Maandamano ya wanahabari Sept 11, 2012

Baada ya waandishi wa habari kumkuta waziri Nchimbi ndie anapokea maandamano yao ya kulaani mauji ya mwandishi Mwangosi wamemkataa waziri huyo kwa kupaaza sauti zao "Hatumtaki waziri Nchimbi"! waziri huyo ameamua kuondoka kwa aibu kubwa kweli ni fedheha kubwa kwa serikali.
 
Kwa mujibu wa Clouds FM jana ni kuwa waandishi wa habari wamezuiwa kuhitimisha maandamano yao viwanja vya Mnazi Mmoja kwa kuwa Halmashauri ya Ilala watakuwa wanafanya shughuli zao hapo!

Hii ndiyo Bongo bwana kuhakikisha kuwa maandamano haya yanadhoofishwa!
Hiyo radio nayo inabidi wanaharakaki wote tuanze kuisusia, kwani radio hiyo na TBC, ni kama mapacha, vyombo hivyo vinaendeshwa kwa propaganda, kwa lengo la kuibeba CCM!
 
Breaking News: Waziri Nchimbi afukuzwa katika maandamano ya waandishi wa Habari Jangwani, Duuuuh Aibu sana
 
du, hapo c waziri amekataliwa ni serikali, kwa kweli aibu yao, ila waandishi waangaliane maana wamesema yalitakiwa yapokelewe na jukwaa la wahariri, wanashangaa kukumta waziri wa mambo ya ndani, inaonekana wao wenyewe bado hawana umoja, kwani walikuwa hawajui waziri yupo? Na kwann mikoa mingne wamezuiliwa?wkt tamko lilitolewa.
je, waandishi wa TBCcm, Habari leo, Uhuru na Jambo leo wapo??

 
Naunga mkono maandamano, kama haki ya msingi ya kila raia kutoa maoni yake. Siungi mkono kitendo cha kuzomea waziri, kwa kuwa tendo la mauaji, si dhamira ya serikali wala chama chochote cha siasa, bali ni utendaji kazi mbovu wa mtu mmoja na wala si jeshi la polisi.
 
kitu chenye ncha kali, kitu kizito, habari za kiintelijensia, upelelezi haujakamilika, tumeunda kamati ya askari kutoka Dar es Salaam kuchunguza kama kilicholipuliwa na askari wa Iringa ni bomu au ni puto - hii bendi iliyoimba hizi nyimbo haijafika bado?
 
Angekuwa na akili timamu angekuwa ameshajiuzulu kwa mauaji yanayoendelea. Lakini sishangai kwani wote wenye mapenzi na CCM akili zao ndo zilivyo.
 
Mhariri wa nipashe anaongea sasa hv kawaasa polisi waache kuuwa wanahabari
 
Nadhani wengi tulio hapa JANGWANI na hata wale wanaofuatilia kwa karibu maandamano ni wazi kwamba Waandishi wa habari walichokifanya siyo kukataa kuongea na Waziri wa Mambo ya ndani bali walichokikataa ni Waziri huyo kuongelea Jukwaani. Nasema hivyo kwa sababu mara tu baada ya kushuka Jukwaani waandishi hao hao takribani wote wameonekana wakimwelekezea vinasa sauti Mh. Waziri, kumpiga picha na hata kumhoji.
 
Back
Top Bottom