Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
Hivi hili tangazo lilitolewa kwenye Daily news tu?
Wenye pesa zao nje ya TZ wametangaziwa vipi kwa sababu sidhani kama kuna kampuni yoyote ya kitanzania ambayo ina uzoefu na utaalamu wa PPP hasa ya barabara na madaraja? Au haya makampuni ya nje yataletwa kupitia connection zao na wanasiasa tu kama Richmond n.k?
Suala la kuwa makampuni ya Tanzania yataweza au la nadhani hilo litaamuliwa na wataalam
lakini mimi nimeliona tangazo mpaka kwenye site ya UNDP na kama kuna kampuni ambayo iko serious kufanya hii shughuli then sidhani kama kutakuwa na tatizo hata kidogo kujua kama kuna tenda imetangazwa sasa sidhani kama kuna tatizo la kupata hizo kampuni kwenye pre qualification
Na hapa inabidi NSSF wapewe apate credits kwani kila kitu kiko wazi na Open sasa hatujui kama huko mbele wanasiasa kama akina Magufuli na akina Mgonja na wapambe wao wakianza kutia mikono yao kama wizara ya ujenzi walivyofanya
Kilichonisikitisha ni kuwa GREY MGONJA deliberately aliamua kutotoa hiyo LETTER OF PRIORITY AND GUARANTEE kwa ajili ya ujenzi wa daraja. Sasa kama si UFISADI sijui ni nini lakini kesho tutakwenda kwenye uchaguzi huku ilani ya uchaguzi haijakamilika
halafu mlikuwa mnatafuta nani wanaomsabotage JK
Sasa hivi hatujui kwa nini directives za Rais zinapuuzwa left and right na cha kujiuliza directives ngapia za Rais hawa jamaa washazipuuza.
Sijui KAPUYA naye kasimama wapi kwenye hili lakini simsikii babisaa lakini usije shangaa kuwa naje kafunikwa na akina Kijazi kwenye hili
In short hii issue ya daraja la kigamboni inaonyesha jinsi gani serikali yetu inavyoyumba. Leo hii nadhani ilitakiwa hii kitu ishakamilika kisha sisi tuanze kulalamikia mambo mengine