Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

Kesi iko mahakamani ya nani atangaze vita 2ngoje mahakama itangaze nani wa kutangaza vita
 
Membe na Lowasa hawaja tanggaza vita bali wametoa maonyo tu na hili ni kutokanananafasi zao za kisiasa katiak nchi hii
Hivyo basi Jemedari mkuu wa vita anasubiriwa uitangaza hiyo vita nae na Kikwete kwa mujibu wa katiba

swali langu ni hili je jemedari wetu ni wa mstari wa nyuma au wa mbele ?
"Gharama ya Vita ni kubwa kuliko ushindi akao patikana huko" Mungu ibariki Tanzania kisha ukaibariki na Africa
 
Hakuna sababu ya vita wakati swala lenyewe linawezakupatiwa ufumbuzi kwa kukaa mezani. Na mgogoro huu haujaanza leo. sasa kwanini vita izungumzwe kipindi hiki? zinaweza zikawa mbinu za kisiasa tusahau mambo mengine. Ni busara tu itumike pande zote mbili malawi na sisi. Wanao sema sema vita naona wanakurupuka, hata wa malawi wakikataa kuna njia zingine za kupata ufumbuzi lakini vita sio ufumbuzi wa tatizo.
 
....Mungu ibariki Tanzania kisha ukaibariki na Africa
Kama vita haitakuwepo MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA, ila kama vita itakuwepo MUNGU IBARIKI TANZANIA, itabidi na wimbo wetu wa Taifa kwa kipindi cha Vita ubadilishwe sababu AKIIBARIKI AFRIKA, nayo Malawi itabarikiwa!
 
Hamna cha utaifa hapa vita ya Uganda ilituacha hoi mpaka Leo sasa ni bora tuwaachie Hilo ziwa vizazi vijavyo vikishakuwa na uwezo vitalikomboa lakini sisi kwa serikali hii ya ccm bado kabisa
 
Kama vita haitakuwepo MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA, ila kama vita itakuwepo MUNGU IBARIKI TANZANIA, itabidi na wimbo wetu wa Taifa kwa kipindi cha Vita ubadilishwe sababu AKIIBARIKI AFRIKA, nayo Malawi itabarikiwa!
ha ha ha ha haaaaaaa ngoja tuone mwisho utakuwaje
 
Hapa ndipo nasi tunatakiwa kuchanganya na za kwetu- hawa wanataka kupata mali kwenye eneo na sisi tumo- tuingieni tuucheze mchezo. ama upande wetu tumebinafsisha? ndo tunataka wote tukose? diplomasia na ya kushirikiana wote tunufaike.
 
ULIKUWA MGAO FEKI WA UMEME ILI KULA PESA ZA TANESCO SASA NAONA DEAL IMEHAMIA VITA NA MALAWI.

Tanzania imekuwa ni nchi ya watu wajanja sana katika maisha yao ya kila siku, ndiyo maana inaitwa 'BONGO' Inaitwa bongo kwa vile kila mtu anajitahidi kutafuta mbinu ili aweza kuishi na kumudu maisha yake ya kila siku amabayo ni mbinde sana kuona unafikisha mwisho wa mwezi. Watu watajitahidi kutafuta mbinu hizi na zile ile wale hata kama mlo ule ni NAJISI lakini lazima wafaulu, rejea mgao wa umeme, watu wamebuni mgao feki ili kujipatia pesa hawajali hata kama shirika likifa au hawajali hata kama watu watakaa gizani, rejea pia rada, watu wameiuzia serikali rada kwa bei mara dufu ili kujitajilisha wao binafsi na siyo serikali ya nchi yao, UZALENDO ule tumekuwa tumuukuta sasa unatoweka nchini kwetu kila mtu anataka mshiko tena mshiko mnono na familia yake, rejea nyumba za serikali, watu wamedhurumu nchi yetu kwa kujiuzia nyumba za serikali kwa bei nafuu na hali wanajuwa wanahujumu nchi, rejea wanyama pori wetu wanavyosafirishwa nje za nchi wakiwa hai wengine wafu hii yote ni kujitajirisha binafsi si kwa ajili ya nchi yetu.

