Tume ya Katiba
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,896
- 1,866
Taaluma inapochanganywa na siasa mbaya sana!
Madaktari kugomea kutibu wagonjwa ni sawa na uuaji. Hawa ni wauaji tu. Nawaomba wajifunze kuhusu ulimboka: Je kama Ulimboka asingetibiwa angepona? Na wagonjwa ni hivyo wajue kuwa wameua watu wengi sana. Wameua sana
We vipi? Tuje tukupe kichapo heavy halafu upelekwe hospitali ukute kuna mgomo usitibiwe we utajisikiaje? Au umeugua serious ukakimbizwa hospital ukakuta mgomo we hali hiyo unaichukuliaje? Unajua kushabikia mgomo kunasababishwa na kuwa na afya njema? Ungekuwa mgonjwa umelazwa halafu hupati huduma yoyote! Jamani,madai yao ya vifaa ni sahihi lakini mgomo hapana! Kwani tusio na uwezo wa kwenda private ndio tunaoumia! Hili sio suala la kushabikia hata kidogo.
Umeichoka amani wewe unataka machafuko amia basi kwenye hizop nchi ulizozitaja.
Matatizo ya madakatri ni
1. wanafikiri wana akili nyingi kuliko watu wengine. Hawajui kuwa kufaulu mtihani siyo kipimo pekee cha akili
2. wanatumia mbinu za kishule kutatua migogoro ya kikazi. Hawatambui kuwa migogoro ya shule na kazini ni vitu viwili tofauti.
3. Viongozi wao wamejipa hati miliki ya kufanya maamuzi yote.
Nina uhakika madaktari wengi tu hawaungi mkono maamuzi, ila wakijaribu kusema wanafungwa mdomo kwa kutumia intimidations za namna mbalimbali.
hata kichaa husema /Hakika umesema
amani inahusikaje hapa?!machafuko yamekujaje hapa? huu ndio wimbo tuliokaririshwa Amani, amani..amani..halafu unakufa kwa magonjwa yanayoweza kutibika kabisa ila unashindwa kusimamia eti unalinda amani!!! aliyekukaririsha huo wimbo hajui hizo shida!!
na suala la kwenda nje..ni kutokana na kukatishwa tamaa tu, wapo wengi tu wapo hospitali binafsi..yaani ratio ya daktari mmoja kwa zaidi ya wananchi 35,000 na serikali yako inazidi kuzidisha upungufu kwa kufukuza wengine na wewe unasema hiyo ni amani?! kweli upeo wetu ni mkubwa kweli!!
labda babako mzazi....katibie kwanza hormone imbalance inayokusumbua..
Madaktari wa Tanzania wanagoma wanawaacha wagonjwa wakikata roho ili walipe maslahi yao...kama kazi ya udakatari aina maslahi badili kazi ingia kwenye siasa.
Yataka ujasiri! Sina hakika kama wote mko pamoja kiasi hicho " hatuko huru ila tuna nidham ya uwoga.
Asante mtaalam kwa uchambuzi makini, inatia moyo tunao wataalam!
Tulikofikia hakuna mshindi, si serikali si wataalam wetu madaktari, si wananchi, si yeyote mpenda maendeleo na amani. Tulipofikia pia tutakosa rafiki wa kutusaidia iwe mawazo au hali.
ili kuwa katika hali salama, tunapaswa kuangalia mbele sana: Suala hili lisiwe la madaktari peke yao. Hili ni suala la taifa zima, linagusa maisha ya kila mtu anaeishi Tz, mwenyeji kwa mgeni. Nina maoni makuu mawili: 1. Wanasheria watupe upembuzi yakinifu juu ya haki ya afya na jinsi inavyopaswa kutolewa kufuatia TZ kuwa mwanachama wa WHO na wanachama wa mikataba mingine inayohusu haki ya afya na nyanja zake zote. Ndani ya baadhi ya hii mikataba kama ule wa haki za kitamaduni na uchumi (the Internationla covenant on economic and socila rights - 1966) ambamo haki ya kufanya kazi inaweza kuhusishwa na haki ya afya inatajwa; kifungu cha 7 cha mkataba huu kinahusu haki ya kufanya kazi na mazingira bora kazini; kifungu hiki kinazungumzia serikali zote wanachama ( TZ ilikuwa miongoni mwa wanachama wa kwanza kabisa kuridhia na kusaini mkataba huu wakati huo - 1966 - Mwl JKN akikabiliana na suala la kukopa kwa ajili ya huduma za jamii - elimu, afya nk.)
