Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,554
Katika mjadala unaoendelea Bungeni kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 4 jioni ya leo April 11, 2023 Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina amesema katika uchambuzi wa ripoti ya CAG anaoendelea kuufanya, amebaini kuwa zaidi ya Trilioni 30 zimepotea.
Ameonesha masikitiko yake kuwa wabadhirifu hawa bado wapo serikalini na Mamlaka haziwachukulii hatua.
Amesema, “Mhe. Naibu spika, kwa summary tu hapa, ubadhirifu wote huu wa CAG ambao mimi nimeainisha na bado naendelea kuainisha ni zaidi ya trilioni 30, trilioni 30. Sasa mkishakuwa na ubadhirifu wa trilioni 30, unakaa kwenye bajeti kufanya nini, yaani unathibitisha pesa zote zikagawanwe?”
Amemalizia “Lazima tuchukue hatua kali Mhe. Naibu spika, kwa watu hawa wanaofanya haya mambo”
UPDATE:
Jenesta Mhagama ameomba mwongozo wa takwimu hizo ambazo kwa maelezo yake amedai zikiachwa kama zilivyo zinaweza kuleta sintofahamu kubwa kwa Taifa kuanzia leo.
Naibu spika Mussa Azzan Zungu amesema Serikali imepewa siku 21 kujibu hoja za CAG hivyo ametoa amri ya kuondoa kwenye Hansard za Bunge maneno ya Mbunge Luhaga Mpiga.