Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

Kweli Lowasa hafai kabisa sijawahi kumsikia akikemea au kulaani ufisadi hata siku moja.
 
kiongozi yoyote anaye tokana na ccm hafai hata kidogo ukiweka samaki mzima kwenye kapu lenye samaki wabovu nae ataoza
 


Nitandelea...

NB: Kwa wageni wa hoja hizi warejee mada yangu ya 2007: Kikwete Siyo Safi, Yes I said it

[/SIZE]

Mzee Mwanakijiji, hakika tafakari yako ni zaidi ya chemsha bongo.
Nimenukuu uzi wa Hutaki Unaacha wa mwaka 2011, Oktoba 13 na nikajiuliza; katika mazingira haya, Chama dola CCM, kinaweza kupambana na ufisadi?
Je vita dhidi ya ufisadi hapa Tanzania inaweza kupigwa bila kugusa Magogoni?
CCM kinaweza kutoa mgombea atakayeweza kumtikisa Citizen No.1 wa sasa pale Magogoni?
Kama Citizen No.1 wa pale Magogoni yuko katikati ya Richmond and Escrow scandals, mgombea toka CCM
ataiokoaje nchi yetu?

Uzi nilionukuu wa Hutaki Unaacha ni huu hapa chini;

Membe be careful, adui wako wa kweli humjui
By Hutaki Unaacha 13[SUP]th[/SUP] October 2011
Mh Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa hajamfahamu adui yake no 1. Hii inatokana na ukweli kuwa vita anayopigana inamhusisha yeye na adui asiowajua. Membe anaamini adui zake wakubwa ni Rostam na Edward. Amepotoka.

Membe napenda nikufahamishe ya kuwa, usipoangalia, yatakupata makubwa zaidi ya yale yaliyompata Harrison. Unapigana na watu hatari na wanaotumia akili nyingi sana kwenye game hili la siasa.

Katika baraza la kwanza la JK uliteuliwa kuwa Deputy wa Home Affairs. Ulilalamika sana kwa JK. SMS ya kulalamika kwako uliyomtumia JK, iliwafikia Rostam na Edward at the same time bila wewe kufahamu. Tafakari kwanza!

Richmond haijaletwa na Rostam wala Edward nchini. Wewe unafahamu vyema jinsi JK alivyocheza dili la Richmond kishamba akishirikiana na Gire baada ya mazungumzo yao huko U.S. Baada ya mambo kuharibika ndipo Rostam na Edward wakashirikishwa. Unafahamu vizuri role aliyoicheza Rostam kuhakikisha angalau Dowans inazaliwa ili kumwokoa JK. Ya Lowassa kujiuzulu unayafahamu vizuri sana sitaki kuyazungumzia kwa sasa.

Sitta hakuwahi kuwa rafiki wa Harrison hata siku moja. Alimtumia tu ili kutimiza malengo yake ya kumwondoa Lowassa kwenye nafasi yake. Wewe ndiye uliyekuwa ukiwachonganisha mara kwa mara JK na PM wake Lowassa. Hata nafasi ya nje uliipata kwa jungu kubwa na la ustadi wa hali ya juu ulilochezewa na vijana wawili wa Usalama wa Taifa kwa kumchafua Lowassa. JK akaanza kukuamini.Ulicheza vizuri karata kwani ulijua fika jinsi gani Sitta alivyomchukia Rostam na Lowassa kwa yale waliyomtendea ili asiwe PM na kwa ustadi wa hali ya juu ukamshawishi Sitta alitumie Bunge ili kumwadhibu Lowassa.

Mwakyembe ana ugomvi wa siku nyingi na Rostam hata kabla ya JK kuwa Rais. Alitumia nafasi hiyo kumnyonga Lowassa na rafiki yake Rostam na kwa bahati mbaya akakiri ndani ya bunge kuwa kuna machafu mengi yameachwa ili kunusuru heshima ya Serikali. Kosa kubwa sana kuwahi kufanywa na mtu aliyepitia idara ya Usalama wa Taifa. Unafahamu vyema kuwa hili kosa ndilo linalomgharimu Harrison huko Appollo. Baada ya Lowassa kuangushwa, ulikumbatiana na Mwakyembe, Rais akawapongeza, mkafurahi, mkabweteka na kumwamini JK. Kosa la pili kubwa.

Kwa bahati mbaya sana ukaungana na Mwakyembe, Mengi, Sitta, na wafuasi wake kwa ajili ya kuutafuta urais tena kwa kumtumia mwanaye Ridhiwani. Hili ni kosa la tatu kubwa kwani ulichanganya kwenye kundi lako watu wasio marafiki wa JK ambao kwa hakika wata-demand umburuze JK mahakamani pindi utakapokuwa rais.

Rostam-JK-Lowassa

1. Hawa ni marafiki wakubwa ambao licha ya wawili kuwa nje ya serikali lakini wote watatu wanaendesha Serikali na hawasiti 'kuwanyamazisha'' wabaya wao wanaogusa interest zao.Individually wanatofautiana ila wakiwa watatu ni wamoja. Membe naomba ufahamu hili.
2. Wewe ulimtaka Sitta awe Spika kwa mara nyingine tena. JK alimtaka Sitta pia lakini katika kikao cha watatu akakubaliana na pendekezo ingawa kwa shingo upande la Anne kuwa spika.
3. JK atakuwa safe kama Lowassa akiwa Rais. Hatakuwa safe endapo mmoja wenu atakuwa Rais. Anafahamu hili fika.
4. Richmond itarudi Bungeni kabla ya 2015.Wakati wa kujadili, wewe na Mwakyembe mko tayari kusema ukweli. Ili kuwazima, Mwakyembe 'ataondoka' then wewe waweza kufuata!. Haya yatafanywa na umoja wa hawa watatu na si individually
5. Ndani ya CC iliyopita zilipigwa kura za siri ili kumfukuza Lowassa uanachama. Kati ya wajumbe 32, 19 walimsupport Lowassa na 13 kwa JK!.Hapa wanaonekana ni wapinzani ingawa wakiwa watatu ni wamoja.
6. JK anaweza kukusikiliza na kujifanya mko pamoja naye. Lengo ni kutaka kujua what's going on in your group ili wawamalize vizuri.
7. JK hakumtaka Bilal, lakini umoja ukalazimisha ndiye awe Makamu wa Rais. Mkapa alitumwa bila kuelewa.
8. Hawa watatu kwa pamoja walimteua Mkama. Wewe hujui hilo ingawa mwenzako Chiligati alishastukia!
9. Membe unafahamu ya kwamba kujivua gamba ni hoja iliyoletwa na Rostam kwa mara ya kwanza kwenye kikao cha watatu hao ili game iishie bungeni kwenye kujadili Richmond upya? Symbion iko nchini Membe. Unajua kaileta nani?. Je, nani kamleta Mama Clinton nchini?
10. Membe muulize Mwandosya akwambie jinsi watatu hawa wanavyomtesa. Umesahau tulipokuwa Marekani jinsi Balali alivyosema kuhusiana na chanzo cha afya yake kuzorota?.
etc, etc, etc, etc

Ushauri wangu kwa Membe
:

Be careful sana katika game hili Membe. Kama kweli unautaka Urais lazima kwanza uufahamu mchezo unavyokwenda. Wenzako wanacheza game nzito na kisayansi zaidi. Know your enemy first. Na kwa kukusaidia, adui yako namba moja ni huo utatu and not an individual person.
 
edward-lowassa.jpg



wewe wasema, lakini sisi lowasa ndo chaguo letuuuu
 
Mwanakijiji

Tatizo la Tanzania siyo ufisadi bali ni ukose wa elimu ambayo humwezesha mtu kutofautisha aliye msafi na fisadi. Upinzani kwa zaidi ya miaka tano imekuwa ikipiga kelele kuhusu ufisadi lakini ikifika uchaguzi wananchi wanashiriki kwenye ufisadi kuchagua mafisadi.

Kumbuka Elimu ni maarifa ya kutambua ambalo ulikuwa hulitambui na kutatua matatizo ya jamii.

Bila elimu bora na yenye kujumlisha utu, bado watanzania wataendelea kuona mwizi kama shujaa na wapiga dili kama watu wajanja.

Hata sasa hivi wananchi wanakosa namna ya kutofautisha Lowasa na wengine kwa sababu ya kukosa elimu.

