Freeland
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 14,481
- 10,233
Hapa hatuchagui mtu maarufu, Hapa tunachagua mtu safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe naye chai. Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu. Samuel (Sitta)! Yusuf (Makamba)! Mnasimama hapa Yusuf (Makamba) mnasema ni tuhuma tuhuma tu! Lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa. Na sisi hapa Mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope halafu ndio nimuombee kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi na nchi nzima inajuasi msafi. Hafai kuwa mgombea wetu. Mwl. Julius Nyerere, NEC Dodoma, Juni 1995 Nyerere, NEC Dodoma, Juni 1995
Asante sana...You made my day
Nalog Off
cc Washawasha
Last edited by a moderator: