Expensive life
JF-Expert Member
- May 2, 2020
- 4,056
- 12,917
Ndugu zangu, ni wapi alipo Rais wetu wa awamu ya nne. Mh. Jakaya Mrisho Kikwete?
Hakuna kipindi ambacho wapinzani waliinjoi kama kipindi cha Kikwete. Walizoa wabunge wengi sana madiwani na wenyekiti wa vijiji.
Maisha ya wapinzani yalianza kuwa magumu pindi tu alipokaa pembeni Mh. Kikwete
Mara mwisho kumuona kwenye majukwaa ya kisiasa ni kipindi cha kampeni, uchaguzi mkuu 2025, ambao wapinzani wakuu Chadema walijiweka pembeni kudai reforms zifanyike kwanza.
Uchaguzi ulighubikwa na kashikashi nyingi, ikiwemo maandamano ya October 29, ambapo tume iliyoundwa na Mh. Samia Suluhu Hassan. Rais wa jamuhuri ya muungano Tanzania kuchunguza kile kilichotokea na kuja na majibu ya vifo vya watanzania 500+ katika maandamano yale.
Kwa sasa nchi yetu imekubwa na kashikashi kubwa sana za kiasa, ikiwemo katiba mpya, uchunguzi huru kwa yale yaliyotokea October 29.
Mh. Kikwete yeye ndiye Rais wetu pekee mstaafu aliyebaki, hivyo kama raia tunamtegemea sana kutuvusha katika giza hili zito, hapa nchini. Ukimya wake unatupa maswali mengi sana sisi raia.