Elimu itasaidia watanzania kujitambua.
Aljazeera, mimi nakubaliana na wewe kuwa tatizo la Tanzania ni Elimu sawa!, lakini katika Elimu hii tuliyonayo ni nini kinakosekana? Maana tukienda jumla jumla tutasema hivyo Elimu, Elimu, Elimu!! Je hatuna wasomi? Hatuna Vyuo vikuu? Hatuna shule za kutosha? Nini kinachokosekana ambacho kinawafanya wasomi wetu wakishamaliza vyuo wawe mafisadi? Leo hii vijana wanaomaliza vyuo hwatulii sehemu moja makazini!! wakipata nafasi wanapiga pesa na kusepa!!! Je ndiyo Elimu tunayoizungumzia?
 
edward-lowassa.jpg


Watanzania wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanaaminishwa kuwa ana maono ya kiuongozi ambayo yakitumika yanaweza kulinasua taifa letu toka hapa lilipo. Wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa ni kiongozi bora ambaye Watanzania wanapaswa kumwangalia kwa matumaini - ndio maana ya "Safari ya Matumaini".

Wapo kati yetu ambao wameshazugika na pendekezo hilo na wamekuwa kama waliorogwa hivi. Wapo baadhi yetu kwa muda wote wa uongozi wa Lowassa (hasa baada ya kuwa Waziri Mkuu na baadaye) tuliona kile ambacho labda kimefichika kwa wengi - Lowassa hafai.

Hii si hukumu juu ya utu wake, heshima au ubinadamu wake; ni hukumu juu ya uongozi wake na maono yake kama kiongozi. Kumkataa Lowassa, maono yake, uongozi wake na fikra zake siyo kumchukia yeye kama Mtanzania mwenzetu au kama binadamu. Ni kuwa na tofauti naye na vile anavyowakilisha kiasi kwamba tofauti hizo hazijawezi kupatana (irreconcilable differences).

Katika siasa ni lazima tuheshimu uwepo wa tofauti hizi na tuelewe ndio msingi wa kutafuta viongozi bora zaidi au chama bora. Kwa kadiri yeye atakavyojaribu kujiuza ndivyo na sisi wengine tutazidi kuonesha kuwa hauziki au zaidi hanunuliki. Hii si chuki ni tofauti tu ya msingi (fundamental difference).

Pendekezo langu linatokana na hili; kwamba zipo na zimedumu tofauti za msingi kati ya maono ya baadhi yetu na maono ya mgombea huyu mtarajiwa kutoka CCM. Tanzania haihitaji maono na uongozi wa Lowassa kwa sababu nyingi tu; nitaanza na moja ya leo na nitaendelea kwenye mada hii hii kila ninapopata nafasi hadi jina lake litakapotupwa na NEC na yeye akaendelea kuwa Waziri Mkuu wa zamani.

Mara kwa mara baada ya sakata lake na katika jitihada za kujirudisha katika umuhimu (relevance) Lowassa amekuwa akizungumzia mwelekeo wa sera zake na kitu kitakachomuongoza. Aliamua kwenda kinyume na mwelekeo wa serikali ya chama chake ambayo iliweka mkazo kwenye "Kilimo Kwanza"; yeye ameamua kuja na hoja ya "Elimu Kwanza".

Alielezea kupinga kwake hoja ya Kilimo Kwanza miaka michache nyuma alipohojiwa katika kipindi cha Dakika45 (kinachorushwa na ITV). Alinukuliwa kusema "Mpango huu wa Kilimo Kwanza umekosa nguvu kwa sababu kuanzishwa kwake hakukuzingatia dhana ya ukombozi wa mwananchi wa kawaida. Tangu awali ndani ya chama (CCM) nilieleza kuwa sitaunga mkono hoja hiyo mpaka kuongezwe mashiko na kuwa Elimu Kabla ya Kilimo Kwanza"

Hoja hii ameirudia tena juzi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ambao bila ya shaka wengi wamekuwa 'charmed' na wingu la umaarufu wa Lowassa kiasi kwamba hakuna ambaye ameweza kumbana vizuri kwenye maswali. Anasema endapo atachaguliwa basi ataelekeza nchi kwenye "elimu kwanza"; kwamba hiki ndicho kipaumbele chake.

