Nilichojifunza toka kwa Polepole:
CCM katika mchakato wake wa kupata wagombea urais imefanikiwa kuwaondoa mafisadi wake wakubwa waliokuwa na matumizi makubwa ya fedha ili kushawishi wajumbe wawapitishe katika uteuzi.
Mfumo ni zaidi ya CCM. Mfumo ni utendaji mzima wa Watumishi wa Umma, Sekta binafsi, Mahakama, vyombo vya ulinzi na usalama na taasisi zake. Kumuondoa Rais peke yake Hakuondoi mfumo.
Watanzania hawahitaji mabadiliko (Change of regime), wanahitaji Mageuzi (Transformation). Mageuzi ndiyo yanayoweza kubadili mfumo na hauwezi kurudia mfumo wa awali tena lakini change inaweza kuwa reversed.
Lowassa si mtu binafsi bali ni taasisi yenye wafanya biashara wakubwa ndani yake, isiyoweza kudhibitiwa kwa maamuzi yake. Ila yeye anaweza kuwadhibiti wengine kama inavyotokea sasa katika baadhi ya viongozi wa vyama vya ukawa kudhibitiwa.
Magufuri katika utumishi wake wote, amehudumu wizara zisizo za muungano ambazo msimamizi wake ni Waziri mkuu. Maana yake majukumu yake ni ya utekelezaji wa maagizo ya Bosi wake, Waziri mkuu. Mfano uuzwaji wa nyumba za serikali.