Madaktari wenzangu: Only "Mass resignation" itawaamsha watawala!

Madaktari wenzangu: Only "Mass resignation" itawaamsha watawala!

Mambo vp wana JF?
Mimi naungana mkono kabisa na maDr. lakini siku nyingi tokea ule mgomo wa kwanza mimi nilikuwa nasema kama madai na kuboresha basi na sisi professional nyingine wangetushirikisha basi. Mimi nauhakika kabisa huu mgomo ungechukuwa wiki moja tu serikali ingekuwa imeshakaa sawa.

Wewe fikiria tu kusewe na maDr. ,nurses, wahudumu wote hadi motuary ,EMD's hadi kwa wakina mama wajawazito, nchi nzima mimi nakwambia ungechukua siku 2 hadi wiki tu. sisi wanasayansi hatuna maneno mengi sisi ni vitendo tu.

Sasa unashangaa maDr bado hawataki kuwahusisha hata manurse tu ndio maana mgomo unakuwa mgumu coz wagonjwa wardini wanachopewa kule ni care tu. Kwahiyo hospitali sio madokta tu jamani.

Nawasilisha hoja.
Hakuna cha ubaguzi wala nini kwani kinachowasumbua nyie niwoga. Maana utakuta nurse wodini anajifanya daktari kuprescribe dawa km mnaujasiri si mngekuwa mmeshaunga mkono siku nyingi. Mmezoea kufaidika kwa nguvu za wenzenu hebu kumbukeni mwaka 2005 maDr wasingegoma hata hiyo mishahara mnayoipata sasa mngeipata wapi? Acheni unafiki.
 
Mtu alizaliwa siku moja na atakufa siku moja. Mass resignation ndio suluhu la ukweli kwani tumeshazoea kuwaona wakitoa takwimu ambazo sio sahihi na wakitaka jamii iwe upande wao, Sasa Madaktari wekeni mambo hadharani wao wanamwaga ugali nyie mwageni mboga, aliye juu umfuate huko huko kwani mshawasubiri kwa miaka mingi kwa ahadi hewa za kutosha sasa ni wakati wautekelezaji.

Kukiwa kweli na Mass Resignation hawana jeuri ya kukubali watu woote waache kazi, walitaraji madaktari toka Iran nako kimeshanuka kwa meli zao kupeperusha bendera yetu na jamii ya kimataifa wanaitazama Tanzania kuliko wakati mwingine wowote
 
serikali ifunge vituo binafsi vyote ambavyo vinamilikiwa na madaktar wanaofanyakazi serikalini na kuhamasisha migomo.
 
Ni unafiki mtupu huo, kila fani ya Afya ina chama chake mbona havijataka kuiunga mkono MAT. Wamezoea madaktari wajenge hoja ili wafaidike wote.
 
Hakuna cha ubaguzi wala nini kwani kinachowasumbua nyie niwoga. Maana utakuta nurse wodini anajifanya daktari kuprescribe dawa km mnaujasiri si mngekuwa mmeshaunga mkono siku nyingi. Mmezoea kufaidika kwa nguvu za wenzenu hebu kumbukeni mwaka 2005 maDr wasingegoma hata hiyo mishahara mnayoipata sasa mngeipata wapi? Acheni unafiki.

Bwanamdogo unachekesha sana, ndio maana manesi wametulia kutokana na maneno kama hayo. wewe unadhani chumba cha upasuaji dokta anaweza kufanya mwenyewe? lakini bila madokta huduma zimeendelea mawodini. tunaishi na kufanya kazi kwa kutegemeana kama Mungu alivyoona hatujakamilika akatuletea hawa kutukamilisha sisi abamu.
 
dah! nawaunga mkono madrs ........maana hata wapigania uhuru hawakujari idadi gani ya watu walikufu katika vita bali wali songa mbele, najua ni kweli ndugu zete wanakufa kwa kukosa huduma. Ila watakuwa wengi zaidi kama huduma hazita boreshwa kwa madrs na hospital zetu pia.
 
