ambapo mwanaume anahisi anaelekea kumwaga shahawa(ejaculation).
Na baada ya kumwaga nje kabla hajaendelea na tendo ahakikishe amesafisha vizuri uume wake au akojoe kwasababu mkojo una tindikali(acid) mbegu za kiume hufa.
Screenshot_20210916-215151_Chrome.jpg

Lactation amenorrhea method (LAM)
Kwa wanawake ambao wametoka kupata mtoto na wananyonyesha hii njia ya LAM_lactation amenorrhea method inaweza kutumika ikiwa ana vifu vifuatavyo a) Hapati siku zake za hedhi b)ananyonyesha c) chini ya miezi sita baada ya kujifungua.
Hii ni nia ya muda mfupi na inapaswa itumike ikiwa mwanamke ana hizo hali tatu tajwa hapo juu.

NJIA ZA MUDA MREFU (MOJA KWA MOJA)
12.FEMALE STERILIZATION (TUBAL LIGATION OR TYING TUBES).

Mirija ya mwanamke ya falopiani inaweza kufungwa ili kuzuia yai na mbegu za kiume kukutana kwaajili ya urutubishaji.Hii inaweza fanywa hospitalini tu
Typical use failure rate: 0.5%
Picha.Google
Screenshot_20210915-121723_Chrome.jpg

13.MALE STERILIZATION _ VASECTOMY
Hii hufanyika kuzuia mbegu za kiume kuufikia uume,hivyo manii ya mwanaume haitokuwa na seli hai za kiume za kuweza kurutubisha yai.
Typical use failure rate: 0.5%
Picha:Google
Screenshot_20210915-121947_Chrome.jpg

NJIA ZINAZOTUMIKA WAKATI WA DHARULA
Njia za wakati wa dharula sio njia zinazopaswa kutumika kila siku kama njia za uzazi wa mpango.Hii hutumika ikiwa wakati wa tendo la ndoa hakuna nia yoyote ya uzazi wa mpango iliyotumika au njia iliyotumika ilishindwa kukidhi vigezo mfano Kondomu kuchanika.

Copper IUD__ Wanawake wanaweza kuwekewa Copper IUD baada ya kufanya ngono zembe ndani ya siku tano.

MORNING AFTER PILL (P2)
Screenshot_20210915-122215_Chrome.jpg

Hii huwa na dozi kubwa ya mchanganyiko wa homoni ya estrogen na progestin au progestin tu.
Hutumika ndani ya masaa 72 ya kufanya ngono zembe. Uwezekano wa kufanya kazi vizuri zaidi huongezeka ikitumiwa mapema zaidi.
• Hakuna madhara ya muda mrefu ambayo mpaka sasa yamegunduliwa yatokanayo ya matumizi ya P2.
• Ikumbukwe kuwa P2 haipaswi kufanywa kuwa mbadala wa njia nyingine za uzazi.
• Mtu aliye na uzito mkubwa P2 inaweza isifanye kazi vizuri kuliko kwa aliye na uzito wa kawaida.
• P2 sio uhakikisho 100% kuwa hutopata mimba ,inafanya kazi 87% na ikiwa hujapata kuona siku zako kwa zaidi ya wiki moja,unashauriwa kufanya kipimo cha mimba.
ATHARI AMBAZO UNAWEZA PATA KWA KUTUMIA P2,hizi huwa ni za siku chache tu.
• Kichefu chefu au kutapika
• Kizungu zungu
• Kichwa kuuma
• Uchovu
• Matiti kujaa
• Maumivu chini ya kitovu
• Mzunguko wa hedhi kuvurugika

Asante kwa kutumia muda wako kusoma.
 
Una washauri vipi ambao wapo addicted na P2 na hawawezi acha?
Kuna watu wanatumia P2 wakidhani ndyo njia pekee ya kuzuia mimba,wengi hawajui njia nyingine za kuzuia mimba.
Kwanza ,anapaswa kufahamu kuwa P2 ilitengenezwa kwaajili ya nyakati za dharula tu na sio mbadala wa njia nyingine.
Pili, P2 ina dose kubwa sana ya mchanganyiko wa homoni tofauti na dawa nyingine hivyo kwa mtumiaji wa mara kwa mara ,ni hakika kuwa hatokuwa na mzunguko unaojulikana.
Yote katika yote ni swala la yeye kupima faida na hasara kisha afanye maamuzi
 
Hello ,Mimi ni daktari mafunzoni ,karibu katika uzi wangu.

Punde tu baada ya wapenzi wawili kukutana kimwili wengi wazo la kwanza kuja kichwani ikiwa hawajapanga kuwa na mtoto huwa ni P2(morning after pill),haijalishi wanakutana mara ngapi,kila wakutanapo ni P2 tu.
Hivi hizi ni kanakwamba hazina madhara?
Au Pipi kifua?
Sasa ni zipi njia bora zaidi za kuzuia mimba zisiyotarajiwa pamoja na njia ya kalenda au P2 ambazo ni maarufu zaidi miongoni mwa watu?

