Maandamano ya Kumpinga JK Washington DC

Status
Not open for further replies.

Kama ni wongo babu kubwa ndio huu, na hata maelezo yote ni kujikanganya tu, ni dhahiri mhuni fulani alileta hii mada hapa na sasa anajitahidi kujisafisha. Yako wapi aliyosema hapo awali anataka kumfungulia mashtaka mwanasiasa fulani nchini marekani?

Pesa za kutoka wapi za kuwagawia mamia ya waandamaji kuwanyamazisha kila mmoja kupata $25,000, kiasi ambacho ni sawa na pesa ya Tanzania Sh. 40.000,000? Sisi si watoto wadogo. Hii si kweli kabisa, ni uwongo mtupu. Uliwezaje kuingia kwenye mkutano wenu na mara ukageuka kuwa mkutano wa kukutana na Kikwete? Kwa nini hamkuondoka ndani ya ukumbi kama mlikuwa na malengo mengine?

Mode jaribu kuhakiki habari za watu wanaoingiza kwenye JF ambazo zinawapotezea watu muda wa kujadili badala ya kujadili mambo mengine ya muhimu zaidi.
 

Mkuu hii kitu "DICOTA" inazua maswali mengi kuliko majibu. Kwanini nasema hivyo: nilimuulizaga mwanakamati mmoja wa "DICOTA" hili swali; "uongozi/wanakamati wa DICOTA wamechaguliwaje"? Akasema wamejitolea. Nikamwambia kwani mna katiba au kitu cha kuonyesha malengo yenu ni nini hasa? Huyu mjumbe alikosa jibu lakunipa. Lakini kwavile tumesoma wote miaka hiyo; aliniambia yeye anachukulia kama social gathering. Nikamuuliza kwahiyo hiyo michango mlikuwa mnakusanya ni kwaajili ya social gathering? Mimi nikamuambia lazima ina ajenda sema haipo wazi na nilimueleza wazi nafikiri ni "CCM" wamekuja kivingine. Nilimueleza ajaribu kujiuliza kama ni just social gathering then nini umuhimu wakualika viongozi wa serikali tena kutoka Tanzania? Na je wanawaalika kuwauliza maswali au ndio business as usual "kusikiliza hotuba na kutoa misifa kem kem" Nikamwambia naona safu ya uongozi ni watoto au watu waliona na relation na viongozi wa CCM. Je hii is just a coincidence? Hakuwa na la kunijibu; kwa jinsi ninavyoona mimi;watanzania wengi as long kuna starehe/mteremko wa aina fulani, basi hawajiulizi maswali magumu wao wanafuata tu.
 

Kishongo una mjua Mwingereza personally? Mbona unasema ni CDM na sio UVCCM kama yeye alivyojitambulisha? Mimi nahisi huyu Mwingereza hana chama is just an attention seeker or just a confused individual if not an opportunist. Inawezekana pia alikuwa member wa chama cha siasa lakini alidhulumiwa au alinyimwa madaraka sasa anatoa frustration zake kivingine who knows. Either way kutumia huyu mtu for "Political attacks" haitawasaidia chama chochote maana sidhani kama kuna mtu ameshawahi kumuona personally. So far anaweza kuji-label vyovyote anavyotaka since nobody knows him. Kule facebook pia alijitambulisha kama UVCCM.
 
Mods kwanini msimpige ban ya kudumu huyu anayejiita Mwingereza?
 
wana JF acheni hasira picha sio hiyo kaweka ya 50 cent & JK hehehe, naona kila mtu katoa "like" aliyomwekea ..
 
Kama huyu Mwingereza ni UVCCM basi ni ishara nyingine kwamba CCM ni wababaishaji na wanaongea sana kuliko kutenda.
Crap!!!!
 
Nilikuwa nadhani mko makini na mikakati, lakini ujinga mliouonesha unaaibisha vijana wa kitanzania. Mnafanya vitu bila mikakati. Sijui mlitaka mhongwe? Maana inaonesha mna njaa tu. Sio wana mapinduzi. Moderator funga hii thread; haina mashiko tena.
 