Serikali kwenye corridors inatamba imeshinda vita na madaktari ...lakini hii ni hatari sana ...itajeuka vita kama ile ya Mahatma Ghadhi na India ..silent protest.....,ni ngumu mno kumeza kuwa madaktari kiongozi wao mkuu ..katekwa kateswa anapigania maisha yake.....Msaidizi wake anatishiwa sana...na mwisho anapigana mahakamani ..asifungwe...........

LAKINI RAIS KWENYE HOTUBA YAKE UKIANGALIA KWA MAKINI ALIJI CONTRADICT SUALA LA DR MPOKI.....ANASEMA ...." madaktari wamegoma pamoja na kiongozi wao[mpoki]..kuukaana mgomo huo ...,na kusema hajawatuma .."
Huyu ni mkuu wa nchi ..ina maana tayari yeye kama kiongozi mkuu nchini na akiwa na taarifa zisizo shaka anajuwa kuwa Dr Mpoki hakuwashawishi madaktari kugoma......Sasa kama ni hivyo njia nzuri kwa serikali wapeleke madaktari wote mahakamani badala ya kuwatisha viongozi wao..
MADAKTARI WAKI KAA KIMYA SAFARI HII WATAONEWA MAISHA YAO YOTE NA HII ITASHUSHA MORALI HATA KWA VIJANA KUWA MADAKTARI.....THIS IS BELOW THE BELT.....UJANJA UJANJA...

Kwa Madaktari wote Tanzania,

Kwanza ninawapa pole sana kwa matukio haya yanayoendelea kwa sasa. Kupigwa na kutishiwa maisha kwa Kiongozi wenu Dr.Ulimboka, na jana kupelekwa mahakamani kwa Mwenyekiti wenu Dr. Mpoki na kufusimamishwa kazi na kufutiwa usajili wa Udaktari kwa wote walio goma.

Hii imedhihirisha kabisa kuwa tangu mwanzo Serikali ya CCM haikuwa na dhamiwa ya kweli ya kushughulikia matatizo na kero zote zilizoibuliwa na Madaktari. Tunachoshuhudia kwa sasa ni ubabe wa serikali wa kutaka kulizima jambo hili kwa nguvu kwa kutumia kila mbinu ikiwemo hii ya kuteka na kuua viongozi wa Madaktari,kuwafungulia kesi na kuwashtaki viongozi wa Madaktari,kufukuzwa kazi na kufutiwa usajili kwa Madaktari wote waliogoma.

Katika hili Serikali ya CCM imeonyesha dharau kubwa sana kwa tasnia ya Udaktari na hili kwa kweli halikubaliki. Serikali imelichukulia swala hili kisiasa zaidi na ndiyo maana hata Dr.Ulimboka walipomkamata walikuwa wakimlazimisha awataje wale walioko nyuma yake huku wakimwambia kwanini anawasumbua na huko walikokuwa wanmpeleka hataonekna tena!Kwa hiyo hapa ni wazi kwamba Serikali imejiingiza kwenye mgogoro huu kichwa kichwa na kuanzan kuwatumia mashushushu wa serikali ili kulimaliza jambo hili.

Waswahili walisema waweza kumlazimisha Punda kwenda kisimani na lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji kisimani. Hapa nina maanisha kwamba kama Serikali imelazimisha kumaliza mgogoro huu kwa mababu isitegemee any good performance and output ya Madaktari kwenye sehemu zao za kazi. Hiyo itakuwa ni ndoto!

