Luhaga Mpina aomba kufanya Mdahalo wa wazi na Waziri Mwigulu Nchemba

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mbunge wa jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina amedai kuwa, kuna upigaji na ubadhirifu wa shilingi trilioni 6.5 katika maeneo ambayo ni ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), IPTL, mradi wa umeme wa Julius Nyerere na mikopo.

Mpina ameongeza kuwa, fedha hizo ni kati ya fedha kiasi cha shilingi trilioni 30 ambazo ameeleza zipo ndani ya ripoti ya CAG mwaka 2021/2022.

Katika kuthibitisha madai hayo, Mbunge Mpina ameeleza kuwa, ameshawasilisha jedwali linaloonesha ubadhirifu na upigaji wa shilingi trilioni 30 na kuongeza kuwa madai hayo ameshayaeleza bungeni katika kipindi cha miezi sita huku Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba ameshindwa kujitokeza kukanusha.

“Mimi nimeshazungumza hayo bungeni zaidi ya miezi sita lakini Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba ameshindwa kujitokeza kukanusha” alisema Mpina

Mpina ameenda mbali kutetea madai yake hayo, kwa kuomba mdahalo na Waziri huyo Fedha kuzungumzia upotevu wa shilingi trilioni 30.

“Namualika Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba katika mdahalo kuzungumzia juu ya upotevu wa shilingi trilioni 30” alisisitiza

Mpina amebeza waliomjibu kuwa fedha anazodai zimepigwa ni nyingi kuliko fedha zote za Tanzania, Mpina amesema

“Mfano watu wamekuibia madini hivi hizo ni fedha za bajeti?hivi watu wakikuibia magogo au fedha za miradi hizo ni fedha za bajeti”
 
Luhaga Mpina kupambana na hao wala rushwa ni kazi ngumu - watakutafutia angle ukishajaa tu kwishaa.
 
Mpina kawavalia njuga mafisadi,aangalie wasimuweke kwenye tajeti,akajaa mazima kwenye mfumo.
 
Back
Top Bottom