Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Aug 8, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Nimeipenda sana kauli hii ya Lowasa katika gazeti la Mwananchi la Leo Jumatano;

  Reginald Simon na Daniel Mjema, Dodoma | Mwananchi | Agosti 08, 2012

  [​IMG]

  KAMATI ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imesema Tanzania imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani na Malawi kama italazimika kufanya hivyo.

  Akizungumza mjini Dodoma jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Edward Lowassa alisema kamati yake imeridhishwa na maandalizi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

  "Tumepewa maelezo na jeshi letu na tumeridhika kuwa ikibidi kuingia vitani jeshi letu liko vizuri sana na limejipanga vizuri sana kwa uhakika, kiakili na kivifaa," alisema Lowassa.

  Kabla ya Lowassa kuzungumza na waandishi wa habari, alifanya kikao cha faragha kilichohusisha pia wajumbe wa kamati hiyo na makamanda wa JWTZ walipofika bungeni kutoa taarifa kwa kamati hiyo.

  Hata hivyo, katika tamko hilo Lowassa alisema Tanzania inatarajia mgogoro huo utamalizika kwa njia za kidiplomasia kwa sababu Watanzania na Wamalawi ni ndugu wa muda mrefu.

  "Ikibidi kuingia vitani jeshi letu liko vizuri sana na kama ilivyo ahadi yao (JWTZ), wako tayari kulinda mipaka ya nchi yetu hadi tone la mwisho. Tunasali sana tusifike hapo," alisema Lowassa na kuongeza:

  "Tunategemea hatutafika huko, lakini kwa heshima ya nchi yetu kama ikibidi kufika huko (vitani) tutafika kulinda mipaka yetu".

  Mwenyekiti huyo ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu, alisema kama Tanzania itafikishwa mahali itabidi damu ya Watanzania imwagike, nchi iko tayari kulinda mipaka yake kwa nguvu.

  Alisema kama itabidi kuingia vitani, itatumia umoja na mshikamano wa Watanzania wa mwaka 1978 wakati wa Vita na Uganda kulinda mipaka ili kulinda heshima ya nchi.

  Alisema mwaka 1978 wakati Rais wa Uganda, Idd Amin na majeshi yake walipochukua sehemu ya Tanzania na kujitangazia ni mali yake, ilichukua hatua kumfukuza Amin.

  "Alijitangazia sehemu ile ni mali ya Uganda hutegemei nchi ikae kimya, hutegemei Watanzania wanyamaze wakati nchi yao imetekwa, tulichukua hatua tukamfukuza hadi nchini kwake."

  Lowassa alisema Kamati ya Bunge inajua madhara ya kiuchumi yaliyotokana na Vita ya Idd Amin na kwamba vita yoyote ikipiganwa lazima kunakuwa na madhara ya kiuchumi.

  Hata hivyo, alisema anaamini mgogoro huo hautafika huko na kusisitiza kuwa, lakini ikibidi JWTZ ni moja kati ya majeshi bora duniani na ni jeshi lililojiandaa vizuri kwa lolote.

  "Wako tayari sisi ni moja kati ya jeshi lililojiandaa vizuri na jeshi bora duniani na la kujivunia. Tuko imara kiakili na kivifaa tena vya kisasa," alisema Lowassa.

  Alisema kamati yake inaunga mkono msimamo ulitolewa bungeni juzi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuhusu mgogoro huo na kwamba ndiyo kauli rasmi ya Serikali.

  Juzi, Waziri Membe alizionya kampuni za kigeni za Malawi zilizoingia katika ardhi ya Tanzania eneo la Ziwa Nyasa kutafiti mafuta na gesi kusitisha mara moja.


  Hapo ndipo huwa namkubali Lowassa kuliko wengine wote ndani ya CCM walau kwa kauli na matendo ya namna hii ukiondoa yale mengine ya ufisadi

  ======
  UPDATE
  ======
   
 2. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Anaweza pia kuwa ndio anaanza mazoezi ya kuwa Amiri Jeshi mkuu 2015
   
 3. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Kwa mara ya kwanza nakubaliana na Lowassa katika tamko thabiti na lisilo la kumung'unya maneno.
  Tunatumaini ndugu zetu wa Malawi watatuelewa vizuri katika hili.
  Wakato mwingine si vibaya kutunisha misuli jirani anapoleta chokochoko.
  Nashukuru Mungu mpango wa reserve army wa JKT nao unaanza karibuni.
   
 4. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #4
  Aug 8, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Na bahati nzuri mpango huo unaanza na wabunge vijana hivyo watakuwa wa kwanza kuwa frontline huko Malawi
   
 5. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Haya ndio maneno aliyoshindwa kusema MEMBE juzi Bungeni. Sielewi nani alimwambia Membe awaite wa Malawi ''WENZETU'' wakati wao wanajiandaa kutupiga kivita.

  Tangu lini adui akawa mwenzako?

  mwenzie Lowassa amesoma mood ya nchi na ameamua ku grab the headlines vilivyo

  so far as far as national security is concerned: LOWASSA 1 MEMBE 0

  game inaendelea
   
 6. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #6
  Aug 8, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Lowassa alishasema viongozi wa serikali ya JK wanaogopa kuchukua maamuzi magumu, hata kutamka maneno magumu wanaona shida hadi EL awasaidie
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,201
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Lowassa ni mwamba wa kaskazini wewe sio mcheza Ngoma Kama Joyce wetu
   
 8. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  eti wa Malawi ni ''WENZETU''
   
 9. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Mkuu Membe ni diplomat, na diplomats wana lugha kama hizo zisizo confrontational.
  Tunajua kwamna itakapobidi Membe atakaa na " mwenzake" wa Malawi kutatua tatizo hili kidiplomasis.