Kinachotakiwa kwa sasa ni lazima Kiwete na serikali yake ya kichovu wakae tena chini na kuliangalia swala hili upya na kwa umakini mkubwa bila kuingiza siasa. Ni dhahiri kwamba washauri wa Rais akiwemo PM,Mawaziri,Katibu Mkuu/K na Makatibu wakuu wanampotosha na kwa vile Kiwete ni Rais dhaifu ambaye huwa hataki kuumiza ubongo wake basi kila analoletewa yeye huwa ni utekelezaji! Ile akili ya mbayuwayu ya kuchanganya akili zake na hayo anayopelekewa sijui kaitupa wapi!!!Inasikitisha sana kwa na Rais wa aina ya kiwete. Hili ni janga la kitaifa na kila kukicha naona Tanzania inaporoka kwa kasi kwenda kwenye anguko ambalo itahitaji msaada wa Mungu kuja kuinuka!

Madaktari endeleeni kuomba,unganeni muwe kitu kimoja ili kuendeleza mshikamano wa kudai maslahi yenu. Lakini pia iweni wangalifu sana kwasababu kati yenu kuna wale ambao wataingizwa kwenye biashara chafu ya UWT kwa kununuliwa ili waweze kuwa informers wa mashushu wa kina Zoka ili kufanikisha mpango wa kuzima kabisa vuguvugu hili la madai yenu ya msingi.

Wishing you all the best.
 
Extremely impressive, umejielezea vizuri. I wish the government ingekua inawasikiliza ili kuboresha huduma za afya na maslahi ya wafanyakazi wa taasisi hizo. Kuna upotoshaji wa hali ya juu wa taarifa, mfano idadi ya wanaotaraji kumaliza this year. Kwa data ulizotoa, kwakweli hali ni mbaya.
 
i suppoted you doctors.Natamani ningekuwa Dr ningeanza mimi kuresign nionyeshe njia.Mi nashauri circulate huu mchanganuo kwa madaktari wote kwa email zao simu zao na wananchi pia.Just onyesha njia kwa kuresign i tell you hata kama wenzake hwakufuata utaishi maisha mazuri kuzidi haya sasa. na kwa kuwa tatizo hapa si serikali na madaktri bali ni wananchi na serikali.Nasema wananchi kwa sababu katika hili tunatakiwa wote kwa pamoja tukote kunadai rais atoke ikulu kwa sababu kashindwa kazi.Na kuwa yeye ni mwajiliwa namba ATOKE AKAE mwingine.
 
Wakiresign wanakomoa serikali au wagonjwa. Uchochezi mwngine hata hauna maslahi
 
For the record nilisupport mgomo wa kwanza, ule uliowahusisha sana mainterns kwa sababu za kizembe za watawala kupelekea kuchelewesha stipends zao. Nina kila sababu za kuwasupport madakatari hata kwenye huu mgomo wao wa sasa lakini kuna kitu knanifanya nifikirie mara mbili kuhusu nia halisi inayosukuma migomo ya madaktari.

Kwanza, madaktari wetu wa sasa wanaonekana kuathiriwa sana na hii kitu inaitwa superiority complex. Wanajijenga sana kimakundi, wana dalili zote za kujitenga baina yao kama wafanyakazi wa sekta ya afya na wafanyakazi wa sekta zingine katika serikali. Hili mimi halinipi sana shida. After all ni kweli wamehenyeka vya kutosha miaka sita si mchezo. Mimi hadi kufika Masters imenichukua miaka mitano tu so somehow ninaheshimu shule yao.

Lakini tatizo linakuja unapoona hata wanajitenga katika sekta yao wenyewe. Daktari na nurses, Medical doctors na Assistant MDs, Madaktari bingwa na wasio bingwa, Registrars na Interns, Wanaofanya kazi referral hospitals na wale wa huku kwetu Bukoba, MOI na wale wa MNH, the list never ends.

"Ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu ukianza huachi" huyu Mzee Nyerere alikuwa nabii au nini? Madaktari wameshindwa hii vita kwa sababu ya dhambi ya ubaguzi. Hawakufahamu kwamba vita haishindwi kwa ubora wa vifaa vya kivita tu au aina ya askari ulio nao bali umoja.

