Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria...

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Rais Samia Suluhu amefanya mabadiliko na teuzi za sura mpya kwenye baraza la mawaziri. Uapisho utafanyika September 1, Ikulu ndogo Zanzibar saa tano kamili asubuhi.
1. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Doto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Awali alikuwa Waziri wa Madini.

2. Amemteua January Makamba kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali alikuwa Waziri wa Nishati.

3. Amemhamisha Balozi Pindi Chana kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Awali alikuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

4. Amemhamisha Steven Byabato kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali, Byabato alikuwa Naibu Waziri wa Nishati.

5. Amemteua Jerry Silaa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Silaa ni Mbunge wa Ukonga, Dar es Salaam.

6. Rais amemteua Anthony Mavunde kuwa waziri wa madini, mwanzo alikuwa naibu waziri wa kilimo.

7. Prof Makame Mbarawa aliyekuwa waziri wa ujenzi na uchukuzi amekuwa waziri wa uchukuzi.

8. Innocent Bashungwa amekuwa waziri wa ujenzi, mwanzo alikuwa waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.

9. Godfrey Kasekenya aliyekuwa Naibu waziri wa Ujenzi na uchukuzi ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Ujenzi

10. Alexander Mnyeti ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Kilimo

11. David Mwakiposa Kihenzile ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Uchukuzi. Ni mbunge wa Jimbo la Mufindi

12. Judith Kapinga ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa nishati, ni mbunge wa viti maalum Ruvuma.

13. Dunstan Kitandula ameteuliwa Naibu Waziri wa maliasili na Utalii, ni mbunge wa Mkinga

14. Stergomena Tax amehamishwa wizara ya mambo ya Nje kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

15. Angellah Kairuki amehamishwa kutoka TAMISEMI na kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii

16. Dkt. Damas Ndumbaro amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba ba Sheria na kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.




View: https://www.youtube.com/watch?v=7bLEuvgVGG4

======

PHOTO-2023-08-30-11-58-52.jpg

PHOTO-2023-08-30-11-58-54.jpg

PHOTO-2023-08-30-11-58-55.jpg

PHOTO-2023-08-30-11-58-57.jpg
 
Mkataba DP World umesababisha waziri, makatibu wakuu wizara ya uchukuzi na ujenzi kupanguliwa,?

1693385238136.png

Picha Toka maktaba : 2022 17 January , Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Balozi Eng. Aisha Amour akabidhiwa rasmi ofisi Tarehe. 17.01.2022.


Vigogo wa Wizara ya ujenzi na uchukuzi :

KATIBU MKUU UJENZI BALOZI MHANDISI AISHA AMOUR AWASILI RASMI WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI


EMMANUEL MBATILO ON JANUARY 13, 2022




Katibu Mkuu Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour (Kushoto), akipokea zawadi ya maua wakati akiwasili katika ofisi za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma



Katibu Mkuu Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour akisalimiana na watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), mara baada ya kuwasili katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dododma. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Ujenzi, Ludovick Nduhiye.



Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kumpokea Katibu Mkuu Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour (hayupo pichani), katika ofisi za wizara hiyo, zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Gabriel Migire - Katibu Mkuu Uchukuzi, Ludovick Nduhiye - Naibu Katibu Mkuu Ujenzi pamoja na Richard Mkumbo - Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango (Sekta Ujenzi).



Katibu Mkuu Ujenzi Balozi Mhandisi Aisha Amour akisaini kitabu cha wageni, mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma
 
Katiba na sheria Dr. Damas Ndumbaro aliwabeza sana walioshiriki mchakato wa katiba mpya wa bunge maalum la katiba juzi.
1693386898991.png


29 August 2023
Wamshukia vikali waziri Dkt. Ndumbaro kuhusu mikakati yake ya kudhoofisha katiba mpya


View: https://m.youtube.com/watch?v=wur22L2_Jn0&pp=ygUISmFtYm8gdHY%3D


28 August 2023

"Wanaotaka KATIBA MPYA Walikimbia Mchakato BUNGENI "Dkt Ndumbaro atupa dongo Mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais SMZ, Mawaziri wakuu wastaafu na wabobezi wengine


View: https://m.youtube.com/watch?v=ur0Th8eNHu0

Huku Dr. Ndumbaro akisikilizwa na kufuatiliwa kwa umakini na viongozi wazito ambao ni Makamu wa kwanza wa Rais SMZ Othman Masoud Othman ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Na mawaziri wakuu wastaafu, John Malecela, jaji Joseph Warioba na Mizengo Peter Pinda. Pia, wapo mawaziri wa zamani wa Wizara ya Katiba na Sheria akiwemo Dr. Mary Nagu, Balozi Mathias Chikawe, Profesa Palamagamba Kabudi, Dr. Harrison Mwakyembe na Dr. George Simbachawene....


Toka maktaba :
6 May 2023

Katiba mpya Rais Samia atoa maagizo mchakato kuanza, Baraza Vyama siasa laitwa​


1693386545754.png

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa lengo likiwa ni kuwashirikisha Wadau katika kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya Vyama vingi vya siasa nchini.

Rais Samia ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao kilichofanyika Ikulu ya Chamwino, kilichohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali kuhusu kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya.

Kikao hicho kimejadili namna ya kushirikisha Wadau mbalimbali na hasa ushirikishwaji wa Wananchi katika mchakato huo kutoka pande zote mbili Tanzania Bara na Zanzibar
 
Back
Top Bottom