Ninakuletea njia 15 za kisayansi zinazoweza kutumika kuzuia mimba(uzazi wa mpango) pamoja na faida na hasara kwa kila njia pendekezwa,pamoja na mapendekezo yangu binafsi kama mdau wa afya.

Uzazi wa mpango ni nini?
• Wapenzi wawili wanapokaa
kujadili na kuamua idadi ya watoto ambao wangependa kuwa nao na kwa wakati gani,ili wapewe mapenzi ya kutosha,matunzo na elimu bora kwa kila mtoto
• Kupanga idadi na wakati wa kuwa na watoto ni jukumu la wote wawili ,sio tu mwanaume au mwanamke tu.
Ni njia zipi za kuzuia mimba (Contraception)?

Zipo njia mbali mbali kulingana na malengo ya wapenzi, malengo yanaweza kuwa;
• Kuchelewesha mimba ya kwanza
• Kuacha muda kati ya mimba na mimba nyingine
• Kupunguza ukubwa wa familia

CATEGORIA ZA NJIA ZA KUZUIA MIMBA
1.Pharmacological and Non pharmacological
2.Short acting and Long acting contraceptives
3.Reversible and Non reversible techniques

SIFA ZA NJIA NZURI ZA KUZUIA MIMBA
1.Ni salama
2.Ifanye kazi kwa 100%
3.Free/ minimum side effects
4.Affordable
5.Acceptable to the user
6.Free of effects on future pregnancies

NJIA ZA UZAZI WA MPANGO ZINAZOTUMIA HOMONI
01.KIPANDIKIZI(IMPLANT)

Kipandikizi ni kibomba kidogo (chenye urefu wa milimita nne) ambacho huingizwa chini ya ngozi ya mkono wa mwanamke. Hutua homoni ambazo hulizuia yai la mwanamke kupevuka na kukuepusha kupata mimba.
Kipandikizi hiki kinauwezo wa kukaa kwa miaka minne lakini hakitakuzuia kupata/kuambukizwa magonjwa ya ngono.
Typical use failure rate: 0.1%
Picha:Google
View attachment 1938565

02.VIDONGE
Vidonge vya uzazi wa mpango ambavyo hutumiwa na mwanamke huwa na homoni ambazo hukuepusha kupata mimba kwa kuzuia yai la mwanamke kutokupevuka na hivi hutumiwa kila siku muda ule ule.Hivi sio sawa na P2.
Vidonge vya uzazi wa mpango havizuii maambukizi ya magonjwa ya ngono.
Typical use failure rate: 7%
Picha:Google
View attachment 1938567

03.SINDANO
Sindano nikama vidonge na kipandikizi – Huzuia yai la mwanamke kupevuka kwa kutumia homoni,hukuzuia kupata mimba na hii huchomwa matakoni au mkononi kila baada ya miezi mitatu. Njia hizi hazitakuzuia kupata/kuambukizwa magonjwa ya ngono.
Typical use failure rate: 4%.
Picha: Google
View attachment 1938570

FAIDA
• Hufanya kazi kwa muda mrefu.
• Hazina athari katika uzalishaji wa maziwa kwa mama
• Uwezekano mdogo sana kupata upungufu wa madini chuma
HASARA
• Hedhi huvurugika
• Kushindwa kuzalisha mayai kwa muda fulani hata baada ya kuacha kutumia sindano.
• Kwa watumiaji wa muda mrefu wa medroxyprogesterone,mifupa kungua uzito ni tatizo.

04.Patch
Patch hubandikwa sehemu za chini ya tumbo,matakoni na sehemu za juu za mwili pia(lakini sio kwenye matiti).Hii ni mpaka ipendekezwe na daktari.
Hufanya kazi kwa kutoa homoni kwenda kwenye damu kama njia ya vidonge na sindano.Unabandika Patch mpya mara moja kwa wiki ndani ya wiki tatu na wiki ya nne haubandiki patch ili upate siku zako.
Typical use failure rate: 7%.
Picha:Google
View attachment 1938575

05.Hormonal vaginal contraceptive ring.
Hii ringi hutoa homoni kama njia nyingine,huwekwa ndani ya uke na huvaliwa kwa wiki tatu na wiki ya nne hutolewa ili kuruhusu hedhi kisha unavaa ringi mpya.
Typical use failure rate: 7%
Picha.Google
View attachment 1938581

INTRAUTERINE DEVICES ( Vifaa vinavyopachikwa kwenye kuta za kizazi)
06.LEVONOGESTREL DEVICE (MIRENA)
Hiki kifaa huachia Levonogestrel kwenye kizazi(uterus).
Picha.Google
View attachment 1938582

07.Copper T intrauterine device
Ni kifaa kidogo ambacho hufanana na umbile la herufi T huwekwa katika kuta za kizazi(uterus) na kinaweza kukaa mpaka miaka 10.
Typical use failure rate:0.8%
Picha.Google
View attachment 1938587
KAMA UNA HALI ZIFUATAZO HUTOPASWA KUTUMIA HIVI VIFAA IUD
• Mimba au kuhisi una mimba
• PID pelvic inflammatory disease
• Uvimbe katika kuta za kizazi
• Kuvuja damu sehemu za siri bila kujua sababu.
• Suspected Cancer.

NJIA ZINAZOWEKA KIZUIZI(BARRIER METHODS)
08.DIAPHRAGM

Hivi huwekwa ndani ya uke kufunika shingo ya mlango wa kizazi(cervix) ili kuzuia mbegu za kiume kuingia.
Ina umbile la kikombe kidogo na huwekwa na chemikali zinazoweza kuua mbegu za kiume(spermicide)
Typical use failure rate: 17%
Picha.Google
View attachment 1938596
09.KONDOMU
Kondomu ni njia pekee ya uzazi wa mpango ambayo
inazuia vyote, mimba, magonjwa ya ngono ukiwemo
virusi vya ukimwi. Zinazuia shahawa za mwanaume
kuingia kwenye uke wa mwanamke.
Typical use failure rate: 13%
Usitumie kondomu na mafuta ya kulainisha au chochote ,husababisha Kondomu kuchanika kirahisi.
Picha:Google
View attachment 1938597
NJIA ZA ASILI ZA UZAZI WA MPANGO
Hizi huusisha kujua siku ambazo mwanamke anaweza pata mimba ili aongeze umakini au kuepuka ngono katika siku hizo.
Ubaya wake: Mabadiliko ya siku za hedhi hufanya njia hii kuwa hatari.
Na hizi ni pamoja na;
• Calendar method
• Kumwagia nje(withdrawing
• Lactation amenorrhea method (LAM)
Kwa wanawake ambao wametoka kupata mtoto na wananyonyesha hii njia ya LAM_lactation amenorrhea method inaweza kutumika ikiwa ana vifu vifuatavyo a) Hapati siku zake za hedhi b)ananyonyesha c) chini ya miezi sita baada ya kujifungua.
Hii ni nia ya muda mfupi na inapaswa itumike ikiwa mwanamke ana hizo hali tatu tajwa hapo juu.

NJIA ZA MUDA MREFU (MOJA KWA MOJA)
12.FEMALE STERILIZATION (TUBAL LIGATION OR TYING TUBES).

Mirija ya mwanamke ya falopiani inaweza kufungwa ili kuzuia yai na mbegu za kiume kukutana kwaajili ya urutubishaji.Hii inaweza fanywa hospitalini tu
Typical use failure rate: 0.5%
Picha.Google
View attachment 1938598
13.MALE STERILIZATION _ VASECTOMY
Hii hufanyika kuzuia mbegu za kiume kuufikia uume,hivyo manii ya mwanaume haitokuwa na seli hai za kiume za kuweza kurutubisha yai.
Typical use failure rate: 0.5%
Picha:Google
View attachment 1938602

NJIA ZINAZOTUMIKA WAKATI WA DHARULA
Njia za wakati wa dharula sio njia zinazopaswa kutumika kila siku kama njia za uzazi wa mpango.Hii hutumika ikiwa wakati wa tendo la ndoa hakuna nia yoyote ya uzazi wa mpango iliyotumika au njia iliyotumika ilishindwa kukidhi vigezo mfano Kondomu kuchanika.

Copper IUD__ Wanawake wanaweza kuwekewa Copper IUD baada ya kufanya ngono zembe ndani ya siku tano.

MORNING AFTER PILL (P2)
View attachment 1938605

Hii huwa na dozi kubwa ya mchanganyiko wa homoni ya estrogen na progestin au progestin tu.
Hutumika ndani ya masaa 72 ya kufanya ngono zembe. Uwezekano wa kufanya kazi vizuri zaidi huongezeka ikitumiwa mapema zaidi.
• Hakuna madhara ya muda mrefu ambayo mpaka sasa yamegunduliwa yatokanayo ya matumizi ya P2.
• Ikumbukwe kuwa P2 haipaswi kufanywa kuwa mbadala wa njia nyingine za uzazi.
• Mtu aliye na uzito mkubwa P2 inaweza isifanye kazi vizuri kuliko kwa aliye na uzito wa kawaida.
• P2 sio uhakikisho 100% kuwa hutopata mimba ,inafanya kazi 87% na ikiwa hujapata kuona siku zako kwa zaidi ya wiki moja,unashauriwa kufanya kipimo cha mimba.
ATHARI AMBAZO UNAWEZA PATA KWA KUTUMIA P2,hizi huwa ni za siku chache tu.
• Kichefu chefu au kutapika
• Kizungu zungu
• Kichwa kuuma
• Uchovu
• Matiti kujaa
• Maumivu chini ya kitovu
• Mzunguko wa hedhi kuvurugika

Asante kwa kutumia muda wako kusoma
NAKUOMBA USIACHE KUNIPIGIA KURA
Mkuu umetumia lugha ya kitaalam mno, andiko lako lingetumia lugha rahisi, yaan ungekuja na njia ya kufikisha ujumbe kwa njia rahisi, uliyoyasema Wala hayana upya, ila ungeyaweka kwenye lugha ya jamii isiyo ya kufundishia ungeeleweka vzr..

Ukiweza fanya editing..
 
Sehemu nilizo tumia English, zilikuwa ni bora ikae english kwasababu kiswahili chake kinge changanya zaidi.
 
Back
Top Bottom