Mimi sioni sababu ya kuwatenga manurse katika madai yenu. Kama suala ni kuboresha sekta ya afya kwa ujumla, nurses utawatengaje? Watawala wetu wana dharau sana lakini si wajinga kama mnavyofikiri. Waliwasoma motives zenu vizuri pale mlipokaa kwenye meza ya majadiliano mara ya kwanza na mkawashangaza sana mlipowaondoa manurses, ma assistant MDs na wenzenu wengine kwenye madai yenu. Wakajua nyie tatizo lenu ni superiority complex. Na wameishinda hii vita maana walipogundua udhaifu wenu wakagongomelea msumari wa kutu kwenye kidonda chenu, kwisha habari.

Hii kitu mnayopropose ya mass resignation is too good to be true kwa jinsi mlivyojipanga. Hamuwezi kutekeleza. Jitambueni kwamba nyie ni sekta ya afya, na sekta ya afya si daktari tu wa round na kuprescribe dawa, kuna yule mama mwenye mavazi meupe anayeshinda na mgonjwa kutwa kucha akisafisha kidonda na matapishi yake na akifatilia hali yake kwa ukaribu. Huyu nae ni wa muhimu sana. Nyie vipi? Kwa umoja mnashindwa na hata madreva daladala?
 
Madaktari msipojisimamia na kudai haki zenu kwa pamoja mjue mmekwisha. Hata mgomo wa awali utakuwa hauna maana na hata damu ya Dr. Ulimboka itakuwa imemwagika bure na mtasulubiwa kwelikweli. Hebu angalia wenzenu wa intern wameshakufukuzwa tayari. Je msimamo wenu kwa wakati huu ni upi? Kuweni pamoja na mdai kurudi kazini kwa wenzenu la si sivyo mkiwa vuguvugu mtakuwa mmefanya usaliti wa kutisha na mtakuja kulaaniwa. Katika vita hakuna nuetrality either you win the war or you perish. Je mmeamua kurudi nyuma? Vitani ukirudi nyuma adui yako anapata nafasi ya kukufuata na kukushambulia zaidi. Kurudi nyuma ni kuishiwa nguvu. Mtasambaratishwa. Pelekeni majeshi mbele hii vita lazima mshinde la sivyo you will perish. Lazima muelewe hili.
Ningependa kutoa pole kwa yale yaliyotokea na yanayoendeleakutokea katika nchini na nje ya nchi kuhusu sisi(madaktari).Pole kwa kumuuguzamwenzetu Ulimboka Steven(Dkt), Kushtakiwa kwa MAT, Kuhojiwa kwa Rais wetu NamalaMkopi(Dkt), Kufukuzwa kwa madaktari walio mafunzoni (Intern doctors), vitisho kwa wakuu wa idara n.k.

Mwaka huu Vyuo vikuu na shirikishi vya afya na tibavinategemea kutoa wahitimu kama ifuatavyo:

-MUHAS (150), KCMC(80), WBUCHS(50), HKMU(55), IMTU(45) naUDOM(0).
Kati ya hawa wapo wageni(foreigners) watakaorudi ktk nchizao, wapo ambao watakwenda kufanya internship katika hospitali za binafsi, nawapo wataenda kufanya kazi katika asasi zisizo za kiserikali(NGO)-kwaniinternship si lazima kufanya, ila hadi pale utakapoamua kufanya kazi katikahospitali. Kinachonishangaza serikali inasema inategemea madaktari 700 kutokavyuoni, inawatoa wapi?

MAONI:
Inawezekana katika kila jambo la nchi hii siasa(propaganda)imeingizwa, lakini si katika fani ya udaktari, hii ni fani(Profession) nainapaswa kuheshimiwa kama ilivyo. Si ajabu kiongozi kufika pale Hospitali yaTaifa na kukosa kipimo na kuambiwa kwenda Aga Khan au Regency, utamsikiaakisema “kwani havipo hapa” ukimweleza kuwa ni vibovu utasikia “wanapaswakuwakumbuka”..hii ni moja ya kauli ya kiongozi mmoja mkubwa serikalini!

