kitalolo,
Wengi wanaoshabikia kauli ya kichochezi ya Lowassa ni wale ambao wamezaliwa katika miongo mitatu hii na ambao hawajui ni kwa kiasi gani vita hugharimu. Hawakumbuki miaka 18 ya kujifunga mikanda, hatimaye ikageuka kuwa miongo 18. Lowassa atafute mtaji mwingine wa kisiasa, hili litamalizwa kwa diplomasia mahiri tuliyonayo.
Chifu nakubaliana kabisa na wewe na
kitalolo.
Nashangaa watu wenye uelewa kufurahia kuingia katika vita kipindi ambacho taifa lipo katika dimbwi la umaskini wa kupindukia. Kila nyanja ya huduma za jamii ipo tenge na ovyo;sasa hizo pesa za kupigana zitatoka wapi? Na itakuwa busara kutumia pesa hivyo,wakati raia tunakula vumbi? Kama athari za vita ya Uganda hadi leo zinaonekana kwenye uchumi,hizi zitakazokuja,itakuwaje?
Pili,hapa tunapaswa kutumia busara na utashi katika suala hili. Kama kuna uwezekano wa kuwepo mafuta hapo ziwani,hivi haiwezi ikawa ni chokochoko inayochokolewa na mataifa ya kaskazini? Je,hawatamani kuona tunatoana ngeu na kuchinjana huku wao wakinufaika kwa kutuuzia silaha,kisha watapeana tenda za ukarabati baada ya vita;huku wakijipenyeza taratibu katika kunywa mafuta hayo?
Kwa mtazamo wangu,taifa kwa sasa halina haja ya kufikiria vita;litumie njia zote za kidiplomasia. Linapoanza kujidai na uwezo wa kijeshi,kuna mataifa yasiyo na mapenzi mema na Afrika,tayari yanajiandaa kutoa supoti ya kijeshi kwa upande wa pili,na hapo naamini kila mtu anaelewa nini kitafuatia. Tafadhali tujifunze yaliyotokea Liberia na Sierra Leone na suala la Blood Diamonds.
Siungi mkono hilo tamko,siungi mkono vita.
Naunga mkono njia za mapatano kwa amani.