Maajabu ya serikali ya CCM: Spika wa Bunge ana kinga na hashtakiwi, Wabunge wanatunga sheria lakini hawalipi kodi!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
12,196
2,000Mbunge anakunja milioni ishirini na mbili (22,000,000/=) kwa mwezi lakini halipi kodi

Mbunge huyo huyo anatunga sheria ya kodi huku yeye akijipa kinga ya kutolipa kodi!

Pesa anazolipwa Mbunge zinatokana na kodi ya ambao hata mlo moja kwa siku ni shida!

KumbeTanzania inajengwa na wazalendo lakini inaliwa na walafi CCM wenye meno!

Yaani Wazalendo wanahangaika juani ili kuwawezesha wabunge CCM kula kivulini!

Kwa ufahamisho tu ni kwamba kwa kuwa idadi ya Wabunge tulio nao inakaribia mia nne;

1. Kipato...
  • Wabunge 400 @ sh. 22,000,000 kwa mwezi ni sawa na sh. 8,800.000,000 kwa mwezi!
  • Wabunge 400 @ sh. 264,000,000 kwa mwaka ni sawa na sh. 105,600,000,000 kwa mwaka!
  • Wabunge 400 @ sh. 1,320,000,000 kwa miaka mitano ni sawa na sh. 528,600,000,000 kwa miaka mitano!
  • Hizi hela wakigawiwa Watanzania wote 60,000,000, kila Mtanzania (vichanga hadi vikongwe) atapata sh. 8,800
2. Mkopo...

Wabunge 400 @ sh. 90,000,000 ni sawa na sh. 36,000,000,000
  • Hizi hela wakigawiwa Watanzania wote 60,000,000, kila Mtanzania (vichanga hadi vikongwe) atapata sh. 600
3. Kiinua mgongo...

Wabunge 400 @ sh. 240,000,000 ni sawa na sh. 96,000,000,000
  • Hizi hela wakigawiwa Watanzania wote 60,000,000, kila Mtanzania (vichanga hadi vikongwe) atapata sh. 1,600
Hii ni kufuru na haikubaliki!
Je hawa Wabunge wanatufanyia nini sisi wananchi zaidi ya kutafuna kodi zetu?

Adui nambari wani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni CCM, period!
 
Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
12,196
2,000
22,000,000 mchanganuo ukoje?
Kipato cha mbunge...

Mbunge analipwa mshahara wa sh 3,800,000 kwa mwezi, Anapata posho sh 8,000,000 kila mwezi, jumla 11,800,000.
Akiwa kwenye kikao analipwa posho ya kikao sh. 240,000 na posho ya kujikimu sh. 120,000, jumla 360,000.

Kwa kuwa Bunge la bajeti linakaa kwa miezi mitatu, akihudhuria vikao vyote anapata 32,000,000 (wastani wa 10,000,000 kwa mwezi)
Katika miezi mitatu ya bunge la bajeti Mbunge ana uhakika wa kukunja 22,000,000 kila mwezi.

Kwa kifupi ni kwamba wanavuna kwenye shamba ambalo hawakushiriki kulilima.

Na hapo hatujaongelea...
  • Mkopo wa gari ............................. 90,000,000!
  • Kiinua mgonggo......................... 240,000,000!
 
Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
12,196
2,000
Huwa najiuliza ni wapiga kura ndio hamnazo au wabunge wanapitishwa kimabavu, hii ni too much. Wafanya biashara wakubwa wanapata msamaha wa kodi.
Cha ajabu hawa wahuni hakuna wanachofanya bungeni zaidi ya kugonga meza. Wanasahau ni wawakilishi wa wananchi na badala yake wamekijika katika kuitetea serikali hata pale Katiba inaposiginwa wazi wazi.

Wanatunga sheria za kuwakomoa wananchi badala ya kuwatetea. Kwa sababu wanatetea tu matumbo yao, hawataki mjadala wowote unaohusu kuandikwa kwa Katiba mpya wakiogopa kunyang'anywa tonge mdomoni.!
 
Paf

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,715
2,000
Asante kwa mchanganuo.

Wabunge wawapo Dodoma wanaishi hotelini kwa gharama zao au wamepewa nyumba na serikali?

Spika hesabu yake ikoje?

Yaani malipo ya mwezi ni sawa na kuchimba kisima kijijini kwangu wananchi wakapata maji
 
Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
12,196
2,000
Peleka mahakamani
Hata huko Mahakamani si wamejaa hao hao makada wa CCM? Nani atakuteua uwe Hakimu au Jaji kama wewe sio kada?

