Maajabu ya daraja la Kigamboni!

Mwanagenzi

JF-Expert Member
Sep 11, 2006
694
212
Naona kama maajabu...
Mmiliki wa hii kampuni, kadri inavyodaiwa na polisi, anatafutwa kuhusiana na kuzama kwa meli yake, Mv Nyamageni, huko Ziwa Nyanza (Victoria!). Juzi juzi wakadai wanamwekea mitego ila anaiepa japo kwa sasa (wakati huo) alikuwa Dar. Haijapita wiki kampuni yake inapewa tenda na wakati kuna kesi ya kuzama kwa meli yake!

Ni kweli kwa sasa hana hatia kwani hajafikishwa mahakamani au kuhukumiwa hivyo, japo ripoti ya Mramba kuhusu kuzama huko kulionyesha kuwa kuna uzembe ulifanyika uliosababisha ajali hiyo, japo kama kawaida ya Bongo, ripoti haikuwekwa yote hadharani. SUMATRA wanasemaje? Idara ya Vivuko mnasemaje? Au ndiyo yale yale ya MIKATABA MIBOVU TULIYOZOEA NCHI HII?

IMALASEKO kuipa serikali mil. 100/- kila mwezi

na Agnes Yamo

KAMPUNI ya IMALASEKO imeshinda zabuni ya kusimamia makusanyo katika vivuko vya Feri, Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Umeme na Ufundi, katika Wizara ya Miundombinu, Mhandisi Mshauri John Ndunguru, alisema IMALASEKO walifanikiwa kushinda zabuni hiyo baada ya kuishinda Kampuni ya Dengard System.

“IMALASEKO imefanikiwa kupata zabuni hii kwa kuilipa serikali sh milioni 100 na kuishinda Kampuni ya Dengard System iliyopanga kuilipa serikali sh milioni 80 kwa mwezi.

“Makusanyo katika vivuko hivyo kwa siku ni kati ya sh milioni 3.5 na milioni 4, lakini baada ya kufunga mtambo wa kukata tiketi, ikabainika kuwa tuna uwezo wa kukusanya mpaka milioni 10 kwa siku,” alisema Ndunguru.

Uamuzi wa serikali kubinafsisha ukusanyaji wa mapato katika vivuko hivyo ulikuwa na lengo la kudhibiti upotevu wa fedha uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watendaji wa vivuko. Kampuni ya IMALASEKO ilishinda zabuni hiyo mwishoni mwa Novemba na imeanza kazi Desemba 4, mwaka huu.

Source: Tanzania Daima 17 Desemba 2006.
 
Mwanagenzi: Hivi haya mambo mawili yanahusiana hee? Naona kama yanatofati na lile la meli halitoshi kumnyima tenda huyu bwana especially kama kesi yenyewe bado ipo katika hatua ya tuhuma. Sijui lakini!
 
Sasa naamini huyu jamaa wa Imalaseko analindwa na serikali na polisi wake.Suala la kusema walimuekea mitego wamkamate ni usanii tu.Inawezekanaje awe anatafutwa na polisi kwa kesi ya kuzama Meli, tena anashinda Tenda ya Serikali? Hapa kunamaswali kibao ya kujiuliza. Inawezekana kwa kwa kuwa ile meli ilizama ziwani, aihusiani na vyombo vya baharini kwa sababu ziwani ni maji baridi na Baharini ni maji chumvi?
 
Kuna mtu na kuna kampuni. Inawezekana kampuni ilishinda tenda, na kuna mtu kwenye kampuni anatafutwa na polisi. Hakuna utata hapo.

Mtu anayetafutwa na polisi hajatiwa hatiani, wala si jukumu lake kuthibitisha kwamba hana kosa.

Serikali inakosa mwelekeo kuhusu kivuko. Mpango sahihi si kutoa tenda ya kukusanya nauli, bali ni kujenga daraja la kuunganisha Kigamboni na Feri, ikibidi kwa njia ya BOT (build, operate and transfer). Fedha za kufanya hivyo zipo, na nielewavyo ni kwamba NSSF walishaonyesha nia ya kuwekeza kwenye hilo daraja. Kinachokosekana ni vision toka serikalini.

