Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

Jamani naomba musishushe ufahamu unaotakiwa kuwa JF. Kabla ya kumusifu huyu mtu hebu kwanza someni kazi na madaraka ya Bunge. Baada ya hapo ndo mutoe sifa.

Kwa matamko yake ya aina hii mimi kwangu nasema ni upuuzi kwa mbunge wa siku nyingi kugeuka kufanya kazi ya Amiri jeshi mkuu. Hana sababu yoyte ya kuzungumza uchafu wake kama huu. Kazi yake ni mbunge basi! Hata kama ana malengo yake mengine hatutegemei display za aina hii.

Tatizo la Lowasa kila wakati anataka sifa zimuendee. Kila wakati anaona kazidiwa na wengine.

Ni aibu ktk JF kuanza kusifu mtu wa aina hii. Naona tunajisahau na kuanza ushabiki. Bunge gani ktk nchi litatangaza vita na kutisha nchi nyingine?

Eti naye anataka kuwa Rais. Basi, asubiri mpaka muda huo ukifika ndo atoe hayo. Kama miguu itakubali kusimama majukwaani maana sasa naona ni hotuba za kwenye sofa.

Mkuu you are being narrow minded.
Dont let your political affiliations na inlinations zikuzibe ufahamu wako wa kujua what is at stake.

Confrontations na Malawi zikianza hazitachagua mtu wa chama chochote na msimamo wake.
I usually dot aggree with EL , hasa katika stint yake ya uwaziri mkuu.

What is at stake here is bigger than your wildest imaginations.

Hivi umejiuliza haya mambo why now?

Is it a coincidence kwamba wakati huu huu na Mama Clinton yuko Malawi?
Na Malawi haikufanya kosa , IMELIGAWA ENEO LA EXPLORATION LILILO NDANI YA SEHEMU TUNALOLIDAI!
Explorers wenyewe:British!

It takes some brains to put two and two together.

Mtu usisahau vile vile kwa tamko hili la Lowassa limetolewa na Sitta na hata Waziri Membe.
Muchunguzi, kwa akili yako would you think that is also a coincidence!
That is called building up the pressure on Malawians.

Hivi wewe ulitaka Lowasa akubaliane na Malawi, usisahau kuwa pamoja na ufisadi wake bado ni mwenyekiti wa kamati ya ULinzi na Usalama.

Mkuu sampling ya hizo facts na analysis yake lazima itoe tamko thabiti- for now it doesent matter who says it, but imesemwa n Tanzania.

Soma link ya jamaa mmoja hapo juu , huko Malawi ujumbe umeshafika.
 
Malawi: 2012, July: "But our terms are clear on this. According to the 1890 ecoland agreement between Britain and Germany, the border between Malawi and Tanzania is the edge of the waters of Lake Malawi. So we are very clear about that but we will continue to engage with Tanzania as a good neighbour," Patrick Kabambe, Principal Secretary, Principal Secretary in the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Malawi quoted by Malawi's Daily Times......

Sijali nani katoa tamko ila kauli hii ya wenzetu ingepaswa kujibiwa kwa jinsi ilivyojibiwa then twende katika meza ya mazungumzo. ieleweke kuwa nchi yeyote duniani ipo tayari kwa vita haswa linapokuja swala la kulinda mipaka, raia wake na mali zao vinginevyo kusingekuwa na jeshi... Kama kuna nchi au utawala ambao utasita kutamka hayo tutaquestion sana autonomy na sovereignity ya nchi husika..Tatizo tuko busy na persoality za watu na tuko biased kichama....

 
Mkuu Jasusi, Lowassa ndiye M/Kiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, hivyo anazo nguvu na mamlaka yote kuzungumzia hili!.

Kwa powers alizo nazo, anaweza kumsummon MFI (Membe), CDF (Mwamunyange), CIS (R.O) na IGP (Mwema).

Utakuwa umechanganya kati ya kuzungumzia uwezekano wa Tanzania kuingia vitani na powers za kutangaza vita!.

Mwenye mamlaka ya kutangaza vita ni Amiri Jeshi Mkuu pekee na hakuna ku delegate jukumu hili!, lakini kuzungumzia nia ya kuilinda mipaka yetu, any leader anaruhusiwa kusema!.

Naendelea kukumbushia posibility ya
"Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!".