Mvunja Katiba Mkuu ndiye huyo huyo Mkuu aliyeapa kuihifadhi, kuilinda na kuitetea na vyombo vyote vya kumsaidia kapewa na kuvimiliki! Na bahati mbaya kwa Tanzania ni kuwa, Mkuu huyo si mwingine bali ndiye Mwenyekiti wa CCM.
 
The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,618
2,000
Wizi wa kisheria,rais,na wabunge hawalipi kodi wamejitungia sheria wasilipe kodi kama kodi ni muhimu kwa nini wao watunge sheria ya kujitoa kwenye kodi hili halikubaliki.
Ndiyo maana sasa wameamua kuwa aggressive kiasi cha kuzuia makongamano ya katiba...

Ndiyo maana hawa "WAZALENDO UCHWARA" wako tayari kuua watu ili kulinda nafasi zao za ulaji...!!

Hii kamwe siyo haki na haikubaliki hata kidogo. Tukatae na kila mtu apaze sauti yake kuhusu hili kupitia kila nafasi na jukwaa atakalopata ili kila mtu wakiwemo watoto wawajue wabaya na maadui zao...!!
 
Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
12,196
2,000
Spika hesabu yake ikoje?
Huyo ndio usiseme kwani kwa nafasi yake kama mtumbuaji mkuu aliwekewa hadi kinga na anaowaongoza! Kwa uchambuzi wa ripoti ya CAG, Bw. Job Ndugai aliwahi kutumwa India kwa matibabu yasiyojulikana na kulipwa dola 1,200,000 sawa na Sh. 2,500,000,000!

Na kusema kweli CCM, kwa miaka zaidi ya hamsini, imeitafuna nchi hii kama nzige, bila huruma na bila kulala!
 
ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
11,178
2,000
Wizi wa kisheria,rais,na wabunge hawalipi kodi wamejitungia sheria wasilipe kodi kama kodi ni muhimu kwa nini wao watunge sheria ya kujitoa kwenye kodi hili halikubaliki.
Hivi mapolisi wanalipa kodi? Mbona wamekaa kimisukule kuwalinda HIVI wasiolipa kodi?
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,943
2,000
View attachment 1857456

Mbunge anakunja milioni ishirini na mbili (22,000,000/=) kwa mwezi lakini halipi kodi

Mbunge huyo huyo anatunga sheria ya kodi huku yeye akijipa kinga ya kutolipa kodi!

Pesa anazolipwa Mbunge zinatokana na kodi ya ambao hata mlo moja kwa siku ni shida!

KumbeTanzania inajengwa na wazalendo lakini inaliwa na walafi CCM wenye meno!

Yaani Wazalendo wanahangaika juani ili kuwawezesha wabunge CCM kula kivulini!

Adui nambari wani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni CCM, period!

Screenshot_20210715-193208_Photos.jpg
 
Ifike wakati sasa tuamke, stahiki zao zipangwe na wananchi siyo wajipangie wao, teknolojia imetufungua sasa
 
sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
5,590
2,000
Kipato cha mbunge...

Mbunge analipwa mshahara wa sh 3,800,000 kwa mwezi, Anapata posho sh 8,000,000 kila mwezi, jumla 11,800,000.
Akiwa kwenye kikao analipwa posho ya kikao sh. 240,000 na posho ya kujikimu sh. 120,000, jumla 360,000.

Kwa kuwa Bunge la bajeti linakaa kwa miezi mitatu, akihudhuria vikao vyote anapata 32,000,000 (wastani wa 10,000,000 kwa mwezi)
Katika miezi mitatu ya bunge la bajeti Mbunge ana uhakika wa kukunja 22,000,000 kila mwezi.

Kwa kifupi ni kwamba wanavuna kwenye shamba ambalo hawakushiriki kulilima.

Na hapo hatujaongelea...
  • Mkopo wa gari ............................. 90,000,000!
  • Kiinua mgonggo......................... 240,000,000!
Kwa hiyo tuseme adui mkubwa wa maendeleo na uhuru wa taifa letu ni Bunge.
Bunge ni kupe,bunge limegeuka wanyonyaji,bunge ni kikwazo cha mwananchi wa kawaida,bunge ni kinyume cha Azimio la Arusha, Bunge ni fursa ya kula bila kunawa,ni bunge ni biashara kubwa isiohitaji mtaji mkubwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom