Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

Jamani mimi naomba kuuliza tu, hii ni kauli ya Lowasa au ni kauli ya Kamati ambayo yeye ndio Mwenyekiti na ameongea kwa niaba ya kamati nzima? i mis some point here!
 
Lowasa ametoa tu status ya jeshi letu. Na hili ni jukumu lake. Hajatangaza vita.

Hata status ya jeshi letu si Lowassa mwenye mamlaka ya kulizungumzia. It is simply cheap politics. Where is our commander in chief? Hivi, wakati wa chokochoko za Idd Amin mlimsikia Kawawa au mbuge yeyote yule akizungumzia juu ya utayari wa jeshi letu? Hiyo ilikuwa kazi ya Commander in Chief. Na as long as we have one, unless you want to tell me we do not have one, no one else can speak on behalf of the readiness of our JWTZ.
 
Sioni sababu ya Tanzania kuingia vitani. Kutetea nini? Rasilimali? Mbona hizi tulizonazo, zinaporwa mchana kweupe tena katikati ya nchi na hatufanyi lolote? Madini, fedha zetu watu wachache wanagawana tu n.k. Kwa maisha ya sasa tukienda vitani tutakula nyasi, hizo gharama za vita mtakazo hesabiwa mh!
 
Kauli hii ya matumaini na ya kujuvunia, tulitarajia itolewa na JWTZ au Rais, lakini hata hiuvyo sio mbaya!

Asante kamati ya bunge!

Unga mkono JWTZ kulinda mpaka ya nchi yetu!
 
Mimi nashangaa chain of command yetu iko wapi. Lowassa yeye ni nani kuzungumza kwa niaba ya JWTZ? Kamanda in Chief yuko wapi? Yaani Tanzania yetu imeshaparaganyika kiasi kwamba yeyote tu anaweza kuzungumza kwa niaba yake? Suala la vita au kuwa tayari kwa jeshi letu ni kamanda in chief peke yake anayeweza kulizungumzia. When was the last time you saw Lowassa inspecting a guard of honour?
Mkuu Jasusi, Lowassa ndiye M/Kiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, hivyo anazo nguvu na mamlaka yote kuzungumzia hili!.

Kwa powers alizo nazo, anaweza kumsummon MFI (Membe), CDF (Mwamunyange), CIS (R.O) na IGP (Mwema).

Utakuwa umechanganya kati ya kuzungumzia uwezekano wa Tanzania kuingia vitani na powers za kutangaza vita!.

Mwenye mamlaka ya kutangaza vita ni Amiri Jeshi Mkuu pekee na hakuna ku delegate jukumu hili!, lakini kuzungumzia nia ya kuilinda mipaka yetu, any leader anaruhusiwa kusema!.

Naendelea kukumbushia posibility ya
"Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!".

Pasco.
 
Maneno ya kujifurahusha hayo! Vijana wa JWTZ hawana morali hata kidogo ! Nani anaenda kupigana vita wakati dhuluma imetapakaa kila sehemu? Hata JWTZ kwenyewe kunafukuta moshi ndani kwa ndani kwa muda mrefu sasa.. Vijana wanaonewa , wanahujumiwa nafasi za masomo, posho halali Na mengine mengi.. Kwa maoni yangu kuingia vitani kipindi hiki imekula kwetu..
Hata mi naona kipindi hiki si sahihi, na pia hela ya vita inatoka wapi? Wakati za mishahara tu hamna!
 
Hata status ya jeshi letu si Lowassa mwenye mamlaka ya kulizungumzia. It is simply cheap politics. Where is our commander in chief? Hivi, wakati wa chokochoko za Idd Amin mlimsikia Kawawa au mbuge yeyote yule akizungumzia juu ya utayari wa jeshi letu? Hiyo ilikuwa kazi ya Commander in Chief. Na as long as we have one, unless you want to tell me we do not have one, no one else can speak on behalf of the readiness of our JWTZ.
Commander in chief wetu matamko yake yanaishia kwenye utetezi wa rada na kebehi kwa madaktari na walimu wanaogoma(mbayuwayu)ya nini kusumbuka na mambo yanayo umiza kichwa bwana Jasusi?
 
Siamini hili; hii ndio sababu ya kwanini siamini anafaa kuwa Rais. Anazungumzia vita leo? kwa lipi hasa? wanataka kuescalate vitu bila sababu ya msingi. Hafai kuwa Amiri Jeshi Mkuu. Kama hii ni sababu ya kwenda vitani basi tumekosa viongozi kweli kweli!
 
JK amemzima Membe kwenye suala la Rada;EL amemzima Membe suala la VITA na Malawi!
 
hatuitaji vita ili tujenge heshima kwa wamalawi, tunaitaji suluhu kutatua mgogoro.

Kama njia za kuadau uhuru zilivofanywa,peaceful means first,ikiprove failure then army struggle inakuwa applied.

Mtu anatanganza vita wafanyakazi waliowekeza nssf wanalia.

Kazi sio kupeleka majeshi,kazi ni kuyahudumia.
Nadiriki kusema hatuitaji ubabe katika hili.
Akili itumike.
 
Nimeipenda sana kauli hii ya Lowasa katika gazeti la Mwananchi la Leo Jumatano;

Hapo ndipo huwa namkubali Lowassa kuliko wengine wote ndani ya CCCM walau kwa kauli na matendo ya namna hii ukiondoa yale mengine ya ufisadi
Hii ni dalili nzuri, kama kosa lake ufisadi wa Richmonduli tuu, then its very simple, lile ni zigo la watu amejitolea kujitwishwa yeye to save faces za watu kama alivyofanya Muokozi, kuzibeba dhambi zetu ili sisi tuokoke!.