Pasco.
Pasco ningeshangaa kama nisingekuona hapa, by the way nakubaliana nawe. Ila umesahau anaweza pia kum-summon Sitta
 
Last edited by a moderator:
hayo ni maoni yako.kama ingekua hivyo wasingeenda kulinda amani nchi za watu.
na kama wangeenda basi wangeharibu nchi ikapata aibu..
NB. japo mie si afande,wakianzisha na-join..navyopenda hizo move!!
nataka kitu 'live',lowasa lianzishe..dhaifu hawezi

huwa tunapenda taifa liwe na watu kama nyie.
 
Niliwahi kusema humu katika uzi mmoja unaohusu hili jambo kuwa tunahitaji viongozi wasiomun'gunya maneneo kama Edwars Lowasa nikirejea alichowajibu wamisri walipoanza kupigia kelele kitendo cha Tanzania kutumia maji ya ziwa victoria kwa kisingizio cha mikataba ya wakoloni nikabezwa...Sikujua kwa nafasi yake atachomoza...when it come to territorial integrity tunahitaji kauli za namna hii hopefully vikosi viko mpakani kumshughulikia yeyote atakayeleta chokochoko....hata ndege inayoruka upande wetu ni kuishusha.... Mazungumzo yaendelee kusisitiza hilo ili wayapate kwenye meza ya mazungumzo...

86% very good
 
Yaani kimama kimekuja juzi tu, Leo kinajua mipaka.

Sio kwamba nakubaliana na anachokifanya huyu mama Joyce, lakini nadhani tunahitaji Rais mwenye courage kama yake ili tanzania iweze kuendelea katika kila nyanja. hatuhitaji rais mpole asiyeweza kuchukua hatua kwa haraka na bila woga
 
Haya ndio maneno aliyoshindwa kusema MEMBE juzi Bungeni. Sielewi nani alimwambia Membe awaite wa Malawi ''WENZETU'' wakati wao wanajiandaa kutupiga kivita.

Tangu lini adui akawa mwenzako?

mwenzie Lowassa amesoma mood ya nchi na ameamua ku grab the headlines vilivyo

so far as far as national security is concerned: LOWASSA 1 MEMBE 0

game inaendelea

kweli kabisa
 
Tanzania has warned that it will be prepared to go to war with Malawi on the ownership of Lake Malawi, also referred to as Lake Nyasa by some countries, thought to have oil deposits.
The two countries have scheduled August 20,this year, in Mzuzu — the northern city of Malawi -for showdown talks on the matter.
Despite Malawi government saying it wants the matter to be handled diplomatically, some overzealous Tanzanian officials have been war-mongering .
Tanzania’s chairman of the parliamentary committee for Defence, Security and Foreign Affairs, Edward Lowassa, is quoted by The Citizen, declaring: “We expect this conflict will be solved diplomatically using the committee of foreign affairs ministers from both countries and using the mediator whenever needed. Malawi is our neighbour and therefore we would not like to go into war with it.”
“However, if it reaches the war stage then we are ready to sacrifice our people’s blood and our military forces are committed in equipment and psychologically. Our army is among modern and stable defence forces in the world,” declared Lowassa.
lowassa-ccm-top.jpg
Lowassa: If it reaches the war stage then we are ready to sacrifice Tanzanian people’s blood

