Heshima mbele wakuu... Naona NSSF wameamka na kuturudishia moyo wa hili lidaraja letu...
Mkuu GT, nadhani ule muziki tulioahidiwa utatusaidia kuangalia hayo mkuu aliyosema (red and underlined)
Inatia moyo kuwa na hizo 6 lanes, hii inaonyesha kuna long term planning hapo..... Bravo to them!!! Kituo cha mabasi ya mikoa ya kusini, pia ni point up kuwe na distribution ya misongamano!!! Hilo la waenda kwa miguu ndio BEST of them all!!!
Sasa kwa hizi data chache naona ka moyo kangu kameanza kufunguka kwa hili swala!!
Mugu Ibariki Tanzania na watu wake!!!
Daraja la Kigamboni sasa kujengwa mwakani
2008-05-27 10:13:51
Na Mwandishi Wetu aliyekuwa Zanzibar
Baada ya wananchi kusubiri kwa muda mrefu na kuonekana kama hadithi za sungura na paka, umetolewa uthibitisho kwamba, daraja litakalounga eneo la katikati ya jiji la Dar es Salaam na Kigamboni litaanza kujengwa mwaka kesho.
Akiongea katika semina ya Wahariri mjini Zanzibar, Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSFI), Bw. Yakoub Kidula, alisema ujenzi wa daraja hilo unatazamiwa kuchukua muda wa miezi 24 kukamilika.
``Ujenzi wa hili daraja unatazamiwa kuanza katikati ya mwaka 2009 na pale utakapoanza rasmi tunatazamia kwamba utachukua kipindi cha miezi 24 kukamilika,`` alisema Bw. Kidula wakati akijibu maswali ya wahariri.
Alisema ujenzi wa daraja hilo ulionza kuratibiwa na serikali toka miaka 60, ulikuwa unakwama kwa sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni fedha.
``Yote yaliyochelewesha ujenzi wa hili daraja si mambo mabaya. Ni sababu ambazo zilikuwa zinalenga katika kupata ufanisi mzuri zaidi,`` alisema mkurugenzi huyo na kuongeza daraja hilo linatazamiwa kuwa na njia sita za kupita magari yatakayokuwa yanatozwa ushuru.
Hata hivyo alisema waenda kwa miguu hawatatozwa chochote.
Awali, mada kuhusu ujenzi wa daraja hilo ilikuwa itolewe na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau, lakini alipata msiba jijini Dar es Salaam na kulazimika kuondoka kabla hawajaiwasilisha.
Mapema akiwasilisha mada hiyo kwa niaba ya Dk. Dau, Mhandisi wa NSSF, Bw. John Msemo, alisema NSSF ilianza utafiti wa awali wa ujenzi wa daraja hilo unaotazamiwa kugharimu Euro milioni 45, mwaka 2003.
``Utafiti wa kina ulifanyika kati ya Juni na Agosti 2004, kisha tukawasilisha mapendekezo yetu serikalini,`` alisema Bw. Msemo.
Alisema ujenzi wa daraja hilo utakapokamilika utasaidia pia upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam.
``Mbali na kupunguza wingi wa watu katikati ya jiji, daraja pia litahamasisha ujenzi wa viwanda na majengo ya biashara kwa upande wa Kigamboni, mahoteli ya kitalii, nyumba zaidi za makazi na kituo cha mabasi ya kwenda mikoa ya kusini,`` alisema Mhandisi Msemo.
SOURCE: Nipashe, www.ippmedia.com