Mada Moto Channel Ten: Julius Mtatiro vs Humphrey Polepole

Mada Moto Channel Ten: Julius Mtatiro vs Humphrey Polepole

Anajaribu kujiosha ili magamba
yamfutie dhambi ya kuipinga katiba yao.
Amesahau kwamba tumeishagundua kuwa kuwasikiliza hawa
wanaojiita wachambuzi wa mambo ya siasa
kumetufikisha hapa.

Tumeamua kujisikiliza sisi wenyewe
tukikosea tukosee wenyewe,na uamzi wetu
ni huu hapa: UKAWA mbele mengine nyuma,
Hakuna kulala mpaka kieleweke.
 
Kwa mtu asiyekusikiliza vizuri anaweza kuona vitu unavyoongea vinamashiko lakini nakuhakikishia unajichanganya sana ndugu yangu.

Wewe sio mchambuzi mzuri wa siasa ila ni msemaji wa chama cha mapinduzi. Jifunze kwa wachambuzi wa siasa kama Prof Kitila na Dr Bana. Wenzako wako dyanamics licha ya kuwa na vyama vyao saa nyingine kwenye ukweli wanasema ukweli hata kama ni ukweli mchungu kwa vyama vyao.

Sasa wewe umekazania Magufuli yuko sawa ata nyumba zilivyouzwa haikua kosa lake si asingeshiriki basi angejiuzulu.

Polepole punguza mahaba unakua unaboa

Big up bro, huu polepole ni shabiki la ccm na anatumiwa kichafua vyama vya upinzani, hakuna mchambuzi wa siasa wa namna hiyo.
 
Nimekuwa nikimsikiliza ndugu Humphrey kwa muda mwingi tangu aanze kuchambua siasa.lakini cha ajabu zaidi anamwingelea mhe.lowassa kuwa si mwadilifu je.chama anachotoka yeye polepole tangu lini kikawa kisafi mbona hasemi haya?

1.Mwenyekiti wa chama chake aliongoza bunge la katiba kuikanyaga katiba ya warioba kwa kutoa maelekezo kwa BMK je nani msafi CCM?
2.Magufuli alipiga kura ya NDIO kama lowassa kwenye katiba pendekezwa je.lini magufuli kawa msafi? mwadilifu? shem on u.
3.Uko CCM chama ambacho kinamsema lowassa ni kapi huku kikimpitisha Endrew chenge kutetea jimbo la bariadi magharibi na prof.Tibaijuka kule mureba!!! shem on u polepole.
4.Unajipa madaraka ya kuchambua nani msafi na mchafu huku unalelewa na chama kichafu nani akuelewe?
5.Unatoa povu kupinga katiba pendekezwa huku waliojitoa kuwaunga mkono na lowassa akiwemo leo hawafai unataka mabadiliko gani wewe dogo janja?

Lowassa kakili na kujitoa wewe umeufyata kila siku unalialia kwenye media katiba! katiba! lini magufuli alimtetea warioba? chama chako kimemvua nguo jaji warioba tukiwa tunaona leo hii nani tutamsikiliza kutoka ccm? wote wasaka tonge HATUKUTAKI.....SHAME ON U!
 
Kuna mambo napata shida kuyaelewa. Inawezekana kabisa mimi ndiye tatizo!!
 
Muda huu tanzania sio wa mwendo wa pole pole,
Mbio hizi haziwezi,ngoja tunaoenda twende,
yeye aje nyuma polepole huenda atatukuta
kwenye kitu inaitwa tanzania tuitakayo.

Kama alivyotetea mawazo ya walio wengi kwenye
katiba mpya,awapishe wengine wamtetee rais
ambaye ni chaguo la wengi.
 
Baada ya hoja yake ya Ufisadi kubolewa akakimbilia lazima tupate Rais anayeweza kudhibitiwa!!!

Kwa Mfano na Mungu atuepushilie mbali Magufuli akiwa Rais pia anaenda kuwa Mwenyekiti wa CCM

Ilhali Mh Edward Lowassa akiwa Rais anakuwa ni mwanachama wa kawaida Chadema!!!

