hippocratessocrates
JF-Expert Member
- Jul 1, 2012
- 3,598
- 1,539
- Thread starter
- #101
Wakiresign wanakomoa serikali au wagonjwa. Uchochezi mwngine hata hauna maslahi
Mkuu thinktank, wakiresign si kukomoa serikali au wananchi!Wao wameajiriwa tu lakini kuajiriwa kwao na mtumishi wako(Serikali) isiwetija ya kuteseka kwao. Ni vizuri pia kuuliza na kujaribu kuadadisi kidogo wale walio katika sekta binafsi na madaktari wa kitanzania walio nje, ni ninikilichowakimbiza huko!!
Kuna kitu tunakiita Job satisfaction, kwamba hata kama ni katika mazingira duni kikazi ukimpatia huduma mgonjwa, akipona wewe kama daktari unafurahi pia,lakini inasikitisha kuona watu wanaujuzi lakini vifaa hakuna, dawa hakunana zilizopo zimekwisha muda wake!! sasa ukiwa kama tabibu unaona bora kwenda mahali pengine ili angalau hata kama hawatajali maslahi yako kiasi uombacho mazingira ni mazuri na wagonjwa wanapona.
Inasikitisha kusoma miaka mingi na kusajiliwa katika mwaka wa saba baada ya masomo na internship na bado unashindwa kuhudumia wananchi ingawa una ujuzi.