Madaktari wenzangu: Only "Mass resignation" itawaamsha watawala!

Madaktari wenzangu: Only "Mass resignation" itawaamsha watawala!

Hili taifa sasa limekosa mwelekeo, maadili na uzalendo. Inataka mtu mwenye akili za mwendawazimu kutofahamu CCM imelifikisha taifa hapa. Cha kushangaza ni genge la watu wachache tu wenye huwezo wa ku-influence wabunge 357-wabunge wa upinzani=?, hili kulifanya taifa zima liwe katika mazingira yasio na dira.

Hapo hapo kuna watu wanaokuja hapa kutaka kutudanganya wanadai mabadiliko kwa kutumia maadili ya Mwl. JKN wakimtukuza kwa fikra na maadili lakini bila ya namna zake. Ukiangalia mwalimu alichokuwa anasimamia mfano katika moja ya quote zake hapo chini:
"There must be equality because only on this basis will men work cooperatively. There must be freedom because every individual is not served by the society unless it is his. And there must be unity, because only when the society is united can its members live and work in peace, security and well-being. Society must have institutions which safeguard and promote both unity and freedom and it must be permeated by an attitude-a society ethic-which ensures that these institutions remain true to their purpose, and are adapted as need arises." -Mwalimu Julius K. Nyerere (Philosophy of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Na kuhakikisha alikuwa anaamini anachosimamia kaondoka madarakani hana utajiri. Kwakuwa alikuwa akiamini kile alichosimamia kwa dhati na mbinu zake ziliendana na mawazo yake.

Taifa bado ni maskini badala ya watanzania kujikita katika mapambano ya kurudisha usawa hili tuwekeze kwenye maendeleo ya taifa na kusambaza utajiri kwa wote. Imekuwa tabia sasa ya walio soma kutaka kuwakamata wale viongozi wachache wa CCM ,wanaoliwazwa na marupurupu hili kupitisha dhambi za wachache. Badala ya hawa wasomi kupigana kuwarudisha hawa watu dunia ya mtanzania wao wanatafuta mbinu za kufika hukohuko juu.

Muumiaji wa kweli hasa katika sangomaa hizi za viongozi wetu wajuu na wasomi wetu ni watanzania maskini ambao wamekuwa mtaji wa waelevu.

Kwakuwa CCM imejikita kwenye ku-invest kwa wabunge hili kuendeleza sera za wizi na uongo, kama kweli tungekuwa na watu wanaotaka maendeleo na mabadiliko kwanini hivi vita visingepelekwa kule kule wanapokutana. Kwanini wasipigane na mbinu chafu za CCM kuendelea kutawala kama katiba yenye kuweka wazi access ya vyombo usalama, ulinzi, sheria na independent bodies hili kufikia lengo hilo. Katiba imedaiwa lakini watu wamejichanganya mpaka priority ya kumtetea mtanzania imepotea imehamia kwenye fikra zingine zenye malengo ya personal gains for the large part yaani muungano.

Maadili ya wasomi yamekuwa ni kutafuta maslahi binafsi kutumia mgongo wa maskini, huwezi kuniambia eti kumtesa maskini kwa kumyima huduma ni kwenye kutaka kumsaidia kwa muda mrefu were did you arrive to such conclusion.

‘Morality requires using our reasons to arrive at a universal moral principle that doesn't depend on wants and desires. We must always treat one another with dignity and respect. And never use anyone as the means to an end.Morality is not about calculating the consequences of our actions. It is about acting out of duty, out of principle doing the right thing for the right reasons.' Emmanuel Kant

Kwenye nchi yenye chaguzi na muda wa kubadili viongozi sidhani ni sawa kuwaadhibu wengi kwa makosa ya wachache. Mgomo wa Madokta si sawa.
 
Ningependa kutoa pole kwa yale yaliyotokea na yanayoendeleakutokea katika nchini na nje ya nchi kuhusu sisi(madaktari).Pole kwa kumuuguzamwenzetu Ulimboka Steven(Dkt), Kushtakiwa kwa MAT, Kuhojiwa kwa Rais wetu NamalaMkopi(Dkt), Kufukuzwa kwa madaktari walio mafunzoni (Intern doctors), vitisho kwa wakuu wa idara n.k.