Augustine Moshi
 
nadhani ni bora kufanya research ya kutosha kuhusu hili kabla ya mtu kupost

details zote ziko kwenye public domain
 
Wewew DrWho unataka utafiti gani zaidi ya huo uliopo!!! Kama hukubaliani na Gazeti la Tanzania Daima lililoandika, basi mwambie huyo Br. wako akalishitaki, Au nawewe umekula cha juu nini kwenye hiyo tender. !!!!
Kama wameweka machine ambayo najua imegharimu pesa nyingi sana na inasaidia kukusanya 10M per day, kwa nini wampe mtu binafsi akusanye 300M na kutoa serikalini 100M,!!!!! Hata kwa Poorman kama mimi hesabu zaziingii kabisa!!! sielewi hao watendaji wa serikali wanafanya kazi kwa manufaa ya nani:??? Na je , Huyu Ari mpya na mwenzake hawalioni hili???. Najua tukifuatilia tutakuta Mramba anahusika tu, kwani mikataba hiyo ni razima imesainiwa wakati wa Mramba.
 
Hizi tender za ushuru huwa zina pesa nyingi sana,ukiona wamesema kuna uwezekano wa kukusanya milioni 10 kwa siku ujue wanaweza kukusanya hata milioni 12.

Kitu ambacho sikielewi ni hichi,kama serikali inajua inaweza kukusanya milioni 300 kwa mwezi,why accept 100? They should have re tendered,maana haikufika hata nusu ya projected figures.

I know someone who has been in involved in something like this before,na amount yenyewe ilikuwa ndogo sana kulinganisha na hii,lakini wote hawakufikia hata nusu ya makusanyo yaliyokadiriwa na ilitangazwa upya.

Sasa huko nyuma walikuwa wanakusanya milioni 3.5 mpaka 4 kwa siku,sasa wanasema watakusanya milioni 10,ina maana walikuwa wanakula milioni 5 au zaidi kila siku huko nyuma,mbona hakuna maswali yeyote kuhusiana na hilo?Hii ni mifano mizuri ya jinsi pesa inavyotafunwa kwenye hii nchi.

Halafu cha ajabu zaidi ni kwamba vivuko vyenyewe kila siku ni vibovu,na havitengamai.Ina maana kama vikifanya kazi vizuri watakusanya zaidi ya hapo. Kwa hio kuna uwezekano mkubwa tu kuwa vinaharibiwa makusudi,ili kuficha hayo mapato zaidi.Ni kama dereva wa daladala anavyomdanganya bosi wake kuwa kashinda polisi siku nzima,kwa hio mapato ya siku hio ni madogo sana,au hakuna kabisa!
 
POORMAN

hebu niweke wazi bro wangu ndio yupi huyo

jambo la pili unajua mimiiku zote huwa niko wary na ripoti za magazeti ndio maana unakuta humu mijadala haiendeshwi kwa sababu gazeti limeeandika kitu

ndio maana kuna topics kama za RICHMOND ambazo zinaulizia FACTS na sio facts za magazetini ambayo mengi yanaandka udaku na ushabiki


sasa hebu wizara ya UJENZI utapewa taarifa yote ya ujenzi wa daraja hilo kwani zipo pale na wewe kama mlipa kod unastahhili kuziona

then utaelewa funding zilitoka wapi za huo ujenzi


ukigonga ukuta nitakupa contact hapo DAR ya kupata nyaraka za contract nzima

sasa baada ya kusoma kwa kina then njooo tujadili
 
Kitu hakijatamkwa na yoyote hapa ni ukweli kwamba kampuni iliyopata tenda lazima itapandisha sana nauli. Hilo lipo, waathirika (watu wanaotumia kivuko mara kwa mara) wajitayarishe kulipa sana! Kuna kitu kinaitwa possession mania. Hata faida ikiwa kubwa, lazima watapenda kupata zaidi, na ikibidi watashirikiana na wanaoidhinisha nauli. Kukamuliwa kwaja! Si mmeona wenyewe Tanesco!

Augustine Moshi
 
Kwanza najiuliza, kulikuwa na umuhimu gani "kubinafsisha" utozaji nauli?

Nadhani usafiri kati ya Kivukoni na Kigamboni, au hata ukiwekwa sehemu nyingine, ni huduma ya serikali kwa jamii na si biashara kama vile usafiri wa mabasi kutoka Dar kwenda Moshi, au Dar kwenda Mafia, mathalani, ambako unaweza kusema waachiwe wafanyabiashara wafanye kazi hiyo. Kivuko kama hicho kichukuliwe tu kama vile barabara ya kati ya Magomeni na Manzese ambako watu (na vyombo vyao) hupita bila kulipia na ndiyo maana ushuru kwenye vivuko (kwa umbali kama huo wa Kigamboni-Kivukoni) unapaswa kuwa mdogo tu kusaidia uendeshaji na si gharama halisi.