Ndio maana sisi wengine tunasema hafai; kwa sababu inaonekana siyo yeye wala chama chake ambao wamelielewa vizuri tatizo linaloikabili Tanzania; tatizo ambalo limeielekeza (orient) Tanzania kufuata njia ya Nigeria. Kwamba tunaweza kabisa kutengeneza uchumi wenye nguvu lakini wa taifa lenye umaskini uliokithiri, lisilo na usawa na la wasomi wasioweza kulipeleka taifa mbele. Tutakishia kujisifia wingi wa wasomi ambao wengi wataishia kwenda nje ya nchi kutafuta maisha. Taifa ambalo litakuwa limegawanyika sana kama Nigeria - licha ya kuwa na wasomi wengi.

Lowassa inaonekana ameshindwa kuelewa au hataki kukubali kuwa tatizo kubwa la Tanzania ni la aina tatu:
1. Ufisadi
2. Ufisadi
3. Ufisadi

Lowassa hatopambana na ufisadi kwa uzito unaostahili kwani haoni kuelewa kuwa ni tatizo la hatari zaidi kwa taifa "kuliko vita wakati wa amani" kama alivyosema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Kutokuelewa kuwa Ufisadi ndiyo sekta haramu yenye nguvu zaidi katika nchi yetu ni kushindwa kuelewa tatizo letu hasa ni nini. Ufisadi umepenya (permeate) kwenye kila sekta nyingine zote (rasmi na zisizo rasmi). Umeathiri elimu, afya, usalama, na hata umoja wa taifa. Kutokulielewa tatizo hili kwa mtu anayetaka kugombea nafasi ya Urais (haijalishi anatokea chama gani) ni kutokuelewa namna ya kukabiliana na changamoto nyingine zote.

Kwa sababu hii peke yake Lowassa na mgombea mwingine yeyote ambaye haweki "ufisadi" kama ajenda yake ya kwanza na kubwa zaidi basi hafai. Kwa sababu atatuzungusha kwenye madudu mengine yote isipokuwa kwenye kumkoma nyani giledi.

Kikwete - kwa wanaokumbuka - alishabikiwa na wengi si kwa sababu ya "Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya" bali zaidi kwa kuwapa Watanzania matumaini kuwa atashughulikia ufisadi vikali. Hotuba yake ya kulifungua Bunge na ile ya Ngurdoto na zile ziara zake za kutembelea Wizara ziliwafanya watu waamini kidogo kuwa hatimaye "kipele kimepata mkunaji". Leo hii miaka tisa baadaye ripoti ya CAG imeonesha kidogo tu kuwa tatizo hili la ufisadi halijapata mtatuzi ndani ya CCM na hata mtu anayeshabikiwa sana kuwa ati anaweza kuwa Rais inaonekana tatizo hili limempita kabisa.

Nikisema "hafai" simsingizii; nasema kilicho dhahiri; I'm just stating the obvious.

Wanaomtaka Lowassa - wapenzi, mashabiki na waumini wake - watuambie vita dhidi ya ufisadi ina umuhimu na uzito gani katika agenda za Lowassa. Wakituambia kuwa "ni mojawapo" ya mambo atakayoyashughulikia tuendelee kumkataa kwa sababu bado atakuwa hajaelewa tatizo letu hasa ni nini kama taifa.

Nitandelea...

NB: Kwa wageni wa hoja hizi warejee mada yangu ya 2007: Kikwete Siyo Safi, Yes I said it

saafi mkuu, naomba topic nyingine ndeeefu ya kumuongelea anayefaa na umtaje jina. Siyo lazima atoke ccccmmm.
 
Safari hii ya matumaini ya kuibiwa imeanza, edo iz unfit, kwa kila idara, mpaka afya yake,

Utabidi ssm wapimwe akili kama wakipitisha, kisha kama atachaguliwa kuwa rais itabidi site tupimwe maana huenda tukawa na shida kubwa..
 
Nimefurahi uchambuzi wako !

CCM chukueni hii itawasaidia kule cc
 
Lowassa hafai kuwa rais;
tunarudi tena kwenye wimbo ule ule wa rostam azizi na chenge wa mafisadi papa.

Heri hata huyo mtoto wa Nyerere.
 