Labda kama hukumsikia, amesema Lowassa sio mtu mmoja, ni taasisi. Nyuma yake ni ana watu wenye nguvu kubwa ya kiuchumi wasioweza kudhibitiwa na mtu yeyote ndani ya Chama na nje ya chama.
 
Nilichojifunza toka kwa Polepole:

CCM katika mchakato wake wa kupata wagombea urais imefanikiwa kuwaondoa mafisadi wake wakubwa waliokuwa na matumizi makubwa ya fedha ili kushawishi wajumbe wawapitishe katika uteuzi.

Mfumo ni zaidi ya CCM. Mfumo ni utendaji mzima wa Watumishi wa Umma, Sekta binafsi, Mahakama, vyombo vya ulinzi na usalama na taasisi zake. Kumuondoa Rais peke yake Hakuondoi mfumo.

Watanzania hawahitaji mabadiliko (Change of regime), wanahitaji Mageuzi (Transformation). Mageuzi ndiyo yanayoweza kubadili mfumo na hauwezi kurudia mfumo wa awali tena lakini change inaweza kuwa reversed.
Lowassa si mtu binafsi bali ni taasisi yenye wafanya biashara wakubwa ndani yake, isiyoweza kudhibitiwa kwa maamuzi yake. Ila yeye anaweza kuwadhibiti wengine kama inavyotokea sasa katika baadhi ya viongozi wa vyama vya ukawa kudhibitiwa.

Magufuri katika utumishi wake wote, amehudumu wizara zisizo za muungano ambazo msimamizi wake ni Waziri mkuu. Maana yake majukumu yake ni ya utekelezaji wa maagizo ya Bosi wake, Waziri mkuu. Mfano uuzwaji wa nyumba za serikali.

kama regime inaresist mageuzi haina budi kubadilishwa. kwa kukataa katiba ya wananchi regime hii imeonekana haiwezi tuletea mageuzi na inapaswa kuondolewa.

CCM ndiyo inaunda serikali hivyokusema ni sehemu ndogo ya huu mfumo ni kujitia upofu.
 
Eti anasema atazunguka nchi nzma kuuelezea uma madhambi ya El.. me najiuliza yeye kama nani sasa kwenye nchi hii? Hapa swala ni kwamba acha yeye hata azunguuke kikwete, mkapa na wengine wote haiwezekani hata kidogo kusikilizwa na watanzania, zaidi sana anazidi kujishushia heshima yake na kutafuta watu tuzidi kumdharau
 
Ulishawahi kujiuliza angetokea Mzee Reginald Mengi amehudhuria graduation yako halafu akakupa hongera na kukuuliza nikupatie shilingi milioni mia tano?-

Nadhani kila mmoja wetu atasema NDIYO kabla hata hazijaisha SEKUNDE TATU baada ya kuulizwa.-

Kwanini umesema ndio?

Sio kwasababu tayari umeipangia hiyo pesa matumizi thabiti yenye tija kwako na kwa jamii inayokuzunguka (ndani ya SEKUNDE TATU). Yamkini angeishia kukunasa kibao pale unavyokuwa ukijieleza utakavyoitumia. Ukweli ni kwamba umesema NDIYO kwa sababu tu ni FURSA YA BURE -imejitokeza. NEEMA IMESHUKA! Na sio kwasababu ulijipanga kuipokea na kuitumia.

Hii inamaanisha nini?

Haukuwa na DHAMIRA YA DHATI na hiyo pesa bali una UCHU WA HIYO PESA basi tu kwa sababu ni fursa ya bure.

Kwenye mjadala wa leo, Humphrey Polepole amesema kwamba "Padlocks" ALISHUKIWA NA NEEMA ya kupata FURSA, hakua anatarajia, kama Daudi vile.

Niwatahadharishe WaTZ. Kuwa Rais ni kuwa na VISION (malengo) inayoambatana na DHAMIRA YA DHATI. Huwezi ukashukiwa na neema ya kuwa Rais halafu ukaweza kuwa rais. Padlocks alikubali tu kwa kuwa ni fursa ila sio kwa kuwa amejipanga na kuwa na malengo na Tz.

