Nchunguzi kwanza tuekewane katika yafuatayo.
1. Amiri Jeshi Mkuu ni mmoja tuu ambaye ndiye mkuu wa Majeshi yetu yote ya Ulinzi na Usalama.
2. Kijeshi chini ya Amiri Jeshi kuna
- CDF-Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
- CSS- Mkurugenzi wa TISS
- IGP - Mkuu wa Jeshi la Polisi
kuna sub component mbili ya
CPS - Kamishna Mkuu wa Magereza na
CIS - Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.
Kila mmoja wa wakuu hao ana comand majeshi yaliyo chini yake. CDF anakomand majeshi na sub components zake za JKT, Airforce na Navy na hawezi
kuwacomand polisi, magereza wala wanausalama na hana mamlaka yoyote ya kumkamata yoyote nje ya comand yake unless ameingia ndani ya teritorial jurisdiction yake kama raia akifanya fujo ndani ya kambi ya jeshi atashughulikiwa na MP na atalazwa Qater Guard!. Vile vile mjeshi asiye Afisa akifanya fujo uraiani polisi wanamshughulikia kama mhalifu mwingine na kuliarifu jeshi husika.
3. Kisiasa juu ya wakuu hao wa majeshi kuna wizara za Ulinzi, usalama na mambo ya ndani ambazo wakuu wa majeshi hawa wanawajibika kwa mawaziri husika hata kama hao mawaziri ni raia!. CDF anampigia saluti waziri wa Ulinzi, IGP anampigia saluti W/Mambo ya ndani etc.
4. Waziri anawajibika kwenye kamati husika ya wizara yake na kamati isipiridhika haiungi mkono bajeji ya wizara husika.
5. Wenyeviti wa kamati husika, wana madaraka kamili ya kuwaita watendaji wowote walio chini ya wizara za kamati hizo!.
6. EL ni M/Kiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama hivyo Membe, Waziri wa Ulinzi na CDF wanaweza kuwa summoned mbele ya kamati anytime!.
7. Moja ya kazi za bunge ni kuisimamia serikali kupitia kamati husika, zile bajeti unazosonewa bungeni, zimepitishwa kwanza kwenye kamati husika zikaridhiwa ndipo ukasomewa. Hivyo wabunge ndio wasimamizi wa serikali.
8. Tunahitaji sana kuwaelimisha Watanzania wenzetu kama wewe kuhusu elimu ya uraia ili wananchi wazijue haki zao.
9. Hata rais wa nchi, tunaoaswa kumheshimu kama binadamu mwingine yoyote kwa kustahili utu na heshima ila ni rais anayepaswa kutubyenyekea, sisi ndio tuliomuajiri na kumlipa mshahara wake na akiboronga tunaweza kunfuta kazi!.
10. Tangu tumepata uhuru miaka 50 iliyopita CCM imekuwa ikitutawala huku inaboronga mwaka hadi mwaka na kwa ignorance ya watu wetu, tunaendelea kuichagua tena na tena na inaendelea kuboronga na kuboronga tena na tena na 2015 tutaichagua tena na tena sababu ya watu kama wewe!.