Ndio Mkuu Mzee Mwanakijiji, unasema kuwa Lowassa Hafai, and yes you said it so what?!.
Ila sio Lowassa tuu hafai, kama nakumbuka vizuri uliwahi kusema hata JK hafai, and you said it!, pia uliwahi kusema hata CCM haifai and yes you said it!, ni JK ndiye aliyechaguliwa na CCM ndich chama tawala mpaka leo, na leo tena amesema Lowasa hafai, sitashangaa ikiwa ni Lowasa na 2015 ni CCM tena, ila hizi "Yes I said It" za Mkuu Mzee Mwanakijiji, zitaendelea kwa hao wanaofuata!.

Na kwa ajili ya kuweka kumbukumbu safi, hizi ni baadhi ya yes I said it za Mkuu

  1. Rostam, Msabaha, Kikwete and Richmond - Yes I said it again ...
  2. Rashid Othman: Umeshindwa Jiuzulu! - Jamii Forums
  3. Ni lazima tugawanyike; Lazima tusiwe na umoja! -Yes I said it ...

    Ingekuwa kauli hizi za Yes I said it, zinaandamana na doing something kuzitekeleza, ingekuwa something, lakini kama ni kauli tuu za Lowassa Hafai! Yes I said It, baada ya hapo nothing more, nothing less, then 2015 rais wetu ni Edward Ngoyai Lowassa, say it or don't, it makes no difference!.
Pasco
Mzee Mwanakijiji ametimiza wajibu wake... kilichopo ni kwamba, endapo mathalani MM angepewa uwezo wa kupiga kura 25 million peke yake na kura hizo pekee kuamua mustakabali wa rais wetu, basi kwa mujibu wa MM ni kheri kura hizo zote aziharibu kuliko kumpa Lowasa! Kinyume chake, kuna wengine endapo wangepewa uwezo huo wa kuhodhi kura 25 million peke yao, basi haijalishi Lowassa anasimama na nani... zote hizo wangempa Lowassa! Haidhuru, kura hizo 25 million tunaweza kuziita a powerful veto vote yenye uwezo wa kuamua nani awe rais bila kuhitaji kura ya yeyote ya ziada... ni tofauti na ile ya UN yenye uwezo wa kukataa peke yake! Hapa ndipo unaposimama umuhimu wa hoja ya MM, haidhuru hata kama Lowassa, hatimae atashinda kwa kishindo hata kama ni kwa 95% na zaidi... bado haitaondoa ukweli wa Lowassa kwamba hafai; si tu kwa mujibu wa Mzee Mwanakijiji bali kwa mwingine yeyote yule ambae hana amtakae kwenye kinyang'anyiro hiki; iwe kutoka chama tawala au upinzani!

I hate to say this lakini ukweli ni kwamba, hata kama JK nae alikuwa fisadi kabla ya hata kuingia magogoni but JK was smart enough as compared to EL! He's smart enough coz' huku mtaani haikufahamika hivyo kwa wengi... Kama alikuwa na tuhuma zozote za ufisadi basi tuhuma hizo ziliweza ku-circulate only among few people... sina shaka hata chembe kwamba hili lilichangiwa sana na zama zenyewe... hazikuwa zama za free flow of information kama ilivyo sasa! Katika hali ya ajabu kabisa, Lowassa anaonekana kuwa the most stupid accused corrupt leader seeking the highest position in the country... YES, I repeat, the most stupid accused corrupt leader seeking the highest position in the country!!! He's top of the stupid accused as a corrupt leader because, pamoja na kwamba kila mtu anafahamu tuhuma za ufisadi dhidi ya Lowassa lakini bado ame-opt ku-side or team up with ALL other accused corrupt leaders! Sitamtaja Serukamba kwa maana yeye ni mganga njaa anayeweza kutumiwa na yeyote yule lakini hakuna nchi hii asiyefahamu tuhuma chafu za ufisadi dhidi ya Rostam Aziz lakini pamoja na yote hayo huyo ni one of the insiders or probably Master-minder wa Lowassa katika kuingia Ikulu! Hakuna hata mmoja Tanzania hii anayefuatilia siasa za Tanzania asiyefahamu tuhuma za ufisadi wa Andrew Chenge... lakini huyu nae ni insider au bila shaka ni Senior Tactic Team Member wa EL katika mbio zake za urais! Hakuna anayefuatilia siasa za nchi hii asiyefahamu tuhuma za ufisadi dhidi ya Nazir Karamagi! Huyu nae ni insider au bila shaka nae ni one of the Senior Tactic Team Member wa EL katika mbio zake za Ikulu! JK hata kama alikuwa na tuhuma za ufisadi, hakuwa mpumbavu kiasi cha upumbavu unaoneshwa na Lowassa na ndio maana wala hakuona taabu wala aibu kumkwepa EL na kumwacha afe peke yake kwenye tuhuma dhidi ya Richmond!