kifungu kinafafanua mazingira bora kuwa ni pamoja na mafao stahiki kwa kila aina ya kazi...hapa tujiulize kama mshahara wa dr ni stahiki yake ikilinganishwa na taaluma na sekta zigine ambazo hazizalishi lakini ni muhimu sana?? ...(7) (ii) kiwango cha maisha kinachoridhisha kwake na familia yake...decent living for them and their families....(b) safe and healthy working conditions...kifungu cha 8 kikitambua haki za wafanyakazi kuwa na vyama vyao kutetea na kusimimia masilahi yao...hiki kimeainishwa kwa upana sana...kifungu cha 12 kinawahusu madaktari zaidi kuwa serikali zote wanachama kutambua haki ya kila mtu kufurahia kiwango cha juu cha afya ya mwili na ubongo ( ...the right of everyone to the enjoyment of the highest attainable standard of physical and mental health...) 12(2) state should take steps to achieve "full realization" of this right...and this to inlcude the follwing:
reduction of stillbirth- rate....; (d) creation of conditions which would assure to all medical service and medical attention in the event of sickness....yaani haturuhusiwi kukubali hali ya mgonjwa kukosa huduma kama mwanachama wa mkataba huu....nk
TZ imeridhia mkataba huu bila reservation - bila maeneo ambayo tunadhani hatuwezi kuyakidhi.. na hata kama tungefanya hivyo...bado tungebanwa na vifungu vingine ambavyo vinaainisha wajibu wa serikali katika mfumo huu ambao ni kuhakikisha haki ya mgonjwa na ya dakatari, nurse na wengine inalindwa...
katika mfumo huu serikali inafanya kazi na madktari kupitia chama chao kujua njia sahihi za uendeshaji na usimamizi wa utaratibu huu; wanasheria wakisaidia kuweka mambo katika mtazamo wa haki na usalama wa pande zote: HAKUNA MSHINDI AU ANAYESHINDWA....
KATIKA hili tunakubaliana ( huu ni mchakato mkubwa wa kitaifa ukihusisha bunge nk)...kiasi cha pato la taifa na jinsi tunavyoligawa kwa nyanja mbali mbali...tukilindwa na sheria ya usawa usio bagua mtu au kundi hata katika mgawanyo wa mapato kwa njia ya mishahara....usawa na kutobaguliwa ( the principle of non discrimiantion and equality of all types) ni moja ya misingi mikuu ya umoja wa mataifa na wanachama wake wote - TZ ni mojawapo na mpaka tumetoa naibu Katibu Mkuu wa umoja huu - tuko mbele sana katika masuala haya...
katika mtazamo huu athari kwa raia wasioweza kulipia matibabu aghali inalindwa ...nia ikiwa kuhakikisha watu wote wanapata matibabu stahiki kwa kila ugonjwa - ikibidi mtu kutibiwa nje iwe ni kwa matakwa yake na uwezo wake - wengi wa hawa huwa wafanyabiashara wakubwa -
kwa hiyo kama kuna kesi mahakama yoyote itaangalia mambo haya na usawia wake na haki itaonekana kutendeka maana mahakama itasaidia pande zote: serikali kusimamia wajibu wake na madaktari kusimamia haki zilizo za msingi kwao. Wananchi tutafaidika na muafaka wa hawa wawili...mahakama na bunge vikiwa katikati....kuhakikisha uwiano sahihi wa masuala yote...