Mwaka huu Vyuo vikuu na shirikishi vya afya na tibavinategemea kutoa wahitimu kama ifuatavyo:

-MUHAS (150), KCMC(80), WBUCHS(50), HKMU(55), IMTU(45) naUDOM(0).
Kati ya hawa wapo wageni(foreigners) watakaorudi ktk nchizao, wapo ambao watakwenda kufanya internship katika hospitali za binafsi, nawapo wataenda kufanya kazi katika asasi zisizo za kiserikali(NGO)-kwaniinternship si lazima kufanya, ila hadi pale utakapoamua kufanya kazi katikahospitali. Kinachonishangaza serikali inasema inategemea madaktari 700 kutokavyuoni, inawatoa wapi?

MAONI:
Inawezekana katika kila jambo la nchi hii siasa(propaganda)imeingizwa, lakini si katika fani ya udaktari, hii ni fani(Profession) nainapaswa kuheshimiwa kama ilivyo. Si ajabu kiongozi kufika pale Hospitali yaTaifa na kukosa kipimo na kuambiwa kwenda Aga Khan au Regency, utamsikiaakisema “kwani havipo hapa” ukimweleza kuwa ni vibovu utasikia “wanapaswakuwakumbuka”..hii ni moja ya kauli ya kiongozi mmoja mkubwa serikalini!

-Si ajabu kumkutaSpecialist akifatilia damu kule Bloodbank,
-Si ajabu kumkuta Specialist analalamika hawezikuendelea na upasuaji kwani gloves zimembana sana(Sio saizi yake) nakushindwa kutumia vifaa vizuri,

Si ajabu kumkuta Specialist akisubiri hadi nguo za upasuajieti nguo hakuna!
Si ajabu kumkuta Specialist amejifunga shirt kichwani kamakofia, Si ajabu kumkuta specialist amevaa gauze kama mask!!
Si ajabu kumkuta Daktari amejihatarisha(being exposed) na damulakini hakuna Post Exposure Prophylaxis(PEP)

Hii ni katika hopitali ya Taifa, sasa jiulize kama hospitaliya Taifa hali ni hii, katika hospitali nyingine hali ikoje??

Kwa specialist, resident, registrar, interns wenye tabia ya kulalamika na kudaimabadiliko, ni mabadiliko yapi mnayoyadai ili hali muda wa mabadiliko hamsimamiimara katika kudai haki yenu??

Sitegemei madaktari wote kudai haki yao (kwani najua wasalitiwapo tu) lakini zaidi ya yote ni hawa wanaokuwa vuguvugu na wanafiki!!


KAMA WAZAZI/WALEZI
:

Mnawafundisha nini hawa wadogo wenu na watoto wenu, kuhusu kudai haki yako ya kikazI, “I know it is wisdom that takes courage to sit down and listen but it is the same wisdom which takes courage to stand for your right”.

KAMA VIONGOZI/WALIMU:
Unapokuwa ukipita round na wanafunzi wako(medical students,interns, registrar, residents), unajisikia nini pale wagonjwa wanapokufiakatika round, kwa sababu tu ya kukosa huduma ambayo ungeweza kutoa kwa mgonjwana kuwa chahu kwa wanafunzi wako? Wanafunzi wanakuonaje wakati ukisema, “in other countries they could have done soand so” wakati muda wa kudai hivyo vifaa na dawa hizo ndio huu? Wanafunziwako wankuonaje wewe kama specialistwakati wenzako wako katika mgomo wewe unapita round, tena wanafunzi wako wakiwana vitambulisho tu bila makoti, wewe ukiwa na koti?

KAMA WASTAAFU NAMADAKTARI BINGWA WATARAJIWA:
Wakati wadogo/watoto wetu(intern doctors) waakiwa wameachiwamzigo huu, najiuliza kwa mfano tunapokuwa katika MWR, Discussion Panel huwatunapima uwiano wa wagonjwa na treatment options:
Leo hii tukipima Option ya MASS RESIGNATION inashindikana?