There are reports that Tanzania has already sent troops to the border but that has not been independently verified.
Malawi’s Foreign Affairs and International Cooperation Minister Ephraim Chiume has since assured that “ this should not be a cause for anxiety or alarm.”
Nonetheless, Tanzania minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Bernard Membe, has ordered Malawi to consider an immediate stop to all gas and oil prospecting activities on the portion of the lake that falls on the Tanzania side.
He told parliament that the Tanzanian government was committed to ensuring that its people are protected “at any cost”.
The conflict time line
According to Chiume, the border between the two countries was defined in the Heligoland Treaty signed by the former colonial powers Germany and Britain on 1st July 1890.
“The Heligoland Treaty defined the border between the two countries as being the edge of the waters on eastern shore of Lake Malawi.
“Furthermore, the Heads of State and Government of the Organisation of African Unity (OAU) made a resolution in 1963 that member states should recognise and accept the borders that were inherited at the time of independence. The African Union (AU) made similar resolutions in 2002 and 2007,” said Chiume.
But Tanzania’s Membe said the conflict started in the early 1960s, when the first Malawian president, Dr Hastings Kamuzu Banda, claimed that Lake Nyasa and the whole of Mbeya in Tanzania were part of Malawi using the 1890-Heligoland treaty.
“But, talks about the matter stopped somewhere as Dr Kamuzu Banda had a relationship with South Africa and Tanzania was in support of South African freedom fighters,” Membe said.
He said serious talks on the matter were revived in 2005, between President Jakaya Kikwete and the late Dr Bingu wa Mutharika, whereby a ministerial committee was appointed by both countries to solve the dispute over the border and the lake’s name.
“The committee met in 2010 and 2012, whereby a number of issues were discussed including some of the aircraft claimed to belong to the oil and gas researching companies from Malawi flying in the Tanzania airspace,” he said.
He told Parliament that Tanzania was interested to end the conflict through round-table discussions and to find a long-term solution.
Tanzania wants 50 per cent share of the lake, but Malawi claims to own the whole of it.
Malawi has awarded Surestream Petroleum of UK a licence to prospect for oil on the lake.
 
Mungu ibariki tanzania yetu. ee Mungu tuepushe na hichi kikombe tusikinywe kwani madhara si mazuri hata tukishinda, ila kama ni mapenzi yako tukinywe, mapenzi yako yatimie katika jina la Yesu mwanao aliye hai. Amen.

94% vema sana
 
Jasusi,

..unajua juma hili kulikuwa na ujumbe wa Malawi uliotembelea bunge la Tanzania.

..binafsi naamini huu si wakati muafaka kuanza kuzungumzia masuala ya military option.

..zaidi, kutokana na msimamo uliotolewa na serikali ya Malawi, sijui serikali yetu inasubiri kitu gani kupeleka suala hili ktk mahakama ya kimataifa.

Joka Kuu,

Diploamsia siku zote ni lazima iaambatane na Millitary Background. Mbinu za kufanikisha dialogue kwa mujibu wa kanuni za kidiplomasia ni

1:Ukarimu
2:coercion
3:ushawishi tu
4:zote kwa pamoja

Lakini katika siasa hizi hasa suala linalohusu ukiukwaji wa sheria za Kimataifa ni lazima kuwe na millitary option ili kuishinikiza Hostile side na jumuiya ya kimataifa kupigania kuingia mezani

Tena ilitakiwa hadi sasa Tanzania iwe imetangaza kurudisha baadhi ya majeshi yaliyopo kwenye peace mission na pia kuanza millitary drilling....
 
Vita vya kupambana na ufisadi ambao umepoteza maisha ya Watanzania wengi kuliko vita ya Kagera vimetushinda.Huhitaji mizinga wala ndege za kivita kupambana na adui huyu ufisadi kwa nini vimetushinda?
Tusijidanganye, Ukiona matamko kama hayo yanatolewa na mtu yeyote ujue serikali iko disorganized ni kama kundi la walevi bar kwamba kila mtu anaweza kusema apendalo na asilopaswa kusema ili Barmaid amwone anafaa.
Hawa wanasiasa wasituvunge. Jeshi letu sii moja tena! kuna tofauti kubwa sana ya kifikra kati ya Officers and men. Serikali na watu wake kwa sasa wako tofauti sana kifikra na kimtazamo. Katika hali kama hiyo vita viwe na hatua ya mwisho kutajwa.
Nakumbuka 1978 ushindi wa JWTZ ulirahisishwa na Raia wa Uganda kuchoshwa na Serikali ya Amin na kutoa siri na ushirikiano kwa jeshi letu. Sisi tumejiuliza kwa kiwango hiki cha utendaji wa serikali,Polisi wetu,viongozi watendaji wa ngazi zote (na CCM pia) wameweza ku maintain hali ya wananchi kuipenda nchi yao au wamedharau kiasi cha raia mipakani kutamani wangekuwa raia wa nchi hizo jirani?
Kwa tamko hilo la EL, kuna mawili, eitha anamdharau anayepaswa kutoa tamko au nchi hii inautawala wa kambale kila kambale ana ndevu hata mtoto au mama wote ndevu tuu.
,

vita vya adui fisadi bado havijaisha mkuu
 
Hakuna taifa lolote duniani ambalo litakuwa tayari ku-sacriffice primary interest kirahisi
Katika Diplomasia inajulikana Primary Interest za Taifa lolote ni

1: Ardhi ndani ya mipaka inayotambulika kimataifa
2:Raia wakndani ya mipaka pamoja na Raia wake walioko nje ya nchi n.k

Hizi ni interest ambazo taifa lolote lipo tayari kutumia millitary option.