Maoni ya 2: yote ya juu yanawezekana tukikubali kusikilizana, kuzungumzana kama ambavyo mchakato ulikuwa umeanza...kwa hiyo ninawaomba madaktari wafanye kazi na wanasheria kuliweka hili katika mtazamo huu na kuhakikisha uratibu makini wakati wa majadiliano. pili katika hili ni kwa serikali kukubali kw mara nyingine kuzungumza na madaktari, pengine na wadau wengine - kubwa likiwa kuweka misingi itakayosimamia mustakabali wa nchi kwa namna ambayo inajengea maeleano katika masuala ya msingi.
Kufuata mikatba ya kimataifa na ya ndani kupitia katiba na sheria zingine...kuna mapana ambayo sijayaweka hapa ambayo serikali inayajua vizuri na ninaamini yakiletwa katika meza ya majadiliano yanaweza kuinua taifa letu kuliko kulididimiza kama inavyotaka kutokea sasa.
raia wa leo wanauwezo kujua mapana na wigo za majadiliano haya: mwisho wa siku wataona ni madaktari na serikali waliowasaliti na si mmoja kati yao!! Kwa hiyo pande hizi mbili zikae pamoja na kufikia muafaka wa namna sahihi ya kufikia muafaka katika hili...la sivyo kwetu raia sauti zetu zinalalama na kusema "....tumewakosea nini (serkali na madakatari) kutughilibu kiasi hili??? Mbona mnatuumiza??
ninaamini na kuomba kuwa hekima ya Mungu ipitayo zote itaongoza na kutangulia pande hizi mbili kufikia makubaliano. Tz tumetatua migogoro mingi ulimwenguni na tunaheshimika sana na majirani na watoka mbali - sasa ni wakati wa kujiganga na migogoro yetu ya ndani. isikilizeni sauti wa wanawake na watoto, wazee, wenye ulemavu wa aina nyingi, wenye mapenzi mema na nchi yetu. Tunawategemea, Tunategemea hekima yenu kulifikisha taifa mahali stahiki. AMINA.
Mkuu wangu Ndivyo Tulivyo na hakika ktk swala la CUF sidhani kama kuna mtu hapa haamini kwamba ni chama cha Kiislaam tena. Walisingiziwa wakaamini nasi tukaamini na sasa kimekuwa hivyo. Nachoogopa ni Chadema nao walisingiziwa baadhi yetu wakaamini na isije fikia nao wana Chadema wakaamini. Hivyo ndivyo Tulivyo ktk kuamini tunayoambiwa.Siku moja nilikuwa naongea na jamaa mmoja toka Ulaya, aliniuliza hivi "Hivi kwa nini Tanzania wananchi hawawezi kuungana kupinga dhuluma mnayotendewa na serikali yenu?" kweli nilikosa jibu sahihi, ila nilichomwambia "Serikali ya Tanzania inatumia udini na vyombo vya habari kudanganya wananchi"
- Dini inatumika pale ambapo inawezekana (Mfano CUF tuliambiwa ni cha kiislamu na walileta mavisu kuua wananchi, kumbe ni uongo, na hapo wakristu hawakukiunga mkono, na ikitokea CUF kaitisha umoja wowote basi atapata tu Islam kwa sababu christian watasema nyie wadini, na hapo umoja haupo, serikali itapeta.
- Vyombo vya habari vinatumika kukanusha yayoiandama serikali (mfano suala la Dr Ulimboka na madakitari kwa ujumla) hapo wananchi wanadanganywa eti hawa jamaa wanadai eti tuwalipe msharaha mkubwa (tena kwa kutaja kiasi ili na wenye mshahara mdogo wawaonee donge ili wawapinge, na hapo wananchi wanaaminishwa kuwa serikali imefanya juhudi ila madakitari ndiyo tatizo.