-Neurosurgeons(4),
-Orthopeadicsurgeons(15),
-Pediatricians(30),
-ObGynaecologists(45),
-Physicians(60)regardless of subspeciality ie Neurolgist, Gastroenterologist,etc.
-Psychiatrist(30)-notpsychologist,
-Surgeons (40)-regardlessof subspecialty like Cardiothoracic, Plastic surgeons etc,
-Otorhinolaryngologist(20),
- Anaesthiologist 25(notanaeshetist),
-Opthamologist 30(notoptician,optometrist)…HII NI IDADI KWATANZANIA NZIMA.

Hofu kwetu kama specialists na hawa residents ni kwamba mafao, lakini tujiulize leo kama Profesa anapewa mafao ya 50,000/=Tshs kwamwezi hii ndiyo inayokufanya usigome au kuamua kuresign? Kweli?

-Cha kushangaza kuna megabrains nyingi sana za kutegemewa lakini wanaact kama hawajui hili, naamini specialists, Residents, registrar nainterns pamoja na medical students tulikuwa na APGAR SCORE ya 10 – 10!! Sasa inakuwaje microbrains ifanye hivi kwa megabrains.

If I weigh the option of mass resignation I believe it fits the puzzle, because I believe it won't take even a month for the government to call us back to the discussion table (UNDER OUR TERMS THIS TIME) , and in the mean time(I dare to believe that none of us can perish because of financial crisis).

On the other side the Government cant import other doctors,look at WHO doctor-patient ratio, every country needs one, and for those whothink they will import, ask yourself these questions from which country? Will theybe able to pay them(THIS should be above their home salary), accommodation,transport?

This is a profession(medical terminologies) and not just mere English, I bet they might needtranslators, how many? Will they pay them? Will those doctors work in thisenvironment or they have to come with medical equipments, medicine? For howlong will they have to stay here? Will they gain trust to people(rapport etc)?

Hebu tusimame pamoja katika hili, mengi yanafanyika bila mpango hukumu kusomwa mahakamani wakati huo huo, interns kufukuzwa ..sasa unajiuliza kesi ya nini kama tayari wameshafukuzwa, na Rais kuingilia madaraka ya mahakama (kutoa hukumu wakati jambo hilo hilo kukataliwa bungeni), lakini kuumizwa sana kwa Dkt,UlimbokaSteven.

PLEAD/CALL: LET US STAND TOGETHER NOW MORE THAN EVER, THIS TIME NOT IN TOTAL TOOLS DOWN BUT IN MASSRESIGNATION.

msipodai haki zenyu kwa kujitoa mhanga mtakuwa kama walimu.
 
Madaktari kugomea kutibu wagonjwa ni sawa na uuaji. Hawa ni wauaji tu. Nawaomba wajifunze kuhusu ulimboka: Je kama Ulimboka asingetibiwa angepona? Na wagonjwa ni hivyo wajue kuwa wameua watu wengi sana. Wameua sana

BAHAKITA at work.
 
Nimeona nikiwa kama mtz ninae itakia nchi yangu mema niwaeleze ndugu zangu ma dr ninyi si wazalendo ila mnacheza na mind za wa tz hili ni dhahiri,katika madai yenu yote mlio nayo ambayo ni takribani kumi na mawili,mmeona ili tuwaone wazalendo mchague dai linalo gusa watz(kuboresha huduma pamoja na vifaa duni) ndio iwe agenda kuu,dr kuzungumzia kwamba anagoma kwasababu ya 3500000 hamzungumzii mkijifanya kwamba mnatupenda sana,sisi tumewafaham kwamba mnataka kutumia watz,mnataka ifike hatua tuichukie serikali na tuingie mitaani,
ila msijisumbue kwani sisi hatuwez kuandamana kwasababu zenu zakisiasa.Bwana Chitage tunakufaham vizuri kwamba wewe ni mwanasiasa mzuri tangu upo chuo.Wekeni siasa pembeni fanyeni kaz.

Ndiyo mkuu baadae ikawaje?
 