Sasa hivi, watu hao hao wanaotaka kujinufaisha binafsi na familia zao wameanzisha DILI la mzozo FEKI na nchi ya malawi ili kupata uhalali wa kutafuna pesa ya watanzania, Ni lazima tuwe macho na njama hizi:-

1. wataanza dili za kununua silaha feki za kupigana na malawi
2. wataanza dili ya kukodi magari makubwa ya kusafirisha silaha feki kwenda mpakani
3. wataanza dili ya kununua dizeli feki kwa ajili vita na malawi
4. wataanza dili ya kununua mafuta mapesi feki ya kulainisha mitambo ya kijeshi
5. wataanza dili ya kuajili wanajeshi feki wa kupigana malawi
6. wataanza dili ya kununua sare za kijeshi feki kwa ajili vita na malawi
7. wataanza dili ya masurufu feki ya kutembelea uwanja wa mapambano
8. wataanza dili feki ya kuchangisha watanzania fedha kwa ajili vita na malawi
9. wataanza dili za vikao feki kwa ajili kujadili vita na malawi
10. wataanza dili feki ya propoganda ya vyombo vya habari ili kuhalalisha vita na ulaji

Watanzania ni lazima tuwe macho na viongozi wa dili hizi ili kuendelea kuibia nchi kwa kuanzisha mzozo feki na nchi jirani ili waweze kunufaika kwa dili feki kama zile za TANESCO, RICHMOND, EPA, AIR TANZANIA, BANDARI, VITALU VYA WANYAMA!!!! Jamani tutafilisi nchi hii, ole wenu baba wa taifa, waziri mkuu sokoine na karume original wafufuke leo ninaimani matajificha ndani ya vyoo vya shimo wote mnao chongo MA-DILI ili kuifilisi Tanzania yetu yenye neema.

 
Who is Lowasa in this country? Where is Jakaya Kikwete?
 
Wakubwa nasema tena,pamoja na serikar yetu kuwa na matatizo rukuki,lakini linapokuja swala la kama malawi ni lazima tuweke itikadi zetu pembeni na tuwe kitu kimoja.sisi JWTZ tunaamini ktk UMOJA na ndio maana ukiona nembo yetu kuna neno UMOJA,sasa basi Niwe muwazi kabisa bila kutafuna maneno,Nikiwa mmoja wa watu ambao kwa namna yoyote ile muda wowote naweza kuteuliwa kuwa mstari wa mbele kwa kadri wakuu wangu watakavyoona inafaa,inatokea inakua,muda wowote ule tukazipanga na Malawi ,tunawapika ndani ya dk 30 na yule mama tunawaletea hapa tena akiwa ajaava hata gauni.Lowasa hajatania,vijana tumejianda na tunahamu sana tena sana.
 
Kwanza nawaomba waheshimiwa wana JF katika kipindi hiki cha mgogoro kati ya Tanzania na Malawi tulete thread na kuchangia kwa kuzingatia maslahi ya Taifa. Tuache SIASA na maslahi.

Pili naomba michango yenu kwa kuzingatia maslahi ya Taifa, ni nani anayestahili kutangaza kwa mara ya kwanza uwezo na nguvu yetu ya kijeshi? Membe alizungumza na kuionya Malawi baadae akaja Lowassa akasema tuko imara na tayari kwa vita! Sasa suala la nani atangaze ni nyeti sana na lina sababau nyingi na athari zake kitaalamu.

kwanza unapaswa kufahamu kuwa jeshi liko chini ya wizara, yenye waziri na ina kamati ya bunge, mbayo ndio inajua mwenendo mzima wa jeshi kimbinu, kivifaa, jitaaluma maana vyote hupitishwa na bunge. Lowasa kazungumza kama mwenye kiti wa kamati ya wabunge wa wizara ya mambo ya ndani maana anajua manunuzi yake, namana linavyojiandaa na idadi yake na sera zake, hivyo kama mbunge kawaeleza wananchi hali halisi ya Jeshi. hajatoa tamko kwamba twende vitani HAPANA, kasema kivifaa na kitaaluma jeshi liko vizuri maana pesa za kununua vifaa na mbinu kujua waajiri kiasi gani jeshi vyote vinapitishwa na bunge.

Lowasa hajatoa amri kwa wanajeshi waende vitani, kaeleza wananchi, anayetakiwa kuwapa amri wanajeshi kuanza vita ni kikwete na ndio maana yuko kimya maana yake vita haijaanza.
Pia ujue suala kama hili ambalo ni nyeti na watu wa mpakani wameanza kuwa na uwoga SIO VIZURI rais kutoa kauli yeyote kwa sasa, maana bado wako katika mazungumzo lakini muda wowote anaweza toa kauli sasa ili jeshi lijipange na wananchi kuwa makini watu wa chini kama akina membe na lowasa ndio wanaongea ambao nchi wanafiki marafiki na malawi wasijesema kikwete katangaza vita.
 
