Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,625
Tukio hilo limetokea wakati waandishi wa habari wakirekodi tukio la wafanyakazi wa makaburi ya Langata kugoma wakilalamika kucheleweshewa mishahara yao, ambapo polisi waliwataka waandishi wa habari waondoke kutoka eneo la tukio.
Shughuli za mazishi zilisitishwa katika makaburi hayo, baada yawafanyakazi hao kugoma sababu ya kutolipwa mishara yao ya miezi 5.
Afisa wa polisi wa kike aliyerekodiwa kwenye tukio hilo akiwanyanyasa waandishi hao kwa kuwasukuma mwandishi na mpiga picha wakiwa wanaripoti tukio hilo amekosolewa vikali na Wakenya.
Mmoja wa wandishi wa habari aliyefanyiwa tukio hilo kutoka Citizen TV, Mary Mouki amesema tofauti kati ya polisi na wao ilizuka baada ya waandishi wa habari kuhoji hatua ya polisi kurusha mabomu ya machozi kwa waombolezaji ambapo wawili walijeruhiwa katika tukio hilo.
Citizen TV