Ni watu wachache walio na msingi imara wanaoweza kusimama na kufanya mambo katika hatua za kuleta ukombozi wa kweli. Waalimu wanajulikana ni dhaifu na hata ajira yao inaonekana kutopewa uzito unaostahili japo wanafanya kazi muhimu kwa jamii. Je madaktari nao ni ajira dhaifu? Huu ni wakti wa kuonesha kuwa watu walio makini na imara, watu wenye akili kubwa wanaweza fanya mambo kwa msingi wa lengo, shabaha na nia. Kwa sasa kilichopo ni nyie kuonesha ikiwa mlikuwa na lengo ama mlifanya kama wasukumwao bila ya kujua wanachotaka. Get up Stand up... Stand up for your rights...(Bob Marley)
 
Madaktari kugomea kutibu wagonjwa ni sawa na uuaji. Hawa ni wauaji tu. Nawaomba wajifunze kuhusu ulimboka: Je kama Ulimboka asingetibiwa angepona? Na wagonjwa ni hivyo wajue kuwa wameua watu wengi sana. Wameua sana


Unazumgumza usilolijua....unafahamu ni wagonjwa wangapi wamekufa kwasababu ya kukosa dawa au vifaa tiba? wewe unajua ni wagonjwa wangapi wamekufa mapokezi kwasababu dawa za dhalura hazipo? wewe vifo ulivyoona ni vile vilivyosababishwa na mgomo....unajua ni wanachi wangapi wamekufa so far kwasababu walipata ajali na kukosa CT/MRI ambayo ingewasaidia madokta kuwapa huduma stahiki na kuokoa maisha yao?
Watu wenye small minds kama zako ndo wanaosababisha wananchi waendelee kuteseka kwasababu kama ungeunga mkono harakati hizi serikali ishaleta vifaa tiba na kujibu hoja za madokta na wagonjwa wamekuwa wananeemeka.

Nikuulize swali, hayo madai ya madokta ya kuboreshewa mazingira ya kazi na mafao yao ni wewe utakayetoa mfukoni hela hizo directly....wao si wanataka hiyo kodi yako ndogo unayotoa ( kama unalipa kweli maana inawezekana ni mkwepaji mzuri) na pesa hiyo kufichwa kwenye mabenki ya uswisi zikusaidie wewe maskini wa kufikiri?
TAFAKARI USIWE POYOYO!!!
 
Asante mtaalam kwa uchambuzi makini, inatia moyo tunao wataalam!

Tulikofikia hakuna mshindi, si serikali si wataalam wetu madaktari, si wananchi, si yeyote mpenda maendeleo na amani. Tulipofikia pia tutakosa rafiki wa kutusaidia iwe mawazo au hali.

ili kuwa katika hali salama, tunapaswa kuangalia mbele sana: Suala hili lisiwe la madaktari peke yao. Hili ni suala la taifa zima, linagusa maisha ya kila mtu anaeishi Tz, mwenyeji kwa mgeni. Nina maoni makuu mawili: 1. Wanasheria watupe upembuzi yakinifu juu ya haki ya afya na jinsi inavyopaswa kutolewa kufuatia TZ kuwa mwanachama wa WHO na wanachama wa mikataba mingine inayohusu haki ya afya na nyanja zake zote. Ndani ya baadhi ya hii mikataba kama ule wa haki za kitamaduni na uchumi (the Internationla covenant on economic and socila rights - 1966) ambamo haki ya kufanya kazi inaweza kuhusishwa na haki ya afya inatajwa; kifungu cha 7 cha mkataba huu kinahusu haki ya kufanya kazi na mazingira bora kazini; kifungu hiki kinazungumzia serikali zote wanachama ( TZ ilikuwa miongoni mwa wanachama wa kwanza kabisa kuridhia na kusaini mkataba huu wakati huo - 1966 - Mwl JKN akikabiliana na suala la kukopa kwa ajili ya huduma za jamii - elimu, afya nk.)

kifungu kinafafanua mazingira bora kuwa ni pamoja na mafao stahiki kwa kila aina ya kazi...hapa tujiulize kama mshahara wa dr ni stahiki yake ikilinganishwa na taaluma na sekta zigine ambazo hazizalishi lakini ni muhimu sana?? ...(7) (ii) kiwango cha maisha kinachoridhisha kwake na familia yake...decent living for them and their families....(b) safe and healthy working conditions...kifungu cha 8 kikitambua haki za wafanyakazi kuwa na vyama vyao kutetea na kusimimia masilahi yao...hiki kimeainishwa kwa upana sana...kifungu cha 12 kinawahusu madaktari zaidi kuwa serikali zote wanachama kutambua haki ya kila mtu kufurahia kiwango cha juu cha afya ya mwili na ubongo ( ...the right of everyone to the enjoyment of the highest attainable standard of physical and mental health...) 12(2) state should take steps to achieve "full realization" of this right...and this to inlcude the follwing:

reduction of stillbirth- rate....; (d) creation of conditions which would assure to all medical service and medical attention in the event of sickness....yaani haturuhusiwi kukubali hali ya mgonjwa kukosa huduma kama mwanachama wa mkataba huu....nk