Malawi Wapewe Mikoa yao Mbeya Iringa na Ruvuma... kama Tuna Heshimu Mipaka ya Wakoloni na Tanganyika Ipewe Burundi Rwanda na Mombasa... Zanzibar nao Sijui Watadai Kitu? Suala la Kuongeza Eneo la Bahari Jusa Muhindi Alikuja Juu Sana
 
kuna ajali iliotokea tabora watu wamekufa lakini bus lilikuwalimejaa kama watu 90 police wapo lakini hawafanyi kazi itakuwa hao wanajeshi ....
si bora waliache hilo ziwa waje waturudishie dhahabu zetu wanazowapa wazungu nani atakubali akapigani kwa faida ya wachache lowasa anajuwa atapata nin cha kumnufaisha
 
Kwa hali ilivyo sasa naona kila mzalendo wa inchi anayeguswa na ulindaji wa mipaka ya inchi at any coast
 
kuna ajali iliotokea tabora watu wamekufa lakini bus lilikuwalimejaa kama watu 90 police wapo lakini hawafanyi kazi itakuwa hao wanajeshi ....
si bora waliache hilo ziwa waje waturudishie dhahabu zetu wanazowapa wazungu nani atakubali akapigani kwa faida ya wachache lowasa anajuwa atapata nin cha kumnufaisha

naomba uweke mambo yote pembeni,harafu usifananishe JWTZ na police kumbuka hatwendi kupiga na mmalawi tukiwa na mabomu ya machozi,...tunaposema tumejianda tunamaanisha.jambo moja tu unalotakiwa kufanya wewe,ni kuweka yote pembeni na kusubr jesh lako tunaenda kufanya nini,hapo ndio utajua kuwa ile kodi yako inayotulipa mshahara inafanya kazi kweli?....stay tune utaniambia wewe na wamalawi wako nin tutawafanya
 
Kwanza nawaomba waheshimiwa wana JF katika kipindi hiki cha mgogoro kati ya Tanzania na Malawi tulete thread na kuchangia kwa kuzingatia maslahi ya Taifa. Tuache SIASA na maslahi.

Pili naomba michango yenu kwa kuzingatia maslahi ya Taifa, ni nani anayestahili kutangaza kwa mara ya kwanza uwezo na nguvu yetu ya kijeshi? Membe alizungumza na kuionya Malawi baadae akaja Lowassa akasema tuko imara na tayari kwa vita! Sasa suala la nani atangaze ni nyeti sana na lina sababau nyingi na athari zake kitaalamu.

Nahusi kama huumgogoro niwakutengenezwa. Na wana ccm wanao utakaurahisi ndo wanatoa maneno makali etitupo tayaria. Mbona hawatuelezi kama walisha kaa mezamoja na malawi marangapi na wakaendelea kukaidi.

Hapa naona noi ccm inataka kupotezea mambomeng yaliyotekea kipindihiki. Migomoya walimu, kusitishwa mafao yakujitoa, issue ya ulimboka ,wabungunge waarushwa, kifocha yule polisi na mengineo mengi.

Ukitaka kumini nininachokuambia linganisha huu mgogoro na ule wakipindicha idiamini . Nyerere alieleza walichojaribu kufanya na mpaka wafikie maamuzi ya vita inakuaje. Hii ni janjayanyani kula maindi mabichi

Huumgogoroo waziwa upo tangia enzi za nyerere lakini haujawahikua hivi na hautakaa uwehivi

Angalie tene kipindi cha mkapa kulikua naishu ya wahutu lakini mkapando aliongea maramoja na tukaimaliza kiume .
Kwahii mimi hamnidanganyi . Ni wanaoutaka urisi ndo wanashindana kusema tupotayari mbona wizara ya ulinzi na usalama haiongeo kitu
 
hivi amiri jeshi mkuu wa malawi hajatoa tamko?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Membe na Lowassa wamevunja katiba kwa kutamka mambo ya vita. Ibara ya 44 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2005 inasema...'Rais anaweza kutangaza kuwapo kwa hali ya vita kati ya ya Jamhuri ya Muungano na nchi yoyote'.

Viongozi wetu waepuke kutamka maneno yanayoashiria vita. wanaweza kujibu hoja bila kuonyesha dalili kwamba vita vyaweza kutokea.
 
Back
Top Bottom