-Si ajabu kumkutaSpecialist akifatilia damu kule Bloodbank,
-Si ajabu kumkuta Specialist analalamika hawezikuendelea na upasuaji kwani gloves zimembana sana(Sio saizi yake) nakushindwa kutumia vifaa vizuri,

Si ajabu kumkuta Specialist akisubiri hadi nguo za upasuajieti nguo hakuna!
Si ajabu kumkuta Specialist amejifunga shirt kichwani kamakofia, Si ajabu kumkuta specialist amevaa gauze kama mask!!
Si ajabu kumkuta Daktari amejihatarisha(being exposed) na damulakini hakuna Post Exposure Prophylaxis(PEP)

Hii ni katika hopitali ya Taifa, sasa jiulize kama hospitaliya Taifa hali ni hii, katika hospitali nyingine hali ikoje??

Kwa specialist, resident, registrar, interns wenye tabia ya kulalamika na kudaimabadiliko, ni mabadiliko yapi mnayoyadai ili hali muda wa mabadiliko hamsimamiimara katika kudai haki yenu??

Sitegemei madaktari wote kudai haki yao (kwani najua wasalitiwapo tu) lakini zaidi ya yote ni hawa wanaokuwa vuguvugu na wanafiki!!


KAMA WAZAZI/WALEZI
:

Mnawafundisha nini hawa wadogo wenu na watoto wenu, kuhusu kudai haki yako ya kikazI, “I know it is wisdom that takes courage to sit down and listen but it is the same wisdom which takes courage to stand for your right”.

KAMA VIONGOZI/WALIMU:
Unapokuwa ukipita round na wanafunzi wako(medical students,interns, registrar, residents), unajisikia nini pale wagonjwa wanapokufiakatika round, kwa sababu tu ya kukosa huduma ambayo ungeweza kutoa kwa mgonjwana kuwa chahu kwa wanafunzi wako? Wanafunzi wanakuonaje wakati ukisema, “in other countries they could have done soand so” wakati muda wa kudai hivyo vifaa na dawa hizo ndio huu? Wanafunziwako wankuonaje wewe kama specialistwakati wenzako wako katika mgomo wewe unapita round, tena wanafunzi wako wakiwana vitambulisho tu bila makoti, wewe ukiwa na koti?

KAMA WASTAAFU NAMADAKTARI BINGWA WATARAJIWA:
Wakati wadogo/watoto wetu(intern doctors) waakiwa wameachiwamzigo huu, najiuliza kwa mfano tunapokuwa katika MWR, Discussion Panel huwatunapima uwiano wa wagonjwa na treatment options:
Leo hii tukipima Option ya MASS RESIGNATION inashindikana?

-Neurosurgeons(4),
-Orthopeadicsurgeons(15),
-Pediatricians(30),
-ObGynaecologists(45),
-Physicians(60)regardless of subspeciality ie Neurolgist, Gastroenterologist,etc.
-Psychiatrist(30)-notpsychologist,
-Surgeons (40)-regardlessof subspecialty like Cardiothoracic, Plastic surgeons etc,
-Otorhinolaryngologist(20),
- Anaesthiologist 25(notanaeshetist),
-Opthamologist 30(notoptician,optometrist)…HII NI IDADI KWATANZANIA NZIMA.

Hofu kwetu kama specialists na hawa residents ni kwamba mafao, lakini tujiulize leo kama Profesa anapewa mafao ya 50,000/=Tshs kwamwezi hii ndiyo inayokufanya usigome au kuamua kuresign? Kweli?

-Cha kushangaza kuna megabrains nyingi sana za kutegemewa lakini wanaact kama hawajui hili, naamini specialists, Residents, registrar nainterns pamoja na medical students tulikuwa na APGAR SCORE ya 10 – 10!! Sasa inakuwaje microbrains ifanye hivi kwa megabrains.