#Urais sio ANDAZI Kaka Humphrey Polepole
 
Pole sana Polepole. Umejidhalilisha mwenyewe.Sifugi maradhi bora nikupe tu ukweli kwamba umechafuka hata uoge maji pipa zima kwa sabuni nzuri .
 
Eti anasema atazunguka nchi nzma kuuelezea uma madhambi ya El.. me najiuliza yeye kama nani sasa kwenye nchi hii? Hapa swala ni kwamba acha yeye hata azunguuke kike te, mkapa na wengine wote haiwezekani hata kidgo kusikilzwa na watanzania zaid sna an azidi kujishushia heshima yake na kutafuta watu tuzidi kumdharau

Kama anajipenda akomee humo humo kwenye TV amwulize nini kilimpata mch. Mtikila tarime mwaka 2010
 
Nimemsikiliza polepoole, anahangaikia tuzo kama za viti maalumu hivyo Kazi aifanyayo anafanya kwa bidii ila jamii ya Tanzania sasa ni tofauti sana na ile ya miaka iliyopita hatima yake Aibu kubwa Kwa polepole
 
Huyu Polepole anadai waziri akifanya kosa lolote lile asishutumiwe bali waziri mkuu ndio anapaswa kubeba mizigo ya mawaziri wadogo?

Nimefurahi sana mtangazaji alipomwuuliza vp waziri Muhongo kuwajibishwa na hapo hapo waziri mkuu kubaki salama.

Tehe tehe tehe teheeee!!!!

Kweli ccm wamekuwa vipofu.

Eeh makubwa basi...
 
Kama issue ni tuhuma gazeti mmawio la wiki hii llimeweka ttuhuma za Jaji Warioba ambao walishirikiana vyema ktk Tume ya Katiba. Aidha mgombea wa CCM Mhe J P Magufuri ana tuhuma kibao za matumizi mabaya ya madaraka ktk uuzwaji nyumba za serikali, upotevu wa mabilioni uliolipotiwa na CAG na kamati ya bunge ya hesabu za serikali, ununuzi wa kivuko kisichokidhi viwango tuhuma ambazo ziliwahi kupelekea waziri wa ujenzi Mustapha Nyanganyi kujiuzulu.

Lakini kubwa hata Ndg Polepole amewahi kutuhumiwa na matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kuendeleza vijana kupitia NGO zake mbali mbali alizokuwa akiziongoza hadi mmoja wa wafadhili DANIDA kusitisha misaada. Hivyo HP hana MORAL AUTHORITY ya kuzungumzia mtuhumiwa yeyote kwa sababu hata yeye ni mtuhumiwa pia.

Tatizo wanaitwa ktk vipindi hivi wahafanyi homework ya kifahamu bachground ya HP wanakurupuka tu kuanzia kwenye Tume ya Wariova
 
Kabla ya kuteuliwa kuwa mmoja wa makamishna wa Tume ya mabadiliko ya Katiba kuwakilisha vijana, Polepole kwa muda mrefu amekuwa akiongoza NGOs zinazolenga kusaidia vijana ikiwemo TANZANIA YOUTH COALITION (TYC) yenye ofisi zilizochoka pale Kijitonyama.

Katika kipindi cha utawala wa Mzee Mwinyi na Mkapa NGOs zake zilipatiwa fedha nyingi sana kuendeleza vijana. Baada ya impact ya fedha zao kutooneka donors wengi wakakata misaada ndipo akaubikia ktk Tume.

Hivyo vijana wa Tanzania wanalalamika kuwa hawana fursa,ajira n.k mmoja wa watu wanaotakiwa kutoa majibu ni Pole pole kwa sababu kwa miaka 20 amekuwa akipatiwa misaada na wafadhili ya kuendeleza vijana chini ya MKUKUTA. Hivyo hivi sasa anajaribu kujijengea kukubalika upya kupitia Katiba na Ukawa.
 
mimi nahisi ccm ni bora waache njama tu na kutumisha watu kuja na propaganda za kijinga,manake kila wakisema ndio wananchi wanazidi kuwa na hasira nao zaidi,kimya pengine kitawanususu japo 5 points
 
Back
Top Bottom