  Katika suala hili Watanzana lazima tuwe kitu kimoja hakuna cha Membe wala Lowassa, ukianza mkong'oto wote itakuwa combat.
   
 10. Kibada

  Kibada Senior Member

  #10
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maneno ya kujifurahusha hayo! Vijana wa JWTZ hawana morali hata kidogo ! Nani anaenda kupigana vita wakati dhuluma imetapakaa kila sehemu? Hata JWTZ kwenyewe kunafukuta moshi ndani kwa ndani kwa muda mrefu sasa.. Vijana wanaonewa , wanahujumiwa nafasi za masomo, posho halali Na mengine mengi.. Kwa maoni yangu kuingia vitani kipindi hiki imekula kwetu..
   
 11. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #11
  Aug 8, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Suala hili la uvamizi liko mahakamani, si vema sana kulizungumzia tutaingilia uhuru wa mahakama. Wazambia wanadai mambo makubwa sana ambapo taifa Kwa Sasa haliwezi kuwatimizia..
   
 12. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,892
  Trophy Points: 280
  Lowassa ndio amir jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama na ufisadi pia
   
 13. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #13
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Waziri wa mambo ya nje wa Malawi naye ni diplomat na ndiye aliyeanza lugha za ovyo

  secondly hiyo lugha ya diplomacy zinatofautiana. Aneye negotiate ni akina balozi Malamula sio Membe, Membe ni mwanasiasa na cha ajabu ameshindwa kusoma alama za nyakati, mood ya nchi na audience aliyokuwa nayo mle bungeni.

  Why should we be expected ku play fair wakati adui ana play rough?

  Membe should have rallied the nation kwa mikwara ya kila namna...then awaachhie hao ma specialists wake wakaongee lugha za kidiplomasia walizosoma pale University of Westminster
   
 14. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Acha nidhamu za woga. JWTZ wenyewe wana hamu ya kupigana.

  Lakini vita siyo kitu cha kushangilia hata kidogo. Inaweza kutuathiri sana. Kwangu mimi naona ni mapema sana kuanza kufikiria hili la kupigana. Juhudi za kidiplomasia zingetumika kwanza kutatua huu mgogoro.
   
 15. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa ulitaka jeshi gani ndo tujivunie nalo?; acha woga wewe, ulitaka tusubiri tujivunie wabunge watakaoendao kutalii JKT?.
   
 16. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,870
  Likes Received: 2,817
  Trophy Points: 280
  Wewe! Hao ni wenzetu. Hujui m-Malawi alishawahi **** Rais wa Zanzibar? Hujui m-Malawi alishawahi kuwa waziri wa fyeza! Hao ni wenzetu! Unawezakuta hata MEMBE naye ana asili ya huko. Maana kuna Wayao, Wanyanja n.k pande zote. Lakini wanastahili kichapo tu hawa hakuna msalie mtume! Nimeona bandiko la Mmalawi NIKUPATEJE hadi hasira. Eti ziwa liishie kupiga mawimbi tu kwetu maji yote ni yao! Ina maana mpaka wao unaruhusiwa kuhama kuft maji?
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mimi nashangaa chain of command yetu iko wapi. Lowassa yeye ni nani kuzungumza kwa niaba ya JWTZ? Kamanda in Chief yuko wapi? Yaani Tanzania yetu imeshaparaganyika kiasi kwamba yeyote tu anaweza kuzungumza kwa niaba yake? Suala la vita au kuwa tayari kwa jeshi letu ni kamanda in chief peke yake anayeweza kulizungumzia. When was the last time you saw Lowassa inspecting a guard of honour?
   
 18. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #18
  Aug 8, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Lowasa ametoa tu status ya jeshi letu. Na hili ni jukumu lake. Hajatangaza vita.
   
 19. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #19
  Aug 8, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutokana na chokochoko waziletazo nchi jirani ya Malawi na kupitia kauli za viongozi wetu Mh.Membe wakati anawasilisha Budget yake na Mh. Lowasa kupitia kikao cha siri cha Kamati yake sasa wakati umefika wa kulipia matumizi ya jina hilo la Makamanda.
  Ikitupasa kuingia vitani basi nashauri wale wote wajigambao kuwa makamanda,wazalendo wa kweli na wapigania haki ni wakati wao kusonga front kama chambo ili wakainusuru Mipaka ya Nchi yetu.
  Kazi kwenu kombania ya Green guard, Blue guard na Wazee wa gwanda.
   
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,800
  Likes Received: 5,084
  Trophy Points: 280
  Jasusi,

  ..unajua juma hili kulikuwa na ujumbe wa Malawi uliotembelea bunge la Tanzania.

  ..binafsi naamini huu si wakati muafaka kuanza kuzungumzia masuala ya military option.

  ..zaidi, kutokana na msimamo uliotolewa na serikali ya Malawi, sijui serikali yetu inasubiri kitu gani kupeleka suala hili ktk mahakama ya kimataifa.
   
Loading...