If I weigh the option of mass resignation I believe it fits the puzzle, because I believe it won't take even a month for the government to call us back to the discussion table (UNDER OUR TERMS THIS TIME) , and in the mean time(I dare to believe that none of us can perish because of financial crisis).

On the other side the Government cant import other doctors,look at WHO doctor-patient ratio, every country needs one, and for those whothink they will import, ask yourself these questions from which country? Will theybe able to pay them(THIS should be above their home salary), accommodation,transport?

This is a profession(medical terminologies) and not just mere English, I bet they might needtranslators, how many? Will they pay them? Will those doctors work in thisenvironment or they have to come with medical equipments, medicine? For howlong will they have to stay here? Will they gain trust to people(rapport etc)?

Hebu tusimame pamoja katika hili, mengi yanafanyika bila mpango hukumu kusomwa mahakamani wakati huo huo, interns kufukuzwa ..sasa unajiuliza kesi ya nini kama tayari wameshafukuzwa, na Rais kuingilia madaraka ya mahakama (kutoa hukumu wakati jambo hilo hilo kukataliwa bungeni), lakini kuumizwa sana kwa Dkt,UlimbokaSteven.

PLEAD/CALL: LET US STAND TOGETHER NOW MORE THAN EVER, THIS TIME NOT IN TOTAL TOOLS DOWN BUT IN MASSRESIGNATION.
 
kama hii ni ukkiukaji wa haki za binadamu je kugoma na kuwaua watanzania mkiwa mmevunja sheria ni kutimiza haki za binadamu? Usiseme hayo watu wamepoteza ndugu zao

Nakubaliana na wewe, hawa ma-dr wameua ndugu zetu kwa sababu za kupigani maslahi ya kushibisha matumbo yao. Siwaungi mkono hata kidogo, hapa nilitaka tu kuwakumbusha kuwa kule wanakopenda kukimbilia, wakidhani UN wana muda wa kupoteza, wapeleke na hili la ma-interns. Kumbuka wameshaomba ulinzi wa Ulimboka kutoka UN (mambo ya kitoto kabisa), sasa kwanini wanapoteza muda kulalamika humu JF, si wapeleke na hili huko huko?
 
wengine wanakenua na kupump madr waache kazi kwa sababu wao wako nje huko wanao uhakika wa kutibiwa. sie wengine hata kusafiri hivi sasa twaingiwa hofu maana ukipata ajali waeza kujiozea zako na kufa a slow painful death huku ukijiona na nduguzo wakikutazama na kuanza matanga ilhali ukiwa hai. mi sijui kila mtu akianza kudai 'haki' yake sijui itakua taifa la namna gani maana nchi maskini kila mtu huona anaonewa! specialsist mzima unalalamikia gloves wewe specialist mzima unakosa ela ya kujinunulia gloves?? acheni huo ubahili! hivi mnajua sie huku maofisini tunanunua karatasi kwa pesa zetu mfukoni na vitu vingine kibao?? wakati mwengine tunasafiri kikazi bila hela na serikali inalimbikiza bila kulipa! hivi mnadhani ni nyie tu wenye matatizo!

Wewe mr. Mhasibu yaani jana nilisaini hela yangu ya nauli sh. 10,000/= kumbe nilipotoka ukaongeza 4 mbele ikasomeka 410,000 hiyo 'cha juu' unaenda kununua karatasi kweli?
 
kuna baadhi ya miradi haitekalezeki au baada ya kuitekeleza huwa failure kwa vile ilipobuniwa LENGO na na MALENGO MAHUSUSI hayakupewa tafakari ya kutosha - na ndio ujumbe unaopatikana katika thread hii. Inawezekana LENGO KUU likawa ni rahisi sana lakini sio ndo mwanzo na mwisho wa kufanikisha mradi
 
Kwa kuwa moja ya mashinikizo ya madaktari kwa serikali ni vifaa ambavyo kwa namna moja au nyingine vingetusaidia moja kwa moja sisi wananchi lakini ktk mataifa yenye uoga wa kudai haki za msingi watz namba moja. hivyo basi tatizo la madaktari ni sisi wananchi ndio tunaosababisha liwepo mpaka leo laiti kama tungeungana na madaktari kwa namna yeyote ile kama walivyo na umoja wenzetu wa misri,syria,libya muhimbili ambayo ni hsptal ya taifa watu wasingeandikiwa refelar kwenda india kupima presha tu au kupasuliwa jipu.
 