Maadam tumeambiwa na mabosi wetu (IFIs) kuwa serikali isimamie utawala na isifanye biashara basi tunafuata tu! Ingekuwa ubinafsishaji huo unaongeza tija, ufanisi au hata kutengeneza ajira ningewaelewa. Sasa kuna haja gani ya serikali kupoteza mapato kiasi hicho? Kwani hawawezi kununua hizo mashine za kutoza nauli kisha wao wenyewe (serikali) wakapata pesa nyingi zaidi ili zitumike kuboresha huduma si tu kwenye vivuko vyetu bali hata kwenye maeneo mengine?? Usafiri kwenye vivuko si sawa na biashara ya maduka ya RTC; ni sawa hayo serikali iachane nayo. Lakini si vivuko...

Siku mwenye mashine akisema zimeharibika huduma ya usafiri itakuwepo au haitakuwepo? Si ajabu nako kuna mkataba wa ajabu ajabu!
 
Japo mlichelewa lakini mmefika, maana Waswahili walisema "Kawia ufike!Imalaseko yafukuzwa kukusanya mapato Feri

na Mwandishi Wetu

SERIKALI imekatisha mkataba na Kampuni ya Imalaseko ya Dar es Salaam iliyoshinda zabuni ya kukusanya mapato katika vivuko vya Feri, Dar es Salaam.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Wizara ya Maendeleo ya Miundominu, kiliiambia Tanzania Daima kuwa mzabuni huyo alifukuzwa Januari 2, mwaka huu, siku chache baada ya kusaini mkataba.

“Kufukuzwa kwake kumetokana na mzabuni huyo kutaka kuwafukuza wafanyakazi wote wa Feri walioajiriwa na wizara kwa lengo la kuwaleta watu wanaowataka wao, jambo ambalo wizara halikukubaliana nalo.

Hata hivyo, baadaye mzabuni huyo aliiandikia wizara barua na kueleza kushindwa kwake kufanya kazi hiyo, na hivyo wizara kuchukua hatua ya kumfukuza,” kilieleza chanzo hiko.

Mzabuni huyo aliyeshinda zabuni ya kukusanya mapato katika vivuko vya Feri na kusaini kuilipa serikali sh milioni 100 kila mwezi, tayari ilikwisha ilipa serikali sh milioni 100 na imefukuzwa kabla ya kufikia mwezi mmoja jambo ambalo ni hasara kwa kampuni husika.

Habari zaidi zilisema kuwa baada ya kufukuzwa kwa mzabuni huyo, kazi ya makusanyo katika vivuko hivyo imerudishwa mikononi mwa serikali na huenda kitengo hicho cha ukusanyaji mapato kisibinafsishwe tena.
 
Jamaa kwa nini alitaka kuwafukuza watu wote ? Kwa nini kaamua kuacha tenda ? Je pesa atarudishiwa ama Mkataba ulisemaje ?
 
Is A Breach Of Contract, Imalaseko Failed To Fulfil The Obligation Can't Sue For Damages! He Wants To Relay On Undue Influence Sign Contract Without Having Enough Knowledge On It
 
Kuna taarifa kuwa kuna watawala ofisi kuu tatu za serikali ambao wana conspiracy daraja la kigamboni lisijengwe. Hii sitoileta kwa style muziki kama MKJJ lakini I wont hesitate to drop names.Hivyo nawaomba radhi wale ambao wataona majina ya hao watawala ambao wako karibu nao

Nipeni muda namalizia ku compile file zima
 
Mkulu GT,

Ni kweli kuna kiwingu kikubwa kimetanda katika sakata zima la ujenzi wa daraja la Kigamboni.

Last time I checked serikali ya Holland wamekubali kutoa grant ya 50% ya cost ya daraja lote. For reasons best known to themselves, wizara ya Miundo Mbinu pamoja na wizara ya Fedha wamekuwa wakikwamisha kwa makusudi juhudi za ujenzi, inasemekana wizara ya Miundo Mbinu wapo radhi daraja lijengwe na watu wengine (mbali na wadachi) na serikali igharamie in FULL.

Sasa swali ikiwa kuna 50% grant yes GRANT sio LOAN ( condition ni kuwa kampuni za kidachi tu ndio zishindanie tenda)ni vipi watu wanang'ang'ania serikali igharamie in FULL?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom