Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,063
- 22,755
Mbunge anakunja milioni ishirini na mbili (22,000,000/=) kwa mwezi lakini halipi kodi
Mbunge huyo huyo anatunga sheria ya kodi huku yeye akijipa kinga ya kutolipa kodi!
Pesa anazolipwa Mbunge zinatokana na kodi ya ambao hata mlo moja kwa siku ni shida!
KumbeTanzania inajengwa na wazalendo lakini inaliwa na walafi CCM wenye meno!
Yaani Wazalendo wanahangaika juani ili kuwawezesha wabunge CCM kula kivulini!
Kwa ufahamisho tu ni kwamba kwa kuwa idadi ya Wabunge tulio nao inakaribia mia nne;
1. Kipato...
- Wabunge 400 @ sh. 22,000,000 kwa mwezi ni sawa na sh. 8,800.000,000 kwa mwezi!
- Wabunge 400 @ sh. 264,000,000 kwa mwaka ni sawa na sh. 105,600,000,000 kwa mwaka!
- Wabunge 400 @ sh. 1,320,000,000 kwa miaka mitano ni sawa na sh. 528,600,000,000 kwa miaka mitano!
- Hizi hela wakigawiwa Watanzania wote 60,000,000, kila Mtanzania (vichanga hadi vikongwe) atapata sh. 8,800
Wabunge 400 @ sh. 90,000,000 ni sawa na sh. 36,000,000,000
- Hizi hela wakigawiwa Watanzania wote 60,000,000, kila Mtanzania (vichanga hadi vikongwe) atapata sh. 600
Wabunge 400 @ sh. 240,000,000 ni sawa na sh. 96,000,000,000
- Hizi hela wakigawiwa Watanzania wote 60,000,000, kila Mtanzania (vichanga hadi vikongwe) atapata sh. 1,600
Je hawa Wabunge wanatufanyia nini sisi wananchi zaidi ya kutafuna kodi zetu?
Adui nambari wani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni CCM, period!