Dkt. Mollel: Matumizi holela ya vidonge ya P2 ni hatari kwa afya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewataka wananchi kuepuka matumizi yasiyo sahihi ya vidonge vya kuzuia mimba maarufu kama P2 ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza pale dawa hizo zinapotumika bila utaratibu ikiwemo mvurugiko wa hedhi.

Dkt. Mollel amesema hayo leo Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati akijibu swali Namba 163 ambapo swali hilo limeulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Dkt. Thea Medard Ntara aliyeuliza Je, kuna mpango gani wa kuruhusu Sayana Press kama njia ya Uzazi wa Mpango badala ya kutumia P2 bila utaratibu.

Amesema P2 ni njia ya dharura ya vidonge vya uzazi wa mpango ambayo hutumika kuzuia mimba kwa mwanamke aliyefanya tendo la kujamiiana bila kinga kwa mfano aliyebakwa au ametumia kondomu ikapasuka na anadhani anaweza kupata mimba asiyoitarajia wakati Sayana Press ni njia ya kuzuia kupata ujauzito kwa muda mrefu, hivyo matumizi ya kuzuia mimba kwa Sayana Press na P2 ni tofauti.

Hata hivyo Dkt. Mollel ameongeza kuwa Sayana Press imesajiliwa na TMDA na inapatikana kwenye vituo binafsi vya kutolea huduma za afya kwa wateja wanaohitaji.
 
Hakunaga hata vya maana wanafanya hapo, mara mia hata wangekua wanafanyia vikao vyao kwenye madarasa ya shule za msingi posho iwe ugali nyama na sukuma week..

Jkitizama akil za wale watu unaona kabisaa kama nchi tumekwama vibaya sana.
WAGANGA NJAA TU WOTE WALEE hawana hadhi hata ya kuitwa watunga sheria. Ni wachumia tumbo tu na wajasiriamalia
 
Sasa kweli mbunge kama babu Tale unategemea nini?
 
Bunge huwa linaundwa na watu waliochaguliwa na wananchi kuwawakilisha.

Hao wahuni waliogawiwa kura, na wengine kutangazwa kuwa ni wabunge na hao mashetani wanaoitwa wakurugenzi kuwa eti wamepita kupingwa, hawana hadhi ya kusikilizwa wala kufuatiliwa na mtu yeyote mwenye akili timamu, anayejua maana ya bunge au mtu yeyote anayejali haki.

Mijadala yao ni sawa tu walevi waliokutana kilabuni, mwisho wa kusikilizwa huwa ni walevi wenzao waliopo hapo kilabuni.

Value your time, never waste your valuable time to listen crooks.
 
Hakunaga hata vya maana wanafanya hapo, mara mia hata wangekua wanafanyia vikao vyao kwenye madarasa ya shule za msingi posho iwe ugali nyama na sukuma week..

Jkitizama akil za wale watu unaona kabisaa kama nchi tumekwama vibaya sana.
WAGANGA NJAA TU WOTE WALEE hawana hadhi hata ya kuitwa watunga sheria. Ni wachumia tumbo tu na wajasiriamalia
Umesema kweli kabisa!
 
Back
Top Bottom