We vipi? Tuje tukupe kichapo heavy halafu upelekwe hospitali ukute kuna mgomo usitibiwe we utajisikiaje? Au umeugua serious ukakimbizwa hospital ukakuta mgomo we hali hiyo unaichukuliaje? Unajua kushabikia mgomo kunasababishwa na kuwa na afya njema? Ungekuwa mgonjwa umelazwa halafu hupati huduma yoyote! Jamani,madai yao ya vifaa ni sahihi lakini mgomo hapana! Kwani tusio na uwezo wa kwenda private ndio tunaoumia! Hili sio suala la kushabikia hata kidogo.
 
wengine wanakenua na kupump madr waache kazi kwa sababu wao wako nje huko wanao uhakika wa kutibiwa. sie wengine hata kusafiri hivi sasa twaingiwa hofu maana ukipata ajali waeza kujiozea zako na kufa a slow painful death huku ukijiona na nduguzo wakikutazama na kuanza matanga ilhali ukiwa hai. mi sijui kila mtu akianza kudai 'haki' yake sijui itakua taifa la namna gani maana nchi maskini kila mtu huona anaonewa! specialsist mzima unalalamikia gloves wewe specialist mzima unakosa ela ya kujinunulia gloves?? acheni huo ubahili! hivi mnajua sie huku maofisini tunanunua karatasi kwa pesa zetu mfukoni na vitu vingine kibao?? wakati mwengine tunasafiri kikazi bila hela na serikali inalimbikiza bila kulipa! hivi mnadhani ni nyie tu wenye matatizo!


Hapo kwenye red:

1. Kwa vile WTZ wachache wamekubali kukanyagwa kichwani na MAFISADI - ndio unataka na madaktari wawe hivyo?
2. Wewe unalipwa shilingi ngapi ambazo unaweza hadi kununua karatasi za ofisi yako??? Au ndio nyie W..I wa nchi hii?
3. Wananchi/Wagonjwa wa Tanzania sio mali ya madaktari - ni mali ya Serikali so Serikali ifanye wajibu wake.

MADAKTARI SONGENI MBELE ................ nyie ni professionals wa hali ya juu - cant compare YOU with any other professional couse you deal with a human health - YOU ARE VERY SPECIAL ...........MSIBABAISHWE NA MAFISADI AMBAO WANAJITWALIA JASHO LA WATZ KILAUNI NA WENGINE SIO HATA WASOMI KIHIVYO E.G. PROF. DEEP WATER mp
 
.. ila watanzania kwahili wategemee balaa katika sekta ya afya labda serikali.. ianza kutimiza madai yao waliyo taka kutimizia.. unajua nn kitaendelea? kwa kuwa madaktari wamerudi kazini kwa kinyongo na kwa lazima na lawama kibao toka kwa wananchi, ninacho ogopa ni kuwa watakuwa wanafanya yale matibabu ambayo ni guideline standard na sio kufogi vitu at least kuokoa miasha ya wagonjwa mfano pop hamna waweza tumia box kustabiliza mguu uliovunjika lakini from now utambiwa kanunue hiyo pop... watanzania hapa tumechemsha… naogoma hawa madokta wanaweza kuwa na hasira na wananchi kwa kuwakebeki kwa majina kadhaa huku ukijua kuwa mwisho wa siku ukiumwa yeye ndo anakutibia … swalli kama seriakli itashinda katika kuzima mgomo huu ishu itakuwa kati ya dokta na mgonjwa jee mwisho wa siku nani ata prove failure?
 
Back
Top Bottom