Bernard Membe alitoa ujumbe ambao ni thabiti kabisa na mara zote nimesema Membe anafanya kazi yake kama wwa Mambo ya Nje vizuri na anafuata principle zote za diplomasiapamoja na mapungufu yake ya hapa na pale.Alionyesha maturity,patriotism na intellectual capacity alipokuwa akijadili hili la Malawi
 
jmushi1, unaamini huu mgogoro?
Mie naanza kuutilia mashaka, japo sina evidence kwa sasa.
Siamini mgogoro,ila naamini kuna watu watataka kuscore "political points"kwenye hii issue,wote waliosema jambo wako kwenye listi ya wanaohusishwa na kugombea urais...so go figure.Ndo maana nikasema bado tunaweza kupostpone hili kwanza coz of our own internal problems,which on my opinion are really big.

Ni kweli kuna dalili za uchokozi kutoka kwa wamalawi,lakini bado naamini kwamba this can be solved diplomatically.Pia usiamini kila habari inayoletwa hapa,kuna za ukweli na za uwongo pia.Kuna taarifa kuwa hao wamalawi wako upande wa Tanzania,na pia taarifa kwamba majeshi yetu yanaelekea maeneo hayo kulinda mpaka wetu na malawi,sasa nashangaa kwanini hawajawakuta hao wamalawi hadi sasa given that wamo ndani ya Tanzania?Ama labda bado hawajafika huko?
 
Last edited by a moderator:
Mimi nashangaa chain of command yetu iko wapi. Lowassa yeye ni nani kuzungumza kwa niaba ya JWTZ? Kamanda in Chief yuko wapi? Yaani Tanzania yetu imeshaparaganyika kiasi kwamba yeyote tu anaweza kuzungumza kwa niaba yake? Suala la vita au kuwa tayari kwa jeshi letu ni kamanda in chief peke yake anayeweza kulizungumzia. When was the last time you saw Lowassa inspecting a guard of honour?

Na wewe acha kuongea pumba huyo kamanda in cheaf wako yuko wapi?mbona hatumsikii?EL hajakosea chochote hapo ameonyesha jinsi kiongozi wa nchi anavyotakiwa awe.
 
Na wewe acha kuongea pumba huyo kamanda in cheaf wako yuko wapi?mbona hatumsikii?EL hajakosea chochote hapo ameonyesha jinsi kiongozi wa nchi anavyotakiwa awe.

umeniwah kumjibu
 
Hii ni kauli ya mtu anayetaka kubaki kuwa relevant politically bila kupima ramifications. Top diplomat hakurupuki na ku-spit fire hata pale pasipostahili na wala nchi haijawa katika hali hiyo ya kuingia vitani wakati huu ambapo mazungumzo yanaendelea. Hata siku moja tamko la vita halitolewi na bunge, wala na mwenyekiti wa kamati ambaye kazi yake ni kushauri na hapa ndipo Lowassa na wafuasi wao wanaposhindwa kuelewa majukumu hasa ya Kamati. Kamwe yeye si waziri kivuli au waziri mbadala (japo angependa iwe hivyo). Uwezo wa kivita haupimwi na utayari wa jeshi lako kwa kupewa taarifa na majenerali bila kujua nguvu za adui.

Mimi nafikiri Membe alikuwa ana-respond kwa swali aliloulizwa na kulikuwa hakuna haja ya ku-spit fire. Ilitosha kutoa onyo na in any case, onyo sahihi na lenye effect ni lile linalotolewa kwa Serikali husika through diplomatic channels, siyo kwenye podium ya bunge au ukumbi wa Msekwa baada ya kuwakusanya waandishi wa habari. If he thought he was going to steal the show, he has unexepectedly exposed his immaturity and lack of diplomatic prowess in dealing with a neighbour. Vita huwa ni mambo ya last resort tena kwenye nchi kama yetu yenye changamoto nyingi za kiuchumi na kijamii.
Thank you, thank you. That is what I was saying too.
 
Back
Top Bottom