DOKEZO MWENDOKASI: Madereva na watumishi wanavyopakiza ndugu zao nje ya utaratibu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Hjalte

Member
Oct 20, 2023
25
100
Kumekuwa na tabia ya hovyo sana inayofanywa na madereva pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mabasi ya Mwendokasi, hasa katika vituo vikuu vya Kivukoni na Gerezani nyakati za jioni ambapo foleni ya watu inakuwa ni ndefu, lakini baadhi ya madereva hubakiza/kuingiza baadhi ya rafiki, ndugu na jamaa zao ndani ya mabasi nje ya utaratibu hata pale walipotakiwa kushuka ili wapange foleni na kukaguliwa tiketi (Kwa wanaoenda Mbezi),na kupanga foleni kama utaratibu ulivyo.

Unakuta gari kabla haijapakia abiria walio kwenye mstari tena kwa muda mrefu,tayari ina abiria 8 hadi 10 walio ndani ya gari na hawajakaguliwa tiketi.

Katika hali nyingine ya kushangaza na ya kibaguzi,ni kwamba baadhi ya watumishi katika vituo vya mabasi haya huwapitisha ndugu,jamaa,na marafiki zao kupandia gari ndani kupitia mlango wa kushoto ambao ni maksusi kushusha tu,na wanaopanda kwa utaratibu wa foleni hutumia mlango wa kulia.

Vitendo hivi vinaondoa usawa na kuleta ubaguzi kwa wasio na ndugu wanaofanya kazi UDART,kwani wanakaa kwenye foleni muda mrefu,lakini kuna watu wanafika na kuondoka ndani ya muda mchache tena wakiwawamekaa kwenye seat.

IMG_20240122_181940_289.jpg
IMG_20240122_181716_870.jpg
IMG_20240122_182424_856.jpg
IMG_20240122_182023_034.jpg
 

Attachments

  • IMG_20240122_182424_856.jpg
    IMG_20240122_182424_856.jpg
    57.1 KB · Views: 5
  • IMG_20240122_182023_034.jpg
    IMG_20240122_182023_034.jpg
    56.9 KB · Views: 2
  • IMG_20240122_182023_034.jpg
    IMG_20240122_182023_034.jpg
    56.9 KB · Views: 6
acha kupanic kwa mambo madogo madogo kama hivi haya mambo yapo katika taasisi zote hospital, TRA, Bandarini, Mashuleni. I bet hata wewe ungekuwa na nafasi sehemu huwezi acha damu tako iteseke.

siungi mkono lakini
Daah kweli juzi juzi nilienda Muhimbili nimekaa foleni karibu masaa matatu alafu kaja Mtu tunaona anapitishwa tu daah iliniuma kimtindo
 
usafiri huo ulishakuwa maji taka siku nyingiiii yani kimsingi nunua gari tu maana ukikimbilia kwenye daladala ndiobalaa kabisaaaaa Bongo hamna kitu kinakwenda smoothly
 
Mmh Africa hatari San, mtu anatetea usawa na haki lakin anaonekana snitch...ivi Africa matendo haya mnaona ya kawaida kweli, mtu kunyimwa haki yko
sio ivo wewe embu assume kama wewe ndio dereva wa mwendokasi ....acha kujifanya kondoo wakati umevaa ngozi ya chui wewe
 
Sasa kila mtu akileta undugu na urafiki ktk sehem za kazi unadhan taifa litakuaje,,.haya masuala usichukulie poa Mzee.jaribu
jaribu ku prove mkuu we chunguza tu katika hata sekta binafsi au makampuni izi mambo zipo sana na ndio moja wapo ya vitu vinavyosababisha nchi hii kuonekana ya ovyo sana ukiachana na rushwa,uwajibikaji mbovu wa viongozi na sisi tunaishi nao ivo ivo tu
 
kwa iyo we shida yako nini aswa? vp wewe ndio wangekua ndugu zako ingekuwaje? na sio mwendokasi tu ata uko sehemu nyingine TRA,TPA,TAA favourtism lazima iwepo mzee
Shida yake,hana mwenyeji UDART! Na yeye anatamani. Au kama vipi ajenge urafiki nae awe anapitishwa
 
kwa iyo we shida yako nini aswa? vp wewe ndio wangekua ndugu zako ingekuwaje? na sio mwendokasi tu ata uko sehemu nyingine TRA,TPA,TAA favourtism lazima iwepo mzee
Kwa vile TRA,TPA,TAA wanafanya inahalalisha jambo hili la kufanya mambo bila utaratibu?
Tujifunzeni basi kujenga hoja wakuu!
Mimi nimeweka ushahidi wa picha hapo,na wewe tafuta ushahidi huko TRA piga kelele ili tukomeshe huu ujinga
 
Back
Top Bottom