Huu upuuzi wenu umenichosha, hakuna kituchochote kinacho eleweka, watanzania sasa tunachangamoto nyingi sana, halafu nyie mnatulazimisha kufuatilia tamthilia isiyo eleweka.
 
Nilikuwa najiuliza sana haya maandamano yalikuwa na lengo gani haswa! sasa naipata picha kusikia kwamba yalipata wafadhili kutoka Bongo nanyi ni wana CCM tena kutoka UVCCM, hivyo kwa mwenye kuelewa anafahamu kwamba hizo Millioni 3 na makundi kupewa Usd 25,000 zinaweza kuwaharibu watu wengi sana...

Kitu kimoja tu ktk historia ya dunia imeonyesha siku zote ni kwamba mwenye FEDHA siku zote ndiye mshindi hata kumshinda mwenye elimu kubwa, kwa sababu fedha siku hizi inaweza kununua elimu - MONEY is POWER...Na ndio maana siku hizi vijana wengi wa CCM wamechachamaa na kumpinga sana JK na sii chama baada ya kutangaza chama kujivua gamba..Na ukiunganisha dots ni rahisi sana kuelewa fedha zinatoka wapi na kwa makusudio gani hivyo lile swali langu la kuuliza mnafanya maandamano ili iweje, limejibika kirahisi kabisa.
 
Dah, still a long way to go kwa ubabaishaji huu!
 
Dah hembu nilipeni na mm huku, manake nimepoteza nguvu nyingi sana kuifuatilia hii li-sred la hovyohovyo!! Vipande vichache vya shilingi vimewaumbua
 
wanakijiji kwa uelewa wangu naye anaishi Marekani. sasa kwenye kuchangia hii mada ambayo wana Tz walioko Marekani wametuchakachua wenzao kwa kujidai wanataka kufanya maandamano wakati siyo kweli mbona yeye achangii??
 
Mimi navyojua wabongo wengi wanaoishi marekani hawana visa za maana alafu ndo mlikuwa mnategemea waandamane. Nazani huyo mwingereza ndio kiongozi wao wanatuaibisha tuu huko.
 
Hawa wapuuzi tu, watakuwa hawana ajira, wabeba maboksi tu. Wameniudhi sana. Usiweke tambo kama huwezi. Ni heri waishi kama kondoo. Hiyo update ya kununuliwa imenifanya nitamani kujinyonga.
 
Mimi nilijua kuwa huu ni usanii hasa waandaaji walipojitambulisha kuwa wao ni wana CCM. Jamani ni lazima tukubali ukweli kuwa wana CCM hawawezi kujisahihisha wenyewe. Hao wasioridhika na utawala wa JK wanatakiwa kutoka ndani ya CCM haraka sana, la sivyo wasitupotezee muda na attention yetu. Sasa nimegundua kuwa mapinduzi ya kweli yatafanyika bongo tu na si vinginevyo. Nyie wasanii mlioko ughaibuni kaeni kimya tu, mtuache muda si mrefu tutaikomboa nchi yetu.

CDM mwendo mdundo, ili kuharakisha mapinduzi hayo andaeni maandamano hapa Dar. Watu wana uchungu usio kifani, na mkizidi kuchelewa watu wataondoa imani na nyie pia na tutajichukulia majukumu ya ukombozi sisi wenyewe.

Nyie UVCCM msitupotezee muda, hamna nia ya kweli ya kuleta mabadiliko Tanzania, yuko wapi Nape na Chiligati. Tumechoka na tumechoka. Msimamo wangu toka awali ni kuwa CCM kamwe haiondoki kwa sanduku la kura, ya Misri, Tunisia, Libya ndio ufumbuzi wa nchi yetu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Kwanini walipokea hiyo pesa kama sio wala rushwa mashwain wakubwa??

Kumbe ilikua njaa tu, mara oooh tutaandamana, mara ohh hili....

pumbavu kabisa... kama mlitaka pesa mngesema jama ndugu zetu mlio bongo huku njaa kinoma tutumieni nauli, nasi tungewatumia

fooking corrupt dudes, what a shame really
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…