Swali ambalo sijapata ni jibu ni message anayokusudia Lowassa kui-deliver kwa Watanzania hususani wale wanaofuatilia siasa za nchi hii! Kwamba, yeye binafsi, Rostam Aziz, Andrew Chenge, Naziri Karamagi wote hawa kwa umoja wao wanasingiziwa na hivyo wameamua kusimama pamoja ili , pamoja na mambo mengine they mean to reveal their innocence to the public? Au labda anataka kutuma ujumbe kwa wafuatiliaji wa siasa za nchi hii kwamba, fuc'k ya'll (fuc'k ya Tanzanians) we don't care what you think or know about us na kwamba kwa umoja wetu we'll stand firm and fight for this post?! Ni ujumbe gani hasa EL anaokusudia kuuwasilisha kwa Watanzania?!

Akili, busara ukichanganya na uungwana wa kawaida hautamfanya mtu kuhoji kwamba, let's say huyu Mheshimiwa EL anasingiziwa... ni mazingira gani yanayosababisha awe ni yeye tu wa kusingiziwa tena wakati mwingine kwenye official platforms kama vile bunge!
 
Mwanakijiji

Tatizo la Tanzania siyo ufisadi bali ni ukose wa elimu ambayo humwezesha mtu kutofautisha aliye msafi na fisadi. Upinzani kwa zaidi ya miaka tano imekuwa ikipiga kelele kuhusu ufisadi lakini ikifika uchaguzi wananchi wanashiriki kwenye ufisadi kuchagua mafisadi.

Kumbuka Elimu ni maarifa ya kutambua ambalo ulikuwa hulitambui na kutatua matatizo ya jamii.

Bila elimu bora na yenye kujumlisha utu, bado watanzania wataendelea kuona mwizi kama shujaa na wapiga dili kama watu wajanja.

Hata sasa hivi wananchi wanakosa namna ya kutofautisha Lowasa na wengine kwa sababu ya kukosa elimu.

Elimu itasaidia watanzania kujitambua.

Elimu ilikuwepo na itaendelea kuwepo, sio kwamba wanaoweka ufisadi kama kipaumbele (priority) wataongoza wananchi wajinga. Inabidi ufikirie jinsi ambavyo wizi wa rasilimali za taifa zinaathiri maendeleo ya wananchi katika kila sekta ikiwemo sekta ya Elimu. Huhitaji elimu kubwa kihivyo kujua kuwa Lowassa ni fisadi, na pia kujua kuwa ufisadi ni tatizo kubwa kwa Tanzania.
 
  • Thanks
Reactions: ELX
Kwa nini unadhani CCM itachagua mtu anayefaa? Anayefaa kwa maslahi ya nani? Kama 2005 walichagua asiyefaa, watakuwa wajinga hivyo leo wachague anayefaa?

Mkuu ni kweli tupu hakuna mtu ndani ya ccm anaeweza kupiga vita UFISADI kwani wote ni sehemu ya ufisadi huo. tena lowasa ndio kabisa hawezi!
 
i agree with you. Jana nimekaa na watu the way wananchi wa hii nchi walivyo wasahaulifu wamesahau kabisa lowasa kama alijiuzulu kwa kashfa ya ufisadi so sote tukashangilia. how comes that leo anakuwa HERO! i wonder...
 
"Hapa hatuchagui mtu maarufu, Hapa tunachagua mtu safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe naye chai. Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu. Samuel (Sitta)! Yusuf (Makamba)! Mnasimama hapa Yusuf (Makamba) mnasema ni tuhuma tuhuma tu! Lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa. Na sisi hapa Mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope halafu ndio nimuombee kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi na nchi nzima inajuasi msafi. Hafai kuwa mgombea wetu." – Mwl. Julius Nyerere, NEC Dodoma, Juni 1995 Nyerere, NEC Dodoma, Juni 1995
 
Back
Top Bottom