Madaktari wa Tanzania wanagoma wanawaacha wagonjwa wakikata roho ili walipe maslahi yao...kama kazi ya udakatari aina maslahi badili kazi ingia kwenye siasa.
wewe chokomaji nlishakwambia sili migongo mbona bado wanfuatilia?? powa tu ngoja nkakununulie dudu la mpingo ucheze nalo...labda babako mzazi....
Kenge,mbuz,bata mzinga,kuku we, Dagaa wabichi,kibua,nyani,ngedere,kuku la kizungu we unafugwa mawazo mpaka akili,s******e we.
Mkuu wangu Ndivyo Tulivyo na hakika ktk swala la CUF sidhani kama kuna mtu hapa haamini kwamba ni chama cha Kiislaam tena. Walisingiziwa wakaamini nasi tukaamini na sasa kimekuwa hivyo. Nachoogopa ni Chadema nao walisingiziwa baadhi yetu wakaamini na isije fikia nao wana Chadema wakaamini. Hivyo ndivyo Tulivyo ktk kuamini tunayoambiwa.
Lakini pamoja na yote haya ni vizuri kufahamu kwamba kila kitu kina sababu zake..Wazanzibar wamegombania saana kile wanachoamini ni haki yao lakini wamepuuzwa kwa miaka hadi imefikia watu kuunda UAMSHO chombo ambacho kinachukua maamuzi ya kuchoma makanisa kama silaha ya kuishinikiza serikali. Madaktari nao wamegoma kama njia ya kuishinikiza serikali isifuate matakwa yao..
Jamani, jamani ni muhimu sana kuelewa who we a dealing with. Ni serikali dhalimu isioyojali hata wafe wananchi wote as long as they stay in power hawatajali kitu. Kati ya sinema nazozipenda sana ni ile ya The Usual Suspect, mkanda huu upo ktk list ya sinema zenye ujumbe mkubwa sana kuhusu uwezo wa binadamu. Katika sinema hii kuna mtu anaitwa Kaizer Soze huyu jamaa aliwekwa kati na majambazi waliomsihka mwanaye na mama yake mzazi ambaye ni mkewe kama Hostage, ili afanye wanavyotaka wao. Kaizer Soze kwa kuwaonyesha hao jamaa nani mwanamme (jasiri) aliwaua mwanaye na mama yake (mkewe) yeye mwenyewe mbele yao na kisha kuwaambia sasa ni imabakia vita baina yake na wao..
Angalia hekima ya sinema hii, unaweza kuona kwa nini Kaizer Soze asikubali matwaka ya hao jamaa lakini on the other hand kwa nini wale watu wawachukue mwanaye na mkewe kama Hostages?...Hivyo, makosa hayawezi kuondolewa na makosa mengine tunajiongezea machungu. Madaktari, mna kila sababu ya ktk madai yenu na ya msingi sana tu isipokuwa maandalizi na maamuzi mlofikia haya ndio tunayoshindwa kuafikiana nayo. Wote tunajua udhaifu wa serikali hii na nadhani zipo njia znzuri zaidi za kupambana nayo..Ni sisi wote kuungana hasa Watumishi wa Umma bila kubagua na kufanya maandamano ni migomo kwa silimia isiyozidi 40..
Tunajua serikali haitatishika sana kutokana na kwamba kuna watu wengi sana hawana kazi leo na wanasubiri nafasi kama hizi kuonyesha Unafiki wao lakini pia wananchi kwa umoja wetu tunaweza kabisa kuishinikiza serikali kupunguza matumizi yake yote ya anasa toka Bungeni, mahakama na serikali maana hakuna sababu kabisa kwa serikali kutumia fungu kubwa la bajeti kwa matumizi ya kawaida ambayo hayahusu utoaji huduma kwa wananchi moja kwa moja. Tupigeni vita sote kwa pamoja matumizi mabaya ya serikali na tuiadhibu serikali maana hili sio swala la Chadema CUF au TLP..