EL amebeba zigo la Richmond ili wengine waokoke, ila sasa kuna kila dalili za zigo hili kumwelemea, utafikia wakati atalibwaga hilo pakacha na mambo yote yatakuwa hadharani, mwenye zigo lake mtamjua!.
 
Wapuuzi wakubwa hawa, wametuulia jeshi letu na maufisadi yao halafu wanakuja na maneno ya kujifariji. Vita ikianza wewe na huyo shoga yako na fisadi mwenzio mwende mkapigane.

Jeshi linaagiza mavifaa mabovu ili mpate nafasi ya kufisadi halafu mnakuja kuwadanganya watanzania kuwa mna vifaa vya kisasa! $h#nz! wakubwa nyie.
 
Hatuna uwezo wa kupigana na Malawi kwasababu hiyo morality ya wananchi, these times around ni huge "luxury". Siyo watu wengi wenye kujivunia utanzania kwa sasa.

Sisemi kwamba hatuna uwezo wa kuwapiga wamalawi,lakini matatizo ya internal ni makubwa kiasi cha kwamba tunaweza kuwaignore wamalawi kwasasa.
 
Tunaomba juhudi za kutatua mgogoro huu kwa njia ya kidiplmasia utumike.
 
Kwanini lakini? Mbona tuna libahari la Hindi, si tuwaachie tu hako kaziwa? Afterall its land locked country!
 
Hatuna uwezo wa kupigana na Malawi kwasababu hiyo morality ya wananchi, these times around ni huge "luxury".Siyo watu wengi wenye kujivunia utanzania kwasasa.

Sisemi kwamba hatuna uwezo wa kuwapiga wamalawi,lakini matatizo ya internal ni makubwa kiasi cha kwamba tunaweza kuwaignore wamalawi kwasasa.
hatuwezi kuwaignore wamalawi kwa sasa, they've been ignored long enough.
Lazima tuwe na suluhisho la mgogoro huu, kama wewe huna uzalendo, kaa pembeni usitake kuwakatisha watu tamaa.

Kila kitu kwako wewe ni siasa tu, hapa hatujali hiyo mivyama yenu ya kipumbavu tunataka wayao,wanyakyusa, wananchi wa ludewa, kyela, nao wafaidike bila shari na ziwa ambalo ndiyo source yao ya chakula, usafiri na mambo mengine ...

Wewe kama unaogopa ni bora unyamaze kimya, maana unaonekana mpumbavu sasa.
 
Siamini hili; hii ndio sababu ya kwanini siamini anafaa kuwa Rais. Anazungumzia vita leo? kwa lipi hasa? wanataka kuescalate vitu bila sababu ya msingi. Hafai kuwa Amiri Jeshi Mkuu. Kama hii ni sababu ya kwenda vitani basi tumekosa viongozi kweli kweli!
Mzee Mwanakijiji, you might be growing too old!. Kwa kawaida as one grows older is also expected to be wiser, nikukosoma siku hizi nakuona you are either becoming less wiser au inawezekana mimi ndio nashindwa to make sense hivyo uwezo wa uelewa wangu ndio unapungua kuweza kukuelewa!.

Hivi kuna sababu nyingine yoyote ya nchi kuingia vitani ambayo ni kubwa zaidi ya nchi kutishiwa mipaka yake?.

Kuna justfied wars na unjustified wars!. Kwangu mimi kitisho cha Malawi ni justified war!. EL is right and he is the not only the one who can make the best president of this country but he is "the one and only best" CCM has!.

Kwa kauli kama hii, ni uthibitisho kuwa yeye tayari ndiye Amiri Jeshi wetu!. Who else?. Nani mwingine yoyote ameweza kujitokeza to stand firm on this national security threat?!.

Naendelea kusisitiza tuendelee kukosoa madhaifu na madudu ya serikali iliyopo kwa nguvu zetu zote, ila pia kama kuna mabaya 99 na zuri moja, hilo moja litajwe!.

Hii kauli ya EL imekuja mahali pake at the right place at the right time!.

Pasco.
 
hatuwezi kuwaignore wamalawi kwa sasa, they've been ignored long enough.
Lazima tuwe na suluhisho la mgogoro huu, kama wewe huna uzalendo, kaa pembeni usitake kuwakatisha watu tamaa.
Kila kitu kwako wewe ni siasa tu, hapa hatujali hiyo mivyama yenu ya kipumbavu tunataka wayao,wanyakyusa, wananchi wa ludewa, kyela, nao wafaidike bila shari na ziwa ambalo ndiyo source yao ya chakula, usafiri na mambo mengine ...

Wewe kama unaogopa ni bora unyamaze kimya, maana unaonekana mpumbavu sasa.
mbona sijaona pahala wamalawi wamesema hawataki hao uliowataja wanufaike na ziwa Nyasa?can you back up you claims?suluhisho la mgogoro ni lipi?huu mgogoro ulivyo,mwenye kuwa juu ni mwenye influnce at the time being,kama mama Clinton yuko nao,wala msijisumbue,kamateni mafisadi kwanza,nchi itarudi kwenye msitari,"umma" utalinda nchi.Kuna pahala panshinda nguvu ya umma?jeshi lipo lakini hata recruiting inafanyika kwenye umma wa wananchi,na sapoti ya vita pia.Hatuna nguvu za "big nations" kujiamulia bila sapoti kubwa ya wananchi.Halafu matatizo tuliyonayo ni makubwa kiasi kwamba kupostpone hii issue ni more relevant.
 
Back
Top Bottom