Nashindwa kuelewa jinsi viongozi wetu wanavyozungumzia kuiingiza nchi vitani kwa mbwembwe kipichi ambacho tukishuhudia kuwa suluhu ya migogoro sio vita bali majabiliano, nashindwa kuelewa kwani ni tuanze kufikiria vita na kuanza kujivunia uwezo tulionao katika vita badala ya kuweka nguvu katika majadiliano ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa mpaka wa ziwa nyasa au malawi kama wente kuugombea wanavyota uitwe.
Tena najiula hawa viongozi wetu wametokea wapi kuja kujadili mambo ya vita wakati huu ambao tunaishudia nchi na dunia kwa ujumla vikiwa kwenye migogoro mikubwa ya kiuchumi. swali lingine linanijia kichwani kujiuliza hivi hizi garama za vita wakati ambapo tunashudia hata hospitali zetu zikiingia kwenye mgogoro na wahudumu wa sekta ya afya wakidai kuwa bhospitali hazina vifaa vya kuwahudumia wananchi kwenye sekta ya afya, Je majeruhi wa vita kati malawi na tanzania watatibiwa katika hospitali gani?.
hapo nipo ninapohisi kuwa serekali haiko makini juu ya hili, ingekuwa serekali iko makini juu ya hili basi kujitapa huko kuwa wako tayari kuingia vitani kungeanzia na huku kwenye vita juu huduma duni ya afya nchini ikiwemo ukosefu wa vifaa tiba na maslahi ya watendaji, mishahara ya wafanyakazi, vita dhini ya rushwa na ufisadi uliokidhiri katika nchi hii.
Baada ya serekali kukamilisha haya basi wanachi tungetoa baraka zetu kwa serekali kuingia vitani na malawi bila kuruhusu na kusisitiza juu ya kutoa fusra kwa majadiliano katika kutafuta suluhu ya mgogoro wa mpaka kati yake na malawi. Tena kwanini hili limekuja wakati huu inawezekana kuna kitu kinaendelea hapa duniani na miongoni mwavyo ni kutolewa kwa taarifa za uwezekano wa kuwepo mafuta katika ziwa hili.
serekali za Malawi na Tanzania lazima ziwe makini san juu ya hili isijekuwa kuna majinchi makubwa yanatusukuma sisi tuingie vitani ili wakati sisi tukizichapa wawo watoe sila watugawie huku wakichota rasilimali zetu na baada ya vita wakituacha tukinuka kwa madeni na hali mbaya ya kiuchumi, ukosefu wa chakula huku tukibakiwa na maandaki makubwa waliyochimba madini, mafuta, gasi na urani,
Tanzania duniani imekuwa ikisifika kwa amani na upatanishi wa nchi nyingi katika ulimwengu huu , hata Mwalimu aliwahi kuongoza tume za kutafuta ususluhishi katika nchi nyingi duniani, kipindi cha Karibuni tulishuhudi Kikwete akisaidia kwa karibu kupatikana kwa mwafaka katika taifa la karibu nasi hapahapa A.
Mashariki la Kenya na Dunia nzima walihsngaa maana Kikwete kaingia tu na mwafaka hapo hapo wakamuuliza alitumia mbinu gani? Hatimaye sasa baada ya kuwa marefarii kwa muda mrefu sasa ni zamu yetu kucheza sijui nani anatupulizia kipenga