TZ imeridhia mkataba huu bila reservation - bila maeneo ambayo tunadhani hatuwezi kuyakidhi.. na hata kama tungefanya hivyo...bado tungebanwa na vifungu vingine ambavyo vinaainisha wajibu wa serikali katika mfumo huu ambao ni kuhakikisha haki ya mgonjwa na ya dakatari, nurse na wengine inalindwa...

katika mfumo huu serikali inafanya kazi na madktari kupitia chama chao kujua njia sahihi za uendeshaji na usimamizi wa utaratibu huu; wanasheria wakisaidia kuweka mambo katika mtazamo wa haki na usalama wa pande zote: HAKUNA MSHINDI AU ANAYESHINDWA....

KATIKA hili tunakubaliana ( huu ni mchakato mkubwa wa kitaifa ukihusisha bunge nk)...kiasi cha pato la taifa na jinsi tunavyoligawa kwa nyanja mbali mbali...tukilindwa na sheria ya usawa usio bagua mtu au kundi hata katika mgawanyo wa mapato kwa njia ya mishahara....usawa na kutobaguliwa ( the principle of non discrimiantion and equality of all types) ni moja ya misingi mikuu ya umoja wa mataifa na wanachama wake wote - TZ ni mojawapo na mpaka tumetoa naibu Katibu Mkuu wa umoja huu - tuko mbele sana katika masuala haya...

katika mtazamo huu athari kwa raia wasioweza kulipia matibabu aghali inalindwa ...nia ikiwa kuhakikisha watu wote wanapata matibabu stahiki kwa kila ugonjwa - ikibidi mtu kutibiwa nje iwe ni kwa matakwa yake na uwezo wake - wengi wa hawa huwa wafanyabiashara wakubwa -

kwa hiyo kama kuna kesi mahakama yoyote itaangalia mambo haya na usawia wake na haki itaonekana kutendeka maana mahakama itasaidia pande zote: serikali kusimamia wajibu wake na madaktari kusimamia haki zilizo za msingi kwao. Wananchi tutafaidika na muafaka wa hawa wawili...mahakama na bunge vikiwa katikati....kuhakikisha uwiano sahihi wa masuala yote...

Maoni ya 2: yote ya juu yanawezekana tukikubali kusikilizana, kuzungumzana kama ambavyo mchakato ulikuwa umeanza...kwa hiyo ninawaomba madaktari wafanye kazi na wanasheria kuliweka hili katika mtazamo huu na kuhakikisha uratibu makini wakati wa majadiliano. pili katika hili ni kwa serikali kukubali kw mara nyingine kuzungumza na madaktari, pengine na wadau wengine - kubwa likiwa kuweka misingi itakayosimamia mustakabali wa nchi kwa namna ambayo inajengea maeleano katika masuala ya msingi.

Kufuata mikatba ya kimataifa na ya ndani kupitia katiba na sheria zingine...kuna mapana ambayo sijayaweka hapa ambayo serikali inayajua vizuri na ninaamini yakiletwa katika meza ya majadiliano yanaweza kuinua taifa letu kuliko kulididimiza kama inavyotaka kutokea sasa.

raia wa leo wanauwezo kujua mapana na wigo za majadiliano haya: mwisho wa siku wataona ni madaktari na serikali waliowasaliti na si mmoja kati yao!! Kwa hiyo pande hizi mbili zikae pamoja na kufikia muafaka wa namna sahihi ya kufikia muafaka katika hili...la sivyo kwetu raia sauti zetu zinalalama na kusema "....tumewakosea nini (serkali na madakatari) kutughilibu kiasi hili??? Mbona mnatuumiza??

ninaamini na kuomba kuwa hekima ya Mungu ipitayo zote itaongoza na kutangulia pande hizi mbili kufikia makubaliano. Tz tumetatua migogoro mingi ulimwenguni na tunaheshimika sana na majirani na watoka mbali - sasa ni wakati wa kujiganga na migogoro yetu ya ndani. isikilizeni sauti wa wanawake na watoto, wazee, wenye ulemavu wa aina nyingi, wenye mapenzi mema na nchi yetu. Tunawategemea, Tunategemea hekima yenu kulifikisha taifa mahali stahiki. AMINA.
 
