Madereva wa Mwendokasi wengi wana msongo wa mawazo. Waziri kaa na hawa watu uwasikilize itapunguza kuharibu magari

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,105
JPM alipoona Mwendokasi Madereva wanadai maslahi alikwenda kuchukua vijana serikalini na JKT akawapa kazi za ulinzi, kukata tiketi,ufundi na udereva. Walioletwa kwa sababu wanawekwa bila sifa wameendelea kujifunza kazi taratibu lakini wakiwa na msongo mkubwa wa mawazo kuhusu lini watapata nafasi ya kulalamika na kutema nyongo?

Hali hiyo ya msongo wa mawazo imekuwa kubwa kiasi kwamba wakaazi wa DAR wanadai hawa jamaa wanaweza kusimamisha gari kituo likiwa limejaa na wakapakia abiria hata kupitia milango isiyotakiwa bila kujali usalama wao.

Leo nimeona pia Dreva mmoja mwenye msongo wa mawazo clip inasambaa ikionyesha alivyovuka vituo bila kusimama huku akiendesha kama vile kabeba magunia.

Kampuni hii ina garage lakini sidhani kama tumewahi kuona tangazo la kutaka kuajiri mafundi.....jiulize mafundi wa kampuni wanapatikanaje? Lakini pia jiulize garage ya kampuni kubwa kama hii ipo wapi? Jiulize kwanini magari yaliyopaki ni mengi kuliko yanayotembea? Usalama wa abiria upo wapi kama hali ipo hivi? Tunasubiri hawa madereva waue abiria ndipo tujirekebishe?

Mhe. Mchengelwa kabla yakusubiri kuletewa mwekezaji na magari mapya pls zungumza na hawa wachache waliopo wakushauri ili unapokwenda kukabidhi Mradi kwa wawekezaji binafsi ujue mikataba iwe na terms gani.

Lakini pia kaa na hawa ndugu uwaulize kama bado wangetamani kufanya kazi na Mradi huu au wapo tayari kurudi kwenye ofisi zao za awali uajiri watu wenye shida na kazi? Haiwezekani watu wanatafuta kazi then Dreva anatishia abiria kwamba wafanye wafanyavyo hiyo siyo ajira yake.

Nakusalimuni

Pia soma
- Dereva wa Basi la Mwendokasi adaiwa kuwapitiliza Vituo Abiria baada ya kukasirishwa
 
Yale magariii yanaishaa yote mkuu we unahisi zile machine mbovu hakuna juu wana enjoy mnaishia kulia na familia zenu nw waanasimamia show wenyewe oyaaa ngapizimepita huko kadhaa mnagawana.

likewise magari zoezi gumu sana wawajaliwale ndugu
 
Maboresho yanayotakiwa kufanyika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka Bus rapid transit (BRT) jijini Dar es Salaam.

Nimebaini changamoto kadhaa zinazotakiwa kutatuliwa katika mradi huu.

Hivyo nimemshauri juu ya maboresho yanayotakiwa kufanywa katika mradi huu. Pitia katika link hii kusoma ushauri wote: Kwako Mkurugenzi mpya wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART): Katatue changamoto zifuatazo….

Pia michango mbalimbali imetolewa na wadau wengine na wameshauri jinsi ambavyo mfumo wa uendeshaji wa haya mabasi unapaswa kuwa ili kwendana na ukuaji wa teknolojia:

Ushauri wote tumeuandika hapa: Kwako Mkurugenzi mpya wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART): Katatue changamoto zifuatazo….
 
Back
Top Bottom