Luhanjo atoa ripoti, Jairo arudishwa kazini

nimerifikilia hili pia ningekuwa mimi nafikiri ningefikiria jinsi ya kujiuzuru.huu ni uhuni watu wako tayari kulindana kwa namna yoyote(serikali full madudu) lakin yatakuja mengi tuone luhanjo kama ataweza. mbya zaidi wana mtafuta aliyepeleka barua- huu ni uttoto sasa
 
<br />
<br />
Wanajf habari hii ni ya kweli kwa sababu BBC SWAHILI jion ya leo wametoa hiyo taarifa usitie ofu ndo serekali ya magamba wanafanya vitu kama magamba tu .
 
Nimechoka kabisa na hii nchi pamoja na sirikali hii ya ******.nahama nchi,nahamia somalia,kule mtu ukileta upuuz ni unajinyongea kwa mtutu na hakuna wa kukuuliza.ngachoka kabisa mmeku,ye wooooomi,kiki Ruwa mangi eh!
 
Serikali kwa mara nyingine inapima uvumilivu wa Watanzania, na kwa wale waliokuwa wanahoji ni kwa nini Philemon Luhanjo hajastaafu kwa mujibu wa sheria, basi leo ndio mtakuwa mmezitambuwa kazi za Wazee hawa pale Ikulu.

Leo sina la kuchangia naelekea jukwaa la MMU, hapa tutazidishana hasira bure bila sababu za msingi.
Reminder: Wale mnaondaa maandamano ya kumpinga huyu Mswahili Mkwerre hapo Washington DC nadhani sababu zenu za kuandamana zinazidi kuongezeka, huyu Mswahili hakifumbiwa macho hii dhiki iliyopo itawamaliza Watanzania. huyu ni shetani kabisa anatakiwa aondolewe madarakani sambamba na Gaddafi.
 
Mm sijui cha kusema washika dau,ss hizo fedha zilichangwa ku-facilitate nini na zinakuwa accounted for kivipi?si public money hizo?sijawaelewa kbs hawa jamaa wawili na mvi zao
 
Unapoingia kwenye thread kama hii hakikisha Daktari wako amekuruhusu baada ya kukufanyia vipimo vyote muhimu kama presha n;k. Rostam aliposema anaachana na Siasa uchwara wengi hamkujuwa ana maana gani, ukweli ni kwamba yeye anaifahamu fika CCM na serikali yake na hakuna mwenye usafi wa kumnyooshea mwenzake kidole.

Kuna huyu dogo anaitwa Nape Nnauye kama hatakuwa amepata somo kwenye hili la Jairo basi atakuwa ni kichaa kuendelea kumuamini Kikwete, wakati Kikwete ametosa Waziri mkuu wake Pinda ambaye alisema wazi mbele ya Bunge na Hansard zipo, kwamba kama angekuwa na Mamlaka basi Jairo angekuwa out, lakini Jairo mamlaka yake ya nidhamu ni Rais mwenyewe.

Tukumbuke wazi kwamba mke wa mfalme hatakiwi hata kutuhumiwa. Je na hili linahitaji kuundiwa kamati teule ya Bunge? Ni nini kazi ya TAKUKURU?
 
Sijui niongee neno gani ili lifae hapa. . .
 
DJ kweli wa mwenyewe, tunabaki hili haliwezekani tu, kesho tunapigwa na kimbunga kingine tunaangaika nacho, hili linakuwa la kujumlisha kama matukio mengine yaliyopita, mimi naamini anayefanya hii kazi ya kucheza na akili zetu ni lazima atakuwa mtu mwenye ujuzi wa hali ya juu sana, kila siku unasikia mavitu ya ajabu tu, watu tunapiga kelele,siku,wiki,miezi,miaka vyote vinapita, viongozi ni walewale maisha ni yaleyale na kelele zetu ni zilezile, ndiyo maana kuna viongozi wakubwa wa nchi yetu wanapenda sana tumia msemo wa kelele za chura.........,
 

Mkuu Mwanakijiji, hivi unafikiri nini madhara ya hii kwa yule Nabii wa Nigeria (Joshua I think), maana huyu alikuwa ana-act kama mwakilishi wake hapa bongo. Kumbuka ujumbe aliotoa kwa shoga yake kuwa Nabii kamwambia kuwa Lowassa will be the next president he he he ... then mara Lowassa kasamehewa makosa yake yote (yepi?). Last week wakati anachangia bajeti ya Wizara ya Maliasili alisema kuwa 'mungu kamwambia' kuna mtu huko 'juu' (ikulu i think) anayeajiri watu wa wilaya moja tu!

Huu mchezo ni kwamba umeenda south, yaani sawa na kuku kutaga mbuzi! maajabu! Na kwa wale wote wanaopenda demokrasia ya kweli na utawala wa sheria na haki basi hawana budi KUFURAHIA huu UTAKASO wa Jairo. It is one of the best thing ever happened this year in my view. veeeery good.
 

Luhanjo anafahamu nguvu ya umma? Kama kweli michango hiyo ilifika 500/m ni kiasi gani cha wawakilishaji wa bajeti na kwa hesabu hiyo wangelipwa bei gani? na CAG ANATWAMBIA NINI KWA UTARATIBU HUO WA KUZICHANGISHA IDARA , NA MICHANGO HIYO INATOLEWA KUTOKA KASIMA GANI KWENYE HIZO IDARA ( IS THIS WITHIN THE AMBIT OF VOTE?) KAMA KUNA REALLOCATIONS JE ILIPATA APPROVAL YA BUNGE? .......................BASI INAUMA SANA?................. INABOA ........... HASWA KWA SISI CCM
 
Shelukindo anatumiwa na 'mtandao' unaohangaika kujinasua kwa kulipua washirika waliowatosa ili kuwa na uwanja sawa wa tuhuma.
Bahati mbaya hesabu zao hazikuwa pevu (pre mature) pengine kuhofia hoja kubebwa na wapinzani .
Shelukindo alijua kuwa zimeshagawiwa na hivyo uchunguzi utaonyesha waliopokea, hapo ingeongeza idadi ya watuhumiwa wa ufisadi ambao wangetakiwa wajivue gamba kama kundi la EL. Kwa bahati mbaya pesa zilikuwa hazijafika mikononi mwa wahusika kwahiyo tuhuma zinabaki kwa Jairo.

Luhanjo anachokifanya ni kuuthibitishia 'mtandao' kuwa hawawezi ndio maana amemrudisha kwa kishindo.
Ikumbukwe kuwa Jairo ni mtu wa karibu sana na JK kwa miaka mingi na automatic ni mtu wa karibu sana na Luhanjo. Kwahiyo kesi ya Jairo mwendesha mashitaka ni Luhanjo na na hakimu ni JMK! tena dhidi ya timu tuhumiwa!!

Hili dili lilipaswa liuzwe kwa wapinzani, lakini kwa siasa za kukomoana na mgawanyiko ndani ya chama'mtandao" wakalichukua kwa jazba kuonyesha nguvu zao. Ime jam! Tutasikia mengi mwaka huu.
 
sasa na pesa alizokuwa amepewa za kujikimu za likizo atarudisha? Au tena akistaafu atalipwa tena au kupewa likizo ya malipo tena jaman pesa zetu hizi watoto wetu wanakosa hata madawati ya kukalia
 
mkuu kweli inashangaza sana juu ya aina ya uchunguzi ulioendeshwa. anasema idara zilizotoa hela c zile zilizotajwa awali hali kadhalika kiasi cha pesa. so was it legal/proper kuchangisha fedha hizo?waliotoa walizitoa wapi? matumizi hayo ni sawa? (kuhonga/kulainisha) baadhi ya wabunge? What i see here c suala la utawala wa sheria bali ni kulindana,, ukisema Jairo alifanya hatia linaibuka swali alifanya kwa muongozo wa nani na ndo kuumbuka/kuanguka kwa serikali ya ccm iliyojaa magumashi
 
Reactions: Nzi
Katika ma PM bogous huyu wa sasa kiboko!
 
Niliposikia tu Jairo kawekwa likizo ya malipo nikajua mchezo umeanza kusukwa. Hakukuwa na uchunguzi makini. Kilichofanyika ni kile wazungu wanaita "white wash," kuwanusuru Jairo na Kikwete.
 
Kama mliusoma mchezo mapema, haya mambo yalikuwa very expected, haiwezekani wapoteze point tatu muhimu, kwa kundi linalojaribu kuwavuruga, so cha kufanya hapa ni kumgeukia Pinda na kumuangalia usoni bila ya kumsemesha kitu, akituuliza tunamuongalia kwa nini ndipo tumuulize kama ameiona report ya Luhanjo kuhusiana na suala la Jairo, atajibu kwa ukali "so what" tumkumbushe "Kauli yako mzee....ile...ile uliitoa pale bungeni kwamba ingekuwa ni maamuzi yako unge....." mpaka hapo atakua amegundua kitu na kuwa unamaanisha nini, hivyo ataanza kujiandaa kulia......
Safari hii tukomae mpaka atuambie kuwa umakini wake uko wapi?

anacheza na mashabiki au anafuata kanuni za utendaji......halafu kiuzushi tumtumbkizie anajisikiajje baada ya chezo kuchezwa vile na kumchoresha mbele ya jamii?

Na kwa ukubwa wa issue na kiwango cha kutofautiana mawazo anaonaje kama atajiuzuru, mpaka hapa lazima alie tu..
 
its realy sad!!!! natamani kulia lakini machozi hayatoki!!! nafiri tumwachie Mungu ipo siku machozi yetu yatafutwa( hii ndo Tanzagiza)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…