Nimeangalia itv taarifa leo na kuona wagonjwa wanabebwa na ndugu zao kwenda private kufanya vipimo kisha kurudi mhimbili na ujue kwa mfano kipimo cha CT scan pale hospitali ya regency ni 282000 wakati ilipokuwepo mhimbili gharama ilishuka hadi 50000......Kwa hiyo wewe furaha yako ni kumzungusha mgonjwa kupata vipimo private wakati vingeweza kupatikana hospitali za serikali? nina mashaka na uwezo wako wa kufikiri!!!
Kwa taarifa yako, watu wapuuzi kama wewe mmechangia kuondoa mgomo kwenye vyombo vya habari (ambao ndo unaisumbua serikali) mmehamishia mgomo mahospitalini ( ambako serikali haijali kinachoendelea huko) matokeo yake wananchi wasio na hatia wanateseka sana na kwa taarifa yako si ajabu vifo vinavyotokea sasa vikazidi vile vya kipindi cha mgomo bahati mbaya wasiasa wahuni kama wewe hawavitangazi.
udaktari ni profession huwezi kuilinganisha na siasa na zamu hii mtajua kutofautisha siasa na taaluma!

we ni mwelevu
 
Ni lazima tupite njia ngumu kuelekea Tanzania/Tanganyika tunayoitaka.....

Nawaunga mkono madaktari mpaka mwisho!

Hatuwezi kuendelea namna hii....

Ahsante kwa andiko hili Dr.... muwe wamoja na mtapata nguvu zaidi..... nawaamini...!
 
Madaktari kugomea kutibu wagonjwa ni sawa na uuaji. Hawa ni wauaji tu. Nawaomba wajifunze kuhusu ulimboka: Je kama Ulimboka asingetibiwa angepona? Na wagonjwa ni hivyo wajue kuwa wameua watu wengi sana. Wameua sana
weak analysis.... i dare to query your IQ.
 
wadau sijui kama ntakuwa nimetoka nje ya mada lakini inasikitisha kwakweli hasa katika sekta ya afya,kwasasa niko Kilosa kijiji kimoja kinaitwa Buyuni leo kuna kijana mmoja leo kaumizwa na machine ikambidi aende duka la dawa kupatiwa huduma ya kwanza maana zahanati yenyewe hakuna mpaka aende mjini kama km 20 hivi kwakweli ni masikitiko makubwa na miaka yetu 50 ya uhuru
 
Ma doctor wenyewe wanafki, maneno mengi vitendo hamna! Yaliyomkuta yale Ulimboka ni madogo? kitu gani cha msingi wamefanya kuonesha kuguswa kwao na hilo tukio badala ya kupeleka tu briefing yao UN kwa kuomba ulinzi? Wabongo wote tu wanafiki na sio wazalendo, it is time we accept that fact! kila mmoja yupo kwa ajili yake na familia yake.
 
Madaktari kugomea kutibu wagonjwa ni sawa na uuaji. Hawa ni wauaji tu. Nawaomba wajifunze kuhusu ulimboka: Je kama Ulimboka asingetibiwa angepona? Na wagonjwa ni hivyo wajue kuwa wameua watu wengi sana. Wameua sana

Hebu muulize Malcopolo wakati anazuga pale Lugalo, vifo vingapi vilitokea kwa ukosefu wa vifaa?

Hebu wapeni madaktari mazingira mazuri ya kufanyia kazi pasipo hata kuwaongezea mshahara muone kama hawatachapa mzigo!

Madaktari ya Ureno wamegoma kisa bajeti ya afya kwa kuwa imepunjwa, unafikiri hawajui madhara ya bajeti finyu ya afya?
 
