Mada Moto Channel Ten: Julius Mtatiro vs Humphrey Polepole

Mada Moto Channel Ten: Julius Mtatiro vs Humphrey Polepole

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Leo channel 10 Ni zamu ya Mtatiro na Polepole. Don't miss saa 4 kamili usiku.

Polepole anasema kuwa wananchi wanataka mageuzi 'transformation' na sio mabadiliko kwa maana ya change.Akasema ukawa wanahubiri kuhusu mabadiliko wakati wananchi wanataka mageuzi.
Mifano aliyoitoa huyu polepole kuelezea hayo mageuzi amejikuta akijichanganya na kwakweli sasa naweza kusema kwa uhakika kabisa huyu jamaa ana agenga yake ya kukipigania chama cha mapinduzi hata kwa kujifanya haelewi ili tu malengo yake yatimie.

Ametaja Muungano.Kwamba watanzania wanataka mageuzi ya muungano.Huu uliopo haufai na umeshindwa.Hili lipo kwenye rasimu ya mzee Warioba ambayo ni moja ya misingi mikubwa ya muungano wa UKAWA.

Ametaja watanzania wanataka raisi ambaye madarajka yake yanadhibitiea na katiba.Yani hana mamlaka ya kupindukia kama ilivyo kwa katiba ya sasa hivi.Hili lipo kwenye rasimu ya katiba ya Warioba ambayo inasimamiwa na UKAWA na kubezwa na CCM na Polepole analijua hilo sana kuliko mimi..

Ametaja kitu kingine cha mageuzi ambacho wananchi wanataka ni kuwa na uwezo wakuwawajibisha wabunge easiowajibika kwenye majimbo yao.Hili pia ni moja ya msingi uliopo kwenye katiba ya mzee Warioba ambayo ni mwimbo ulioifanya UKAWA ukawepo......
.
Sasa najiuliza haya makusudi ya kutoa hoja za kijinga kabisa huku akijicontradict mwenyewe huyu Polepole ni kwa manufaa ya nani?Mifano yake ya hiyo anayoita transfomation yote ni mihimili ya katiba ya wananchi na haikubaliki kabisa CCM.Sasa bado anataka watu wachague CCM kupata transformation zipi wakati zote zipo kwenye agenda ya UKAWA?Na yeye ni shahidi kuwa ccm hawataki hayo mambo na ndo moja ya kitu kilichompa yeye umaarufu kwa kuwasema sana ccm kuwa wanapuuza maoni ya wananchi

Leo hii sarakasi anayopiga huyu polepole ni kwa manufaa ya nani?Polepole atueleze sasa kuwa hata kwenye mchakato wa katiba yeye alikuwa anaigiza tu kuwa anaiunga mkono katiba ya wananchi huku akijua chama chake hakiwezi kuipitisha ili tu kutafuta wafuasi ambao watamwamini ili aje kuwadrive upandevwa ccm kwenye uchaguzimkuu.Hapo nitamuelewa sana lakini kinyume na hapi anajichanganya sana huyu jamaa
 
Leo huyo "mchekeshaji wa mfalme" pole pole akizengua
mkuu mtatiro mrambe vibao 2 vitatu hivi ili kumrudisha
kwenye mstari maana dogo ana jisahau sana.
 
Last edited by a moderator:
MJADALA WA WAZI KATI YANGU NA HUMHREY POLEPOLE LEO SAA 4 USIKU!

Muda si mrefu nimepokea simu ya mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha CHANNEL TEN kwamba naalikwa kwenye mjadala wa masuala ya nchi ambao pia utahudhuriwa na ndugu Humphrey Polepole leo Ijumaa saa 4.00 usiku LIVE.

Kwa moyo mkunjufu kabisa nimekubali mwaliko huo. Sitatumia mjadala huo na ndugu yangu kuonesha kuwa mimi naweza kuliko yeye, La hasha! Nitautumia kuwaelimisha watanzania wajue WAPI NCHI YETU IMEJIKWAA na wapi inapaswa KUINUKA. Kila mmoja, yeye na mimi, ana cha kujifunza kwa mwenzake.

J. Mtatiro,

Dsm.
 
Safi sana coz msigwa alipwaya sana cku ile maana aliambiwa ukweli,:nadhani hata Mtatiro atakutana na hilo
 
Bora Mtatiro anajua kujenga hoja sio yule anaejiita Mchungaji ilikuwa ni aibu.

Badala ya kujenga hoja anamshambulia Polepole binafsi, na alichokera zaidi kusema watanzania wengi hatuujui ufisadi.!
 
Rejea ukurasa wa mtatiro facebook


tunachotaka waeleze ukweli juu ya siasa za maji taka zinazoendelea na kuliaminisha taifa kuwa ndo siasa za kile kumbe ni kutumia wenye afya ndongo ya akili mwa maslahi yao,

 
Unakurupuka kutoa habari wakati habari yenyewe sio kamilifu. Tunaomba muda

Muda si mrefu nimepokea simu ya mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha CHANNEL TEN kwamba naalikwa kwenye mjadala wa masuala ya nchi ambao pia utahudhuriwa na ndugu Humphrey Polepole leo Ijumaa saa 4.00 usiku LIVE
 
Ni ujinga mtupu kukaa kumzungumzia lowassa ni fisadi, wakati magufuli nae ni fisadi wa bilion 262
 
Bora Mtatiro anajua kujenga hoja sio yule anaejiita Mchungaji ilikuwa ni aibu.

Badala ya kujenga hoja anamshambulia Polepole binafsi, na alichokera zaidi kusema watanzania wengi hatuujui ufisadi.!
Wote hao Polepole anakwenda kuwatoa nockout.
 
Ni ujinga mtupu kukaa kumzungumzia lowassa ni fisadi, wakati magufuli nae ni fisadi wa bilion 262
Ushahidi tafadhali, Lowassa watu wana ushahidi wakiwemo UKAWA wenyewe, Polepole, CCM na Marehemu baba wa Taifa.
 
Kwanini hao Channel ten wanampa popularity pole pole peke yake?? Ana haki miliki ya kipindi? maana kila muda ni yeye tu kwanini wasitafutwe wengine kutoka vyama vingine, yani awe ni pole pole versus wengine why??

Kuna harufu mbaya by the way nitakuwa naangalia mpira wa Man U kuliko kumuangalia Polepole.
 
pole2 hana hoja tena....kwasababu kila mtu anajua ataongea kuhusu lowasa...sio deal tena atafute kazi nyingine
 
Bora Mtatiro anajua kujenga hoja sio yule anaejiita Mchungaji ilikuwa ni aibu.

Badala ya kujenga hoja anamshambulia Polepole binafsi, na alichokera zaidi kusema watanzania wengi hatuujui ufisadi.!


kweli hatujua ufisadi hakuna mtanzani mwenye akili timamu na ameenda shule sio mkuuzulia madarasa ambaye angeshangilia upuuzi wa vyama kutumia watu wenye kashifa za ufisadi kungombea nafasi za kuongoza nchi kwa majibu mepesi yanayokuja kwa wakati usio sahihi.
 
Hata uwe mdaharo wa namna gani hautaweza itoa kura yangu kwa Lowasa.
Ahsante.
 
Polepole twende taratibu unawaumiza vijana.njtakuwepo hiyo saa nne kushuhudia mtanange.
 
Muda umeandikwa juu kabisa ktk paragraph ya kwanza mnanyong'ang'ana muda wwkati kaandika?nyie vipi
 
Back
Top Bottom