Kwa kuwa moja ya mashinikizo ya madaktari kwa serikali ni vifaa ambavyo kwa namna moja au nyingine vingetusaidia moja kwa moja sisi wananchi lakini ktk mataifa yenye uoga wa kudai haki za msingi watz namba moja. hivyo basi tatizo la madaktari ni sisi wananchi ndio tunaosababisha liwepo mpaka leo laiti kama tungeungana na madaktari kwa namna yeyote ile kama walivyo na umoja wenzetu wa misri,syria,libya muhimbili ambayo ni hsptal ya taifa watu wasingeandikiwa refelar kwenda india kupima presha tu au kupasuliwa jipu.
Siku moja nilikuwa naongea na jamaa mmoja toka Ulaya, aliniuliza hivi "Hivi kwa nini Tanzania wananchi hawawezi kuungana kupinga dhuluma mnayotendewa na serikali yenu?" kweli nilikosa jibu sahihi, ila nilichomwambia "Serikali ya Tanzania inatumia udini na vyombo vya habari kudanganya wananchi"
  • Dini inatumika pale ambapo inawezekana (Mfano CUF tuliambiwa ni cha kiislamu na walileta mavisu kuua wananchi, kumbe ni uongo, na hapo wakristu hawakukiunga mkono, na ikitokea CUF kaitisha umoja wowote basi atapata tu Islam kwa sababu christian watasema nyie wadini, na hapo umoja haupo, serikali itapeta.
  • Vyombo vya habari vinatumika kukanusha yayoiandama serikali (mfano suala la Dr Ulimboka na madakitari kwa ujumla) hapo wananchi wanadanganywa eti hawa jamaa wanadai eti tuwalipe msharaha mkubwa (tena kwa kutaja kiasi ili na wenye mshahara mdogo wawaonee donge ili wawapinge, na hapo wananchi wanaaminishwa kuwa serikali imefanya juhudi ila madakitari ndiyo tatizo.
 
We vipi? Tuje tukupe kichapo heavy halafu upelekwe hospitali ukute kuna mgomo usitibiwe we utajisikiaje? Au umeugua serious ukakimbizwa hospital ukakuta mgomo we hali hiyo unaichukuliaje? Unajua kushabikia mgomo kunasababishwa na kuwa na afya njema? Ungekuwa mgonjwa umelazwa halafu hupati huduma yoyote! Jamani,madai yao ya vifaa ni sahihi lakini mgomo hapana! Kwani tusio na uwezo wa kwenda private ndio tunaoumia! Hili sio suala la kushabikia hata kidogo.

ambacho hukijui ni kuwa wangapi sasa huwa wanakufa mahospitalini bila ya mgomo kuwepo...
Pili haujui kuwa daktari huwezi kumlazimisha akutibie...think here?
Tatu hujajiuliza kwa nini serikali katika madai yote madaktari dai kubwa lilikuwa ni kuboresha huduma kwa kupata vifaa tiba na madawa lakini hadi leo hawajatoa ahadi hata moja kwenye hili wanabaki kusema milioni saba milioni saba ili tu kuwalaghai wale wasiokuwa na uelewa kama wewe hapa

fikiria ndugu kama huwezi kufikiri uliza uelimishwe kama ambavyo mimi hufanya...
 
Usifikiri watz ni wa p.u.uzi,tunafaham ma dr wanamadai mengi sana na niyamsingi lakini kamwe watz hatuwez kuandamana kwani ma dr wamekuwa wa p.u.u.z kwakuchanganya siasa kazini,wameona ili watz tuwape surpot wajidai kwamba wanatupenda sana kwa kuweka msisitizo zaidi kwenye kuboresha hosptl na kujifanya mishara sio agenda yao,ma dr sisi tumewagundua nyinyi si wazalendo kinacho wasumbua ni maslahi binafsi haya mengine ni siasa tu!

kweli wewe ni mzalendo kwa sbb unakula tanzanite,gold,diamond,uranium ,gas .....etc pampja na akina DHAIFU na kichaka chake cha majmbazi aka sirikali

au hauli hata sumni lakini umeridhika asilimia moja ya watanzania SIRIKALI NA DHAIFU kula asilimia 96 ya mkate wa watanzania milioni 45
 
Go..doctors the blood of Ulimboka will not lost for nothing.
 
Back
Top Bottom